Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

JK hawezi kua na nyimbo juu ya Richmond na yeye ni walewale tu, kusema kwamba TANESCO wangeingia gharama kwa kuvunja mkataba na R'sio kweli kwa sababu kama R'ni kampuni feki basi tulikua na kila sababu ya kuvunja mkataba huo kwa kipengele cha udanganyifu,Kwamba wenzetu wamekua sio waaminifu juu ya utaalamu wao. Point hii pekee ilikua ni kigezo kikubwa sana cha kuvunja mkataba.
 
Mkuu FEMS,
Nadhani sasa kwa upande wangu umeeleweka. Kwamba kwa mujibu wa habari uliyosoma huamini kama JK alidanganywa kwani alikuwa anaelewa in and out ya kile kinachoendelea Richmond. Kwa hiyo alipokuja na kauli hii"
He said the government negotiating team had been looking for cheap power generation at a reasonable price and considerable conditions. There is only one company which offered that, he said.
He added that Richmond was the only company that accepted to sell power to Tanesco at 4.6 cents. The power committee was convinced by the terms
.

alikuwa kwa makusudi ameamua
kutudanganya Watanzania.

Nia yangu ilikuwa nikutaka kujua uko wapi kati ya pande mbili ya kudanya na kutokuwa na hatia. Lakini kwa maelezo uliyotoa ni wazi kuwa unakubali kuwa JK ni fisadi na aliamua kuja kuwadanganya Watanzania ili kutimiza azma yake ya Wizi kupitia Richmond.
 
IPO SIKU MSHUA ATADANGANYWA KWAMBA YEYE SI RAIS ATAKUBALI.....Aliwahi kuuliza mzee butiku siku moja...kama waziri wetu wa fedha kadanganywa kwa swala la EPA na bado hataki kuwajibika ipo siku atadanganywa na kuitoa hazina yote ya nchi.....
 
Nasikia wanasema JK ni very clever man sasa inakuwaje ?
 
IPO SIKU MSHUA ATADANGANYWA KWAMBA YEYE SI RAIS ATAKUBALI.....Aliwahi kuuliza mzee butiku siku moja...kama waziri wetu wa fedha kadanganywa kwa swala la EPA na bado hataki kuwajibika ipo siku atadanganywa na kuitoa hazina yote ya nchi.....

Mkuu Achebe
Hii ni msumari kumoyo.
Inasikitisha kuona mtu mzima kama waziri anadanganywa halafu hachukui hatua.
Kuhusu Muungwana kudanganywa nadhani anayo nafasi kubwa sana ya kudanganywa uliko waziri maana yeye anakuwa anamilikiwa na vyombo vya taasisi yake hivyo hawezi kuja mtaani kujua kinachojiri zaidi ya kupelekewa ishu na vijana wake. Ila naamini anakumbuka ujasiri wa Baba wa Taifa alivyokuwa anafuatilia ishu mtaani tena kwa kustukiza....
Ila tatizo lipo ktk hili... Je akigundua kadanganywa anachukua hatua ipi?? Mbona Hosea, Mwanyika bado wanaendelea kibabe kukalia viti vyao wakati ofosi zao zinahusika kumdanganya????????
 
Kule Dodoma alipoulizwa na mwandishi wa VOA kuhusu.......ni wakati gani aliwahi kujisikia vibaya...or something like that........jibu lake lilikuwa

......nilijisikia vibaya sana baada ya kudanganywa kuhusu mtu fulani.......halafu nikamfukuza kazi.......nikaja-prove baadaye kuwa taarifa niliyopewa haikuwa kweli.....hii ilinisikitisha sana........na kuanzia sasa nitakuwa makini ili kosa kama hili lisitokee tena...........

Najaribu kufikiria namna ya ku-peg hii standard ya JK na issue nzima ya KUDANGAYWA + MAAMUZI YAKE

....tik tak tik tak tik tak
 
Ndio nimemaliza na sasa nimejikuta niko "speechless" na mimi kuishiwa maneno ni nadra sana. I need to take a vacation sasa.. this is too much. Nadhani ikipatikana hiyo ya EPA inabidi tumpigie saluti Tai sasa.

