Waziri Masha aikana Richmond
na Sitta Tumma, Mwanza
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
JINAMIZI la kashfa ya Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, lililowang'oa vigogo kadhaa serikalini, limeanza kuwafuata mawaziri mikoani.
Waziri aliyekumbwa na jinamizi hilo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, ambaye jana alilazimika kukana hadharani kuifahamu Richmond.
Hali hiyo ilitokana na waziri huyo kubanwa mbavu na mwananchi mmoja akitaka aeleze kuhusu chimbuko la Richmond, kwani wakati sakata hilo linatokea alikuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Waziri Masha ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana, alitakiwa kuwaeleza kinagaubaga kuhusiana na suala hilo, kwani ni moja ya vitu vilivyosababisha kuwepo kwa mfumko wa bei nchini.
Matukio hayo yalitokea wakata waziri huyo alipokaribisha maswali, kero na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika Kata ya Isamilo, jijini Mwanza, ikiwa ni hitimisho la ziara yake hiyo.
Katika mkutano huo, mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Edward Mboje, alimtaka Waziri Masha kuwaeleza bayana Watanzania kuhusu tuhuma hizo, kwa kuwa inadaiwa anaifahamu Kampuni hiyo ya Richmond.
Mboje pia alimtaka waziri huyo afafanue hilo, kwani wakati sakata hilo linaibuka alikuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa nafasi aliyonayo sasa.
"Mheshimiwa waziri, kumekuwepo na tuhuma mbalimbali kuhusu sakata la Kampuni ya Richmond. Tunaomba utueleze hapa leo, kampuni hii unaifahamje, kwani wakati sakata hili likiibuka ulikuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini.
"Kwa kiasi fulani tunaamini Richmond unaitambua vizuri na huenda inakugusa……na kwa hii kampuni asilimia kubwa imechangia kuibuka kwa mfumuko wa bei, tunaomba utueleze hili leo hapa," alisema Mboje huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Akijibu maswali hayo, Waziri Masha alieleza kutoitambua wala hahusiki na tuhuma zozote dhidi ya Kampuni ya Richmond.
"Ndugu zangu, mimi sihusiki na lolote, wala huyu Richmond simfahamu kabisa ndugu zanguni…..kwani hata kamati teule ya Bunge iliyoibua sakata hili haikuniita kunihoji wala kuniuliza.
"Kamati hiyo ingelikuwa inafahamu kwamba na mimi ni mhusika au ninaifahamu hii kampuni wangenihoji, lakini kwa vile sihusiki sikuulizwa wala kuhojiwa, kwa hilo jamani mimi sihusiki kwa namna yoyote na huyu Richmond," alijitetea Masha.
Kuhusu mfumko wa bei unaoonekana kukithiri siku hadi siku hapa nchini, alisema suala hilo si la hapa nchini pekee, bali ni la nchi nyingi na kwamba mfumko huo hausababishwi na Kampuni ya Richmond.
Akifafanua zaidi alisema bei ya mafuta kwa ujumla imepanda duniani kote na kwamba Tanzania haizalishi mafuta na kwa kutambua hili, tayari serikali imekwisha kuweka mikakati maalumu ya kupunguza mfumko huo.
"Jamani hata Marekani na Uingereza wanalia na mfumko wa bei kama tunavyolia sisi hapa…..kwa hiyo tuvumilianeni kwani serikali inaangalia uwezekano wa kupunguza hali hiyo kama si kuitokomeza kabisa," alisema waziri huyo wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alijiuzulu wadhifa huo Februari 7, mwaka huu baada ya kuhusishwa katika vitendo vya ufisadi na Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza suala hilo. Kamati hiyo ilikuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.
Mbali na Lowassa kujiuzulu wadhifa huo, mawaziri wengine wawili waliojiuzulu kutokana na kutajwa katika kashfa hiyo ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, alipozungumzia suala hilo kwa mara ya kwanza mbele ya wapiga kura wake, alidai kuponzwa na uaminifu wake dhidi ya watendaji waliokuwa chini yake wakati wa ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kupitia Kampuni ya Richmond.
