Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Mmesikia Tanesco wako mbioni kuongeza bei ya umeme kutokana na gharama za uendeshaji kuongezeka!! Hivi kwanini watu wanafikiri Watanzania ni wajinga sana!!... Mr. President livunje hili shirika and spare us the misery please!!

MJJ.
Tatizo si TANESCO. Tatizo ni wanasiasa kuingilia TANESCO kwa maslahi yao binafsi. Hawapi TANESCO nafasi ya kujiendesha. Watafanya maamuzi mabaya ya kujinufaisha wao, (RICHMOND, IPTL, SONGAS, NETGROUP) na mzigo wa kupandisha kodi ili kufidia uozo watapewa TANESCO ili waonekane wabaya kwa jamii.
 
Chief, lakini ni wanasiasa ndo walioiunda Tanesco na ndio walioifanya iwe ilivyo! Ni vigumu wanasiasa kujiondoa moja kwa moja kwani wanawajibika kuja na sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi. Mapendekezo ni yaleyale:

a. Tanesco ivunjwe na iwe kampuni tatu tofauti ya uzalishaji umeme (ambayo itakusanya umeme toka kwa wazalishaji wengine Songas, IPTL, n.k), Kampuni ya Usambazaji, na kampani ua Uuzaji.

b. Sheria iliruhusu watu binafsi na mashirika binafsi kuweza kufanya mambo hayo matatu pia na hivyo kuleta ushindani wa kibiashara.
 
JK USE YOUR PRESIDENTIAL POWER NOW

Habari Tanzania

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Richmond Development iliyoahidi kuingiza megawati 20 za umeme katika gridi ya Taifa mwishoni mwa wiki iliyopita, imeshindwa kufanya hivyo na sasa imeendelea kukaa kimya.

Ahadi za kampuni hiyo kwa mara ya tatu zimeshindwa kutimia, baada ya Desemba 2 uongozi wa kampuni hiyo kuahidi kuwasha mitambo kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita lakini ahadi hiyo haikutimia.

Meneja Mkazi wa Kampuni ya Richmond, Naeem Gire, alikaririwa na gazeti hili Jumamosi Desemba 9, mwaka huu akisema kuwa walikuwa wanafanya jaribio la mwisho kabla ya kuruhusu umeme kuingia katika gridi ya taifa.

"Tunatarajia leo tutafanya majaribio ya mwisho ya kiufundi kwa kuiwasha mitambo hii, baada ya hapo ndio tunaweza kuiwasha moja kwa moja endapo haitaonyesha hitilafu ya kiufundi," alisema Gire.

Hata hivyo, vyanzo vya habari ndani ya kampuni vimesema kuwa hadi jana mitambo hiyo ilikuwa haijawaka na mafundi wa kampuni ya hiyo walikuwa wanaendelea kutoa jasho kuhakikisha umeme huo unaunganishwa katika giridi, lakini hadi jana jioni, walikuwa bado hawajafanikiwa.

Chanzo cha habari kilicho karibu kampuni hiyo kilisema jana kuwa huenda umeme huo ukapatikana baada ya saa 72 kuanzia jana jioni, hii ikiwa na maana kuwa huenda ukapatikana kuanzia kesho Jumanne.

Kama kawaida, eneo la mitambo hiyo jana lilikuwa na ulinzi mkali na watendaji wa kampuni hiyo hawakupatikana wala kujibu simu ili kuelezea hatua waliyofikia na kueleza ni lini hasa umeme wao utapatikana na kuingizwa katika gridi ya taifa.

Umeme huo wa Richmond unaosubiriwa kwa muda mrefu ni sehemu ya kwanza ya kiwango kinachotakiwa kuzalishwa na kampuni hiyo, kabla ya kuleta mitambo mingine ya kuzalisha awamu ya pili ya mewagawati 80 ili kutimiza kiwango cha megawati 100 zilizokubaliwa katika mkataba wake na serikali.