Mwana kijiji mi naomba kidogo unisaidie kwa hili, mi naona hichi kichwa cha habari cha hii single yetu tuibadilishe ili watu wengi zaidi waweinterested kuisoma na hii habari izagae /iwafikie watanzania wengi iwezekanavyo,maana nadhani lengo ni watz kujua jinsi nchi yao inavyo kufa wakiwa wamesimama

Hebu nenda kacheki hii thread ambavo si watu wengi wameiview nadahani ni sbb ya heading yako

MAPAMBANO BADO YANAENDELEA
 
Rejea report ya Mwakyembe:

gharama ya kununua mtambo mpya 100MW toka kwa wazalishaji ni $45.00 million. leo hii serikali inakodisha 40MW kwa $155.00 million. Watanzania bado wanaangalia tu. Kwa nini tusimwage damu kwa week moja watakaosalia mambo yataenda sawa. na kuhakikisha kwamba wale mafisadi wote tunawatafutia sniper wa kuwamaliza mmoja baada ya mwingine. tukianzia na Mkapa/Lowasa/Karamagi/Mramba/Yona/Mwakapugi/ na wengineo. Maana gharama ya kukodi sniper mmoja toka majuu ni $100,000.00 kwa kila kichwa. Kwa vichwa kumi ni $1,000,000.00. hivyo ni bora kukodi sniper kuliko kupoteza $155,000,000.00.0 tutabaki na faida kubwa ya $154,000,000.00.
 
Mtu yeyote anayekuthamini hawezi kukufanyia au kukubali kuingia mkataba wa namna hii. Nimekuja na conclusion moja tu. Watanzania tunadharaulika saaana.Viongozi wetu wanatudharau saana, kwani wanajua, tu-wajinga kweli kweli. Na hii nikwa sababu tumekuwa tuking'ang'ania kukichagua chama cha CCM ambao viongozi wake ndo wanaotufanyia huu uovu. Maana ya kuendelea kuwachagua na kuwashangilia, ina maana moja tu, kuwa tunakubaliana na upumbavu wanaotufanyia. Yaani hata baada ya kuonyeshwa kuwa RDL ni ma-"TAPELI", kamati eti ya Ufundi na Viongozi wetu wakaona kwa kuwa pesa ni za wajinga ngoja ziliwe tu.
Hapa sio Lowassa tu ila na hiyo kamati ya ufundi wanatakiwa wachukuliwe hatua kali.

Nimekuwa nikisoma mada mbalimbali humu na kuona kuwa kuna mapungufu mengi katika viongozi wetu ambao tumewachagua wenyewe. Kwa kawaida, kama mtu uliyemchagua hakufai, wakati ujao humchagui tena. Lakini kwa muda mrefu sasa, nimeona kuwa trend ya uchaguzi ni kuwachagua viongozi wale wale tu, au wale wenye sifa zinazofanana na wale waliopita. Ni vizuri kuwa hapa JF tunaweza kuona kwa upeo na kujadili mapungufu ya uongozi wetu, je mwananchi wa kawaida anajua hivyo? Wananchi wengi waliopo vijijini bado wana imani uliochanganyika na uoga mkubwa kwa viongozi na serikali. Tofauti na nchi nyingi za magharibi ambapo viongozi wanawaogopa wananchi na kufanya kila njia wasikosee, nchini mwetu wananchi wanaogopa viongozi na kuwafanya kuwa wao ndio wenye nchi. Sasa ni jinsi gani ujumbe ua habari tunazoongelea JF zitaweza kuwafikia wananchi wapiga kura, ili waweze kufanya maamuzi ya busara katika kuchagua viongozi ambao watawafaa?? Maana tutaongea hapa JF na mambo mengi tatabakia kuwa academic.
 
Rejea report ya Mwakyembe:

gharama ya kununua mtambo mpya 100MW toka kwa wazalishaji ni $45.00 million. leo hii serikali inakodisha 40MW kwa $155.00 million. Watanzania bado wanaangalia tu. Kwa nini tusimwage damu kwa week moja watakaosalia mambo yataenda sawa. na kuhakikisha kwamba wale mafisadi wote tunawatafutia sniper wa kuwamaliza mmoja baada ya mwingine. tukianzia na Mkapa/Lowasa/Karamagi/Mramba/Yona/Mwakapugi/ na wengineo. Maana gharama ya kukodi sniper mmoja toka majuu ni $100,000.00 kwa kila kichwa. Kwa vichwa kumi ni $1,000,000.00. hivyo ni bora kukodi sniper kuliko kupoteza $155,000,000.00.0 tutabaki na faida kubwa ya $154,000,000.00.

