Sakata la Escrow: AG Werema amvaa Kafulila, Amwita tumbili asiyeweza amua mambo ya msituni

Sakata la Escrow: AG Werema amvaa Kafulila, Amwita tumbili asiyeweza amua mambo ya msituni

Sasa na wafadhili wamenuna!
Kwa hiyo tutakula nyasi kama mnyama farasi? ?

kalimizzle;
Wazo lako zuri saana. Weye si wa kwanza kutushauri tule nyasi. Hata Mh. Basil Pesambili aliwahigi kutupa ushauri wa kula myasi ili ndege mbovu sana ya rais inunuliwe yeye ajipatie 10%.
Ushauri mzuri tu kwa Watz wenzangu. Tungojee chenji itakayo anza kuletwa kwetu kesho kutwa tuu December, 14th. Tuzichukue, tuzile vizuri tu kwani hata kutuloga hawawezi kwani nao waliziiba, kwenye kura tuwape wapinzani. Tangu mitaa, kata, jimbo hadi Magogoni. Tuweke mali mapya from upinzani.
Masikio yetu yasisikie neno jingine lolote ila Upinzani tuuuu. Tusikubali kudanganywa ati upinzani hawaja jipanga, waliojipanga wametulamba mno ka koni vile. Sasa baaaaasiiiiiiii
 
Naona sasa pamefika patamu ila ukweli utajulikana.
 
Werema alishalipwa mgao wa 2bilioni kwenye wizi wa 200bilioni.

Haya ni mawazo yako wewe wenzako wachache, fedha za escrow ni stahiki halali ya IPTL na itabaki hivyo na ripoti ya kihasibu ya CAG itasema hivyo, hayo ya ufisadi ni kelele zenu na ajenda tu za kisiasa.
 
1. Kumwita mtu tumbili ni tusi.
2. Kumwita mbunge tumbili si tusi tu kwa mbunge, bali kwa wote waliomchagua pia.
3. Mwanasheria kujihusisha katika lugha ya matusi ya jumlajumla kama haya kunashusha hadhi ya taaluma.
4. AG kutumia lugha isiyo staha nailiyo na matusi bungeni ni kulidharau bunge zima na hivyo nchi nzima.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida bunge la asubuhi limemaliza kwa mvutano mkali baada ya Kafulila kuomba muongozo juu ya ESCROW na wizi uliofanyika.

Ndipo AG alipoitwa kutoa maelezo kwanza, alianza kushambulia vielelezo vya Kafulila kuwa ni vipeperushi tu hali hiyo ilipelekea Mnyika kudai kuhusu utaratibu lakini mwenyekiti [Zungu] akampotezea.

AG aliendelea kuonyesha ubabe na kumtaka Kafulila wakutane nje kama anamambo mengne ila bungeni kunautaratibu wake [walikuwa wakimwingilia wakati anazungumza wakionesha kutokubaliana naye].

Akazidi kupandwa na hasira akamwambia Kafulila wewe ni sawa na tumbili hasiyeweza kuamua mambo ya msituni [Msemo wa kijaluo kwa mujibu wa AG].

Kelele zikazidi mwenyekiti amehairisha bunge amemtaka Kafulila na Mnyika wapeleke ushahidi wao juu ya Escrow kwa CAG na PCCB.

Nadhani jioni kutazuka miongozo tena!

Yani huyu jaji mkuu hajui ethic ya kazi kabisa
 
Jamani Kiswahili sasa kinanajisiwa...sijui ni kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Mtu akiandika Kiingereza cha kuokoteza niko tayari kumsamehe lakini Kiswahili tena lugha ya Taifa! Hakika inasikitisha...hivi tumbiri ndio mdudu gani!
TUMBILI , labda anayeandika tumbiri kazoea lafudhi ya kipare
 
kinachotakiwa ujumbe ufike tu hayo mangine ni mwembembe tu
kweli kabisa mkuu, ila hizi simu zetu za sasa zinaharibu kabisa maneno, mfano hilo nililo highlight hapo, hope ulikusudia kuandika mbwembwe
 
Tanzania ni raha sana kiongozi mkubwa serekalini anamtukana mtanzania mwenzake live bila chenga na anaacha anaendelea kutanua, mareka ukwimwita binaadamu mwenzako tumbili utakoma bila kujali nyazifa au uwezo gani wa fedha
Waafrica ni wabaguzi sana , Suarez alimuita evra nigga akashughulikiwa kwa ubaguzi.
 
Haya ni mawazo yako wewe wenzako wachache, fedha za escrow ni stahiki halali ya IPTL na itabaki hivyo na ripoti ya kihasibu ya CAG itasema hivyo, hayo ya ufisadi ni kelele zenu na ajenda tu za kisiasa.
------ wewe nyokooooo
 
Msishangilie jamani. Namkumbuka Mtemi Mkwawa na uganga wake wa ajabu. Kugeuza risasi kuwa maji. Matokeo yake ni maji maji, mwishowe kunyongwa.
Tumbili, anajiamini saana tu, lakini, kaushauri kangu. Nimesikia fununu kuwa baba mwenye kaya anarudi na akija kabla hajaingia kule Magogoni, nasikia atii stop ya kwanza ni pale Mjengoni kwa ma/bi kinda. Unajua atasema nini???
Baba kaya hatabiriki. Kama orodha za wauza sembe/ngano anazo, anwani za wamaliza tusker anazo mpaka nyumba wanazo kaa. Hakuna chochote walicho fanyiwa. NASEMA; We Tumbili, huu ni upepo tu unavuma, nao haukai, utapita tu na shamba la bibi litatulia. Wavunaji wataendelea. Hakuna mtu aliyejua kuwa kuna pahala zimewekwa/zimelundikwa tena pesa nyingi namna hiyo baada ya EPA. Leo, sijui zingine zi wapi, zikilapuliwa, kelele za Tumbili tutazisahau na kukimbilia huko.

soma tena histiria vizr co mkwawa Mkuu
 
Habarini wakuu,
Kama kawaida JF ni kisima cha hazina kuu ya Elimu na Habari makini.

Hivi karibuni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu, Dr John Pombe Magufuri alikuwa ziarani mkoani Kigoma, huko alipata kufanya mambo mengi ya kimaendeleo ikiwamo kufungua mradi wa ujenzi wa Barabara.
Tunamuomba Allah amjaalie kutimiza ndoto zake Rais wetu.

Lakini kama kawaida kauli zake hazijawahi kumuacha mtu salama,
Akiwa huko Ndugu Kafulila alibahatika kupewa pongezi za dhati, kutoka moyoni kwa Mkulu wa Nchi. Maumivu yakamuangukia yule aliyemuita Kafulila "Tumbili".
Toka siku hiyo Kafulila ameendelea kuwa lulu ktk magazeti na mitandao ya kijamii kutokana na kinga hii aliyopewa na Mheshimiwa Rais, huku waliomuita Tumbili wakihanikizwa kwa maneno mabaya. Hao watu ni kinanani, kama ni mmoja basi ni nani? Alikuwa na mamlaka gani wakati huo? Mbona hakuna anayemtaja kwa jina??


Naamini humu mko wengi wajuvi wa jambo hili, hebu nifunueni na kisha mniweke wazi ktk ukungu huu uliotanda kichwani mwangu wakuu..!!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom