Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Kama mnakumbuka, baada ya mitambo ya kuzalisha megawati 20 kuletwa, hao Richmonduli walisema mitambo iliyobaki itatoka South Africa. Could there be any connection with what is happening now?
 
Muulizeni JK intergity na honesty yake kwa Tanzania iko wapi ?
 
Lunyungu

Huwezi tu kuuliza swali namna hiyo wewe unafahamu. Watu wote tutakucheka lazima uwe na logic behind. Kama unataka watumie wana London maswali unayotaka waulize [kwenye PM] na hiyo porojo ya hapo juu ondoa.
 
Kama ni Porojo Dua achana nayo tuendelee na kukata issue ila message imefika .
 
Duuuuh !
Dowans inatoka South Afrika?...
Mazingaombwe ya Nabii haya!...
 
These guys are not even ashamed? They've stolen enough and now they want to cover their backs. we are not going to sleep.
 
Labda wakati wanauza huo Mkataba hawakujua kama kampuni wanayoiuzia iko Afrika Kusini? Si mtu amwendee huyo kibosile wa Tanesco na kumuuliza ilikuwaje asema kampuni ni kutoka Uarabuni?
 
Mzee Mwanakijiji: Ile artilce yako imetoka katika gazeti la Tanzania Daima. Ila mwandishi kaibadilisha kidogo. The bad news is that the author did not even acknowledge the original source! Anyway, angalau itawafikia watu wengi zaidi. Here we go:


Richmond kiboko wa mazingaombwe!

Dennis Msacky



KUNA mjadala mkubwa ambao unaendelea hasa kwa raia wa Kitanzania wanaoishi katika nchi za Uingereza na Amerika.


Mjadala huu si mwingine ni sakata la umeme, tena si umeme wa Mtera na Kidatu, bali ni kuhusu Kampuni ya Richmond, ambayo ilitamba kwa makeke kwamba ingetatua angalau kwa kiasi fulani tatizo la umeme. Watu hawa ambao wameingia katika mjadala huu si watu wa mzaha, bali ni wasomi waliobobea katika masuala mbalimbali ya kijamii, wana uzalendo na nchi yao, wanasikitikia viongozi wetu walivyo na upofu wa kujua baya na jema, wanasikitika na kuhisi kwamba ujio wa kampuni hii ni ‘dili' la baadhi ya watu.


Mjadala huu umezua mengi, sasa wengine wanasema kwamba kama ni bingwa wa mazingaombwe, basi Richmond inakwenda kwa Kasi Mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya, yote hasa yanaashiria kwamba mambo si shwari kwa masuala kadhaa kwa viongozi wetu.


Watanzania wamefanyiwa mazingaombe, wana maswali kemkemu ya kuuliza, lakini hayupo wa kujibu, kila mmoja anapiga chenga. Kuna siku hizi chenga wanazopiga zitajulikana, hapo ndipo wataanza kusaga meno. Maana wahenga walisema, muosha naye huoshwa.


Msomaji hebu fuatilia kisa cha Richmond kuifanyia serikali mazingaombwe ya mwaka na baada ya hapo tafuta jibu la maswali yaliyo chini kabisa.


Sasa kwenye fani ya mazingaombwe kuna vitu vikubwa vitatu. Cha kwanza kinaitwa wepesi wa mikono (sleight of hand), cha pili ni viinimacho (illusion) na cha tatu ni kupoteza lengo (distraction).


Ili mazingaombwe yafanikiwe na kuwa na mvuto ni lazima vitu hivyo vitatu viende sambamba na kwa wakati muafaka.


Sasa mwanamazingaombwe aliyebobea atahakikisha kuwa watu wanashuhudia mtu anaingizwa kwenye sanduku (sleight of hand), sanduku linakatwa nusu kwa upanga (illusion), huku mwanamazingaombwe anawaeleza na kuwachangamsha watu kwa maneno na porojo (distraction).


Pindi lile sanduku likiunganishwa tena na yule mtu aliyewekwa humo akatoka mzima (restoration), basi watu watapiga makofi na kumsifia mwanamazingaombwe kwa onyesho zuri na mwanamazingaombwe huyo atachukua pesa zake na kuandaa onyesho jingine, na wale ambao hawataki kufikiri juu ya nini wameshuhudia wataendelea kupiga makofi na kuchekelea.


Alichofanya jasusi, ni kutoboa siri ya mazingaombwe! Watu wa Richmond wameleta mazingaombwe ya hali ya juu na nusura wafanikiwe kumrejesha mtu akiwa bado mzima kutoka kwenye sanduku.


Watanzania walitaka kuridhishwa na onyesho zuri la ‘Umeme'. Ndipo wanamazingaombwe kutoka Houston, Marekani walipotokea na vikolokolo vyao vya mazingaombwe. Wakawaambia Watanzania kuwa wana uwezo wa kuleta nishati (kumkata mtu nusu bila kumuumiza) tena kwa bei rahisi. Watanzania wakaamini na wakawapa nafasi.


Kwa vile wanamazingaombwe wetu hawakuwa na lengo wala uwezo huo, iliwabidi wafanye viinimacho. Ndipo wakaagiza ‘majenereta' ambayo hayakuweza kufika kwa muda muafaka. Wakaanza kuyatengeneza, na ‘kuyaseti' ili baadaye yazalishe umeme (ndiyo kumweka mtu kwenye sanduku kwa taratibu huku watu wakiangalia). Wakaleta na wapiga picha Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere kuona majenereta yanavyoletwa na ndege kubwa zaidi duniani ya mizigo. Watanzania wakapiga makofi na kushangilia.


Wakati watu wanajiuliza hivi kweli wataleta umeme hawa (je, kweli mtu ataungika?), basi wanamazingaombwe wa Richmond wakaanza kutuhamasisha pamoja na washirika wao (serikali) wakilumbana na kukandiana hadharani (distraction).


Lengo likiwa kununua muda. Wakati watazamaji (Watanzania) wakiendelea kushangaa nini kinaendelea, tukatangaziwa kuwa jenereta liko tayari kuanza kazi, na kwamba wanasubiri Tanesco wakubali umeme wao. Wakati huo wote, Richmond walikuwa wanasubiri mvua.


Hatimaye, dua zao zikasikika na mazingaombwe ya mwaka yakafanyika. Mabwawa ambayo yanatumika kuzalisha umeme yakajaa maji, umeme wa Richmond haukutumika, mkataba wa Richmond na Tanesco ukauzwa kwa kampuni nyingine ya kigeni, ambayo tuliambiwa kuwa ina uwezo wa kuifanya kazi ya Richmond, mwenye kutengeneza pesa akatengeneza pesa, na Watanzania wakabakia kushangilia umeme wa kudumu.


Rais Jakaya Kikwete akashangilia na kuwapongeza viongozi wenzake majasiri, hodari na makini kwa jinsi walivyoshughulikia tatizo la umeme.


Onyesho la mazingaombwe la Richmond likafanyika kwa ufundi mkubwa. Kwa vile Watanzania hawajagundua kuwa wameshuhudia mazingaombwe, basi mwaka huu wanasubiri onyesho jingine lenye kuhusu mkataba mwingine, na gurudumu la mazingaombwe na viinimacho linaendelea kubingirishwa. Ndugu msomaji, ingawa makala hii imeonekana kuwa na mzaha kwa kiasi fulani, lakini hicho ndicho ambacho kimetokea.


Hata umeme wa Richmond usingekuwapo sasa, Watanzania tungepata umeme kwa kuwa Mungu amesikia kilio chetu na kuleta mvua, lakini pia lazima kujiuliza, kwanini Richmond wameuza kampuni yao kwa wengine, kuna nini? Watawala wanapaswa kutuambia.


Je, hawana uwezo? Au wanaogopa kwamba wanaweza kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria hapo baadaye? Je, ni Richmond ndio walitafuta hii kampuni ya kuinunua?


Kwanini Tanesco ilikubali kuiuza haraka haraka tena hivyo? Haya ni maswali mengi ambayo Watanzania wanapaswa kuambiwa na serikali yao waliyoiweka madarakani. Watanzania katika zama hizi za utandawazi hawataki tena kitu kinachoitwa mazingaombwe. Huu ni wakati wa sayansi na teknolojia. Mazingaombwe, hayatatufikisha kokote, na ndoto zetu zitabakia tu kuwa ndoto za alinacha.