Mkuu mbona una kasi ya kuua tu ? Tuanzie mahakamani , tuweke rekodi vyema na iwe historia kwa wajai baada ya sisi na kuua kwanza si jambo jema.JF kuua si lugha yetu mkuu .Najua una machungu na naheshimu sana maoni yako lakini .............................
 
Nakubariana nawe kabisa mkuu, kuua si tabia yetu na inabidi tumuombe mungu atuepushe
Lakini kwa upande mwingine naona inaweza kutokea wakati wowote kwa sababu
Viongozi wengi wameshajua kuwa hakuna lolote wanalofanya na serikali yao ya kishikaji, na Raia wamechoka pamoja na kwamba wanashindwa kusema kitu, lakini ukweli ni kuwa watu wako tired ile mbaya
sasa hapa ikitokea machafuko na watu wakapotea, ili litakuwa sio jambo zuri hata kidogo, lakini nadhani hawa jamaa watajua kuwa watu hawataki masihala tena
na hili linasababishwa na vyombo vyetu vya sheria havitendi haki hata siku moja jamani, wewe watuhumiwa wanasomewa kesi ni wale wasiojulikana na masikini, ila wale matajiri hata siku moja, na ukimfunga anakata rufaa na anashinda kesi, mfano mzuri ni Nyari, yuko nje anakula maisha, na aliyesaidia kumtoa ni EL

Sasa watu wamechoka na msije kushangaa watu wanaingia vitani na Mafisadi jamani.

Kokolo alieyezoea kuua watu ni CCM .Tunaona waua kwa risasi za moto kisa kura na chaguzi , wanaua kwa wizi wa ma bilioni na kuacha dada zetu na akina mama wanakufa kwa uchungu , hakuna dawa , hakuna zahanati , wanatuua kw akudumaza Elimu , kukosa huduma muhimu kama maji tunapata vimea vya kila aina .Hawa CCM waache watuue ila hapa JF tutafute altenative na si kuwaza kuua hapana .We seek for Justice na si kuua.
 
Moto kuwaka bungeni keshokutwa hoja ya Richmond kuibuka upya
* Wabunge sita kutoa hoja binafsi
* Ni mtihani wa kwanza kwa Pinda

Na Mwandishi Wetu

WIKI ijayo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kupata mtihani wake wa kwanza bungeni atakaposimamia mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watu waliohusika katika kashfa ya Richmond.

Mtihani kwa Pinda unakuja kutokana na kuwapo taarifa kwamba suala hili la Richmond limewagawa wabunge katika sehemu mbili. Wapo baadhi ya wabunge ambao wanadaiwa kuwa kambi moja na baadhi ya watu wanaotuhumiwa katika kashfa hiyo wakiendesha kampeni ya kuhakikisha suala hilo linakosa nguvu ya kujadiliwa katika kikao hicho na wengine wanaokwenda na mtazamo wa Watanzania.

Wabunge hawa pamoja na baadhi ya wana CCM wenye ushawishi mkubwa ndio ambao pia waliweka kambi Butiama wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kuhakikisha kuwa hoja ya mafisadi kuchukuliwa hatua kichama inaizimwa. Hata hivyo, wapo wabunge ambao wanapa na kuhakikisha kuwa suala la Richmond linajadiliwa na watu wote waliohusika na kashfa wanachukuliwa hatua bila upendeleo.

Joto la kashfa ya Richmond limezidi kuongezeka baada ya wiki hii bunge kutoa taarifa iliyokuwa ikituhumu kuwapo kwa kundi la watu nchini linaloeneza uvumi wa kutaka kumchafua Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, Samuel Sitta. Taarifa hiyo ya bunge ilikwenda mbali zaidi kwa kueleza kwamba njama hizo za kutaka kumchafua spika kumhusisha na ubadhirifu wa fedha za bunge zimekuja hivi sasa wakati bunge bado linashunglikia suala la Richmond.

Ni kutokana na hali hiyo ya mvutano mkubwa kuhusu Richmond, Waziri Mkuu Pinda atakuwa na mtihani kama kiongozi wa serikali bungeni kusimama kidete kuhakikisha kuwa ahadi yake ya kuona watu waliohusika na kashfa ya Richmond wanachukuliwa hatua zinazoshaili inafanyika.