Alidai hahusiki kwa namna yoyote kwenye kashfa hiyo na akawasukumia tuhuma hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, Wizara ya Nishati na Madini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao kwa pamoja walihusika na mchakato mzima wa kuipata Kampuni ya Richmond.
Wakati Lowassa akijitetea hivyo, Karamagi naye alikanusha kuhusika katika sakata hilo, huku Dk. Msabaha akidai kutolewa kafara.
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 21 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
hivi huyu masha anafikiri watu hawamfahamu,huyu si ndio yule alieshikwa mkono na lowassa kuingia siasani,sasa km alishikwa mkono na lowasa kuingia pale na akawa naibu waziri wa nishati unafikiri huyo lowasa angemwambia afanye juu chini ili hawa richmond wapate dili lile,na lowasa kasema ya kua kajiuzulu kwa ajili ya walio chini yake mmoja wao ni huyu masha,ingawa hakutajwa na lowasa nae anajua kila kitu kuhusu richmond kitu kingine cha kipuuzi anachosema masha nikwamba hata uingereza na marekani wanalia mfumuko wa bei,mwananchi wa mwanza anahusika vipi na mfumuko wa bei wa uingereza na marekani,hayatuhusu ya wamarekani na uingereza tunaongela yetu,au yeye masha ni waziri huko uk,usa, majibu ya kupuuzi kabisa anatoa, kwa hiyo mbona uingereza na marekani wakifanya jambo zuri hamuwaambii wananchi nasi tanzania tutafanya jambo hili sababu uingereza na marekani wanafanya kwa wananchi wao,kwa vyovyote vile masha hawezi kusema haijui richmond na alipokua pale lazima lowasa angemtumia tu, masha na magai si ndio walikua wanasheria binafsi wa lowasa,sasa leo atatosa vipi haijui richmond wakati mteja wake ndio muhusika,masha tunakujua kuliko unavyojijua bora utulie.
na mstari wa mbele, calif/usa, - 17.03.08 @ 09:11 | #2539
Ni vizuri sasa kwamba wananchi wenyewe wameanza kuelewa na kuwataka viongozi wao wajieleze mbele yao.
Kuna ukweli ndani ya mawazo ya wananchi hawa. Masha anaweza akahusika, kama sio moja kwa moja basi ni kupitia IMMMA. Yeye hana ujanja, asubiri kunyolewa. Bahati mbaya hata EPA yupo maana IMMMA mndio waasisi wa Deep Green!
Pole ndugu yangu Masha, umeingia kwenye siasa wakati mbaya, na um,eingilia kwenye tundu bovu.
na Amk, Dar, - 17.03.08 @ 09:16 | #2540
MASHA ACHA KURUKA KIUNZI RICHMOND UNAIFAHAMU VIZURI SEMA WEWE KWA SABABU HAUKUITWA NA KAMATI TEULE UNAPATA SABABU YA KUIRUKA. HAYA TUYAACHE TUPE MAELEZO KUHUSU EPA NALO HAULIFAHAMU AU NDIO LUGHA ZETU MAMBO YANAPOKUWA HADHARANI KILA KITU HAMKIFAHAMU.
na MKATAMBUGA - 17.03.08 @ 09:21 | #2543
Mimi nadhani sisi wananchi wa Dsm tumuombe JK atuitie uwanja wa taifa, viongozi/bangusilo + resignees wafuatao tuwahoji wenyewe kwa ujumla wao ili asitokee mtu wa kuruka kutokujua / kuhusika na uvundo huu/ule.
1. Lowasa
2. Karamagi
3. Msabaha
4. Mwanyika
5. Chenge
6. IMMMA Advocates + Masha
7. Mwenyekiti wa Board ya Tanesco
8. Government Negotiation Team
9. Hosea
10.Watu wa manunuzi wa Tanesco
Wenye wasaidizi kama Mwanyika, aje na hao lawyers aliowatuma kushiriki, Lowasa naye aje na hao wanasheria waliomkataza kuuvunja mkataba (asisingizie kwa maneno matupu tu)
8.
na bubu - 17.03.08 @ 09:59 | #2551
Waziri Masha awe mkweli haiwezekani akiwa naibu waziri asijue habari za Richmond hata kidogo.Ni tatizo la kutamani madarka na kusahau KISOGO chako.
na silvester - 17.03.08 @ 10:27 | #2554
Haya kumekucha, na jua halizami mpaka kieleweke. Maandiko matakatifu yanatueleza kuwa Joshua alisimamisha jua mpaka kikaeleweka. Watanzania watasimamisha jua mpaka kieleweke.
