Sakata la ESCROW: IPTL na PAP Watinga Mahakama Kuu kuomba ufafanuzi wa Kisheria wa Maazimio ya Bunge

IPTL kwend mahakamani ni jitihada za kuling'oa meno bunge na Sasa Rais Pia wasiweze kuligusa dubwana hilo. Mihimili yote linataka kuinyamazisha isifanye lolote kuhusu iptl
 
Sijawahi kusikia BUNGE limeshtakiwa ila kwa mara ya kwanza nadhani duniani BUNGE letu linashtakiwa na MUWEKEZAJI aliyefilisi nchi/Taifa.

Ndiyo shida ya SERIKALI kuwekwa kwenye mifuko ya matakoni mwa wawekezaji.
 
Sarakasi za wamiliki wa IPTL/PAP zimechukua sura mpya na jana walitinga mahakamani kuzuia utekelezwaji wa maazimio ya bunge kwa kile walichodai kuwa bunge limeingilia kazi za serikali na mahakama.

Wamewashitaki Spika wa bunge, waziri mkuu na mwanasheria mkuu wa serikali.Pia wameweka hilo zuio.
 
Ndiyo, hili lilitarajiwa. Ni maofisa hao hao wa serikali na wanasheria wa serikali na wezi wa fedha hizo wanaochezea mahakama za Tanzania watakavyo. Wanaona udhaifu uko wapi. Wanafundishana. Kufikia Oktoba, 2015 tutaona mengi. Kwa hiyo sasa nchi inatawaliwa na IPTL?
 
Sheria inasemaje kuhusu suala lililojadiliwa BUNGENI?Ninavyofahamu kwa uelewa wangu mdogo,huwezi kumshtaki MBUNGE,SPIKA,AG Hata WM wakiwa wanafanya kazi zaoza kibunge ndani ya BUNGE.

Labda wameenda kupinga MUHONGO & Company waiadabishwe na RAIS.

Kazi tunayo,inamaana hata RAIS hana uwezo wa kufanya kazi zake za msingi sababu ya Mtoto Mpendwa PAP?
 
Mkuu hata mbunge pia huwezi kumfikisha mahakamani kwa wajibu aliotimiza bungeni
 
Sijawahi kusikia BUNGE limeshtakiwa ila kwa mara ya kwanza nadhani duniani BUNGE letu linashtakiwa na MUWEKEZAJI aliyefilisi nchi/Taifa.

Ndiyo shida ya SERIKALI kuwekwa kwenye mifuko ya matakoni mwa wawekezaji.

mkuu hata mm bado najiuliza kama kweli kuna nafas ya mtu binafsi kulishkaki bunge. Hii ni kejeli ya hali ya juu na zaid sana analishkaki bunge na kuiamuru dola kutofanyia kazi mapendekezo ya mhimili mwingine. Na hili anataka mhimili mwingne wa 3 ndo utumike kuzitia bakora mihimili mingne. Yani huyu ni mdudu gani anaeitesa nchi kias hiki
 
Sasa nimeamini kuwa ukiwa mpenzi wa CCM lazima uwe na akili za maiti. Hebu tuitazame JF ilivyo sasa. Wale wakereketwa wa hilo chama ambao wanapingana na maazimio ya Bunge wanasahau kuwa Bunge lililotoa azimio hilo 80% ya wabunge wake ni wanaCCM hivyo tunaweza kusema kuwa CCM imeridhia hatua zichukuliwe lakini kwa vile walionufaika na scandle hiyo ni wana ccm basi wanajitoa akili na kuona maazimio hayo ni ya kuiua CCM.
Ugonjwa huu wa ushabiki mbona unaharibu akili zenu? Kweli serikali yenu inaaibishwa na kakampuni kama IPTL na nyie mnakuja kubwabwaja hapa kuwa sasa PAC (Bunge) inakomeshwa na mahakama? Nchi inavuliwa nguo nyie mnaona kama vile wanakomeshwa wapinzani kwa vile hoja ililetwa na Kafulila? Kama hoja ya Kafulila ingekuwa haina mashiko 80% ya wabunge ambao ni CCM wasingeweza kutoa azimio lile.
Mnahitaji tiba tena ya lazima.
 