Kama atakwama kusimamia serikali kuwachukulia hatua au timu aliyoiunda ambayo kwa mara ya kwanza ilimaliza kazi mapema kabla ya muda wake itakuja na mapendekezo hafifu ambayo haya maslahi kwa nchi, huenda ndiyo ikawa safari ya Pinda kuanza kuporomoka. Wananchi bado wana imani na Pinda wanajua kwamba ni waziri mkuu mwenye msimamo ambaye husema kweli bila kuuma umma maneno yake.

Katika bunge lililopita aliapa kuwa wale wote watakaobainika kuhusika na kashfa hiyo bila ya kujali nyadhifa zao serikalini au ndani ya chama, watachukuliwa hatua za kisheria kama kawaida. Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya kisiasa nchini wanaona Pinda ana kibarua kigumu kuwabana watu waliohusika katika kashfa hiy kutokana na ukweli kwamba ni watu wenye 'nguvu' hata ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wana mizizi kiasi kwamba chama kinawagwaya.

Ukweli huu unadhihirishwa na kitendo cha CCM kushindwa kujadili hoja ya kuwachukulia hatua kichama watu wanachama ambao wanadaiwa kuchafuka kutokana na kuhusika katika kashfa za ufisadi. Hata hivyo, Pinda naye ameanza kujitenga na mtihani huo, kwani hivi karibuni alikaririwa akisema kwamba baada ya kuipokea ripoti hiyo ataifanyia kazi na hatimaye kuiwasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hatua na maelekezo yake.

Ripoti ya tume hiyo inafuatia taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa Zabuni ya Kampuni ya Richmond ya Houston, Texas Marekani ambapo Wabunge hao walijadili taarifa hiyo na kutoa jumla ya mapendekezo 23 ambayo serikali iliahidi kuyafanyia kazi. Timu hiyo ya Pinda inahusisha wawakilishi kutoka Ikulu, sekretarieti ya mawaziri,Tume ya maadili, TAMISEMI, Wakala wa Manunuzi (PPRA), Makandarasi, Utumishi wa Umma na Mipango, itapitia mapendekezo hayo na kutoa dira ya namna ya kuyatekeleza. Tume hiyo iliundwa kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bunge Iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe kutoa mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa na serikali kwa waliohusika na kashfa ya Richmond. Alitaja baadhi ya mapendekezo hayo kuwa Msajili wa Ofisi ya BRELA kuifuta Kampuni ya Richmond na wamiliki wake wote kufunguliwa kesi ya jinai, kisha serikali kuangalia uwezekano wa kusitisha malipo kwa kampuni ya Dowans.

Alisema serikali pia ilitakiwa kuendesha uchunguzi wa kina kubaini taarifa tete kuwa taarifa ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuhusu Richmond ilichezewa na kuitafuta taarifa halisi ya taasisi hiyo. Mapendekezo mengine ni serikali kujiepusha na utaratibu wa matumizi ya mawakala katika manunuzi ya Umma, Sheria ya manunuzi (PPRA) ipewe meno zaidi na ifanye kazi kwa kujitegemea bila kusimamiwa na Wizara ya Fedha.

Kamati hiyo pia ilipendekeza serikali kupitia upya mikataba yote na kuweka kumbukumbu ya mikataba hiyo katika ofisi za bunge, timu ya Serikali inayoshauri mikataba (GNT) iwajibishwe, aliyekuwa waziri wa nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wawajibishwe. Wakati huo huo, wabunge sita wanatarajia kutoa hoja binafsi zitakazojadiliwa katika kikao cha bunge hilo.

Siku za hivi karibuni Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wameonekana kuwa mwiba kwa serikali ambapo wamekuwa wakihoji bila woga utendaji wake kwa maslahi ya wananchi. Wabunge hao kila mmoja tayari wamepeleka hoja binafsi katika maeneo tofauti huku wengi wao wakihoji moja kwa moja utendaji wa serikali na matumizi mabaya za umma. Wabunge waliopeleka hoja binafsi ni Raphael Chegeni (Busega), William Shellukindo (Bumbuli), Alloyce Kimaro (Vunjo), Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki), wote wa CCM na mmoja kutoka Chadema, Said Arfi (Chadema).
 
Wananchi bado wana imani na Pinda wanajua kwamba ni waziri mkuu mwenye msimamo ambaye husema kweli bila kuuma umma maneno yake.

