Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Ili kuweza kuthibitisha tuhuma tajwa hapo juu, TAKURU iliamua kufanya uchunguzi ili kupata majibu ya hoja za ki-uchunguzi kama ifuatavyo:-

2.1 Kufahamu wamiliki wa kampuni ya Richmond.

2.2 Kufahamu iwapo utaratibu wa zabuni ulifuatwa.

2.3 Kufahamu iwapo kulikuwa na upendeleo wowote katika utoaji zabuni kwa kampuni hiyo ya Richmond.

2.4 Kiasi cha fedha kilicholipwa kwa kampuni hiyo mara baada ya kusainiwa mkataba.

2.5 Kufahamu kiasi cha fedha kilichokuwa kimelipwa kwa Richmond hadi tarehe kampuni hiyo ilipokabidhi shughuli zake kwa kampuni ya Dowans.

2.6 Kufahamu uhusiano uliopo kati ya kampiuni ya Richmond na Dowans.

2.7 Kufahamu sababu za Richmond kujiondoa na kuwapa Dowans shughuli zao.

2.8 Kufahamu iwapo kulikuwa na hasara yoyote ambayo serikali itakuwa imeipata kutokana na kampuni ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme kwa mujibu wa mkataba wake, kisheria.

2.9 Kufahamu iwapo kulikuwa na uzembe wa upande wa serikali (kupitia timu ya wataalamu-GNT) katika kusimamia mchakato mzima na hasara iliyotokana na uzembe huo.

2.10 Kufahamu iwapo kulikuwa na kamisheni iliyokuwa imetolewa kwa watendaji wakuu wa serikali yetu.

2.11 Kufahamu iwapo kuna mabadiliko ya kiutekelezaji kiufanisi baada ya Dowans kuchukua shughuli hizo toka Richmond.

2.12 Kufahamu iwapo kulikuwepo na mapungufu yoyote katika mchakato mzima na upana wa athari zake.

3.0 Ushahidi uliopatikana..................coming up next......!
 
Mzee Es..hapo nakufagilia..lete data....kumkama nyani.....malizia...Tunakusubiri kwa Hamu..naona usiku watu wengi hawajasoma hii nondo yako...
 
3.0 Baada ya TAKURU kufanya uchunguzi wa kina na wenye umakini wa hali ya juu, ushahidi uliopatikana umeweza kuthibitisha mambo yafuatayo:-

3.1 Wamiliki wa kampuni ya Richmond:-
Richmond Development Company LLC, ni kampuni iliyosajiliwa tarehe 09 Novemba, 2003 huko Houston - Texas nchini Marekani. Ambapo wakurugenzi wa kampuni hiyo tajwa Richimond ni Mohamed Adam Gire na Mohamed Haque ambao ni raia wa Marekani na ni wafanya biashara nchini humo wanaotambulika kisheria za nchi hiyo.

Adama Gire, ndiye mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, na kwamba Richmond Development Company, LLC ya huko Houston-Texas, ni kampuni mama ya kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited!, ambayo ilipata usajili wake hapa Tanzania tarehe 12/07/2006. Wakurugenzi wa kampuni hiyo hapa Tanzania, ni Naeem Gire, ambaye ni raia wa Tanzania, na mwingine ni Mohamed Gire, ambaye ni raia wa Marekani, kampuni hiyo inamiliki hisa 1,000,000 kwa mchanganuo ufutao:-

Richmond Development Company LLC, ambaye mtendaji wake mkuu ni Mohamed Adam Gire, inamiliki hisa 750,000. Naeem Gire anamiliki hisa 250,000. Aidha maofisa wengine wakuu wa kampuni hiyo ni Mohamed S. Huque na Khatri, ambao ni raia wa Marekani.

Kampuni ya Richmond Development Company (T), ilipewa Certificate of Incentives No. 120007 tarehe 23 Oktoba 2006 na Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC). Kampuni hii ilisajiliwa ili kuweza kutekeleza shughuli za kampuni ya Richmond Develeopment, LLC baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kukodisha mitambo ya uzalishaji umeme wa dharura na shirika la Umeme Tanzania(TANESCO).

Coming up next............Taratibu za utoaji wa zabuni
 
nadhani inafahamika tokea mwanzo kwamba hii dili lilikuwa rushwa tupu ( na off course wala rushwa hawataki kuitwa wala rushwa ) acha mie nikapumzike nikasikilize taarabu mahusiano !!
 