mkuu hata mm bado najiuliza kama kweli kuna nafas ya mtu binafsi kulishkaki bunge. Hii ni kejeli ya hali ya juu na zaid sana analishkaki bunge na kuiamuru dola kutofanyia kazi mapendekezo ya mhimili mwingine. Na hili anataka mhimili mwingne wa 3 ndo utumike kuzitia bakora mihimili mingne. Yani huyu ni mdudu gani anaeitesa nchi kias hiki

Nyerere aliongea kwenye moja ya hotuba zake kuhusu SERIKALI kuwekwa mfukoni mwa wafanyabishara.Sasa huyu ni muwekezaji na ameiweka SERIKALI yote Mfukoni mwake,na sasa analiweka BUNGE letu pia kwenye mifuko yake.

Hapa ndipo wabunge wasimame kumuweka huyu Singasinga kwenye nafasi yake.Haiwezekani a mere muwekezaji kufanya chochote anachotaka sababu tu ya vijisenti alivyoiba na viongozi wetu.
 
nyerere alikuwa dictator,dunia ishabadilika sasa,inabidi mzoee ,mtoto wa kiume kulialia haipendezi
 
IPTL kwend mahakamani ni jitihada za kuling'oa meno bunge na Sasa Rais Pia wasiweze kuligusa dubwana hilo. Mihimili yote linataka kuinyamazisha isifanye lolote kuhusu iptl

Walai nakuambia IPTL kwenda mahakamani ni mpango mkakati wa JK na timu yake hilo liko wazi ili kutuzuga wakina pangupakavu
 
nyerere alikuwa dictator,dunia ishabadilika sasa,inabidi mzoee ,mtoto wa kiume kulialia haipendezi

Kwanza mie siyo mtoto wa Kiume,ni Mwanamama ,mwenye akili timamu na siyo za kukamatiwa,ninayeipenda nchi yangu kwa kupitiliza na ninauwezo wa kumwambia yoyote ukweli bila kuwa na UWOGA.

Sidhani kama ni sahihi anachofanya huyo SINGASINGA,kwa kujiona bora zaidi na yuko juu ya serikali na sasa analiingilia bunge.Serikali imepwaya na sababu viongozi wetu ni wahusika wakuu wanajificha nyuma ya pazia ,wote kuanzia kwenye ile nyumba ya magogoni pamoja na wanaojiita wasomi mawaziri wote wamelifikisha TAIFA letu hapa.

Wahusika wote pamoja na huyu SIngasinga wanatkiwa kwa sasa wawe wanatumikia kifungo na pesa zetu wamerudisha.
 
Mahakama ndiyo sehemu pekee ya kupata haki safi sana PAP kutafuta haki yenu.

Wewe ni lyapugile kwelikweli mahakama zilizofurika rushwa zitatenda haki gani? We kama umetumwa kawaambie bado hatuja lala
 
Kwanza mie siyo mtoto wa Kiume,ni Mwanamama ,mwenye akili timamu na siyo za kukamatiwa,ninayeipenda nchi yangu kwa kupitiliza na ninauwezo wa kumwambia yoyote ukweli bila kuwa na UWOGA.

Sidhani kama ni sahihi anachofanya huyo SINGASINGA,kwa kujiona bora zaidi na yuko juu ya serikali na sasa analiingilia bunge.Serikali imepwaya na sababu viongozi wetu ni wahusika wakuu wanajificha nyuma ya pazia ,wote kuanzia kwenye ile nyumba ya magogoni pamoja na wanaojiita wasomi mawaziri wote wamelifikisha TAIFA letu hapa.

Wahusika wote pamoja na huyu SIngasinga wanatkiwa kwa sasa wawe wanatumikia kifungo na pesa zetu wamerudisha.

Tetty umezungumza ukweli ikulu ndipo wezi wanapofichama
 
Nimeuzungumza lakini unauma kweli kweli.Hebu fikiria Mtu uliyemuamini ukampa dhamana ya kuongoza ghafla anageuka DALALI wa kuuza nchi.
 
Walai nakuambia IPTL kwenda mahakamani ni mpango mkakati wa JK na timu yake hilo liko wazi ili kutuzuga wakina pangupakavu

Kwa hiyo KESI hiyo inamzuia Mheshimiwa sana aka Prof wa Kichina kuwawajibisha waliowateua?
 
Back
Top Bottom