Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Ni sawa kama waliimba Richmond maana Msanii EL anajua vyema kunani .
 
Mambo ya kasi na ari na CCM kushika hatamu .Jiulize nani kafungwa hatamu? Mliwapa wenyewe sasa mnalia nini ?
 
Jasusi na Rev,

Huyu ni mwandishi wa PM, acheni kejeli kwi kwi kwii

FD
 
Wanabodi,

Kusema ukweli mimi imefika sehemu nimekata tamaa kabisa na ndio maana hata michango yangu katika hii bodi imepungua kabisa .Mimi naona Tanzania inaongozwa na watu ambao rushwa ni part and parcel ya maisha yao . Rais anasima na kutetea Rich - monduli bila ya wasi wasi na wakati huo huo anajua hii kampuni aijawa registered .

Mimi nasema hivi Tanzania tutaendelea kuwa maskini mpaka siku ya mwisho kwani mentality za hawa viongozi zinatia huruma.
 
Na hawa hawa ndio wanaotuvuga kuwa watapitia upya mikataba ya madini? Inaudhi.
 
Wanabodi wenzangu,

Mimi wakati mwingine huwa mgumu kuelewa na mwepesi kusahau, hivyo naomba mnisaidie na mnivumilie!

Naona kuna mawazo kwamba kuuzwa kwa RDC kutatuathiri. Sielewi kwa nini iwe hivyo.

1. Kwani wangebaki wao (RDC) kungekuwa na tofauti gani nzuri au bora zaidi?

2. Kama hao Dowans ni wa-kimataifa zaidi, si ni bora kuliko RDC?

3. Kama hao Dowans wataendelea na sisi (Tanesco) kwa mkataba huo huo tofauti ni nini?

4. Kwamba tumeliwa kwa vile "umeme wa maji" upo si ni bahati tu na si kwamba hao RDC wala serikali yetu walitabiri kuwa maji yangejaa na hivyo kuwa RDC hawakuhitajika?

5. JK, alipoenda huko ghuba alikaririwa na vyombo vya habari kusema kuwa kuna wawekezaji wa huko wanaotaka kuwekeza kwenye uzalishaji umeme nchini. Je, ndiyo hao Dowans?
 
Invicible,
Ile $9 mil a month ni subsidy kwa TTCL. And no one raises an eyebrow.
 
Mwanagenzi, tatizo ni kuwa maswali yako hayo hakuna anayeweza kuyajibu kwani hatujui mkataba unasema nini! Tunachoona ni vyombo vya mwanamazingaombwe vinapelekwa kwa mtu mwingine na tunaambiwa onesho litaendelea!! sasa, sisi tutajuaje makubaliano yao.. hata fedha ya kununua mkataba huo ni siri!!
 
Bravo Mwanakijiji,Naomba article yako ya "Mazingaombwe ya Mwaka" ipeleke kwenye magazeti ya Nyumbani ili nao waisome!Imefika wakati sasa watanzania wafumbue macho kwa mambo yanayowahusu.Hawa watawala wetu wametufanya wapumbavu mno,wanafanya chochote wanachokitaka bila UOGA wala HAYA.Mmmmmh jamani imetosha, watuonee huruma nasi tuweze kuishi kwa matumaini!
 
Wanabodi wenzangu,

Mimi wakati mwingine huwa mgumu kuelewa na mwepesi kusahau, hivyo naomba mnisaidie na mnivumilie!

Naona kuna mawazo kwamba kuuzwa kwa RDC kutatuathiri. Sielewi kwa nini iwe hivyo.

1. Kwani wangebaki wao (RDC) kungekuwa na tofauti gani nzuri au bora zaidi?

2. Kama hao Dowans ni wa-kimataifa zaidi, si ni bora kuliko RDC?

3. Kama hao Dowans wataendelea na sisi (Tanesco) kwa mkataba huo huo tofauti ni nini?

4. Kwamba tumeliwa kwa vile "umeme wa maji" upo si ni bahati tu na si kwamba hao RDC wala serikali yetu walitabiri kuwa maji yangejaa na hivyo kuwa RDC hawakuhitajika?

5. JK, alipoenda huko ghuba alikaririwa na vyombo vya habari kusema kuwa kuna wawekezaji wa huko wanaotaka kuwekeza kwenye uzalishaji umeme nchini. Je, ndiyo hao Dowans?

Majibu:
1.Whether tofauti ingekuwa nzuri au mbaya,tayari wameshakuchukua hela ya walalahoi.Mkwe m-bovu akiendelea kuwepo kwenye ndoa unaweza kumpeleka kwenye baraza la usuluhishi wa ndoa au kumminya ampe talaka mwanao.Akiingia mitini....you can guess the consequences
2.Na kama hao Dowans ni wa Kimataifa walikuwa wapi siku zote hadi wasubiri kuwakwamua Richmond ilhali sera ya kukaribisha wawekezaji imekuwepo for over 10 yrs now?By the way,who knows if Dowans sio haohao Richmond lkn wameamua kuiga stori ya "Sheraton baadae Movenpick"
3.Suala sio KAMA Dowans wataendelea na mkataba bali KAMA WATAWEZA KUZALISHA UMEME.Kuendelea na mkataba sio tatizo,hata Richmond "waliendeleza mkataba" kwa miezi kadhaa (ulisainiwa July or August)
4...Didnt understand the question
5.Were you implying kwamba JK alipokwenda ziarani nchi za Ghuba alikuwa amepewa meseji na Richmond ya kuwatafutia watu wa kuwakabidhi mkataba uliowashinda?At least umetusaidia kufahamu kuwa all along JK na Richmond walikuwa kitu kimoja,and when he said he would bring investors he was in fact saying he would bring Dowans to "buy" the Richmond's contract.
 
Mwashangaa nini I told u kuwa Richmond watajivua. Mmeona sasa? Haya kalageni baho na uboza wenu! Masikini Tanzania. Nchi ya kutafunwa tu.
 
Invicible,
Ile $9 mil a month ni subsidy kwa TTCL. And no one raises an eyebrow.

Ni TTCL au IPTL? Kadiri nnavyofahamu capacity charges kwa IPTL ni kama Tsh bilioni tatu. Ni hayo makampuni mengine yaliyoongezeka ndio gharama imeongezeka. Au labda nimechanganya mambo?
 
Mwashangaa nini I told u kuwa Richmond watajivua. Mmeona sasa? Haya kalageni baho na uboza wenu! Masikini Tanzania. Nchi ya kutafunwa tu.

I see! Ndugu yangu wewe mkali. Sijui upo karibu kiasi gani na system, maana post yako ya tarehe 11 December ulisema kwamba muda si mrefu hao jamaa watajitoa baada ya kuuwasha umeme wao. It has happened in almost exact way you predicted.
 
Anaweza kuwa ndiye Naam Gere mwenyewe...just a wild guess
 
Please guys feel hurt and take then matter serious . Kuna uhuni mkubwa serikalini sasa tuwe focussed badala kuanza utani . Richmonds wamejitoa how ? Mkataba ulikuwa unasemaje ? Nini jibu ama tamko la Serikali ? Wamejitoa ina maana pesa wamechukua machine mbovu wanatuachia ?
 
Hivi mnataka kuniambia hakuna mtu humu aliyeuona mkataba huo au ambaye anaweza kunipenyezea mimi... huu mkataba hautawekwa hadharani na serikali hadi mtu jasiri mwenye mapenzi na nchi atafanya hivyo. Mimi niko tayari kuweka hadharani kama mtu atanipenyezea....mwanakijiji@journalist.com
 
Back
Top Bottom