Mawembasa1979
JF-Expert Member
- Feb 26, 2015
- 2,540
- 3,333
Mkuu mbona unalialia sana kwani mmejipangaje mwaka huu!Wacha wakapate haki yao huko.TFF imejaa uzandiki unafiki na upendeleo wa wazi. Mwaka jana AZAM F.C walipokwa pointi tatu bila hiyo timu pinzani iliyocheza nao bila hata kukata rufaa ya kupewa pointi tatu. Walifanya hivyo ili AZAM F.C izidiwe pointi na timu ya Yanga timu ya Rais Malinzi.
Si bure Simba imemis Libolo!Simba waende tu ili kuleta nidhamu na uadilifu kwenye usimamizi na utawala wa soka nchini ambao umeshuka kwa kiwango cha kutisha. Na Simba wafanye kweli wasilete uhuni, watafute pesa waende FIFA, ushindi ni guaranteed. Kule hakuna kupiga kura au kuangalia kamati ina wajumbe wangapi wa Yanga au Simba. Ni kanuni tu.
Malinzi na genge lake wanaendesha soka kwa kufuata upepo unavyovuma badala ya kuangalia kanuni zinasemaje. Kama kweli Simba wanalalamika kesi zao zote hazijatolewa maamuzi ila zile ambazo ziko againsta wao zinasikilizwa hata wakati wa sikukuu ujue kuna tatizo kubwa zaidi.
Tunataka maandamano kwanza halafu FIFA baadae!Maandamano FC aka Mezani FC.
Vipi kuhusu rufaa ya Polisi dhidi ya Simba ilivyokataliwa sababu ya kanuni? (kutolipa ada ya tufaa)Hivi unajua unachokiandika? Ikimchezesha mchezaji mwenye kadi 3 za njano ni kupokwa points automatically. Haina haya ya kuandika barua wala rufani. Kumbuka mwaka jana Azam alivyonyang'anywa points na mbeya city akapewa. Mbeya city hawakuandika barua wala rufaa hata sms hawakutuma cz it's something automatically.