Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Siwezi kujua kiasi. Lakini kumbuka Dowans wamenunua mkataba wa Richmond, kampuni ambayo iliingia nchini bila hata senti tano. Hata kama Dowans hawajalipwa, expectations za kulipwa ile millioni 172 ipo. It is another IPTL
 
Mnapiga kelele lakini Lowasa an JK wanazidi kupeta na hawana wasi wasi .
 
Siwezi kujua kiasi. Lakini kumbuka Dowans wamenunua mkataba wa Richmond, kampuni ambayo iliingia nchini bila hata senti tano. Hata kama Dowans hawajalipwa, expectations za kulipwa ile millioni 172 ipo. It is another IPTL
Na kuna zile ambazo walishalamba hao Richmond Kama Down Payments kwa ajili ya kwenda kutafutia hayo majenereta au vipi?
 
http://www.reuters.com/article/scienceNews/idUSL2849214220070328?feedType=RSS

Ndani ya miezi sita kuna project hiyo ambayo ni sustainable, halafu ni rahisi vile vile. Kwa dola 172 million tungekuwa na projects mbili na nusu kama hizo. Watawala wetu wanafakiria kula tu hata kama wameshavimbiwa.

Sijui niseme nini Lakini inasikitisha kuona Tuna Rais na Mawaziri na Manaibu wapatao sitini na wanakaa vikao hivi hakuna hata mmoja ambaye ameweza hata kuonyesha kutoridhika kwa kuhoji kwenye kikao uhalali wa kuwa na project kama ile ya Richmond Aka Dowans .What hell were they doing?
 
Deni la Tanzania linaendelea kuwa kubwa kutokana na mikataba hewa na viongozi kutumia pesa kwa fujo na ukubwa wa cabinet. Je wataendelea kufanya hivi hadi lini?
 
Habari WanaJF,

Hii habari hapa, inanipa vision kwamba wanaCCM wanataka kumtoa Lowassa madarakani, wanahofu naye sana! Sasa sijui actually tatizo lake ni nini. Labda wewe mwenzangu unaweza kunisaidia. Soma Habari Hapo Chini!!

Wabunge CCM waapa kufa au kupona na Mkataba wa Richmond

Kutoka gazeti la 'wapinzani wetu' Tanzania Daima,
na Martin Malera, Dodoma


BAADHI ya wabunge wa Bunge la Muungano, wameeleza kusikitishwa na hatua ya serikali ya kulitolea maelezo suala la mkataba kati ya Richmond na Shirika la Umeme (TANESCO) kwenye vyombo vya habari badala ya bungeni.

Wameapa kulifuatilia suala hilo, ambalo linategemewa kujadiliwa wiki hii katika kikao cha Bunge kinachoendelea mjini hapa, hadi waliohusika katika mkataba huo wawajibishwe.

Msimamo huo wa wabunge, umetokana na hatua ya gazeti moja la Kiswahili litolewalo kila wiki, kuchapisha barua inayodaiwa kuandikwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwenda kwa Waziri wa Nishati na Madini, wakati huo, Ibrahim Msabaha, akimtahadharisha kuwa makini kuhusu mkataba na Kampuni ya Umeme ya Richmond Development Corporation. Dk. Msabaha sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Habari za kuaminika zinasema kuwa, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanakutana leo mjini hapa na Waziri Mkuu, kuhusu suala la Richmond, huku wakiwa na siri kubwa moyoni ya kufichua ukweli wa suala hilo linaloisumbua serikali kwa muda mrefu.

“Labda chama kinataka kutuziba mdomo kuhusu suala hili, lakini hakitafanikiwa, kwani wabunge tumeapa kufa au kupona kulifuatilia suala hili mpaka ukweli ujulikane,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Mbali ya wabunge wa CCM, wabunge wa kambi ya upinzani, nao wameandaa hoja binafsi kuhusu suala la mkataba wa Richmond uliotumia zaidi ya sh bilioni 200, lakini bado kampuni hiyo imeshindwa kuzalisha umeme na kuamua kutoa zabuni hiyo kwa kampuni dada ya Dawons.

Vyanzo vya habari viliiambia Tanzania Daima jana kuwa, juzi na jana, baadhi ya wabunge wa CCM walikuwa na vikao visivyo rasmi kwa nyakati tofauti kujadili uhalali wa serikali kutolea ufafanuzi suala la Richmond kupitia vyombo vya habari badala ya kulileta katika vikao na kamati za Bunge.