Hii ni mara ya tatu, umeme wa Richmond kushindwa kuingia katika gridi ya taifa kama ilivyoahidiwa baada ya mara ya kwanza kuahidiwa na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Dk Ibrahim Msabaha kuwa ungeingia Oktoba 20, na baadaye Waziri wa sasa, Nazir Karamagi kuwa umeme huo ungepatikana kabla ya Desemba.

Kuzidi kuchelewa kwa kampuni ya Richmond kuingiza umeme katika gridi ya taifa, kunazidi kukaza kitanzi cha karamagi ambaye aliahidi kuwa megawati zote 100 za Richmond, zitakuwa zimeingizwa katika gridi ya taifa kabla ya Januari mwakani.

Waziri Karamagi alitoa ahadi hiyo Novemba 23, mwaka huu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo aliahidi kuwa mgawo wa umeme ungekwisha kabla ya Januari mwakani.

Karamagi, Waziri mwenye dhamana na masuala ya umeme, alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa sekta hiyo, ilikuwa katika jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa tatizo hilo, ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi kwa zaidi ya miezi sita sasa, linamalizika kabla ya Januari.

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa waziri anayeshughulika na masuala ya umeme kutoa ahadi kama hiyo. Mtangulizi wa Karamagi, Dk Ibrahim Msabaha, pia aliwahi kutoa ahadi kama hiyo, akisema makali yangepungua mwishoni mwa Oktoba lakini hali haikuwa hivyo.

Badala yake, makali ya umeme yakazidi kuongezeka na ingawa haikuwekwa wazi, inaelezwa kuwa ni moja ya sababu zilizomfanya Rais Kikwete amhamishie katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Akizungumza kwa kujiamini siku hiyo, Waziri Karamagi alisema jitihada mbalimbali za dharura zinafanywa kwa lengo la kumaliza mgao wa umeme uliopo sasa.

Alisema jitihada hizo ni pamoja na kuhakikisha kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Richmond, yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100, inafungwa haraka ili hadi kufika mwezi huu, iwe imeanza kuzalisha umeme kikamilifu.

Alisema kazi ya kufunga awamu ya kwanza ya mitambo ya kampuni hiyo, yenye uwezo wa kuzalisha megawati 20 ambayo iliwasili mwezi uliopita kutoka Marekani, inakaribia kukamilika akisema mafundi wamefikia asilimia 80 ya ufungaji wake, hali inayotia matumaini kuwa megawati hizo 20 zingeanza kuzalishwa mapema mwezi huu.

Alisema awamu ya pili ya mitambo ya kampuni hiyo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 80 ipo katika maandalizi ya mwisho kuletwa nchini wakati wowote kuanzia sasa, ili iweze kufungwa na kufanya jumla ya megawati zitakazozalishwa na kampuni hiyo kuwa 100.

Hata hivyo, wasiwasi uliopo ni kwamba huenda ufungaji wa mitambo ya awamu ya pili usikamilike katika kipindi anachokitaja Waziri Karamagi, hasa ikizingatiwa kuwa mitambo yenyewe bado haijawasili nchini.

Wasiwasi huo unatokana na ukweli kwamba mtambo wa kwanza wa Richmond uliwasili nchini Oktoba 21, 2006 na jana, Desemba 10, bado kazi ya kufunga na kufanya majaribio, ilikuwa bado ikiendelea. Watu wengi wanahoji kuwa iwapo mtambo wa megawati 20 unachukua zaidi ya mwezi mmoja kufungwa na kuanza kazi, ni wazi kuwa kazi itakuwa ngumu zaidi kwa mtambo wa kuzalisha megawati 80.

Mchanganuo unaonyesha kwamba ili mgawo wa umeme uishe ni lazima Richmond wakamilishe kujenga mitambo yote kabla ya Desemba 31, mwaka huu.

