Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

sie tulie tu, haki ya nani, kuna mtu alisema humu ndani kwamba hawa jamaa wana-take advantage ya njaa, umaskini, illiterate ya watanzania wengi kujinufaisha !!
 
Nadhani hakuna aliyetegemea majibu tofauti na haya kutoka PCB, hawa jamaa ni sawa na kesi ya nyani na hakimu awe ngedere.
 
Kwani hii kesi ilipelekwa lini huko ? Chanzo cha kesi kwenda huko ni nini ama Spika amekuwa pre empted ili hoja isiende Bungeni ?
 
jamani hii nchi sasa tumeingiliwa na hawa majangili,hakuna jipya katika serikali ya ccm.kila kukicha ni ufujaji wa hali ya juu wa rasilimali za nchi yetu.
Tunahitaji kufanya maandamano ya kutaka serikali iliyopo madarakani ijiuzuru na kuitisha uchaguzi mpya utakaotupa serikali mpya.
mwinyi alituuza kwa waarabu,mkapa kwa makaburu,jk naye anatupeleka kama watoto yatima.
watanzania tuamke hatuna sababu ya kuendelea kulala.
 
PCB yaisafisha tuhuma za rushwa Richmond
Jonas Songora na James Magai

TAASISI ya Kuzuia Rushwa nchini (TAKURU) imeisafisha kampuni ya Richmod Development Company dhidi ya tuhuma za rushwa zilizokuwa zikiikabili katika uingiaji wa mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kwa TANESCO.

Akizugumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Takuru , Upanga jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Takuru, Edward Hosea alisema kuwa hakuna ushahidi wowote uliopatikana kuthibitisha vitendo vya rushwa, uzembe, au upokeaji wa kamisheni kwa watendaji wa serikali.

Kusafishwa huko kwa tuhuma za rushwa dhidi ya kampuni hiyo, serikali na wadau wengine kunakuja baada ya kuwepo mingong'ono ndani ya jamii na hata serikali na bunge.

Alisema kuwa uchunguzi huo ulithibitisha kuwepo kwa mapungufu ya kawaida katika utendaji na ambayo hayakuhusisha rushwa au manufaa ya aina yoyote ile kwa upande wa watendaji na hakuna hasara iliyosababishwa na mapungufu hayo.

Katika ushahidi uliopatikana kufuatia uchunguzi huo, Hosea alisema kuwa kampuni ya Richmond Development Company, LCC ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited inayomilikiwa na Naeem Gire ambaye ana uraia wa Tanzania na Mohamed Gire ambaye ni raia wa Marekani, ilifanikiwa kushinda zabuni iliyotangazwa na TANESCO baada ya kuyashinda makampuni mengine manane yaliyojitokeza.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo ilishinda zabuni hiyo baada ya Kamati ya tathmini yenye watu kumi na mbili, wakiwemo wajumbe wanane kutoka TANESCO, mjumbe mmoja mmoja kutoka Wizara za Fedha, Nishati na Madini, na wajumbe wawili kutoka Kampuni ya ushauri ya Laymeyer International ya Ujerumani ambayo ni kampuni ya ki- ufudi kwa TANESCO.

Hata hivyo kutokana na hali ya dharura na uharaka wa kutatua tatizo la umeme, alisema kuwa serikali iliamua kuingilia kati na Waziri Mkuu aliamua kuunda kamati ya watu watatu ilio kuharakisha zoezi hilo baada ya kuona kuwa utaratibu wa kutumia soko la kimataifa la wazabuni ungezidi kuchelewesha upatikanaji wa umeme.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Katibu Mkuu Hazina ilipewa jukumu la kuishauri serikali kwa uharaka zaidi, na kuweka vigezo ikiwemo mzabuni kuthibitisha uwezo wake kiufundi, uthibitisho wa bei kutoka kwa mzabuni, na kueleza muda atakaotumia hadi kuanza uzalishaji, ambapo kampuni ya Richmond ilithibitika kuwa na sifa zinazotakiwa.

Aliongeza kuwa Richmond ilithibitisha kuwa na sifa zinazotakiwa kwa kushirikiana na kampuni kubwa ya Pratt and Whitney yenye uzoefu mkubwa katika utengenezaji na uzalishaji wa umeme na pia kuthibitisha kuwa inaweza kuingiza umeme ndani ya wiki kumi na nne.

Akizungumzia kuhusu kushindwa kutekeleza kwa mkataba ambao Richmond iliingia na serikali, Hosea alisema kuwa baada ya kuthibitishwa Richmond kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba, serikali haikuilipa kampuni hiyo hadi ilipouza kazi zake kwa kampuni ya Dowans Holding SA Disemba 21, 2006 ambayo ndiyo inastahili kupewa malipo ya usafirishaji mtambo.

