Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Mzee Bob,

Heshima yako mkuuu! Hilo neno ulilosema halikuwa lina -click kichwani mwangu isipokuwa ndiyo hasa tafsiri yake, labda sasa tuwalaumu wananchi na taifa kwa ujumla!
 
Nashukuru kuwa inaonekana sasa baadhi ya wanaJF mmeanza kuona ukweli kuwa pengine tumekuwa tukilaumu sana viongozi waovu waliowekwa na wananchi wajinga(Kama huyo dada wa Holland).Nafikiri ni wakati sasa umefika tuwaambie wananchi ukweli.Kwa maana ingine tuwaonyeshe na kuwaeleza namna wanavyochangia katika kuwepo kwa hali duni na mikataba mibovu.Tunapowalaumu viongozi pekee yake,watanzania wanajiona kama wao hawana hatia.Waache ujinga na wabadilike.Tuache kufanya hatima ya nchi yetu kama ushabiki wa mpira. Kuwa hata timu yako ikifungwa na kushushwa daraja we unaing'ang'ania tu.Kibaya ambacho wanaccm wanashindwa kugundua ni kuwa inapokuja kwenye hali ngumu haichagui cha CCM au wanaupinzani:Makali ya maisha yanakuwa sawa kwa wote.
 
Uchaguzi ni uchaguzi, na utawala ni habari nyingine, wakati wa uchaguzi tunagawanyika, lakini uchaguzi ukiiisha tunakuwa taifa na chama kilichoshinda ni lazima kitawale kwa visingizio vinavyokubalika kisheria au kidemokrasia, kwamba kina tekeleza sera za ahadi zao za uchaguzi wa wananchi,

kwa maneno yako hapo juu, tatizo linaonekana kuwa ni incompetence from all levels of members of society, yaani kuanzia wananchi, waliosoma na wasiosoma, na hasa viongozi wetu wa pande zote mbili, yaani CCM na upinzani,

Sasa who is to blame here? Jibu la haraka haraka linaweza kuwa we were not ready kwa uhuru, I refuse to believe kwenye hili jibu, ingawa ni very attracting as a jibu la haraka!

Au labda viongozi na wananchi wabongo hatuelewi elimu na maana yake, maana si tunasoma shule zile zile walizosoma watu wa Botswana, mbona matokeo kwetu hakuna ya hizo elimu?
 
sasa kuwaalumu wanapokwenda bungeni kutekeleza waliyotumwa na chama chao ambacho ni chama tawala kilichochaguliwa na wananchi waliozikubali sera zao, na wakati sheria ya Jamhuri inwaweka viongzi hao wawili yaani PM na Spika kwa ajili ya kukisaidia chama tawala kutekeleza ahadi zake kwa wananchi ambao ndio taifa lenyewe sidhani kama unakuwa fair kwa wananchi na taifa kwa ujumla!

ok, asante sana nimekupata ! kwa hiyo una maana ccm imewatuma hao waliochaguliwa kwenda kuwanyamazisha wabunge wengine huko bungeni ? if so, mbona wao ( ccm ) hawaku-lay out plan yao kama democrats walivyofanya marekani juu ya plan yao ya iraq ?? kama wangesema mapema kwamba wanaenda kuwanyamazisha midomo na kutumia nguvu zao za uongozi SIDHANI kama hata mmoja wao angewapigia kura hawa jamaa ! After all, mzee es umesema mambo muhimu sana hapa, nadhani kilichobaki ni kuwaelimisha wananchi wengi walio bongo wanaoshabikia tu ccm wakati wa kampeni, kempeni zikiisha wanaanza kumwaga vilio, kweli hili ndio suala muhimu la kufanya, na nadhani wana JF wataliunga mkono, naombeni tutafute njia mbadala ya kuwafikia wananchi walio bongo ili wapate elimu kabla ya uchaguzi 2010 ili tuone kama hii strategy itafanya kazi, ni matumaini yangu it will work ! congrats mzee es
 
Mzee Wangu Kada,

ahsante kwa heshima na ikurudie, mimi ninaafiki mawazo yako kuhusu ku-reach out kwa wananchi,

ingawa bado I am lost na na hawa the so called wananchi maana ni pamoja some educatin institutions kama Mlimani, kwani ninakumbuka na wao pia walikuwa mstari wa mbele katika kumpigia debe kiongozi mmoja wakati wa uchaguzi wa rais, sasa ninajiuliza swali what was their bases?