Katika barua hiyo ambayo inadaiwa iliandikwa Septemba 21, mwaka jana, Lowassa anajaribu kujivua lawama kuwa hahusiki na matatizo yaliyojitokeza katika mkataba wa Richmond kwa madai kuwa ni Waziri Msabaha ndiye alikuwa akiushughulikia.

Kwa mujibu wa barua hiyo yenye kichwa cha habari ‘Yah: Kampuni ya Richmond Development Company’, Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine alisema: “Kama unavyofahamu, yapo maneno mengi sana yanayosemwa kuhusu uwezo wa kampuni tajwa kuagiza Gas Turbines kama ilivyopewa mkataba na Tanesco baada ya kushinda zabuni.

“Inawezekana hivi vikawa ni vita vya kibiashara, lakini kwa sababu maneno haya yanasemwa na watu wengi na tofauti, ni vizuri UKAJIRIDHISHA kwamba kampuni hii itaweza kutekeleza kazi hiyo,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo.

Wabunge hao pia wanahoji uhalali wa serikali kumtwisha Dk. Msabaha mzigo wa Richmond huku ikijua kuwa waziri huyo pamoja na wengine wote, hawana uwezo wa kuingia na kuidhinisha mikataba ya mabilioni ya fedha bila suala hilo kufikishwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu na kwenye Baraza la Mawaziri.

Mmoja wa wabunge ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini, alisema kuwa serikali imedhamiria kumfanya Dk. Msabaha kuwa ‘mbuzi wa kafara’ katika suala la Richmond, lakini wamejiandaa kumtetea kwa hoja, kwani waziri huyo hana mamlaka ya kuidhinisha mkataba huo wa mabilioni ya fedha.

Baadhi ya mambo yanayohojiwa na wabunge wa CCM, ambayo wameahidi kuwa, lazima kesho yatalipuka kwenye kikao hicho, ni pamoja na nani mmiliki wa Kampuni ya Richmond na kwa nini serikali imeshindwa kurejesha fedha hizo zaidi ya sh bilioni 200 baada ya kampuni hiyo kushindwa kuzalisha umeme.

Wabunge hao wanasema fedha zilizotumika kuingia mkataba na Richmond pamoja na zile zinazotumika kwenye kampuni zingine za kukodi kuzalisha umeme, zingeweza kujenga mabwawa zaidi ya matano ya kuzalisha umeme kama bwawa la Mtera.

Bwawa la Mtera lilijengwa mwaka 1977 na kumalizika 1981 kwa gharama ya sh milioni 318.56 na ujenzi wa kituo cha umeme wa megawati 80, ilikuwa sh milioni 15.86.

“Fedha za mkataba wa Richmond kama zingetumika kujenga mabwawa kama ya Mtera, tungekuwa na mabwawa zaidi ya matano na suala la umeme lingebaki kuwa historia,” alisema mbunge huyo.

Wakati akijadili muswada wa rushwa wiki iliyopita, Mbunge wa Kyela, Dk. Harison Mwakyembe alielezea kushangazwa kwake na hatua ya serikali kupeleka barua ya siri ya waziri mkuu kwa gazeti hilo wakati Bunge na hata kamati za Bunge hazina taarifa ya kuwapo kwa barua hiyo.

“Sisi wabunge na kamati husika, hatujaonyeshwa mkataba wa Richmond, japo tumejitahidi kuomba, lakini hatujapewa maelezo yoyote kuhusu sakata la Richmond. Kwa nini serikali haioni umuhimu wa kulileta suala hili bungeni na kuamua kuthamini vyombo vya habari?” alihoji Dk. Mwakyembe katika mchango wake huo.

Hadi sasa, Tanzania ina miradi ya dharura mitano ya kuzalisha umeme wa kukodi. Mbali ya Richmond ambayo sasa ni Dowans, pia kuna mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 40 kutoka Kampuni ya Aggreko ya Falme za Kiarabu (UAE) ambao unagharimu dola za Kimarekani milioni 61, umeme wa megawati 100 kutoka Kampuni ya WARTSILA ya Finland ambao unagharimu Euro 57,550,000 na umefungwa Ubungo.

WARTSILA pia inatarajia kujenga mtambo mwingine wa kuzalisha umeme wa kukodi eneo la Tegeta, Dar es Salaam na unatarajiwa kugharimu Euro milioni 41 na mradi mwingine wa megawati 40 uko mjini Mwanza ambao unaendeshwa na Kampuni ya Alstom, unaogharimu dola za Kimarekani milioni 116.