Katika bunge lililopita aliapa kuwa wale wote watakaobainika kuhusika na kashfa hiyo bila ya kujali nyadhifa zao serikalini au ndani ya chama, watachukuliwa hatua za kisheria kama kawaida.

Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya kisiasa nchini wanaona Pinda ana kibarua kigumu kuwabana watu waliohusika katika kashfa hiyo kutokana na ukweli kwamba ni watu wenye 'nguvu' hata ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wana mizizi kiasi kwamba chama kinawagwaya.

Ukweli huu unadhihirishwa na kitendo cha CCM kushindwa kujadili hoja ya kuwachukulia hatua kichama watu wanachama ambao wanadaiwa kuchafuka kutokana na kuhusika katika kashfa za ufisadi.

Hata hivyo, Pinda naye ameanza kujitenga na mtihani huo, kwani hivi karibuni alikaririwa akisema kwamba baada ya kuipokea ripoti hiyo ataifanyia kazi na hatimaye kuiwasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hatua na maelekezo yake.

This is a joke of the year! Kesi ya ngedere unaipeleka kwa Tumbili JK ataweza kumtosa RA au EL?Tusubiri tuone itakuwaje!
 
Jukumu kama ni lake basi kuufanya kuwa rahisi au mgumu, kama ni mtihani basi hilo litatokana na yeye mwenyewe kutafuta mazonge lakini kila kitu kipo kweupe ni kuachia sheria zichukue mkondo wake na hakuna jingine ,na maana ya kujiuzulu ni kwa mtuhumiwa kuipa sheria nafasi ya kutumika ,ndio hata Ditopile alijiuzulu ili apelekwe mahakamani ,very simpo ila kama anataka kujaribu kuonyesha ufundi na ujuzi zaidi kuna watu wanataka ateleze tu ili aporomoke kimaadili.
Kwani Tanzania hakuna Mwanasheria wa Serikali ambae mpira huu ndio anaepaswa kuucheza.
 
Hatutakubali kugeuzwa geuzwa akili yetu kama wanavyofiriaa...tumechoka kunyanyaswa .....kitu kiko wazi wanataka kukigeuza...tumeshituka.....ipo siku nchi haitatawalika
 
Hakuna mwana CCM mwenye nguvu wala ushawishi kwenye mambo mabaya! wote ni wamoja. Sisi watz ndio hatufahamu nguvu tuliyo nayo dhidi yao. Wakati umefika ya kutumia nguvu yetu kuwaadabisha CCM, kwanza tuanze na mwenyekiti wao! Yeye ndiye anaongoza juhudi za kuwafunika wahalifu, kama rostam na lowasa ni bora zaid ya maslahi ya watanzania basi atuachie ofisi yetu afuatane nao wakafanye ulanguzi! Tuna imani na bunge litafanya kazi yake vzr tena this time. Rostam lazima a face justice! Yeye ndiye mastermind wa richmond scandle. Tuko pamoja na bunge hata pinda akipindisha this time hawatoki!
 
Wabunge wazozana kuhusu Richmond
Mgaya Kingoba, Dodoma
Daily News; Thursday,April 17, 2008 @08:57

SUALA la Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM) kuzuiwa kutoa maelezo binafsi kuhusu Richmond, jana lilisababisha wabunge wa upinzani na wa CCM wazozane. Wabunge hao walikuwa wakihoji ni kwa nini hakupewa nafasi ya kutoa maelezo yake ndani ya chombo hicho kama alivyoahidi Spika.

Mjadala huo uliibuka baada ya Naibu Spika, Anna Makinda, kuwasilisha tamko kuhusu utaratibu wa kuwasilisha hoja binafsi; na ingawa katika maelezo yake hakuna popote alipomtaja Mbunge huyo wa mkoani Tabora, baadaye ilidhihirika kuwa ni kutokana na suala la Rostam.

Ijumaa iliyopita, Spika Samuel Sitta aliliambia gazeti hilo kwamba Mbunge huyo wa Igunga hataweza kutoa maelezo yake kwa mujibu wa Kanuni ya 54, kifungu kidogo cha nne, ambacho kinaeleza kuwa suala likisha kujadiliwa bungeni na kutolewa maamuzi, halitajadiliwa tena.

Baada ya maelezo ya Naibu Spika jana, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisimama na kuhoji kama shauri la Mbunge likizungumzwa ndani ya Bunge linaweza kuzuiwa na chama chake.