Lakini ninakubaliana na wewe kuwa tunahitaji kupanga mikakati ya ku-reach otu wananchi na some goood news!
 
nadhani wananchi walikipigia kura chama na sioi kuangalia policy za candidate, kitu ambacho kitatokea hapa marekani uchaguzi huu wa mwaka huu mwishoni ambapo kwa tabiri zangu nasema kwamba wananchi watapigia CHAMA kura na sio mgombea, chama chenyewe ni DEMOCRAT, hivyo basi yoyote atakayesimamishwa kupitia dem. ujue ndio rais ( samahani kutoka nje kidogo ya topic )!!!!!!!!!!!
 
Tanzania: Power Cuts Still Order of the Day

Arusha Times (Arusha)
February 24, 2007
Posted to the web February 26, 2007
Edward Selasini And Innocent Kisanga
Arusha

Drought or no drought Arusha is still facing frequent power cuts and in fact parts of the Central Business Area have been in total darkness for about two weeks.

Since February 10 until we went to press on Wednesday the whole of the Central Market Place and Pangani area, Azimio street, and CCM headquarters had no power because of a blown out transformer. Apparently TANESCO could not replace the transformer as it had no spare one in store neither could it buy one immediately from ABB Tanelec. TANESCO could not also pay for the transformer up-front and surprisingly, with all it might as a government parastatal, it is also not credit worthy.

Residents and people running businesses in the affected areas could not understand why TANESCO was not in a position to immediately replace a blown out transformer that is manufactured and is in stock in Arusha. "We have been pleading to TANESCO daily to solve the problem. Their technicians kept telling us that they owe ABB Tanelec a lot of money and they cannot loan them any more. Should we really suffer because of that?" queried an angry businessman along Azimio road who preferred anonymity.

He added, "What has that to do with us? We are paying our bills and I don't understand why should we be punished for 12 consecutive days!" Dr. Peter Mhando who runs a private hospital known as KAM MEDICS and Laboratory Services in Pangani area said his services were paralyzed because he has some equipment that cannot be run by a generator.

He said he had to refer some of his patients to the Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) in Moshi for some services which could no longer be offered because of prolonged black out. It is hectic now to my patients, they have to drive long distances to be attended."

The black out did not also spare the ruling party (CCM) Regional Headquarters which houses many offices and business premises including a local radio statio, Radio 5, which since February 10 has been off air.

As meat vendors at the Central Market Place suffered a devastating blow due to the Rift Valley Fever outbreak, those selling fish and chicken equally suffered because of lack of power to preserve the products. "Now we cannot stock large amount of fish. We order small quantities that we can sell the same day. That is not good business, said Hawa Ali at the Central Market Place.

TANESCO 's Regional Manager, Engineer Martin Kalokola told The Arusha Times on Tuesday that he was aware of the problem but he had no spare transformer to replace the dysfunctional one. He said he was in the process of acquiring one and it was expected to be installed on February 21.

"Tomorrow a new transformer will be in place and that means an end to the problem," he said. But to the Arusha residents and businesses the transformer failure is just part of an ongoing power problem. The town, despite the end of power rationing last December, still experiences unexplained frequent and prolonged power cuts, almost daily.

The central business area is the most affected area and a myriad of generators are humming daily emitting noxious smoke outside shops. Along Boma Road, for example, where the offices of the Arusha Times are located, there at least three power cuts daily sometimes lasting four hours.

TANESCO's regional manager declined comment on the frequent power outages saying that he was traveling to Dar es Salaam on February 21 to meet with top authorities of the company. He said he would be in a position to explain the cause of the problem when he returns to Arusha.
 
Dowans kama IPTL tofauti bei ya umeme

Na Midraji Ibrahim

SERIKALI imesema mkataba kati yake na Kampuni ya kufua umeme ya Messre Dowans Holdings SA hauna tofauti na ule wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), isipokuwa katika bei ya umeme.

Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wabunge wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara, waliotembelea eneo inapojengwa mitambo ya kufua umeme wa dharura ya kampuni ya Dowans.

Dowans inauzia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), uniti moja ya umeme kwa senti 4.99 za dola ya Marekani, wakati IPTL inauza uniti moja kwa zaidi ya senti 11 za dola za Marekani.

Kulingana na habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho, Karamagi alitoa kauli hiyo, wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kuhusiana na gharama watakazoingia walipa kodi kuilipa kampuni hiyo.

Kutokana na kauli hiyo, gharama kubwa ambazo mzigo kwa wananchi zitaendelea kubebwa hadi ukomo wa mkataba huo utakapofika ambao kama kipengele hicho hakikuguswa na marekebisho yaliyofanyika utamalizika baada ya miaka miwili.

Kulingana na mkataba wa IPTL, serikali inatakiwa kulipa Sh3.5 bilioni kama 'capacity charge' na Sh4.5 bilioni za kununua umeme, ikiwa mitambo hiyo inazalisha uniti zote 100.

Kampuni hiyo ambayo ilinunua mkataba wa Kampuni ya Richmond Development iliyoshindwa kuzalisha megawati 100 za umeme, ilikuwa ianze uzalishaji wa megawati 80 na kuingiza kwenye gridi ya taifa ifikapo Machi 5, mwaka huu lakini ilishindikana na kupewa muda zaidi hadi Machi 15.

Hata hivyo, Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara, ilipotembelea kampuni hiyo juzi, ilielezwa kuwa megawati hiyo zilikuwa zikitarajiwa kuingizwa kwenye gridi ya taifa Aprili 15, lakini itategemea kuwasili kwa swichi kutoka Marekani.

"Kulingana na maelezo yao, hata hiyo Aprili haiwezekani kwa sababu wanasema swichi hiyo ni nzito ambayo inatakiwa kusafirishwa kwa meli. Ndio maana waliomba hadi Juni," kilieleza chanzo chetu kutoka ndani ya kamati.

Tanesco imerekebisha mkataba huo ambao Dowans iliurithi kutoka Richmond, na sasa itatakiwa kuingiza megawati 80 zilizosalia kwenye gridi ya taifa ifikapo Mei mwaka huu. Tayari, megawati 20 kati ya 105 zinazotakiwa kuzalishwa na kampuni hiyo zimeingizwa gridi ya taifa.

Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa Tanesco, Kabiruddin Abdulla, alisema bado wanategemea megawati 80 kutoka Dowans, lakini hawajui ni lini zitazalishwa na kuingizwa gridi ya taifa.

Wakati uongozi wa kampuni hiyo ukieleza hivyo, Waziri Karamagi, aliwaambia wabunge kuwa uzalishaji wa megawati 64.5 unatarajiwa kuanza Aprili, huku uzalishaji wa megawati 20.5 ukitarajiwa Juni mwaka huu.

Katika mkakati wa kurekebisha sekta ya umeme, Karamagi alisema bei za umeme zitarekebishwa kwa kuzingatia na kutambua umuhimu wa gharama ambazo zinakidhi gharama za uzalishaji wa Tanesco ambazo ni pamoja na kununua umeme kutoka makampuni yanayofua umeme.

Karamagi alisema, deni la IPTL litanunuliwa ifikapo Julai na mitambo ya kampuni hiyo itakuwa inatumia gesi ifikapo Januari 2009.

"Sh1.5 trilioni kugharimia mpango wa uwekezaji wa Tanesco, Ifikapo Aprili shirika litakuwa limepatiwa mkopo wa Sh300 bilioni na kuongeza ufadhili wa Songas ifikapo Septemba mwaka huu," alisema.
 
Hivi serikali itaendelea kuwaongezea muda hawa matapeli mpaka lini?Kuna sababu gani za msingi zinaozuia kutumia mapungufu ya deadline kupita bila ya kuzalisha umeme kuwatimua na hasa ukizingatia Mkataba huu tayari ulikuwa ni ghali na hasara kwa Taifa?Hivi ni kipi kinachowafanya iendelee kuwabebisiti hawa Richmond A.k.a Dowans?
 
