Simba waende tu ili kuleta nidhamu na uadilifu kwenye usimamizi na utawala wa soka nchini ambao umeshuka kwa kiwango cha kutisha. Na Simba wafanye kweli wasilete uhuni, watafute pesa waende FIFA, ushindi ni guaranteed. Kule hakuna kupiga kura au kuangalia kamati ina wajumbe wangapi wa Yanga au Simba. Ni kanuni tu.
Malinzi na genge lake wanaendesha soka kwa kufuata upepo unavyovuma badala ya kuangalia kanuni zinasemaje. Kama kweli Simba wanalalamika kesi zao zote hazijatolewa maamuzi ila zile ambazo ziko againsta wao zinasikilizwa hata wakati wa sikukuu ujue kuna tatizo kubwa zaidi.