Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Gembe safi, tupe mambo, wengine ofisi zetu haturuhusiwi kuwa na radio hila kupitia JF twapata mambo huku kazi zaendelea. Chunguza kuhusu huyo waziri aliyekataa ni nani?
 
[SIZE="7"]MIMI NADHANI JK NAYE YUMO HATA KAMA SWAHIBA WAKE KAJIHUDHULU.KWA NINI JANA ALIKUWA ANALIFANYA ILI JAMBO KAMA ILIMEANZISHWA NA CCM WAKATI NI WAPINZANI.[/SIZE]
 
Japo niko mbali na radio na tv lakini JF ni kila kitu, hisia zangu zanituma kuwa huyo mtu atakua chenge tu huyo!
 
HAPA TUME YA KAZI GANE TANA JAMANI
Bado kuna tabia ya kuogopana ila najua Muungwana Jumatatu anawa fire out wale wote ambao Tume imewapendekeza. Kimsingi BWana Pinda hajaunda Tume ila amesema anahitaji watu kutoka sehemu mbalimbali ili kushughulikia suala hili ila JK atachukua maamuzi ya kulisaidia taifa ambayo yanaweza tangazwa baada ya Busha kuondoka.
 
Kifupi ni kuwa ROSTAM atatakiwa kuja kujieleza kwenye bunge lijalo kutokana na matamshi yake juu ya kamati huo ndio ulikuwa uamuzi wa spika .

Bunge lijalo ni mwezi wa nne kuanzia tarehe 8.

Bunge tayari limeahirishwa hadi muda huo.
 
Gembe
Asante kwa persona devotional yako ya kutuletea vitu live kutoka jumbani hapo DODOMA. Masikio yako wazi kwa kila kinachojiri hapo
 
Chenge, kwakuwa yeye alianza tangu mwanzo alionyesha kuipinga ripoti kabla hata haijasomwa!
 
teh teh..kwanini Chenge na asiwe Dr. Batilda Buriani?

Batilda analia kilio cha Mbwa gofather wake kamwagwa. Maana mamvi ndiye alieyekuwa mtawala wake. Huyu bado si mwizi maana ana roho mbaya sana hata kwa house girls. Nadhani hawa ni akina Chenge .
 
Chenge ndiye ana maslahi ya moja kwa moja na mikataba hiyo yote, kwani yeye ndiye aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali hivyo kimsingi ndiye aliyekuwa mshauri mkuu wa serikali kwa mikataba yote hiyo. Ikifunguliwa hawezi kupona kama ilivyo kwa akina RA,EL na wengineo. Buriani hana maslahi yoyote kukataa, zaidi ya hasara kwake kisiasa.
 
Hapo ni watu wawili tu, Dr Maltida Buriani na Chenge, sidhani kama kuna mwingine
 
Kifupi ni kuwa ROSTAM atatakiwa kuja kujieleza kwenye bunge lijalo kutokana na matamshi yake juu ya kamati huo ndio ulikuwa uamuzi wa spika .

Bunge lijalo ni mwezi wa nne kuanzia tarehe 8.

Bunge tayari limeahirishwa hadi muda huo.

Nadhani itakuwa mara ya kwanza kusimama Bungeni kama sikosei, sababu mara zote huwa anawasilisha maswali tu kwa njia ya Maandishi. Lets wait and see...! Mpaka tufike huko kila kitu kitakuwa kimeshapangwa! Kwanini asimuandikie barua haraka ndani ya siku mbili kutoa maelezo yake.?

Nadhani kuna maneno aliyasema Mwanakijiji, Kambi ya Lowassa ilikuwa inajipanga kuja kumtetea Bungeni, hii inaweza kuwa ndio wakati umefika na si mabli zaidi ya 8th April 2008. Ndio utakuwa Mwisho wa Mtandao.

Ila tujiulize swali, Itakuwa vipi kama Rostam akiamua Kujiuzuru ubunge??
 
Hapo ni watu wawili tu, Dr Maltida Buriani na Chenge,sidhani kama kuna mwingine



Burian amewahi kuwa wizara ya sheria ? Au is there any connection? If I may ask maana naonekana kupitwa na nyeti hii hapa. Tafadhali saidia
 
Mambo hayoo

Jina Richmond lazua balaa Dar

na Lucy Ngowi

KASHFA ya Richmond iliyosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, wiki iliyopita, na hatimaye kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri, imeanza kuzua balaa katika viunga vya Jiji la Dar es Salaam.
Balaa hilo limeanza kuwakumba wamiliki wa majengo mawili tofauti ya Richmond Hill na Richmond Tower ambao sasa wanalazimika kuanza kazi ya kung’oa vibao vilivyoandikwa Richmond kwenye majengo yao hayo baada ya kuwapo kwa tishio la wazi dhidi ya biashara yao.