Richmond iliingia mkataba na TANESCO wa kuzalisha umeme wa megawati 100 katika kipindi ambacho nchi ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la umeme kuliko wakati mwingine wowote.

Hata hivyo, Richmond hawakuweza kutimiza masharti na badala yake shughuli za kampuni hiyo zilichukuliwa na Kampuni ya Dowans ambayo ilitakiwa kuanza kuzalisha umeme hadi Machi mosi mwaka huu, lakini haijaweza kufanya hivyo.
 
Hii habari hapa chini ya nyuma kidogo lakini sijui imefikia wapi...

Richmond contract investigated

President Jakaya Kikwete is planning to set up a commission to investigate the award of a contract to the small American firm Richmond Development Corporation.

According to a source in the Tanzanian State House, President Jakaya Kikwete is considering the idea of creating a commission to investigate the $172 million contract awarded a few months ago to the small American company Richmond Development Corporation (RDC). As could have been expected, this firm had not been able to complete the first part of its contract within the specified time, namely the installation of 20 MW of generating capacity. However, this contract concerning a total of 100 MW and signed without the knowledge of the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco), was not terminated. RDC has support in high places and the son of a member of the government is believed to sit on its board. If Kikwete goes through with his idea, the investigating commission would be constituted next week, with the former Prime Minister Joseph Warioba as chairman and the High Court judge Mussa Kipenka as his assistant.

Source: ION
 
Kwahiyo suala hili halitojadiliwa tena Bungeni au vp? Hii kweli ndio Tanzania. Tuna ubavu wa kukomalia dakika kwa gharama ya Mil 100 na kwa faida ya "Busara" na "Ushauri nasaha" wakati issue zenye maslahi ya taifa mmh.. we haya weh!
 
Hii habari hapa chini ya nyuma kidogo lakini sijui imefikia wapi...

Richmond contract investigated

President Jakaya Kikwete is planning to set up a commission to investigate the award of a contract to the small American firm Richmond Development Corporation.

According to a source in the Tanzanian State House, President Jakaya Kikwete is considering the idea of creating a commission to investigate the $172 million contract awarded a few months ago to the small American company Richmond Development Corporation (RDC). As could have been expected, this firm had not been able to complete the first part of its contract within the specified time, namely the installation of 20 MW of generating capacity. However, this contract concerning a total of 100 MW and signed without the knowledge of the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco), was not terminated. RDC has support in high places and the son of a member of the government is believed to sit on its board. If Kikwete goes through with his idea, the investigating commission would be constituted next week, with the former Prime Minister Joseph Warioba as chairman and the High Court judge Mussa Kipenka as his assistant.

Source: ION
Huyu ni muongo kwani nimemsikia kwa masikio yangu mara mbili akitetea Mkataba wa Richmonduli na kueleza kwa makini kwamba walifanya hivyo kwasababu ilikuwa nafuu na lengo lilikuwa kukabiliana na mgao na uamuzi wa ulifikiwa kwa makini.Sasa wanaosema waendelee kusema.Sasa inakuwaje leo iundwe tume wakati alisema walikuwa makini........................Hapa ninanusa harufu ya kupewa ulaji wanatume wengine ili waendelee kusema mkataba ulikuwa sahihi na hauna harufu ya rushwa.Sasa tume ya nini kwanini yeye kama Amiri jeshi hao jamaa wameshindwa kutekeleza ahadi yao ya kutupatia umeme ktk muda muafaka kwanini wasiwatimue.
 
Haya ndio tunataka kusikia badala ya kuwa na Bunge butu "Rubber Stamp". Kama kweli Sitta atasimama imara kuhakikisha mikataba yote ya madini, Richmonduli, Radar, Net Group Problems, Ndege ya Rais, Magari ya jeshi, Helicopters n.k. inapelekwa bungeni kujadiliwa, basi nitakuwa tayari kushiriki katika maandamano ya kumuunga mkono katika kilio chake na kilio cha Watanzania wengi.
~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*
Sitta aishangaa serikali kuhusu Richmond

Martin Malera

BUNGE la Jamhuri, moja ya mihimili ya dola, halijaridhishwa na msimamo wa serikali wa kuficha mikataba mikubwa, ambayo imeingia na kampuni za nje katika sekta mbalimbali za uchumi.

Spika wa Bunge la Muungano, Samuel Sitta, jana aliliambia gazeti hili kuwa, Bunge halijaridhishwa na msimamo wa serikali kuhusu kuficha mikataba hiyo.