Kutokana na tatizo sugu la umeme, serikali ililiagiza Shirika la umeme Tanzania TANESCO, litafute njia ya haraka ya kuweza kutatua tatizo la umeme nchini. TANESCO iliiishauri serikali kwamba njia ya haraka ilikuwa ni kutafuta mitambo ya kukodisha itakayotumia gesi ili kuweza kuzalisha umeme wa dharura.

Serikali ilikubaliana na ushauri wa TANESCO na kuiagiza ianze mchakato huo mara moja.

TANESCO, walitanganza tangazo la zabuni Namba PC/010/2006 la tarehe 27, February, 2006. Ambapo tarehe 01/03/2006 bidding documents zilitolewa kwa wazabuni. Tarehe 13/03/2006 ndiyo ilikuwa mwisho wa kurudisha bidding documents, na ilisogezwa mbele hadi tarehe 20/03/2006. Tarehe hii ilisogezwa mbele baada ya wazabuni wengi kuomba ufafanuzi kwenye bidding documents, na ni makampuni manane (8) ndiyo yaliyorejesha bidding documents, ambayo ni yafuatayo:-

....to be continued.......
 
Let's see how the story unfolds.

Uchangiaji na uchambuzi wa mambo namna hii katika mtandao huu wa JF ndio unaotufanya baadhi yetu tuendelee kurudi hapa mara kwa mara.

Ahsante kwa kazi hii nzuri Mzee Es.

Mpangilio wa utekelezaji wa uchambuzi/uchunguzi walioufuata PCB unapendeza na unaeleweka.
 
1. M/S REAL ENERGY (UK).

2. M/S AGGREKO INTERNATIONAL (U.A.E.).

3. M/S RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY LLC (USA).

4. M/S REMCP SPA (ITALY).

5. M/S APGUM CO. LIMITED (GERMANY).

6. M/S GLOBELEO LTD (UK).

7. GAPCO (T) LTD (TANZANIA).

8. M/S QUANTUS (GERMANY).

TANESCO, iliunda kamati ya tathmini (Evaluation Committee), yenye watu kumi na mbili (12). Wajumbe nane kutoka TANESCO, Mjumbe mmoja toka Wizara ya Nishati, Mjumbe mmoja toka Wizara ya Fedha, Wajumbe wawili toka Kampuni ya Ushauri ya Lahmeyer International (GERMANY) ambayo kwa kisheria na kawaida ni kampuni ya ushauri kwa TANESCO.

Lakini baada ya mchujo wa kwanza, katika kutathmini makampuni hayo manane (8), makampuni yote hayo nane yalionekana kama kukosa sifa kulingana na vigezo ambavyo vilikuwa vimewekwa na TANESCO, na ndipo Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO iliiiagiza Bodi ya Zabuni ya TANESCO kufanya International Shopping. Kutokana na hali ya dharura na uharaka wa kutatua tatizo la umeme, serikali iliona kwamba utaratibu wa kupata mzabuni kwa njia ya International Shopping bado ungechelewesha mchakato, hivyo Waziri mkuu aliunda kamati maalum ya viongozi watatu (3).

..........to be continued.........!
 
Mzee Es,
Hizo zote ni kampuni mbuzi tu... Sielewi lini viongozi wetu watajifunza kwamba kuna makampuni ambayo hayapeleki maombi ya tender kwa nchi maskini!... Ni jukumu la nchi maskini kuomba hizo Kampuni kuwekesha nchi maskini. Yaani sisi ndio tunajieleza kwao kama vile JK alivyokwenda Nasdaq kujitanganza. Miradi mikubwa ya Infrastructure na hasa ktk Umeme, Reli, Maji na Mawasiliano ni miradi inayohitaji kuwa makini sana ktk maamuzi...
Sasa sielewi kama Ulaji ndio ulisukuma maamuzi yao ama ni kutoelewa wenzetu hua wanafuata utaratibu gani ndani ya soko huria!...

Endelea uncle shusha vitu!
 
1. M/S REAL ENERGY (UK).

2. M/S AGGREKO INTERNATIONAL (U.A.E.).

3. M/S RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY LLC (USA).

4. M/S REMCP SPA (ITALY).

5. M/S APGUM CO. LIMITED (GERMANY).

6. M/S GLOBELEO LTD (UK).

7. GAPCO (T) LTD (TANZANIA).

8. M/S QUANTUS (GERMANY).

TANESCO, iliunda kamati ya tathmini (Evaluation Committee), yenye watu kumi na mbili (12). Wajumbe nane kutoka TANESCO, Mjumbe mmoja toka Wizara ya Nishati, Mjumbe mmoja toka Wizara ya Fedha, Wajumbe wawili toka Kampuni ya Ushauri ya Lahmeyer International (GERMANY) ambayo kwa kisheria na kawaida ni kampuni ya ushauri kwa TANESCO.