Tanzania Daima jana ilishuhudia mafundi wakimalizia kung’oa maandishi yanayong’ara yaliyoandikwa Richmond Hill katika moja ya majengo hayo mawili, lililopo Mtaa wa Chake Chake, Masaki, Dar es Salaam.

Walipofika waandishi wa Tanzania Daima katika eneo hilo, mafundi hao waliacha kuendelea na kazi ya kumalizia kung’oa maandishi mengine yaliyokuwa kwenye jengo la pili ambalo nalo lilikuwa na maandishi hayo hayo.

Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi wa Kampuni ya OMIMS Ltd inayomiliki majengo hayo pacha ya Richmond Hill, Sultan Mitha, alisema walilazimika kuyang’oa maandishi hayo baada ya kubaini kwamba yamekuwa yakiwaletea matatizo yanayoathiri biashara tangu Kamati ya Teule ya Bunge iwasilishe ripoti yake bungeni wiki iliyopita.

Akitoa mfano, Mitha alisema siku tatu zilizopita, mmoja wa wateja wao ambaye ni Mzungu alikabiliana na usumbufu wa kutupiwa mawe na wananchi wakati akiwa katika gari lililoandikwa Richmond.

“Tumeamua kufuta kwa sababu watu wanapiga mawe magari yetu wakati hawajui kuwa, hakuna uhusiano wowote kati ya Kampuni ya Richmond yenye kashfa na hii ya kwetu. Hili ni jina tu la kibiashara tunalitumia.

“Tumeamua kufuta maandishi haya kwenye majengo yetu na magari ya wateja wetu, kwa sababu watu wanayapiga mawe,” alisema mkurugenzi huyo.

Katika kuonyesha tofauti kati ya kampuni yao na ile ya Richmond Development Ltd, ndugu wa Mitha aliyejitambulisha kwa jina la Jaffary Mohammed, alisema wao hawawafahamu kabisa wakurugenzi wa kampuni hiyo yenye kashfa.

“Kwa kweli tunasikitika kwa kuwa hatuna uhusiano wowote wa kibiashara, ila tunasoma tu kwenye vyombo vya habari,” alisema Mohammed.

Alisema ujenzi wa majengo hayo ambayo ni makazi ya watu, ambayo hadi sasa zinaishi jumla ya familia 86, ulianza mwaka 2000 na ukakamilika mwaka 2004.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, jengo la Richmond Tower lililopo Mtaa wa Mindu, lina familia 62 wakati lile la Richmond Hill la Masaki lina familia 24.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio zimeeleza kwamba, miongoni mwa watu wanaoishi katika majengo yanayomilikiwa na kampuni hiyo, ni watoto wa waliokuwa mawaziri wawili katika Baraza la Mawaziri lililovunjwa wiki iliyopita ambao hawakuteuliwa katika serikali iliyotangazwa majuzi.
 
Sidhani kama anaweza kujiuzulu, there is where he get the influence he has, the immune he enjoyes, so there is where he those strong ties he has, naamini hata weza kujiuzulu.
 
Burian amewahi kuwa wizara ya sheria ? Au is there any connection? If I may ask maana naonekana kupitwa na nyeti hii hapa .Tafadhali saidia

There is a bit connection between Batilda Burian and the former Edward Lowassa, Mie namuamini Halisi na Mzee Mwanakijiji kwa Speculation, wanaweza kutupa
 
This is a direct copy from Wikipedia about Almeda University. Tulichojifunza kutokana na ripoti ya Mwakyembe ni kuwa serikali yetu ilipumbaa katika kufanya utafiti wa kutosha kujua uwepo na uhalali wa kampuni ya Richmond, wabia wake wa kibiashara na haikushtuka hata pale kampuni hii ilipokosa credit. Sasa tunajua kuwa kama serikali haitafiti, basi sisi wenyewe tuwe watafiti.

Simfahamu wala sina ubaya wowote na Mh. Mustafa Mkulo, waziri wetu mpya wa fedha. Lakini baada ya kuangalia wasifu wake ulioonyesha ana shahada ya pili ya uongozi wa biashara (MBA) kutoka Almeda University, nilipatwa na shauku nijue zaidi kuhusu hicho chuo. Cha kushangaza ni kuwa hiki chuo hakiko accredited huko Marekani na kimewekwa kwenye kundi moja na vyuo vyenye kutoa shahada zisizo za kweli (diploma mill).

One may call me a paranoid person but I think many will agree with me that it's only fair to question the credentials of a person leading our treasury and advising our president on fiscal matters after seeing what Richmond/RDC/RDEVCO did to our country.

Ikiwa huyu mtu aweza kufoji vyeti ktk level ya MBA hivi kumkabidhi fuko letu la fedha ni sawa na kuuza nchi... another Balali in making...
 
Back
Top Bottom