Alisema kuwa Bunge haliridhishwi na sababu inayotolewa na serikali kwamba kuipeleka mikataba hiyo bungeni ni kuingilia mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge na serikali.

Kwa hali hiyo, Sitta alisema sasa hivi, Kamati ya Uongozi ya Bunge, inafanya utaratibu wa kutaka kukutana na serikali, ili wajadiliane na kuliweka suala hilo sawa, kabla Bunge halijaanza kujadili mikataba mbalimbali ambayo serikali imeingia kwa niaba ya wananchi.

Hata hivyo, Sitta aliliambia gazeti hili kuwa, wakati jitihada hizo zikiendelea, ili kuweka utaratibu wa kudumu kuliruhusu Bunge kuijadili mikataba hiyo, mkataba wa kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, ambao umepigiwa kelele sana, utajadiliwa na Bunge wakati wa kikao kijacho.

Alisema Richmond ni moja ya masuala yaliyomo katika ripoti iliyowasilishwa kwake na Kamati ya Kudumu ya Uwezeshaji na Biashara, ambayo inatakiwa kujadiliwa.

Sitta alisema ripoti hiyo haikuweza kujadiliwa katika mkutano wa saba uliomalizika wiki iliyopita, kutokana na ufinyu wa muda.

Alisema tayari ameshapata ripoti ya Kamati ya Uwezeshaji na Biashara inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo (CCM), yenye kurasa zaidi ya 100, ambayo ina taarifa mbalimbali na moja kati yake ikiwa ni Richmond.

Sitta alitoa kauli hiyo jana wakati alipoombwa kutoa ufafanuzi wa kauli ya Naibu Waziri wa Mipango na Uwezeshaji, Gaudence Kayombo aliyekaririwa akisema Bunge haliwezi kujadili mikataba mbalimbali iliyoridhiwa na serikali kwani kufanya hivyo ni kuingilia mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge na serikali.

Katika mkutano uliopita, akijibu swali la Mbunge wa Bububu, Cosmas Masolwa, aliyetaka kujua iwapo serikali ina mpango wa kuileta mikataba mbalimbali ili iangaliwe na Kamati za Bunge, Kayombo, alisema serikali haina mpango huo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa ni kuingilia mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge na serikali.

Kauli kama hiyo iliwahi kutolewa Februari mwaka jana na Dk. Juma Ngasongwa wakati huo akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Alisema: “Hatuwezi kuleta mikataba hiyo bungeni. Ninachowashauri wabunge wawe wanawahoji mawaziri wanaohusika na sekta husika na siyo kudai mikataba iletwe hapa bungeni.”

Akifafanua kauli hiyo, Sitta alisema Kamati ya Uongozi wa Bunge inatarajia kukutana na serikali kujadili juu ya suala hilo, ambalo limeanza kuleta sura mbaya na kutaka kupora haki za wabunge.

Alisema wabunge hawaruhusiwi kuhoji mikataba iliyoko kwenye mchakato wa maridhiano, lakini mikataba hiyo ikishakubaliwa, inakuwa si siri tena na wabunge na wananchi, wana haki ya kujua kilichomo ndani yake.

“Mikataba inapokuwa kwenye mchakato, pale ni sawa na jikoni, Bunge haliwezi kuingilia, lakini ikisharidhiwa, hapo si siri tena, na kama wabunge wanataka kuhoji, wanaweza kufanya hivyo.

“Sawa na mtu mnamtuma kwenda Canada, kule anachozungumza ni kitu chenye manufaa kwa taifa, lakini akirudi unamwambia ulichozungumza huko ni siri, haiwezekani,” alisema Sitta.

Alisisitiza kuwa, wabunge ni wawakilishi wa wananchi ambao wana haki ya kujua mambo mbalimbali kupitia wabunge wao, ikiwemo suala la mikataba mbalimbali inayoridhiwa na serikali.

Hata hivyo, Sitta alisema suala la mkataba wa Richmond ni suala dogo katika taarifa ya kamati hiyo, kwani ina mambo mengine mengi na kuhoji uhalali wa vyombo vya habari kung’ang’ania suala la mkataba wa Richmond.

Mbali ya kupingana na msimamo huo wa serikali, Sitta pia alipinga kauli inayodaiwa kutolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKURU), Edward Hosea, kwenye vyombo vya habari kuwa, suala la Richmond lipo mikononi mwa ofisi yake na kwamba kwa sasa haliwezi kujadiliwa na Bunge wala taasisi yoyote.