Alisema lengo la mgao ni kupunguza matumizi ya maji katika maeneo ya kuzalisha umeme ambako kina kimepungua na kwamba utaratibu huo utawezesha maji kidogo yaliyopo yaendelee kuendesha mitambo hiyo hadi Desemba wakati mitambo ya dharura ya kuzalisha umeme itakapoanza kufanya kazi

JK use your power now to strip this dubious contract.
 
does he have any balls left in him? He couldn't fire Msabaha, He couldn't fire Ditopile... halafu unategemea kweli aingilie kati mkataba huu? Atakuambia wanaogopa kesi mahakamani (kama yale ya IPTL) ila kama angekuwa na kaubavu kokote na kujitambua kuwa yeye Rais wa Tanzania basi mkataba huu usingechukua muda wote huu!

Kabla hajavunja mkataba huu, hana budi kubadilishwa washauri wake na wasaidizi wa karibu kwani kwa namna fulani wanatumikia matumbo yao!
 
Mwanakijiji,

Una mantiki, lakini hawa jamaa ambao unawaita wasaidizi wake nadhani wana walakini mwingi. Aidha nina wasiwasi na wale wanaompa taarifa za masuala husika ambayo ni ya kitaifa na si kichama.

Inasikitisha pale ninapoona maamuzi ambayo RAIS anaweza kuyachukua kunusuru taifa yako wazi na bayana lakini yanachukua muda mrefu au hata hayashughulikiwi na mengine yanashughulikiwa bila kuangalia athari zake kwa taifa letu (Mfano kuingiza Rwanda & Burundi EAF kabla ya kupata maoni ya wananchi yaliyokuwa kwenye mchakato).

Nahisi kuna watu walio karibu na mheshimiwa ambao huingia hapa, somo kwao ni kuwa wananchi tumechoka na ushauri usio na manufaa wampao rais. Si kosa la JK, ninyi mnaomshauri mna makosa makubwa ambayo madhara yake ni makubwa.

Nasikitika kila nikiandika naandika lawama, sipendi hivi ila ukweli nalazimika kwani ninachoona ni kuwa watu wanasifu utekelezaji wa majukumu tena mengine madogo tu na kusahau kukumbushia yale makubwa. Hii imekaa vibaya, haijatulia kabisaa.

Chonde chonde wenye njaa zenu na wapenda sifa za kuonekana kuwa karibu na Mhe. Rais, linusuru taifa letu. Si lenu tu; ni letu sote. Kumbukeni, siku za kuishi ni chache na sote tuna hukumu inatusubiri huko mbeleni... Angalieni vizazi vyetu vijavyo vitaathirika namna gani tokana na ushauri au utendaji wenu mbovu au wa walakini ambao mnaona wananchi wengi wanaupigia makelele.

Ushauri: Fikiria mara mbilimbili, mikataba inayopigiwa kelele na watanzania, matabaka makuu ya kipato yaliyojengeka miongoni mwa watanzania, tuhuma mbalimbali zinazotolewa na uchunguzi unaochukuliwa pamoja na matunda ya uchunguzi wenyewe...

Ndio, kuna mazuri mnafanya lakini sisi si wajibu wetu kusifu kwani ndio maana mpo na sio sisi. Tekelezeni wajibu wa kumkosoa Rais si lazima azunguke mwenyewe kila sehemu. Lakini kama anapenda kwenda mwenyewe na si kuwatumia ninyi... Ana la kujibu pale atakapoenda mrama!
 
Kama si kesho basi sio mbali mtasikia richmond wamejitoa. Na watafanya hivyo baada ya wao kufanikiwa kuuwasha umeme. Hicho ni kitendawili na itabidi mkitegue.