Nafikiri inapokuja suala la Watanzania kupata elimu,viongozi wetu hawataki kabisa kusikia jinamizi hili maana wanajua haya ndo matokeo yake. Mambo ya ndio mzee yanaisha. Ripoti ya REDET inko wazi, viongozi wameungwa mkono na watu ama wenye 'elimu' ndogo au wasiokuwa na 'elimu' kabisa.
Nirudi kwenye hoja. Tanzania ni ya ajabu mwanangu. Rostam, hausiki, Kadamange, hausiki, Msabaha, kafara, Mwanyika, ni safi sana, (hausiki)Hosea, alifuata aadili nasheria (hausiki), mwingine anatuambia ni umonduli tu ila yeye hausiki, Kikwete hausi.. ooh sori huko najitoa, simo!! Inahitaji PhD ya 'uhusika' ili mtu kuelewa haya viongozi wetu wanayotuambia. Kama kila kiongozi hausiki, Richmondu ilipewa tenda na nani? Je ni Ndimala na mwenzake waliomwagiwa tindikali? Au Mbowe? Nadhani ni Mtikila. Je viongozi waliopo chini ya waziri mkuu sio pamoja na naibu waziri. Masha kama kweli ulukuwa hujui lolote, hapo wizarani ulikuwa unafanya nini? Si heri ungekuwa unalala nyumbani tu? Na huu uwaziri umepataja mtu usiyejua chochote? Haiingii akilini. Masha maswali ni mengi kuliko majibu. Na hayo mambo ya kujifananisha na Marekani acha kabisa, maana umefika huko unajua kukoje na tofauti ya athari za mfumuko wa bei kati ya USA na TZ unazijua.
na kukuz, singapore, - 17.03.08 @ 10:28 | #2555
kwa ujumla Serikali ya CCM imetuchosha jambo la maana hawa jamaa ni kukaa kushoto na kupisha watawala wapya wasio na konekisheni za ujinga kama huu.Mfano Masha na Ngereja wanaonekana kana kwamba ni watu wapya lakini wameletwa pale na Lowassa pamoja na Rostam Aziz kwa maana nyingine tunatawaliwa na viongozi walewale wenye sura tofauti.Masha anapo ongelea mfumko wa bei mbona Kenya wao si mkubwa kama wetu?kwani Kenya wanazalisha mafuta?ni siasa mbovu za Kikwete na Serikali yake aliyekuja na mbwembwe nyingi za maisha bora kwa kila Mtanzania,mabadiliko halisi huwa ni kuweka chama kipya madarakani si kuweka mtu mwingine wa chama kilekile.
na Kamule, Mwanza,Tanzania, - 17.03.08 @ 10:47 | #2565
Watanzania tumeyasikia mengi na tumeyaona mengi sasa tunataka hatua zichukuliwe, tena zichukuliwe na sisi wenyewe.
Makampuni mengi kati ya hayo yaliyochukua pesa za EPA yanonekana kuwa na mkono wa CCM, ukiondoa Deep Green ambayo hiyo moja kwa moja ni ya CCM. Ufisadi wote unaofanyika nchini unawagusa viongozi na wanachama wa CCM maana wao ndio wako serikalini. Hawana mtu mwingine wa kumtupia lawama!! Sasa hatua zianzie hapo.
Tunataka CCM na serikali yake watwambie wao wako wapi katika yote haya. Kwa mfano tukija kuthibitisha kwamba kweli Deep Green ni ya CCM na kwa hiyo hela yetu ilienda kwenye uchaguzi (Mahindra, n.k.) sisi Watanzania tuwape adhabu gani? Nafikiri ufumbuzi ni mmoja tu: MHESHIMIWA RAIS AKUBALI KWAMBA YEYE NA CHAMA CHAKE WAMEWASALITI WATANZANIA, WATUOMBE MSAMAHA NA AVUNJE SERIKALI YAKE NA KUITISHA UCHAGUZI MPYA UTAKAOSIMAMIWA NA UMOJA WA MATAIFA.