Naibu Spika alimtaka Hamad ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, kutoa mfano katika suala kama hilo na Mbunge huyo wa CUF alilitaja suala la Rostam, ambaye alisema licha ya Spika kuahidi kuwa Mbunge huyo atatoa maelezo yake ndani ya Bunge, chama chake kimemzuia kufanya hivyo.

Baada ya kupewa mfano huo, Naibu Spika alisema amefurahi kuulizwa kwa hoja hiyo, na hivyo kuanza kutoa darasa kwa wabunge na waandishi wa habari kuhusu Kanuni zinazoongoza chombo hicho cha kutunga sheria, akivitaja vifungu vya 55, 109 na 110 kuhusu suala la Hoja Binafsi.

Kwa mujibu wa Naibu Spika, utaratibu wa kuwasilisha Hoja Binafsi unaelekeza kuwa suala hilo ni lazima kwanza Mbunge aliwasilishe kwa chama chake na kisha ndipo lipelekwe kwa Katibu wa Bunge.

"Kutokana na utaratibu huo uliowekwa na Kanuni za Kudumu za Bunge, hoja yoyote binafsi inayokusudiwa kuwasilishwa bungeni inapaswa kuzingatia utaratibu ulioainishwa kwenye Kanuni za Kudumu za Bunge, ikiwa ni pamoja na utaratibu wa hoja husika kupitia kwanza kwenye Kamati ya Chama cha Siasa kinachohusika, kabla ya kuwasilishwa kwa Katibu wa Bunge," alisema Makinda.

Aliongeza: "Ieleweke wazi kwamba Bunge haliwajibiki kuzuia hoja yoyote itakayokuwa imetimiza masharti yaliyoainishwa katika Kanuni za Kudumu za Bunge.

"Utaratibu huu unakusudia kuepusha fikra potofu kuwa hoja binafsi za wabunge zinakwamishwa na viongozi wa Bunge na vile vile kuepusha migongano inayosababishwa na hoja hizo kuwasilishwa kwa Katibu wa Bunge kabla hazijapitishwa na Kamati za Chama cha Siasa kinachohusika".

Hata hivyo, Makinda alisema maelezo ya sasa ya Rostam, yalizuiwa kwa sababu yalionekana yote aliyoyasema yalikuwamo katika mchango wake wa maandishi katika Mkutano wa 10 wa Bunge, Februari 15 mwaka huu alipochangia mjadala wa ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ya Richmond chini ya uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe.

Naibu Spika alisema kutokana na hilo, Kanuni ya 54, kifungu kidogo cha nne, kinamzuia Mbunge huyo kuwasilisha maelezo yake, kama alivyoeleza Spika alipozungumza na gazeti hili Ijumaa iliyopita alipoeleza ni kwa nini hoja hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, haitafikishwa mbele ya Bunge.

Jibu la Naibu Spika halikumridhisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), hivyo akataka Mwongozo wa Spika, akitumia Kanuni ya 68, kifungu cha saba.

Mbunge huyo alimtaka Naibu Spika kueleza kwa nini Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ilimzuia Rostam wakati suala hilo ni la Bunge; na akamtaka Naibu Spika atoe ufafanuzi wa masuala mawili; atangaze msimamo wake kwa sababu ni mjumbe ndani ya Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM na pili, kanuni zinaelekeza kuwa Mbunge atawasilisha hoja zake bungeni kwa njia za maswali, maswali ya nyongeza, maelezo binafsi na maelezo ya mawaziri.

Hivyo, alimuomba Naibu Spika kuwa suala hilo la Rostam lilirudi kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge ambayo inao wajumbe kutoka upinzani, kwani alidai CCM inataka kuwabana wabunge wake ndani ya chombo hicho kikuu cha kutunga sheria nchini.

Naibu Spika akijibu alisema: "Zitto hauko sahihi. Suala hilo ni la Kanuni na kwa maandishi ambayo tayari yako katika Hansard. Hili ni suala la taratibu na Kanuni, halina uhusiano na chama. Tuwe wakweli. Waandishi wa habari na wabunge wanazifahamu vizuri Kanuni zetu.

"Lipo Azimio la Musoma ambalo limeeleza wazi kuwa wabunge wa CCM watakuwa huru kutoa maoni yao ndani ya chama chao na katika Bunge. Watu wasishindane kwa maneno na ufundi wa kusema," alisema Makinda ambaye kauli zake zilishangiliwa na wabunge wa CCM.