Mie nina wasiwasi hata hizo 20MW kama zitakuwa zimeingizwa kwenye gridi.
 
Mie nina wasiwasi hata hizo 20MW kama zitakuwa zimeingizwa kwenye gridi.
Kama kweli hii serikali ya awamu ya nne imekusudia kuipitia mikataba yote yenye mapungufu na kuitia Taifa Hasara na Huu Mkataba nao ulikuwa bomu sasa tumepata nafasi kwa hawa wahuni kutofikia deadline ,Kinachonishangaza kila deadline ikifika baada ya kufuata mkataba ulisema nini na kuwatimua na kuokoa Hasara kwa manufa ya taifa wanawaongezea muda ili waendelea kutupatia hasara?What's going on?Huyu Karamagi anajaribu kutueleza nini?
 
Sisi CCM hatuwezi kuwasikiliza nyie wadanganyika .Kama mnataka kupitia mikataba ina manaa mtaleta balaa Tanzania . Hawa wawekezaji wanatuwezesha sis CCM kupata hela za kampeni na kuongoza Nchi kwa amani.Tutaendelea kuheshimu mikataba hii hata hakuna wataalam wa mikataba Tanzania kama alivyosema Mwenyekiti ndugu JK , lakini ndiyo inatusababisha tunapeta.

Zimbabwe Oyee

Mnao hoji mikataba yetu na watu wetu Go Hang
 
Swali ni kwa nini tunawalipa Dowans kwa huduma ambazo hawajatoa? Kwa usemi mwingine ni kwamba tunawalipa Richmonduli, kwa sababu hawa waliuza mkataba wao kwa Dowans. Kwa usemi mwingine ni kwamba we are paying for services we are not receiving! Au kuna mtu anayeweza kunielimisha?
 
Swali ni kwa nini tunawalipa Dowans kwa huduma ambazo hawajatoa? Kwa usemi mwingine ni kwamba tunawalipa Richmonduli, kwa sababu hawa waliuza mkataba wao kwa Dowans. Kwa usemi mwingine ni kwamba we are paying for services we are not receiving! Au kuna mtu anayeweza kunielimisha?
Hiki ndiyo kinachonishangaza mimi na kwanini tusitumie nafasi iliyojitokeza mara kadhaa kwa kushindwa kwao kutimiza ahadi na kuwamaliza ki mkataba?Kuna kitu kinaendelea hapa ambacho mimi na wewe hatukijui Bali tunaweza tukahisi tu!
 
Jibu lenu ni kwamba wasanii wote 2 JK na EL they hold much of the companies money hawawezi kuacha kula pesa za wajinga sisi Wadanganyika ama mnasemaje ?
 
Benki ya Dunia yataka bei ya umeme ipande

na Mobini Sarya

BENKI ya Dunia imewataka Watanzania kuelewa kuwa bila kupandisha bei ya ankara ya umeme, shirika linalojishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa nishati hiyo, Tanesco, litakufa.
Benki hiyo imebainisha kuwa Tanesco inalazimika kuongeza bei ya umeme ili kuweza kumudu ongezeko la gharama za uzalishaji wa nishati hiyo muhimu kwa uchumi na maendeleo ya nchi.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es salaam jana na mtaalamu wa Nishati kutoka Benki ya Dunia, Ralph Karhammar, katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwamo viongozi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, kujadili namna ya kuboresha sekta ya nishati nchini.Akitoa mada katika mkutano huo, Karhammar alisema kuwa pamoja na kuwa uamuzi wa kupandisha gharama za umeme ni hatua chungu kwa wateja wadogo wadogo, lakini Tanesco haina njia ya mkato.

Alisema kwa kiasi kikubwa, utendaji wa Tanesco unaendana bega kwa bega na ongezeko la gharama za uzalishaji wa nishati hiyo. Alisema kupanda kwa gharama za uzalishaji na usambazaji umeme kunatokana na kupanda kwa gharama ya vitu vingine kama vile ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia. Alisema bei ya umeme ni kiashiria cha hali ya uchumi kama ilivyo kwa bei ya bidhaa nyingine, hivyo kulilia bei ya umeme ipungue wakati bei nyingine zipo juu, ni kulionea shirika hilo.

