King Kisali
JF-Expert Member
- Nov 20, 2019
- 1,041
- 1,349
Sakata la kanisa lililoripotiwa kupiga muziki mkubwa sana masaa 24 na lililojengwa katikati ya barabara , limeingia sura mpya baada ya serikali kuchukua hatua na kulizuia kuendelea kujengwa na kuendelea na shughuli zozote za ibada , baada ya maofisa wa serikali kufika kanisani hapo Jana na kubandika zuio hili , ambapo baadhi ya waumini wa kanisa hilo walikuwepo . Baada ya maofisa wa serikali kuondoka mchungaji aseme hawambabaishi , akabandua zuia hilo na kusema hawawezi kumfanya kitu na jumapili ataendelea na ibada kama kawaida hawawezi kumfanya kitu chochote yeye ni mwamba serikali haimuwezi kwa lolote .