Hili ndio suluhisho pekee litakaloiondoa Tanzania mikononi mwa mafisadi waliokubuhu. Ikiwezekana viongozi wote wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa hizi waorodheshwe na kupigwa marufuku kugombea nafasi yoyote katika jamii. Hili litakuwa fundisho kwa mafisadi watarajiwa.
Taifa hili halitakuwa huru kama hatua kali kama hizi hazichukuliwi, tena haraka iwezekanavyo.
Lengo sio vita dhidi ya chama wala serikali, bali ni vita dhidi ya mafisadi bila kujali mlengo wala mwelekeo wao.
SHIME WATANZANIA, AMKA KUMEKUCHA!!!
na Kam, Dar, - 17.03.08 @ 11:49 | #2570
Masha anajua kila kitu kuhusiana na Richmond,tena ni bora kama atakaa kimya kwasababu watanzania wa leo sio wajinga.
na G KABONDE, ARUSHA,TANZANIA, - 17.03.08 @ 12:02 | #2572
Nasema ipo siku,tena inakuja kwa kasi ya ajabu!!2mechoshwa na "usanii"!!yuko wapi yule Mungu wa kisasi na hasira?Yule Mungu wa agano la kale?tunamhitaji aje tena kwa watanzania,aje haraja mungu wa gadhabu,aliyewatupilia mbali wamisri ndani ya bahari ya shamu,Mungu wa hasira aliyempa Musa adhabu ya kutoiona nchi ya ahadi japo alikuwa nabii wake,Mungu wa visasi nahasira,aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa misri kwa kiburi cha Farao dhidi ya waisraeli!mungu aliyeshusha moto kwa sodoma na gomora,aliyeshsha ghalika kwa watu waliokosa kumtii NUHU,AJE HARAKA KTK MIOYO YA WATANZANIA,MUNGU WA JINO KWA JINO!!HATUMTAKI MUNGU WA AGANO JIPYA,ANAYEHIMIZA KUJITOA MHANGA NA KUTESEKA KWA AJILI YA WENGINE,MUNGU GANI ANAYEHIMIZA KUWA AKUPIGAYE SHAVU LA KUSHOTO MGEUZIE NA KULIA?ETI AKUOMBAYE KUMSINDKIZA KM3 WE MSNDIKIZE KM6!AKUIBIAYE KANZU WE MPE NA JOHO??ATUTKI KUENDELEA NA MUNGU HUYU,ANAYETUHIMIZA TUWASAMEHE WEZI WA RICHMOND NA EPA!WAMEIBA FEDHA ZETU WANATAKA NA HAKI YETU PIA,WAMEIPA KWA NJIA YA RICHMOND NA IMMA WANATAKA TUWASAMEHE,HATUMTAKI MUNGU ANAYETETEA "MALAYA"WA KISIASA WASIPIGWE MAWE!!HATUTAKI KAULI ZA ASIYE NA DHAMBI NA AWE WA KWANZA KUWATUPIA MAWE "MALAYA" HAWA WA KISIASA!!TUNATAKA TUWATUPIE MAWE,SABABU SISI SI MAKAHABA WA MALI ZA UMMA!!!HATUJAJILIMBIKIZIA FEDHA ZA BOT KWA NJIA YA EPA KTK KIMVULI CHA "IMMA"!TUNAMTAKA MUNGU WA SHARI TUAMSHE MAPAMBANO!!KTK KUDAI HAKI TUCHAGUE "FUJO" BADALA YA WOGA!!!TUMWAMBIE MASHA "STOP" KWA UWONGO NA WIZI WAKO KWA NJIA YA "IMMA","IMMA" ILIYOIBA FEDHA BOT NA SASA IMETOA MAWAZIRI(Masha)NA JUGDE!!"IMMA" INAYOTUNZA WATOTO WA MARAIS WA BARA NA VISIWANI!!WAKATI SASA UNAKUJA!!
na Mdanganyika, TZ, - 17.03.08 @ 12:08 | #2575
iko siku
na mi - 17.03.08 @ 13:03 | #2589
Mnakumbuka toka mikataba ilipoanza kusainiwa wananchi na vyomba vya habari vilipiga sana kelele kuwa mikataba ni mibovu???