Suleimani
 
Haya mimi sitakuwa mtabiri ila hivi ndivyo mambo yatakavyokuwa:

a. RDC watauwasha huo mtambo na kuingiza umeme kwenye gridi ya Taifa na wote watapiga makofi na kuseme "si tuliawaambia hawa wamo!" Na JK na wapambe wake watakokea na kupiga picha eneo la tukio na kupeana mikono huku mioyoni mwao wamewainulia watanzania kidole katikati! Nyuso zao zitakuwa zimejaa tabasamu.

b. Watanzania wasahaulifu wataanza kuimba nyimbo za "Kikwete Mkombozi" na "Lowassa Kiongozi Mahiri, jasiri na hodari" Wataimba kama ule wimbo wa "Makali Hodari, kaenda safari!"

c. Baada ya wiki chache majenereta yatazimika tena, itakapoulizwa sababu mtapewa sababu kama vile "Tunahitaji majenereta yenye nguvu zaidi kwani hatukutarajia mahitaji makubwa ya umeme kama haya hivyo mitambo yetu imeshindwa kuhimili kazi"

d. Watu watakasirika na kukata tamaa. Serikali itawataka watulie kwani mipango imefanyika ili kuingiza majenereta mapya toka Uchina na Japani!

e. Watanzania wasahaulifu watapiga makofi na vigelelegele na kuimba "Kikwete mkombozi"...

and the circle continue hadi pale ifikapo 2009!! hapo ndipo serikali kupitia CCM wataandika Ilani Mpya ya Uchaguzi na jambo moja wakataloahidi kulishughulikia kwenye kipindi kijacho ni tatizo la Nishati!!
 
Mwkj,
Yaani watawainulia Watanzania kile kidole cha katikati?
 
Mambo yameanza. Someni habari hii kutoka gazeti la Mwananchi la leo.

Richmond yarusha bomu Tanesco

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Richmond Development Corporation (RDC) imelibebesha Shirika la Umeme (Tanesco) lawama kwamba ndiyo kikwazo cha wao kuanza kuzalisha umeme kama ilivyopanga kutokana na kupewa gesi chafu.

Kauli ya Richmond imo kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotoa jana jioni, ikiwa ni siku ya tano sasa kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza ahadi yake ya kuzalisha umeme wa megawati 20 na kuunganisha kwenye gridi ya taifa tangu Ijumaa iliyopita.

Katika taarifa hiyo, Makamu wa Rais wa Fedha na Utawala wa kampuni hiyo, Zahoor Gire, amenukuliwa akisema kwamba ingawa wamefanikiwa kufunga mitambo yao tayari kwa kuzalisha umeme, juhudi zao zimekwamishwa na Tanesco ambao wanawapa gesi yenye mchanga.

“Wakati wa majaribio ya kawaida ya wahandisi wa Richmond Development Corporation waligundua kwamba gesi waliyopewa na Tanesco haikufikia viwango vya mtambo,” inasema sehemu ya taarifa hiyo ya ukurasa mmoja.

Gire alisema kwamba kuwasha jenereta kwa kutumia gesi yenye mchanga iliyotolewa na Tanesco, inaweza kuharibu mitambo na hivyo kuleta hasara ya muda na fedha kwa serikali.

Pia alisema RDC imechukua tahadhari zote kuhakikisha kwamba kunakuwa na usalama na upatikanaji wa umeme wa dharura wa uhakika kutatua tatizo la umeme nchini, “lakini sasa mafanikio ya juhudi zetu yanategemea Tanesco kutupa gesi safi.”

Kutokana na hali hiyo, taarifa hiyo ilisema kwamba Richmond sasa inasubiri ratiba kutoka Tanesco itakayoainisha vipi na lini gesi safi na ya kutosha itapatikana.

Gire amenukuliwa katika taarifa hiyo akisema kwamba mara baada ya wahandisi wake kugundua hitilafu hiyo katika gesi, waliwataarifu rasmi Tanesco, hasa wakisukumwa na uelewa wao kwamba umeme wa dharura unahitajika sana kwa sasa.

Akizungumzia malalamiko ya Richmond, Meneja Uhusiano wa Tanesco, Daniel Mshana, alithibitisha kuyapata na kwamba waliwajibu jana.

