Sakata la Jerry Silaa kuvunja majumba ya watu nchi nzima: Johnson Mahululu aidai serikali ya Tanzania bilioni 20

Duh!!
Mkuu ilikuaje hiyo.....??
Aliwatandika risasi au....??
 
Mkuu argument yako doesnt hold.
Custodian wa official records za Ardhi ni wizara yenyewe, and they undoubtly know who the authentic owner of the parcel of land is.
And you have the audacity to dispute THAT?
Just make a quick buck from your client.
Yes, I have the audacity to dispute this...

Kumbuka kuwa, Wizara ya ardhi ambao kweli ndio custodian wa official records wa nyaraka zote zihusuzo mambo ya ardhi ambaye Waziri wake ni Jerry Silaa na kamishina wake ndio players wa mgogoro huu..

Na utakuwa ni mjinga sana kudhani na kuamini kwamba, kwa kuwa hawa ni custodians wa nyaraka zote zihusuzo ardhi, basi wao hawawezi kushiriki kwenye hujuma za kijinga kama hii na kuzua migogoro isiyo na kichwa wala miguu..

By the way, unadhani ni kwanini mtu huyu (Johnson) wanayemwita tapeli wanashindwa kumpeleka mahakamani ili waka - prove kuwa wao ni legitimate custodians kwelikweli na badala wanamficha kwenye vituo vya polisi kinyume cha sheria?

Yaani ukisikiliza maelezo ya waziri na ukasikiliza maelezo ya aliyevunjiwa nyumba na waziri Jerry Silaa, mtu yeyote mwenye akili na ufahamu sawasawa atatambua moja kwa moja kuwa, waziri huyu ame - mess up big time..

In my opinion, waziri Jerry Silaa hakupaswa kuchukua maamuzi haya yeye tu kwa staili ile. Alipaswa kuwashauri hawa wenye mgogoro waitumie mahakama kuamua mgogoro wao..

Na kama waziri wa serikali haiamini mahakama, basi ni wazi kuwa iko shida ktk mifumo yetu ya utawala..
 
Duh,pole sana mkuh .ila ukweli wahanga ni wengi sana walio dhurumiwa aridhi kwa kwa kigezo cha pesa na conections
 
Ni wafanyakazi wajinga tu ndio wanaofanya michezo hiyo, mtu mwenye akili zake timamu awezi jiusisha. Maana anaelewa akiingia waziri kichaa kwenye hiyo wizara au raisi mkali anaweza jikuta lupango.

Ardhi kuna three way back up verification system kuna file number ya offer au hati; hard copy 1 wanabaki nayo wao, nyingine anapewa mteja na data base ni sehemu ya tatu (ambayo sidhani kama ni rahisi kuichezea).

Haya mambo ya kusumbuana yanawezekana vipindi kama hivi, Iła kipindi cha Magufuli najua watu awapendi kusikia hilo jina na si lengo kumtaja kwa sababu za siasa Iła uhalisia wa muda wake hii biashara iliisha.

Nashangaa sana hawa wenye migogoro ambayo ipo way back walikuwa wapi kipindi cha Magufuli. Shangazi (sio wadamu rafiki wa mama na alikuwa na migogoro ya viwanja vya wanae wanne Tegeta vyote vilivamiwa), jamaa yetu mwingine kiwanja chake Mwananyamala mtu alijenga, dada yangu wa tumbo moja kuna nyumba aliachiwa na bibi yetu mtu akajimilikisha baada ya sister kukaa ulaya kwa miaka 20.

Wote hao ni diaspora mmoja tu huyo shangazi ndio alirudi na wote hao waliangaika kwa miaka bila ya mafanikio alipoingia Magufuli tu; wote wakapata haki zao. Sema huyo mwenye nyumba baadae Magufuli akaipiga chini ipo eneo la barabara kwa madai yake bila ya fidia (ajabu nyumba imejengwa miaka ya 70) huko.

Sasa hawa wanaoishi Tanzania najiuliza walikuwa wapi kipindi hiko.
 
sijakupa like sababu mimi ni mbaguzi wewe huna jinsia lakini umeongea point kongole.
 
Mahakama tukufu lazima kuheshimiwa waziri alipe bil 20 za mdai ili kulinda heshima za mahakama ,pumbavu kabisa ,yani waziri anasimama na kusema kama serikali imesema basi ,ujinga gani huu, waziri lazima elewa hata kabla yake wizara ilikuepo na itaendelea kuwepo .

Mwanasheria ameeleza ameeleza vizuri sana ,mtu baraza la kwanza kashindwa, mahakamani kashidwa alafu waziri anajifanya vaa mziki mzima mzima

Nasema kesi hii nimewahi ivaa nikiwa Tanga , but mhusika alipiga magoti akiwa Bombo hospital , maana uyu ndugu yupo na pesa mie sina pesa,Simanishi kwenye mgogoro huu maana wakwangu ilikua tofauti kidogo

Kwamba

Mwenye mali amekufa na kuacha wajane watatu , na bi mdogo wa marehem kaolewa na bwana mmoja mjinga hivi, alafu uyu mjinga anataka lazimisha mali ikiwemo mashamba ayamiliki wakati hata kwenye mirathi ,marehem hakuyaingiza kwa sababu moja au mbili ambazo siwezi sema hapa

Nilimnyoosha ipasavyo ,Mungu sio Mwanadam
 
Pole sana, siku nyingine fuata sheria na taratibu za nchi.
 
Bahati mbaya wakati wenzako wanaenda shule, wewe ulikuwa unasubiri uji jikoni, ukapewa kazi ya kuchochea kuni
Wacha ujuaji wewe wala hunijui sikujui. Kama ndiyo muhusika katika majaji feki wewe endelea na dhambi zako tu.
 
Inawezekana
 
Waziri, Mkuu wa mkoa au Wilaya na kamati yoyote ile hawana mamlaka ya kuboma mahali bila kibali cha mahakama.
 
Kuna shida kubwa sehemu
 
Kila siku mnaambiwa mjenge mifumo imara kwanza ya kutenda haki katika nchi kwa kuandika katiba mpya. - bado CCM wanawadanganya kwa kutengeneza matatizo kisha kuja kuyashughulikia waonekane wanachapa kazi.

Migogoro kama hii hayawezi kuisha kwa ziara za viongozi hao hao waliyoitengeneza.

Poleni watanzania, hadi hapo mtakapoamua kuandika KATIBA MPYA KWANZA ili mjenge mifumo imara ya utawala wa nchi yetu, vinginevyo ni maumivu tena makali hasa kwa 80% ambao ni makapuku wenzangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…