Watawala hebu tuambieni kisa cha Richmond kukimbia dili za fedha za walipa kodi.


Haiingii akilini kwamba umeanza mradi, hata bado hujaona matunda yake na kuamua kuuza kwa watu wengine. Kuna jambo ambalo limejificha, Watanzania wanataka ukweli wa jambo hili, msipofanya hivyo hawatawaamini, na umaarufu wenu utaendelea kushuka kila kukicha, jinsi pia hali zao za kiuchumi zinavyoshuka kila kukicha.


Mwisho nawatakia mwaka mpya, na kuwaambia watawala wasikubali mazingaombwe ya aina hii, werevu watatucheka.

Dennis Msacky ni mwanahabari mwandamizi, na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa
Email: msackyd@yahoo.com
 
Haya si mafanikio ya CCM ? Mbona mwana KJJ uka andika haya kama makala hii ni yako ? Nilidhani debe unalopiga ni kwamab CCM is good zaidi ya Chadema na ndiyo maana uko CCM ?
 
Mwanakijiji,
Waliosema mitambo inatoka Afrika kusini si uongozi wa Tanesco. Ni akina Gire wa Richmond. Kwanza walisema wana shida za usafiri wa ndege za mizigo Marekani. Baadaye wakasema wamepata usafiri wa mitambo. Baadaye kidogo wakasema mitambo imenunuliwa kutoka Afrika kusini. Kwa hiyo wa kuulizwa si uongozi wa Tanesco bali wasanii wa Richmond.
 
Procurement body to sift Richmond, Aggreko deals
JIANG ALIPO
Daily News; Wednesday,January 17, 2007 @00:05

A PARLIAMENTARY committee yesterday directed the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) to scrutinise if there was any wrong doing in the tendering process that led to engagement of Richmond Development Corporation (RDC) and the Aggreko in an emergency power supply project.

Talking to the 'Daily News', some of the members of the Parliamentary Committee of Finance and Economic Affairs said PPRA was assigned the task during a meeting with the lawmakers in Dar es Salaam.

"We have asked them to investigate the tender procedures and then report to us whether the procedures were followed or not," said the MPs.

The two companies were given a tender to produce 140MW upon installation of the generators to cope with power crisis in the country Procurement body to sift Richmond, Aggreko deals last year. Aggreko was required to produce 40MW, while RDC was to contribute 100MW.

It was reported that when the tendering process was carried out mid-last year, RDC's offer was rejected by Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) - though it was the lowest bid - on grounds that it did not have a proven record of generating power.

Tanesco picked Aggreko and Globeleq for the tender but a ruling was unilaterally made later in favour of RDC. Six other companies had also tendered to supply gas-generated electricity.

However, the Vice-Chairman of the committee, Mr Adam Malima, declined to give details of the meeting, saying it was a normal procedure for it to meet government institutions under Ministry of Finance.

"They have given us a report on their performance today (yesterday), which I have no doubt about, and asked them to prepare some other things. We will meet them again on Saturday.

"This is a normal procedure, there is nothing spectacular. We have discussed a lot of things with them," he said.

Mr Malima said they are interested in PPRA because more than 50 per cent of government finances are spent on procurement. "This is a very important institution with a major role in national development," he said.

Section 9 of Public Procurement Act 2004 empowers PPRA to initiate investigation on any government or public institutions' procurement procedures.


RDC WALIKATALIWA KUTOKA MWANZO LAKINI SHINIKIZO KUTOKA MAHALA FULANI NDIO LILILAZIMISHA RICHMONDULIAN WASHAMIRI JE WHO ARE THEY?
 
daymn... haya.. najisikia kupata heshima hata kama jamaa hakuweka original source.. kwa sababu mimi nimeshawaambia yoyote ninayoyaandika na kuyasema ambayo yana manufaa kwa Taifa sijali ni nani anayatumia! ila next time ahakikishe ameondoa mambo mengine ambayo yalikuwa kwenye original kama jina "Jasusi" kwani hapo nilikuwa najibu na kupongeza maneno aliyosema Jasusi, mtu mwingine hataelewa isipokuwa awe ni msomaji wa JF!
 
RDC WALIKATALIWA KUTOKA MWANZO LAKINI SHINIKIZO KUTOKA MAHALA FULANI NDIO LILILAZIMISHA RICHMONDULIAN WASHAMIRI JE WHO ARE THEY?