“Hili tulishalikataa tangu zamani na hata kwa akili ya kawaida, suala likiwa TAKURU haliwezi kuzuia kujadiliwa, lakini linapofikishwa mahakamani, hapo huwezi kuhoji.

“Kwa mfano, kesi ya Kasusura, alipokuwa mahakamani, wabunge hawawezi kusema ooho kaonewa au…, lakini Richmond kuwa mikononi mwa TAKURU haitupi sababu ya Bunge kutojadili,” alisema Sitta.

Kauli hiyo ya Sitta inafuatia kuulizwa na gazeti hili kuhusu barua aliyoandikiwa na Kamati ya Uwekezaji na Biashara ya Bunge iliyopendekeza kwa Spika, Bunge liunde kamati ndogo ya dharura kuchunguza mchakato mzima uliosababisha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuingia mkataba na kampuni iliyokosa sifa ya Richmond Development Corporation kwa lengo la kuzalisha umeme wa dharura.

Barua hiyo ya Februari 5, mwaka huu, ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, ina kichwa cha habari kisemacho: ‘Haja ya suala la kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond kuchunguzwa na Bunge sasa’.

Kamati hiyo ilisema inajiuliza maswali mengi kuhusu Richmond, kama wanavyojiuliza wananchi wengi, lakini kwa vile haiwezi kuuona hata huo mkataba kati ya Richmond na TANESCO, hivyo kamati inaona haja na dharura kwa Bunge kuunda kamati teule kuchunguza mchakato mzima uliosababisha kampuni iliyokosa sifa stahili kuruhusiwa kutekeleza mradi mkubwa wa kitaifa,” ilisema barua hiyo.

Katika barua hiyo, kamati hiyo inasema moja ya hadidu za rejea za kamati teule itakayoundwa kuchunguza suala hilo, iwe ni kupata maudhui ya mkataba kati ya Richmond na TANESCO na kupendekeza kwa Bunge sampuli ya mikataba inayofaa kwa taifa, ambayo itafuatwa kwenye mikataba ya baadaye ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa nishati ya umeme nchini.

“Mheshimiwa Spika, hoja ya kuunda Kamati Teule tumeijenga kwenye ripoti ya kamati kuhusu utekelezaji wa shughuli za kamati kwa mwaka 2006, taarifa ambayo kamati inakuomba uitafutie muda ili iwasilishwe bungeni katika mkutano huu (uliopita), kuiwezesha hoja hiyo kupata baraka za Bunge,” ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ilitaja maswali yanayohitaji majibu ya serikali kuwa ni kwanini TANESCO iliamua kuingia mkataba na kampuni hiyo ya Marekani, ambayo toka mwanzoni ilidhihirisha kutokuwa na uwezo wa kiutendaji na kifedha kuweza kutekeleza mradi huo.

“Kwa mradi nyeti kitaifa kama huo wenye kugharimu fedha nyingi, iliwezekanaje kwa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini kuiamini kampuni ya kigeni bila kuifanyia uchunguzi wa awali hata kwa kutumia ubalozi wetu Marekani katika hali ya dharura?

“Kamati ina taarifa za maamuzi ya mwisho kabisa katika mchakato huo kufanywa na Government Negotiating Team (GNT), iliyoundwa na Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. GNT ilisukumwa na sababu zipi za msingi kuiteua Richmond wakati ushauri wa kitaalamu wa TANESCO ulionyesha wazi kuwa kampuni hiyo haikuwa na sifa stahili?” iliendelea kuhoji barua hiyo.

Barua hiyo iliendelea kuhoji sababu za TANESCO kutovunja mkataba na Richmond baada ya kampuni hiyo kushindwa kutekeleza sehemu ya mkataba wake.

“Ni nini kilichoshawishi TANESCO kuikubali Richmond kurithiwa na kampuni nyingine huku shirika hilo la umma likitambua wazi kuwa hatua hiyo ingesogeza utekelezaji wa mradi huo mbele zaidi?

“Athari za kusogeza mbele utekelezaji wa mkataba huo, ni utekelezaji kuanza kipindi ambacho taifa halihitaji kabisa umeme wa ziada (kama sasa), huku taifa likilazimika kulipia mabilioni ya fedha kila mwezi kwa mitambo iliyofungwa tu, lakini haizalishi umeme,” ilisema barua hiyo.

Taarifa ya kamati hiyo ilitokana na kikao chake na Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Januari 25, kuhusu utekelezaji wa maagizo ya kamati ya kipindi cha fedha, mipango ya shirika ya muda mfupi na muda mrefu na maendeleo ya miradi ya uzalishaji umeme wa dharura.

