Sakata la jezi feki mhusika anaogopwa ,serikali imeshindwa kumtaja vilabu vimeshindwa kumtaja ,polisi tutajieni huyo mtu ninani?

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Yale Yale Kila mtu analalama TU! Mhusika hatajwi, waziri kaenda mpaka eneo la tukio kashindwa kumtaja mhusika.

Sandaland mwenyewe aliahidi atamtaja lakini naona katishwa, kaogopa kakunja mkia, jeshi la polisi hawamtaji analindwa na anafunikwa funikwa.

Kuna hatari akabambikiwa mtu mwingine kabisa ili kumlinda huyo taita mwenyewe, habari za chini ya kapeti ni mtu mzito na yupo sana kwenye vilabu hivi.

Nasisitiza kwamba mtajeni kama hamuwezi kumtaja mnamuogopa acheni kutupa stori za hayo matambala yenu
 
Wewe mwenyewe inainekana unamjua ila unaogopa kumtaja kwanini unawalaumu hao wenzako?

Unawalaumu watu hawamtaji kwenye TV wakionekana sura zao au kwenye radio wakisikika sauti zao wakati wewe una ID fake hujulikani huonekani na bado unaogopa ku type tu, dah!
 
Nakupa code......

Ukitataka kuvuta bangi unahitaji vitu vitatu ili bangi ikamilike yaani msuubaaa

.1...Riz.
.2..bangi iwe namba moja kwa ubora (0ne)
.3.mixer (gozo,nyota ext..

Natumain ushamjua muhusika kama wew ni mvutaji wa kanka
 
Tumuombe bingwa wa kutegua vitendawili vigumu GENTAMYCINE atufungulie code
 
Nchi imeoza kwa rushwa, unadhani mzigo wa 10B anaweza kuagiza mtu wa kawaida?
 
HSC
 
Unataka wengine wamtaje wakati wewe mwenyewe unazunguka tu, mtaje kwa jina ni Fulani. Sasa maneno mengi kumbe huna lolote.
 
Sisiemu ipo chini ya raia feki na huyo muingiza jezi pia ni mmojawao ...nchi imetekwa na viongozi wenye uraia feki kwa sababu ya siasa za kipumbavu za ccm

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
Hii nchi ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…