Aliongeza kuwa Richmond ilipaswa kuilipa TANESCO fidia ya ucheleweshaji huo kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 kwa siku kuanzia Februari 20, 2007 kwa vile shughuli za Richmond ziliuzwa kwa Dowans, adhabu ambayo kwa sasa italipwa na kampuni hiyo.

Taarifa hiyo ya uchunguzi imekuja kufuatia malalamiko yaliyojitokeza kufuatia mchakato mzima wa utoaji zabuni ambapo serikali iliingia mkataba wa kukodi mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kufuatia kina cha maji kupungua katika mabwawa ya kuzalishia umeme ambapo serikali iliingia mkataba na Richmond kupitia TANESCO mwezi Juni 23, 2006.

Hata hivyo baadhi ya watendaji wa serikali walishutumiwa kuwa wamiliki wa kampuni hiyo ambayo ilishutumiwa sana kutokana na kuchelesha uletwaji wa majenereta hayo ya kuzalisha umeme wa dharura.

SOURCE: http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari1.asp
 
Wanaforum,

Hivi hii sio move ya kuvunja nguvu za bunge kulijadili hili swala? kama PCB wametoa clean bill of health, Wabunge wanaweza kuhoji lolote kuhusu Richmond?
 
Unajua kuna mambo mengi sana kwenye Richmod zaidi ya hata rushwa; kwa mfano, nani anapaswa kuwajibishwa kwa kampuni hii kushindwa ku-deliver?

PCB kazi yake siku zote ni kuwasafisha vigogo wa CCM na viwingu vya rushwa. Kwa maana ingine hii basi inawezekana inatumiwa kabisa katika kufanikisha vigogo kula rushwa bila mikwaruzo na wasiwasi wa kukamatwa. Yaani ndio yaleyale polisi kuwasindikiza majambazi wanapoenda kuiba! Hapo ndipo CCM walipotufikisha!
 
Akina Maduhu na Mohamed Saleh (Tanesco) naona wanachekelea ile mbaya. Saleh alipiga trips 3 Houston na mradi wa Richmond ulivyopitishwa tu, akastaafu na kazi Tanesco. Talk about timing.
Na hawa ni samaki wadogo:=(
 
Maelezo ya Hosea si sahihi kulingana na ukweli uliopo uwanjani.

Taarifa zilizopo Richmond walishalipwa kabla hata ya kutekeleza mkataba wao. Na si kweli kuwa walikuwa hawajalipwa mpaka walipouzwa kwa Dowans.

Vilevile si kweli kuwa Dowans wanailipa Tanesco dola 10,000 kwa siku kwa kuchelewesha kutimiza mkataba kuanzia Feb, 2007

Najua nitaulizwa ushahidi, nilionao ni ushahidi wa kimazingira kwa jinsi ninavyo wajua watu hawa wangekuwa wanajitangaza kila siku kuwa wanaopata hasara ni wao kwani wanatulipa dola 10,000 kwa siku.

Jumba la sanaa limepata msanii mwingine mahiri Edward Hosea
 
I am speechles Sina lakusema.One of the days they will bring us a postmortem report telling us that the Daladala driver who was shot,at point blank range by Ditto,died from Natural Causes.Hii ndiyo nchi yetu tunaivunia .Long live our Commrades.
 
RICHMOND... mabilioni ya pesa.... Umeme hakuna, watu wanatanua.

Tanzania! wacha bwana
 
This is sad story, na ninakubaliana na wananchi wengi waliotangulia,

but, wakati umefika wa kuwa na sheria ya Public Informatin Act, kwa sababu ninajua kuwa hawa PCB hawakupewa any information on the ishu, kwa hiyo wameishia pembeni tu na kutoa uamuzi, au hawakugusa kabisaaa,

hivi huyu jamaa Hoseee alipoteuliwa ni si niliona mada moja inahusu Cv yake na kama sikosei kuna wajumbe waliosema kuwa ni mtu makini au?
 
hivi huyu jamaa Hoseee alipoteuliwa ni si niliona mada moja inahusu Cv yake na kama sikosei kuna wajumbe waliosema kuwa ni mtu makini au?

hata mimi kwa jinsi ndogo niliyomfahamia[not in person]enzi za kamanzima,alivyopewa nafasi nikasema...mkata kuni kapewa shoka jipya...kazi itaboreshwa. lahaula la kwata.....sasa ndio haya.....we acha tu!

hebu kwanza,labda wameshamloga![sio kwa kwenda bagamoyo] maanake kwa stahili hizi mawazo ya kiswahili ndio hushamiri vichwani mwetu!....hivi mungu kaenda likizo nini,kwenye suala hili?
 
Back
Top Bottom