"Hauwezi ukasema bei ya umeme ipungue wakati uchumi uko chini, lazima kwanza (uchumi) ukue na kipato cha wananchi kiongezeke, ndipo unaweza kufikiria gharama hizo, kwa sasa gharama za umeme zinategemeana na hali ya kupanda vitu kama mitambo ya kuzalishia umeme," alisema.

Akitoa mfano, alisema kuwa iwapo Tanesco itapanga kununua mtambo wa kuzalisha umeme kwa mkopo, ni lazima wawe na mahesabu yanayoonyesha jinsi watakavyolilipa deni hilo. Aliongeza kuwa haiwezakani kwa Tanesco kununua mitambo, vipuri na mafuta kwa bei ya juu na kisha kuzalisha umeme ambao itauuza kwa bei ya chini.

Kwa upande mwingine, mtaalamu huyo aliishauri serikali kutafuta njia zitakazoisaidia kujiondoa haraka katika mikataba ya nishati yenye gharama kubwa kama ile ya IPTL.
"Serikali inaweza kununua mitambo ile na kuimiliki," alishauri. Alipoulizwa na gazeti hili kwa nini Benki ya Dunia haitoi ufadhili kwa Tanesco ili kupunguza gharama za uzalishaji, Kamishna wa Madini Msaidizi, Ngosi Mwihava, alisema kuwa benki hiyo ina tabia ya kukopesha katika miradi ambayo inalipwa haraka.

Hata hivyo, alisema kuwa benki hiyo imeipa masharti serikali kuhakikisha kuwa ankara za umeme zinaendana na gharama za uzalishaji. "Wao hawapendi kuona gharama zikipungua kwa mtumiaji, wanachotaka ambacho tunakifanyia kazi ni kuhakikisha kuwa kama tumezalisha umeme kwa shilingi mia, basi mtumiaji atalipia kiasi hicho pamoja na faida kidogo ili shirika liweze kulipa madeni na kuendelea, vinginevyo litakufa… wanasema na ni kweli kuwa hauwezi kuzalisha umeme kwa shilingi mia halafu ukauza kwa shilingi 90," alisema Mwihava.

Mwihava alisema kuwa mazungumzo ya jana yalikuwa ni sehemu ya mjadala mpana wa kuitaka Benki ya Dunia kufadhili miradi mitatu. Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Tanzania Energy Access Programme pamoja na mradi wa kuboresha miundombinu ili kuhakikisha umeme unawafikia watumiaji vijijini. Kuhusu mradi wa kuboresha miundombinu, mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia alisema kuwa unatarajiwa kuanza mwezi Agosti na utagharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 100, ukiwa na lengo la kufikisha umeme vijijini na kupunguza tatizo la kukatikakatika kwa umeme

nb; hivi hawa watatukamua mpaka lini,huku tunakokwenda sio kuzuri hata kidogo.
 
JK ana wakati mgumu basi maana maneno yake ya Jukwaani kama hawezi kuyaweka katika vitendo basi itakuwa kazi nzito lakini he can walk away na kuwa watu wake wa ku spin, akina Es, DrWho, Kulikoni wako kazini kuhalalisha lolote .
 
JK!
Ataota Mvi na Nywele kunyonyoka kwani aliwakumbatia kwa kuwatembelea na kumpa sifa ,Sasa hawa wanapokusifia matokeo yake ndiyo hayo watakuburuza kila sehemu,Tusubiri mengi yatajiri! Hawajui Hawa alifikiri wanampenda kumuita a Good Guy!
 
Wazee,

Nafikiri kuwa serikali haiwalipi Dowans kwa umeme ambao hawajaanza kuuzalisha, labda hizi MW20 walizoingiza kwenye gridi ya taifa. Kama kuna mwenye data za uhakika aweke hapa, yaani kiasi gani cha pesa kimeshalipwa hadi sasa, n.k.
 
Back
Top Bottom