Lakini baada ya mchujo wa kwanza, katika kutathmini makampuni hayo manane (8), makampuni yote hayo nane yalionekana kama kukosa sifa kulingana na vigezo ambavyo vilikuwa vimewekwa na TANESCO, na ndipo Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO iliiiagiza Bodi ya Zabuni ya TANESCO kufanya International Shopping. Kutokana na hali ya dharura na uharaka wa kutatua tatizo la umeme, serikali iliona kwamba utaratibu wa kupata mzabuni kwa njia ya International Shopping bado ungechelewesha mchakato, hivyo Waziri mkuu aliunda kamati maalum ya viongozi watatu (3).

..........to be continued.........!

"Lakini baada ya mchujo wa kwanza..................."

Tunasubiri hiyo kamati ya viongozi watatu (3) itakayotajwa na sifa za wahusika zilizowezesha uchambuzi wa kina na ziada na kuiwezesha Richmond kupeta, licha ya kwamba na wao walikuwemo katika huo mchakato wa mwanzo wa makampuni ambayo hayakuwa na sifa zilizokidhi mahitaji.
 
1. Katibu Mkuu Hazina - Mwenyekiti.

2. Katibu Mkuu Wizara ya Nishati.

3. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kamati ilipewa jukumu la kulishughulikia suala hili na kuishauri Serikali kwa uharaka zaidi. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, waliteua mwakilishi/wawakilishi kutoka ofisi zao na ikaundwa timu ya ufundi (Technical Team), ambayo ndio ilifanya majadiliano na wazabuni. Timu hii ilijumuisha wajumbe wanne (4) kutoka TANESCO, Watatu (3) toka Wizara ya Nishati, Mmoja toka Wizara ya Fedha.

Kamati hiii ilipewa jukumu la kuweka vigezo ambavyo ni muhimu na kuacha vile ambavyo vilionekana kuwa so muhimu, lakini kuachwa kwake hakutaathiri utekelezaji wa mradi.

Hata hivyo kamati/timu hiyo iliweka vigezo vifuatavyo na ndivyo vilivyotumika katika kufanya majadiliano.

..........Itaendelea..............!
 
Mzee Kalamu,

Heshima mbele mkuu, mimi ninafikiri harufu mbaya inaanza kunukia kwenye, maneno yafuatayo:-

".....Kutokana na hali ya dharura na uharaka wa kutatua tatizo la umeme, serikali iliona kwamba utaratibu wa kupata mzabuni kwa njia ya International Shopping, bado ungechelewesha mchakato, hivyo WAZIRI MKUU aliunda kamati maalum ya viongozi watatu............."

I smell something kuanzia hapa!

............to be continued..........
 
Jamani tatizo la Richmond ni nini?

1. Wameleta genereta
2. Bei yao ni nafuu

Hivyo sioni hizo kampuni nyingine zingefanya nini zaidi. Ukubwa wa kampuni si sababu ya huduma nzuri kinacho zingatiwa ni mahitaji ya wananchi kwa bei nafuu.
Tatizo ambalo Tanesco imefanya siyo kuchagua kampuni ndogo kwani genereta si kitu ambacho ni lazma kampuni iwe kubwa, lakini tatizo ni kwamba Tanesco na serikali ingeweza kununua hiyo genereta yenyewe kutoka kiwandani bila kupitia wabia ambao ni namna nyingine ya kula rushwa. Watu serikalini wanatumia ubia ili waweze kula rushwa kwani ni vigumu sana hawa wala rushwa wakaenda kuhonga kampuni kubwa kama GE. Hata kama tenda ingetolewa kwa kampuni kubwa bado rushwa ingeliwa kwani tatizo ni namna tender zinavyotolewa na si kampuni inayopewa. Kumekuwa na maneno mengi sana kwamba Richmond haina uwezo lakini je ni uwezo gani? Richmond haijaombwa wataalamu bali genereta na kununua genereta hakuhitaji uwezo wowote zaidi ya pesa, hivyo kwa mtu yeyote mwenye pesa na anajua ni genereta gani inahitajika basi angeweza kutoa huduma hiyo. Ndiyo Richmond inarushwa lakini imekuwa wazi kwa sababu mwenye kampuni ni Mtanzania na watu wanaongea lakini kila tender ya Tanzania ina rushwa Rada, Madini, Ndege ya raisi n.k. Mfano mzuri ni ndege la raisi hiyo ndege mpya ukienda hapo Geogia kwenye kampuni ya Gulf Stream ndege mpya kama ya raisi ni $10m hata kama uki customize haiwezi kuzidi $20m sasa inawezekana vipi imeuzwa $40m bei ya boeing 703? ni kwa sababu ya tender na tender ni njia ya rushwa kila mtu anajua hivyo hata raisi. Kwa nini wasingeweka deal wenyewe na wakalipia gharama za kuipeleka nyumbani kwani hiyo service ipo lakini ni rushwa. Hivyo Watanzania wenzangu tusiishie kuisema richmond kama wenyewe tu ndiyo wabaya kila tender Tanzania ina rushwa, na Richmond watu wamekuja juu kwa sababu ni Mtanzania. Richmond ni hafadhali kuliko deal nyingine kwa ingawa ameonga ni mtanzania na gharama yake ni nafuu lakini hizo deal nyingine zilikuwa over-priced. Hivyo kama tunataka kutatua tatizo tuanzie kwenye mizizi ndugu zangu.
 