Wakati umefika sasa, watu wawe wanatajwa majina, hata kama walikuwa karibu karibu tu na mikataba ya utata kama huu.
Mtu kutajwa katika kuhusika na (kwa mfano - negotiations) za mkataba si lazima kuwa amekula rushwa, lakini angalau itakuwa ni kianzio kizuri cha watu kuanza kujua ni akina nani waliokuwa wanahusika na mkataba mzima; na humo humo wala rushwa wanaweza kutambulika kirahisi!
 
Dua,

Hii habari kidogo inatia moyo na sijui kama hao PPRA hawatazimwa kutokana na nguvu ya wahusika!
 
Home News
Tanesco mum on power cuts
DAILY NEWS Reporter
Daily News; Friday,January 19, 2007 @00:06

THE Tanzania Electric Supply Company (Tanesco), yesterday denied knowledge of intermittent power cuts that has affected Dar es Salaam for the past two weeks.

Public Relations Manager of Tanesco Daniel Mshana told the 'Daily News' that he was not aware of the problem and if any, it could have been a unique case.

"I am not aware of any power cuts. If any, it might be a local problem," Mr Mshana said.

The investigations conducted yesterday however, revealed that by yesterday alone, Dar es Salaam had experienced power cuts for more than five times.

It could not be established whether Tanesco had re-introduced power rationing, as was the case in previous days. Recently, Tanesco assured the nation that there would be no more power rationing for the next one year.

They said all six hydro plants in the country were generating 464MW beyond the national demand of 450MW.




Tuliambiwa hakutakuwa na mgao hadi 2008 kama mvua hazitanyesha – kulikoni?
 
Wandugu,
Nakumbuka kwenye forum hii kwa miezi kadhaa tulikuwa tukijadili kwa nguvu suala la madawa ya kulevya na kuhusika kwa vigogo na majina 100 aliyopelekewa rais. Wengine waliidunisha hoja kwa kuilaani kwamba ni juhudi za serikali katika kulitia maji suala la kashfa ya Richmond, na wengine wakatabiri kuwa mgao wa umeme ukiisha na suala hili litakwisha...KUNA UKWELI KATIKA HILI? na kama ndio hivi ni kweli hata JAMBOs tumeingia kwenye mtego huu wa kujadili suala kama upepo, tukitegemea propaganda za watawala za nini tuzungumze wakati gani? Naomba kutoa hoja.
 
Wabunge wataka Tanesco ichunguzwe

2007-01-20 10:27:28
Na Joseph Mwendapole


Baadhi ya wabunge wa CCM na wa upinzani wamesema kuna umuhimu wa kuchunguza mapato na matumizi ya TANESCO kutokana na hofu ya kuwepo ubadhirifu na ulaji rushwa unaolidhoofisha shirika hilo nyeti nchini.

Wabunge hao wametoa kauli hiyo kufuatia shirika hilo kuendelea kukubaliwa kila mara kupandisha umeme.

Hivi sasa shirika hilo limekubaliwa kupandisha nishati hiyo kwa asilimia 6.7.
Wabunge hao pia wamedhamiria kuibana serikali katika kikao kijacho cha bunge ili ishushe bei ya umeme.

Wakizungumza na Nipashe jana, Wabunge hao walisema wataibua hoja ili waelezwe sababu za kuiruhusu TANESCO kupandisha bei ya umeme kwa kiasi hicho.

Mbunge wa Jang�ombe (CCM), Bw. Mohamed Rajab, alisema amekerwa na hatua hiyo ya kupandisha gharama za umeme na kuahidi kuifikisha hoja hiyo Bungeni.

�Mimi binafsi juzi nilienda kununua umeme wa Sh. 20, 000, nikakatwa Sh. 8,000 za Ongezeko la Thamani (VAT) na Sh. 3,330 za gharama wanazoziita za huduma... sasa kwa mwananchi wa kawaida huo ni mzigo mkubwa sana,� alisema.

Mbunge wa Kinondoni (CCM), Bw. Idd Azan, alisema katika mikutano yake mingi na wananchi, amekuwa akipokea malalamiko ya kupanda kwa bei ya umeme.