Katika barua hiyo, kamati ilimtaka Spika kuipangia muda hoja hiyo ili ijadiliwe bungeni, lakini Sitta anasema hoja hiyo haikujadiliwa kwa sababu ya kukosa muda.
 
Mzee six nae msanii sana, yaani anavuta shuka wakati kushakucha!
 
Kamati hiyo inayoongozwa na ndugu Shelukindo ina uwezo mkubwa sana ambao kamati yenyewe haifahamu. Kwa hakika inaweza kumwita waziri yeyote ili kuhojiwa na pia kuchunguza mikataba yeyote ambayo serikali imefanya kwa manufaa ya nchi. Kamati inauwezo wa kumhoji hata Waziri Mkuu.
Mzee Sitta hana haja ya kuibembeleza serikali au kuitongoza ifuchuwe mikataba yake. Mara nyingi mtu huficha vile vitu vibaya lakini vizuri unavitangaza ili upate sifa!

Tumekwisha ambaiwa kwamba mikataba yote ina dosari pale Rais Kikwete aliposema hadharani kwamba Tanzania haina wataalamu wa kufanya mikataba.

Sio hiyo Richmond tu twataka mkataba wa Radar pia ujadiliwe Bungeni.


MUUNGWANA AKIVULIWA NGUO ANACHUCHUMAA.

Twataka Serikali pia ichuchumae wakati itakapovuliwa nguo hapo Bungeni!
 
Kwa mujibu wa habari hii kutoka ION...

Kikwete in the firing line
The installation of new electricity capacity by certain foreign companies is running late, causing suspicion that could fallout on President Kikwete.

President Jakaya Kikwete may have been badly advised to tell Tanzanian journalists at the beginning of the year that he would be “amazed” to learn that the United Arab Emirates company Dowans Holdings had been paid in advance for a project to install 100 MW electricity generating capacity. This company had taken over the contract left uncompleted by Richmond Development Company (RDC) and has good contacts with heavyweights in the Chama cha Mapinduzi (CCC, government party). It has still not completed the contract and has been given further time, until May or June 2007. Accordingly, MPs now want to debate the matter since according to some official documents Dowans is indeed one of the four firms the Tanzanian government has already paid $400 million for energy projects. Dowans is thus believed to have received the sum of $102 million, Wartsila 133 million for two electricity power stations, Aggreko $61 million and another company operating in the Mwanza region $115 million. The CCM MP Anne Kilango Malecela raised the issue last week. However, the Minister for Energy and Mines Nazir Karamagi did not deny it in Parliament but subsequently issued a denial.
 
Mwanakijiji,

Done! Any other topics to be joined? Nimeona wengi wanafungua topic lakini zikiwa na topic mama kwenye jamvi hivyo kunilazimu kuziunganisha.

Najua hawana makosa kwani nyingine kuzipata yataka uwe unajua masuala ya mtandao walau kidogo zaidi ili u-search forum kupata related topic na kuweza kuandika kwenye topic husika.

Taratibu tutafanikisha tu; wazo langu ni kuwa ukiona mtu kafungua mada na unajua kuna nyingine yenye ujumbe unaoshabihiana na alioandika mtumie ujumbe pembeni mwambie kakosea a-copy na ku-paste kwenye topic husika na ile aliyoifungua aifute (lakini najua si wote watakubali!).

You're welcome
 
EDWARD HOSEA, DG wa PCB, amesema kwamba mkataba wa Richmond na serikali ulikua halali na usio na harufu yoyote ya rushwa.

Amesema ilikua ni wakati wa dharura na ndio Waziri Mkuu, Edward Lowasa akaamua kuunda kamati ya Wataalamu, Katibu Mkuu, Hazina, (G.Mgonja), Katibu Mkuu Nishati na madini, na Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, baada ya kuona kwamba kupeleka tenda ya kimataifa, umeme wa dharura utachelewa.

Akasema tena hakuna kiongozi aliyethibitika kupewa rushwa wala kamisheni. \

Maelezo ya ziada baadaye.
 
Kwani mlitegemea nini haswa pale aliposema pia kwamba amefunga uchunguzi wa rushwa ya bunge.
Ila tumekwisha kama hali ikiwa ndio hii .
 
tokea lini mla rushwa bongo akajitangaza hadharani ?? sasa sishangai chochote maana nisije nikastaajabu ya firauni !
 
Back
Top Bottom