kama sikosei kelele hizo zina umri wa miaka kama kumi hivi
mnakumbuka waliitetea sana na kuamini kuya yameisha na watz watasahau???
nani alifikiri kuwa kuna siku LOWASSA... LOWASSA na kundile wangeondoka kwaaibu kubwa hivi (hata kwa watotot wadogo mifano yawizi imebatizwa kwa jina la LOWASA)
kwakuwa serikali yetu huwa haitumii akili watajidai kufunika hizi ishu zote
labda baada ya miaka kadhaa wawe wamekufa maana kuvio vya watu wanaeteseka MUNGU huwa havipuuzii
kweli IKO SIKU
na mi - 17.03.08 @ 13:09 | #2590
Napenda viongozi vijana lakini hawa: yaani Masha na Kihiyo Nchimbi hawana sifa za kuwa mawaziri. Tayari wanachemsha na bado watachemsha zaidi. Mheshimiwa rais wetu JK acha habari za mahusiano binafsi, angalia uwezo wa watu. Jana nchimbi anadai bilioni moja, Hapa masha analialia kwa kulinganisha TZ na developed countries, alidhani akitaja nchi hizo watu watazubaa; Upuuzi mtupu. These are uncomparable items and will so remain.
na ngaka - 17.03.08 @ 13:21 | #2593
Hongera kwa wa Tanzania wenzangu kwa kuanza kuwa na mwamko wa kukemea maovu.
na JM - 17.03.08 @ 13:24 | #2596
Big up wa TZ kama kweli mmegundua serikali iliyopo madarakani hawana machungu na raia wao wachovu kupindukia!! 2010 tuwapige chini.NB: Mabilioni yaloibwa yarudi .
na Joachim, Tanzania, - 17.03.08 @ 14:05 | #2601
Big up wa TZ kama kweli mmegundua serikali iliyopo madarakani hawana machungu na raia wao wachovu kupindukia!! 2010 tuwapige chini.NB: Mabilioni yaloibwa yarudi .
na Joachim, Tanzania, - 17.03.08 @ 14:05 | #2602
Masha huyu asijaribu hata kidogo kuwahadaa watanzania. Tunayajua mengi sana kuhusu yeye na kampuni ya IMMMA. Asidhani hatujui kuwa yeye ndiye alishirikiana na hawa wezi wanaojiita wawekezaji kupora rasilimali yetu ya madini kwa kuwasaidia kuingia mikataba isiyo na kichwa wala miguu. Huku akijua ya kwamba alipaswa kuweka mbele utaifa lakini yeye aliuzika kwa uroho wa dola za waporaji wa madini yetu.Na hizo fedha alizojilimbikizia kutoka katika madini yetu ndio zilimsaidia kushinda kura za maoni kwa kutoa rushwa kwa wapiga kura wa CCM. Na aliyekuwa mbunge wa mwanza kipindi hicho marehemu Steven Kazi alipolalamikia rushwa na ukiukwaji mwingine wa taratibu za uchaguzi huo wa kura za maoni, baba yake wa kambo Lowasa na mafisadi wengine walihakikisha kuwa haki haitendeki hadi akapitishwa kugombea ubunge wa Nyamagana.Kwahiyo Masha ni zao la ufisadi kwani hata madaraka aliyonayo ni kutokanana na utiifu wake kwa mafisadi wakongwe. Nadhani nayeye yuko mbioni kuhitimu kozi ya ufisadi ndio maaana anajifanya mbuni!!!