Nijuavyo ni kwamba serikali nyingi duniani, pamoja na mashirika mengi ya kimataifa hutumia 'tender' kama njia ya kupata mali au huduma zenye viwango, na zenye bei nzuri. Sasa kama 'tender' za Tanzania ni za rushwa, ina maana taratibu zinazoifanya njia ya 'tender' iwe ya haki na ukweli hazifuatwi. Hiyo sio 'tender.'

Nadhani umefanya haraka mno kuhitimisha na kuikingia kifua Richmond. Tuvute subira kidogo, Mzee Es aendelee kutufumbulia yaliyojili.

1. Je tunajuaje kuwa jenereta zilizoletwa na Richmond bei yake ni nafuu?
2. Kwa mtizamo wako hakuna hasara yoyote iliyotokana na mradi huu. Mimi sidhani kuwa hiyo ni kweli.
3. Ninakubaliana na mawazo yako kuhusu ununuzi wa 'dharura.' Kwa kuwa ukosefu wa umeme ilikuwa ni 'dharura' (Sijui ni vipi serikali haikujua kuwa kina cha maji kinapungua haraka - na kila mwaka hutokea hivyo hivyo), basi serikali ingechukua jukumu la moja kwa moja kununua hilo jenereta. Ni kama vita vya Kagera, kama huwezi kusubiri taratibu za 'tender' kujenga daraja, na huku adui akikuchakaza.
 
Halafu leo kwenye Daily News kuna heading isemayo.."TOURS BOSS NABBED OVER GRAFT"....the amount involved..30,000 shillings!!
Hii news iko 2nd page kwenye Govt newspaper!
RICHMOND,zilch!
 
Mzabuni kuthibitisha uwezo wake wa kiufundi. Mzabuni kueleza iwapo tayari ana mitambo ya megawati 100 kwa ajili ya kukodishwa. Mzabuni kueleza muda atakaoutumia mpaka kuanza uzalishaji.

Baada ya kufanya majadiliano kwa kuzingatia vigezo hivi, Richmond Development Company LLC, ilithibitika kuwa na sifa hizo zinazotakiwa na hivyo kuwa mshindi, na hii ilitokana na ukweli kwamba kampuni hii ilishirikiana na kampuni ya Pratt & Whitney yenye uzoefu mkubwa katika utengenezaji na uzalishaji wa umeme. Mwakilishi wa kampuni hiyo aliithibitishia kamati kwamba watashirikiana na Richmond Development Company LLC, katika masuala ya kiufundi na jenereta zipo tayari, Kampuni ya Richmond pia ilithibitishia kamati kuwa itaweza kuingiza mitambo hiyo na kuanzisha uzalishaji mali ndani ya wiki kumi na nne (14). Kampuni hii ya Richmond Development Company LLC ilikuwa na bei ndogo ya ($ 0.0699) kwa unit moja, ikilinganishwa na kampuni nyingine hasa zile nne za mwanzo ambazo timu iliona zinafaa, kampuni hizo kwa nafasi zake ni:-

1. Richmond LLC - $ 0.0699.

2. Renco - $ 0.12

3. Aggreko - $ 0.0878

4. Apgum - $ 0.074.

Bei hizi pia zinajumlisha gharama za gesi.

........to be continued.............!
 
Mzee Es,
Shukran tupo nawe!

