Sakata la Kampuni ya Lugumi: IGP na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani watupiana mpira

Sakata la Kampuni ya Lugumi: IGP na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani watupiana mpira

Kwi kwi kwi kwi mie nilidhani nanihii haogopi kulamba moto kumbe eeh! ile kauli mbinu ya HAPA KAZI TU! ni usanii wa mwingine wa awamu ya tano kama ilivyo ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya pamoja na Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana kwenye awamu ya nne.

..

....Mkuu BAK moto haulambwi
 
Ahsante sana Mkuu, nashukuru sana kwa hii taarifa, huwezi kumpa nchi mgombea aliyepigiwa debe na Mkapa na Kikwete na ambaye alikuwa katika Serikali za awamu ya pili mpaka ya nne ambako madudu chungu nzima yalitokea halafu ukategemea kuwepo na mabadiliko makubwa nchini. CCM bado ni ile ile ndiyo sababu hata baadhi ya wapokea rushwa na mafisadi hawana wasiwasi wanajua hakuna wa kuwagusa vinginevyo nchi itawaka moto.

Duh, BAK, umetokea wapi tena! Karibu sana, nilianza kuingiwa na wasiwasi kuhusu uwepo wako humu. Naomba nikupe tahadhari moja tu, viwavi vingi vimemwagwa humu na wapo wenzetu wachache wamesalimu amri na kuweka silaha chini kwa ule mtindo wa if you can't fight them, join them.

Taasisi za serikali zilizokuwa mstari wa mbele zikihusishwa na ufisadi bado ziko pale pale...Jeshi la Polisi lipo pale pale, jukumu lao kubwa kwa sasa ni kuwashughulikia wanaokosoa serikali. Badala ya kuwalinda raia wema na mali zao, wamejikita katika kukilinda chuo cha Mafisadi na wahitimu wake!
 
Kuna kila dalili hapa hakukuwa na mkataba au kama ulikuwepo basi wajanja wameshauiba na kuuchana ili kupoteza ushahidi katika hili sakata la mabilioni chungu nzima.
wewee umerudi ulipotelea wapi?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa utaratibu Mkataba unatakiwa uwe wapi? Ulipo Mkataba mhusika ndiye aupeleke huo Mkataba.
Kwani Mkataba ulikuwa kati ya Wizara au Idara ya Police? Police department ndiyo iliyofanya malipo au Wizara?
Haki na isimame
 
Back
Top Bottom