Wanabodi wenzangu,
Mimi wakati mwingine huwa mgumu kuelewa na mwepesi kusahau, hivyo naomba mnisaidie na mnivumilie!
Naona kuna mawazo kwamba kuuzwa kwa RDC kutatuathiri. Sielewi kwa nini iwe hivyo.
1. Kwani wangebaki wao (RDC) kungekuwa na tofauti gani nzuri au bora zaidi?
2. Kama hao Dowans ni wa-kimataifa zaidi, si ni bora kuliko RDC?
3. Kama hao Dowans wataendelea na sisi (Tanesco) kwa mkataba huo huo tofauti ni nini?
4. Kwamba tumeliwa kwa vile "umeme wa maji" upo si ni bahati tu na si kwamba hao RDC wala serikali yetu walitabiri kuwa maji yangejaa na hivyo kuwa RDC hawakuhitajika?
5. JK, alipoenda huko ghuba alikaririwa na vyombo vya habari kusema kuwa kuna wawekezaji wa huko wanaotaka kuwekeza kwenye uzalishaji umeme nchini. Je, ndiyo hao Dowans?