�Nimefanya mikutano kama mitatu na wapiga kura wangu, kila sehemu malalamiko ni umeme, kwa hiyo lazima tuiulize serikali tatizo ni nini,� alisema Bw. Azan.

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Bi. Lucy Owenya, alisema serikali inapaswa kushusha gharama hizo ili ahadi yake ya kupeleka umeme vijijini kwa ajili ya kupunguza uharibifu wa mazingira itekelezeke.

Alisema bila kufanya hivyo, wananchi wa vijijini watashindwa kumudu gharama hizo, hivyo kuendelea kukata miti kwa ajili ya kupikia.

�Wakati Net Group Solution inaingia mwaka 2002, serikali iliahidi kuwa umeme utashuka, sasa badala yake unapanda, tutauliza kwa nini wanawatwisha mzigo walalahoi,� alisema.

Alihoji ziliko fedha ambazo kampuni hiyo ya kigeni ilikusanya, ambazo alisema Watanzania wengi walitarajia zingetumika kushusha bei ya umeme.

Mbunge wa Ziwani Pemba (CUF), Bw. Ali Said Salim, alisema kama gharama za uzalishaji umeme zimepanda, serikali ilipaswa kupandisha bei ya huduma ambazo si lazima kufidia gharama hizo.

Alisema umeme ni kitu cha lazima, hivyo kupandisha bei ni kuwakandamiza wananchi wa kipato cha chini kwa kuwa umeme ukipanda kila kitu kinapanda.

�Serikali imesema inataka maisha bora kwa kila Mtanzania, sasa haya ndiyo maisha bora? Maana tumeshazungumza sana kuhusu umeme lakini serikali ikiamua mara nyingi haibadili msimamo,� alisema Bw. Salim.

Mbunge wa Biharamulo (TLP), Bw. Phares Kabuye, alisema TANESCO haiwezi kuwa na sababu za msingi za kupandisha bei ya umeme kwa kuwa imekuwa ikikusanya fedha nyingi.

Alisema serikali inapaswa kutafuta kiini cha tatizo ndani ya shirika hilo nyeti kwa kuwa licha ya makusanyo kuwa makubwa matatizo yanaongezeka kila siku.
�Napendekeza shirika hili lichunguzwe mapato na matumizi yake, haiwezekani kila siku kukawa na matatizo wakati biashara wanafanya na fedha wanapata, kuna nini? � alihoji Bw. Kabuye.

Bw. Kabuye alisema inawezekana kuna rushwa na ubadhirifu wa fedha unaosababisha shirika hilo kushindwa kujiendesha.

Alisema inawezekana kuna njama baina ya wafanyakazi wa shirika hilo na wamiliki wa viwanda wanaolipa fedha kidogo tofauti na matumizi yao hivyo kulidhoofisha shirika.

�Wateja wapo na kila nyumba, baa, viwanda, umeme unatumika lakini shirika liko hoi kwa nini? Lazima tutafute suluhisho la kudumu,� alisema Bw. Kabuye.

Kamati ya Bunge ya Uwezeshaji na Biashara, jana ilipanga kuiweka �kitimoto� Menejimenti ya TANESCO, lakini haikufanya hivyo kutokana na nyaraka za shirika hilo kuchelewa kuwafikia Wabunge.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema Wabunge wameona ni vyema wasome nyaraka hizo kwa umakini katika kipindi cha wiki moja, kabla ya kukutana na menejimenti hiyo.

�Nyaraka tumezipata jana jioni (juzi) na unajua TANESCO ni shirika nyeti linalogusa maisha ya wengi, kwa hiyo tunataka tusome kwa umakini ndipo tukae nao,� alisema Dk. Mwakyembe.

SOURCE: Nipashe
 
Siku za nyuma hili suala nilishaliongelea..topic za madawa ya kulevya waliibua ili kuzima soo la mgao wa umeme na RICHMONDULI.na mikataba yenye utata ya madini.Watandanyika wakatupata na tukasahau mambo muhimu.
 
Walipewa muda wa Krismas watanue. Naona Krismas imekuja na kuisha, mwaka mpya umeanza, Januari inamalizika na wanaendelea kutanua. Ikija Februari wasanii watazua suala jipya ili wadanganyika waendelee kulala.
 
Back
Top Bottom