Mshana alisema kwamba Richmond walielezwa tangu mapema kwamba wanatakiwa kufunga kifaa cha kuchuja gesi hiyo kama walivyofanya wenzao wa Aggreko kama mkataba baina yao unavyoelekeza.

“Kulingana na mkataba Richmond wanapaswa wa-provide filters za kuchuja hiyo gesi, hili si jukumu la Tanesco,” alisema Mshana.

Alisisitiza kwamba mwenye jukumu la kutoa gesi kwa Richmond si Tanesco bali ni Songas. Songas ni kampuni inayosafirisha gesi kwa bomba kutoka Songosongo hadi jijini Dar es Salaam na pia kufua umeme wa gesi katika mitambo yake iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, taarifa za ndani ambazo Mwananchi inazo zinaeleza kwamba mkataba wa Tanesco na Richmond umetoa jukumu la kutoa gesi kwa Tanesco na si kwa Songas.

Malalamiko haya ya Richmond yanafungua ukurasa mpya wa rekodi yake ya utekelezaji wa mkataba baina yake na Tanesco ambao ulisainiwa Juni 23, mwaka huu ukiipa (Richmond) jukumu la kuzalisha umeme wa megawati 100.

Baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, iliwachukua Richmond hadi Oktoba 29, mwaka huu kuwasilisha nchini mitambo yake ya awali ya kuzalisha megawati 20 za awali.

Kulingana na mkataba huo, kazi nzima ya usafirishaji, ufungaji hadi kuwasha mitambo inatakiwa ikamilike katika kipindi cha siku 150, ikiwa imekamilisha uzalishaji wa megawati 100.

Richmond awali ilisema kwamba ilikuwa inatafuta ndege kubwa za kukodi kusafirisha mitambo yake ambayo ilidai ilikuwa ikihitaji ndege kubwa sana za mizigo ambazo hazipatikani kirahisi.

Mitambo hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Marekani ambako kampuni hiyo ina makao yake makuu. Kampuni hiyo imeandikishwa Houston, katika Jimbo la Texas nchini Marekani.

Hadi sasa wananchi wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuona mitambo ya Richmond ikiwashwa ili walau kupunguza makali ya mgao mkali wa umeme ambao sasa unafanyika hata saa za usiku.

Hali ya kukosekana kwa umeme wa uhakika ilianza kujitokeza mapema mwaka huu na mgawo wa kwanza kutangazwa Februari mwaka huu.

Mabwawa ya maji ya Kidatu, Kihansi na Mtera, yamo katika hali mbaya kutokana na kukosa maji baada ya mvua kutokunyesha. Uzalishaji wa umeme wa nguvu za maji umepungua baada ya kufungwa kwa mabwawa na mengine kuzalisha chini ya kiwango chake.

Richmond kama walivyo Aggreko, walipata zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kutumia gesi lakini hadi sasa ni Aggreko tu ambayo imeweza kutekeleza jukumu lake.
ends

Source: Mwananchi Online Edition 11 December 2006
 
daymn... it is happening fast than I thought... Jasusi yes.. si unajua pale unapojua kuwa mbele ya picha lazima uoneshe tabasamu lakini moyoni umejaa dharau?...
 
Hivi makampuni mangapi ya Dar yanatumia gesi ya umeme toka Songas na sijawahi kusikia hili la "gesi yenye mchanga?".. halafu gesi ikiwa na mchanga hiyo gesi tena?!! Kwanini wasiseme kuwa tatizo ni mitambo yao haiwezi kutumia "gesi yenye mchanga" wakati makampuni kama Wazo Hill wanatumia?...

Mr. President this is it, toa Agizo la Rais (Executive Order) kuwa RDC imekatazwa kuendelea kufunga mitambo, wanatakiwa waondoe vitu vyao na wakinuna waende mahakama ya Kimataifa ya Biashara!!
 