Kwaujumla tunayo mengi kuhusu ubovu wa Masha na jinsi asivyostahili kuwa kiongozi lakini kwa leo yatosha ila asiendelee kutuinmbia ngonjera zake za kifisadi tena, bora atulie tuliiii!!!
na Peter Pierre, tz, - 17.03.08 @ 14:09 | #2604
Watu wanapita ila dola na vyombo vyake vinabaki palepale daima. Ipo siku CMM na vikaragosi vyake havitakumbukwa milele. Hata Hitler ilifika siku akasahaulika. Uzuri wa mtu ni pale hujampa pesa na madaraka. Ukilogwa kumpa hivyo vitu viwili tayari umemloga. Nani angejuwa kuwa tabasamu ya Kikwete kumbe ni unafki mtupu kwa wananchi. Mimi binafsi simchote kidole mtu yeyote serikalini isipokuwa JK. Chanzo cha yote haya ni JK. Yeye ndiye mtuhumiwa Na.1 wa Richmond na Epa. Kama siyo, yeye kama msimamizi ya nchi na kama kweli yuko safi anawezaje kuyanyamanzia haya yote. Milion 152 Tsh kwa siku, fedha za EPA na kashfa zingine ambazo zimefichwa kama kweli anajali nchi hii na wananchi kwa nini anafumbia macho haya yote? ANAHUSIKA. yeye aondoe sheria ya kinga ya ma Raisi kama kweli ni mwanaume. Utaona watu watajitokeza kuwashitaki wote na ndipo ukweli utajulikana. Kweli inauma kuona sisi Watanzania tulio wengi tunateseka kwa sababu ya watu wachache. Eti viongozi. Hamfai kabisa kuongoza nchi hii. Mtu mmoja alinambia kuwa JK alishindwa kuongoza siku ile alipoapichwa kuongoza nchi. "Kejeliiii"
Eti Masha mwanasheria. Wa chuo kikuu gani wanafundisha uongo na kuuhalalisha eti kwa sababu ya kadhamana ya uaziri. Utakwisha siku moja na utabaki Masha ule wa IMMA na Deep Green. Hadhi ya yako na ujana wako umeupaka matope eti kwa kuwafumbia macho wahalifu. Ulimchinda nini Mrema aliyeona uozo na kuondoka. Sema unacho kijua. Lazima una lakusema ila umefumbwa mdomo. Eti mwanasheria.
na Kanakanini, Arusha, - 17.03.08 @ 14:22 | #2610
NILIWAHI KUONA MANENO KWENYE PICK UP MOJA IMEANDIKWA KWA NYUMA 'KANZU MPYA SHEHE YULEYULE' NDIO YALIYOJITOKEZA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI JIPYA KINA MASHA WASIOJUA CHOCHOTE KINACHOENDELEA KWENYE WIZARA ZAO, AKINA KAPUYA, AKINA CHENGE NA MABEST WA MKUU AKINA NCHIMBI ILIMRADI WAWEMO KWENYE BARAZA PANGA PANGUA,LINADHIBITISHA BARAZA JIPYA NI KIINIMACHO.HUYU MASHA KAMA NI FISADI ALIKUWA KOZI NA HILI LISINGEGUNDULIKA ANGEKUJA KUWA MWL KAMA WENZIE KWA HIYO MAFISADI KWENYE BARAZA JIPYA WAMO JAPO WANATUDANGANYA WATANZANIA UKIVAA NGUO MPYA BASI NA WEWE NI MPYA.
na mishi daud - 17.03.08 @ 15:18 | #2623
Madaraka ya kupeana kirafiki yana mwisho wake na hauko mbali. Huyu Masha anafikiri akitaja uingereza na marekani atazuzua wananchi. Ujinga mkubwa huu. Wasiwasi wangu wasije wakaanza kumfuatafuata huyo mwananchi na kuanza kumtisha kama ezi za akina lowasa waliowatisha walimu wa mtoto hukohuko mwanza eti kwa sababu alihoji kuhusu kupeana nafasi zaidi ya moja. Lahana hizo za kujiona miungu watu ndo zimewaweka kijiweni leo. Sasa huyu masha siku zake zinahesabika naye na mbaya zaidi ni pale atakapothubutu kumtisha huyo mwananchi baada ya kumkoroga kwenye moyo kiasi cha kujichanganya nakutoa majibu ya kijinga.
na mlilia juani, Mwanza, - 17.03.08 @ 15:22 | #2624
Hii nchi tunakokwenda tutakamatana mashati. Anayeweza kuokoa hilo lisitokee ni JK tu. Tujifunze kutoka Kenya, hawakujua, kama walijua walipuuza, kama watakamatana siku moja. JK historia itakutaja kama mtu wa namna gani...??
na Timo, Mwanza, - 17.03.08 @ 15:24 | #2625