Ilionekana kama malumbano yanaweza kuchukua nafasi yake, kwani Zitto alisimama tena na safari hii alianza kwa kuwataka wabunge wa CCM kunyamaza; kisha akamueleza Naibu Spika kuwa suala la Rostam ni Hoja Binafsi na alisisitiza nia ya kutaka suala lake likajadiliwe na Kamati ya Uongozi.

Naibu Spika alisimama na kueleza kuwa asingependa iwe malumbano, na kueleza kuwa suala la Mbunge huyo wa Igunga, limejadiliwa kwa kuzingatia taratibu za Hoja Binafsi.

Mbunge pekee wa CCM aliyesimama kuchangia hoja hiyo alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah ambaye alikuwa na hoja mbili; akihoji kwa nini Zitto 'amedandia' hoja hiyo wakati hakuwa muulizaji wa kwanza na akahoji wapinzani hao wana maslahi gani katika suala hilo.

Naibu Spika alifunga mjadala huo kwa kusema, "Sisi sote interest yetu ni wananchi."

Suala la Rostam ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wahusika wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, liliibuka tangu kuanza kwa Mkutano wa 11 wa Bunge, Aprili 8, mwaka huu, na lilishika kasi na kutawala mazungumzo yasiyo rasmi ya wabunge baada ya kubainika kuwa Mbunge huyo amezuiwa na Kamati ya Uongozi wa CCM kutoa maelezo yake bungeni.

Mwenyewe alikuwapo Dodoma kwa siku tatu za kwanza za mkutano huo, lakini baadaye akatoweka, na alipozungumza na gazeti hili Ijumaa iliyopita, alisema anamheshimu Spika, anakiheshimu chama chake na akasisitiza kuwa hahusiki na kashfa ya kampuni hiyo inayodaiwa ni ya kitapeli.

Katika mchango wake wa maandishi ulioko kwenye Hansard ya Februari 15, mwaka huu, Mbunge huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mweka Hazina Mkuu wa CCM na sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya CCM, alisema:

"Napenda kulihakikishia Bunge lako kuwa sina hisa wala umiliki wa aina yoyote katika kampuni hizi mbili (Richmond na Dowans) na nina hakika Kamati Teule, inafahamu ukweli huu. "Mheshimiwa Spika, kaulimbiu yako ya kasi na viwango, haijadhihirika katika utekelezaji wa majukumu ya Kamati Teule.

Ulipobaini Kamati haijatoa mapendekezo kwa sababu ya muda kutotosha, uliwaongezea muda na upo ushahidi kuwa Kamati ilikuwa ikiendelea kumalizia kazi zake mpaka wiki ya kwanza ya Bunge.

"Inashangaza kwamba Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe na wewe Mheshimiwa Spika, ambao kwa pamoja mlikuwa na wajibu wa kuhakikisha kila mtuhumiwa anatendewa haki, kwa kupewa haki ya kusikilizwa, mlipuuza haki hii ya msingi kabisa ya raia."

Wakati huo huo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo hatajibu maswali ya papo kwa papo ya wabunge kwa sababu atakuwa Kenya ambako atashuhudia kuapishwa kwa Baraza la Mawaziri la nchi hiyo lililotangazwa Jumapili iliyopita na Rais Mwai Kibaki.
 
Mhh,

Tanzania yetu hii, yaani waziri mkuu wa Tanzania anakwenda Kenya kushuhudia kuapishwa kwa baraza la mawaziri wakati kuna very hot issue kama ya Chenge na Rostam?

Kuna kazi kweli huko bongo ......
 
Kipindi cha maswali na majibu bungeni ni kipya, na hivyo si muhimu kwa 'viongozi' wetu. Sishabikii kitendo cha PM kwenda kwa jirani wakati huku kuna suala la muhimu la kutolea majibu, kwetu sisi hili si la kushangaza, unakumbuka kitendo cha Mwinyi ambaye aliamua kwenda kucheza ndombolo wakati Muhimbili kulikuwa na tatizo. Hii inaonesha kuwa kuna kitu sisi watanzania tunapaswa kufanya na hii inaweza isihusishe sanduku la kuraViziwi wakisikia, watasikiliza nyimbo zote.
 
Back
Top Bottom