Kulaleki!

Yaani hapo ndio nimechoka kabisa, what the hell is going on? jamaa wameshindwa kuheshimu mkataba na sasa wanaturushia mpira tena, why not kick them out! yaani nchi yetu ndio imekuwa kichwa cha mwendawazimu?
 
Mwanakijiji umezidi kulalamika na wewe. Gas hiyo chafu ina mchanga RDC ni kampuni ya kimataifa, inataka gas safi na sio gas chafu kama hiyo ya SONGAS. Toka lini magenerator yakapewa gas chafu?? Hiyo ni hatari sana na imebidi RDC kukodisha zile ndege kubwa kuja kurescue mitambo yao isije ikaharibika. Maengineer wamesema hii ni crisis kubwa sana kwani kuwapa gas chafu haina solution, lazima generator ziondoke.

RDC imetoa mfano, hata magari lazima yapewa petrol safi, laa sivyo yatarudishwa Japan au Germany!! ahahahahaahha

Yaani hawa RDC kwa kweli hawana hata aibu. Kwenye magari jamani si kuna Gas filter au air filter ambazo zinaondoa uchafu?? Mbona hizo ni parts ambazo ndio the cheapest kwenye mitambo?? Yaani huyu GIRE anadhani Watanzania ni wapumbavu kiasi gani??

Sasa cha ajabu Aggreko, Songas wanamitambo na wanatumia gas hiyo hiyo, kwa hiyo RDC ni kampuni bogus?? I guess ameprove mwenyewe.

Sisi huku uswazi mbona hata chai tunaweka chujio voola majani yote yanakamatwa na kichujio chai inakuwa powa.

Kuna problem kubwa mno imegundulika, RDC wanataka visingizio sasa.
 
Hii ndio bongo bwana. Nchi changa na ya majaribio ya aina zote. All sorts of experiments seem to work pretty well in this bongoland.
 
Habari inasema...
"...Akizungumzia malalamiko ya Richmond, Meneja Uhusiano wa Tanesco, Daniel Mshana, alithibitisha kuyapata na kwamba waliwajibu jana.

Mshana alisema kwamba Richmond walielezwa tangu mapema kwamba wanatakiwa kufunga kifaa cha kuchuja gesi hiyo kama walivyofanya wenzao wa Aggreko kama mkataba baina yao unavyoelekeza.

“Kulingana na mkataba Richmond wanapaswa wa-provide filters za kuchuja hiyo gesi, hili si jukumu la Tanesco,” alisema Mshana.

Alisisitiza kwamba mwenye jukumu la kutoa gesi kwa Richmond si Tanesco bali ni Songas. Songas ni kampuni inayosafirisha gesi kwa bomba kutoka Songosongo hadi jijini Dar es Salaam na pia kufua umeme wa gesi katika mitambo yake iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, taarifa za ndani ambazo Mwananchi inazo zinaeleza kwamba mkataba wa Tanesco na Richmond umetoa jukumu la kutoa gesi kwa Tanesco na si kwa Songas.

Sasa hapa ndiyo habari ianze!
 
Richmond wanaanza kucheza loopholes za mkataba, msije shangaa kuwa at the end of the day Tanesco ndio wataoneka kuwa ndio wamechelewesha kupatikana kwa umeme!
 
Nisikilizeni kesho, nina ujumbe mzito kwa Watanzania wenzangu na kwa Mhe. Rais.. huu ukimya unaudhi!!
 
Kichekesho ;richmond Wanasema Wanashindwa Kuzalisha Umeme Kwa Sababu Gesi Wanayopewa Na Tanesco Ni Chafu...lakini Agreco Na Songas Wanatumia Gesi Hiyo Hiyo,,wanatafuta Sababu Tu...wafukuzwe Na Walipishwe Fidia...ricmond Is Blaming Tanesco For A Polluted Gas>
 
Back
Top Bottom