Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau, katika kile kinachoonekana kuwa huenda Bunge likaingia tena kwenye mgogoro na Mahakama juu ya sakata la ESCROW, Leo Mwanasheria wa IPTL na PAP, Joseph Makandege amesema kuwa wamepeleka shauri Mahakama Kuu kuomba ufafanuzi wa Kisheria juu ya Maazimio yaliyotolewa na Bunge juu ya sakata la ESCROW. Mtakumbuka kuwa IPTL na PAP walitoa taarifa ya kupinga maazimio hayo na kuyaita ni ya kipuuzi.
Inaonekana IPTL na PAP wametafskari vya kutosha na wameona kuwa kuna haja ya Mahakama Kuu kutoa ufafanuzi juu ya maazimio hayo hasa kutokana na kuonekana kuwa yanaingilia mihimili mingine ya dola na yanajichanganya.
Source: TBC1