Kuna watu wamekuwa wakibisha kuwa spika wa bunge hapendelei chama tawala, mara zote wanadai wabunge wa upinzani ndio hawana nidhamu, je aliyemwita Kafulila tumbili alichukuliwa hatua gani? je kama wabunge wa ccm wananidhamu mbona walishangilia na kupiga meza wakati Kafulila anatukanwa? Je mbunge wa upinzani angemwita mbunge wa ccm tumbili kamati ya maadili ingenyamaza?
Leo Rais Magufuli anapomsifia Kafulila kuwa ni mzalendo wa kweli alitetea raslimali za nchi je chama chake kilimuunga mkono Kafulila au uvccm walimtukana na kumkashfu, leo utasikia uvccm wakijitokeza hadharani kumuunga mkono Rais kwa kumsifia Kafulila.
Kama Rais amediriki kusema kuwa kafulila alikuwa anapelekwa mahakamani kwa ajili ya kutetea maslahi ya taifa, anaweza pia kukubaliana na mimi kuwa Lissu anapelekwa mahakamani kwa ajili ya maslahi ya taifa?
CCM mnaumbuka sasa, mliyemsifia anawavua ngua hadharani