Kamundu,

Inabidi ulifuatilie swala la Ricmond toka mwanzo naona kuna mengi yamekupita.. Haikuwa swala la supplier wa generators kumbuka uamuzi huop umefikiwa baada ya kuona Option kubwa na muhimu zaidi kutupwa nje. Je, tatizo la Umeme dar lilianza jana? hapana ila limewekwa hadi lilipofikia mahala hakuna njia tena. Unafahamu vizuri kwamba maintanance sio kabisa utamaduni wa Mwafrika hata usome vipi bado utakuwa mzito.

Hata hivyo nafikiri kipengele alichotanguliza Mzee Es, kinajibu vizuri swali lako. Soma - Mzabuni kuthibitisha.....hapo nadhani hata wewe ungekuwa ktk kamati hiyo ungetoa maamuzi tofauti pamoja na kwamba it is the last option!
 
Kwa kuzingatia matokeo haya, Richmond LLC, iliitwa kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kuingia mkataba. Hivyo basi timu iliongezewa mtaalamu wa sheria kutoka ofisi ya Mwanasheria mkuu, ambaye jukumu lake ilikuwa kutoa ushuari wa kisheria wakati wa majadiliano hayo. Timu pia iliongezewa wajumbe kutoka CTI, BOT, na mjumbe mmoja aliongezewa kutoka Wizara ya Nishati. Katika majadiliano hayo, pia kulikuwepo wajumbe wanne kutoka Richmond LLC.

Mkataba huu ulikuwa na kipengele kinachoruhusu Mzabuni kuuza/kukodisha shughuli zake kwa kampuni nyingine kwa sababu za kimsingi ambazo mteja wake TANESCO, atakubaliana nazo na bila masharti ya msingi ya mkataba.

Kwa kuzingatia uwezekano wa kampuni husika kuchelewesha utekelezaji wa mradi huu, mkataba pia uliweka kifungu kwa ajili ya kutoa adhabu endapo uzalishaji hautakuwa tayari hadi kufikia tarehe ya mwisho ambayo ni 10/02/2007. Hivyo basi mkataba huu ulikuwa na kifungu kitakachoiadhibu kampuni hiii kiasi cha $ 10,000 kwa siku ambazo ni karibu (Shillingi 12,800,000), kuanzia tarehe 02/02/2007 hadi hapo itakapoanza kuzalisha umeme kiasi cha megawati 100.

........Coming up next...(...Kufahamu Kiasi Kilicholipwa Na serikali mara baada ya mktaba kusainiwa......!)..........!
 
Duh..Mzee Es unapata wapi data? na watu wa TAKURU hawajafanya Press Conf...huoni kuwa unakuwa hatari ktk nyeti za Serikali?....au ..ok tusubiri sie ni kufuatili hizi taarifa....then tutakuwa na cha kuchangia........
 
Kwa mujibu wa mkataba huu, kampuni ya Richmond LLC, ilipaswa kulipwa kiasi cha nusu ya gharama ya "Letter of Credit", $ 15,348,299.00 mara baada ya kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha kwamba mtambo ya kwanza pamoja na baadhi ya vifaaa kwa ajili ya ufungaji wa mitambo mingine itakayoletwa vimeshapatikana na kupakiwa melini. Na nusu iliyobaki $ 15,348.299.00, baada ya kuwasilisha nyaraka kuthibitisha mitambo iliyobaki imepatikana na kupakiwa melini.

Serikali pia ilipaswa kulipia gharama za usafirishaji wa mitambo hiii. Ushahidi umethibitisha kuwa Richmond LLC, ilishindwa kutekeleza masharti ya mkataba, hivyo serikali haikuilipa kampuni hii kiasi chochote cha fedha hadi ilipouza kazi zake kwa kampuni ya Dowans Holding SA, ndiyo iliyostahili kulipwa malipo hayo ya usafirishaji wa mtambo wa kwanza, $ 4,865,000.00 , uliongia nchini tarehe 21/10/2006 kwa ndege na si Richmond LLC, tena ni baada ya Richmond kushindwa kabisaa kutekeleza masharti ya mkataba.

...Coming up next............"Sabbau za Richmond kuuza shughuli zake"...........!
 
Nadhani tatizo lilianzia hapa. Baada ya kugundulika kuwa hawafai, kulikuwa hakuna haja ya kuwapaka mafuta tena ili waonekane wanafaa. Hatua zote alizofanya waziri mkuu na watu wake hazikubadilisha ukweli huu.

Back
Top Bottom