Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Hivi mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!!
Mambo ambayo yametokea na kusababishwa directly na Awamu ya nne japo kwa 75% ni:-
1. Richmond Saga, ambalo ni matokeo ya pressure ya matatizo ya umeme na ukame, tatizo ambalo alirithi, nakumbuka akina Jenerali Ulimwengu walivyokuwa wanaipressure serikali itangaze hali ya hatari, ili taratibu za Procurement zifuatwe ili kupata suluhisho la umeme haraka.
2. Buzwagi, ambapo tatizo ni sheria yenu ya madini, mpaka sasa hakuna aliyesema amekosea kifungu gani cha sheria..., other than kwamba London hotelini, etc etc..
3. Nikumbusheni...
Mengine ni ya kurithi tu!!! sasa kwa kuwa yanatokea kipindi chake na watu ni wasahaulifu basi kila kitu kimetokea kutoka kwa Awamu ya nne...
Ukiniuliza naona awamu ya nne imesababisha watu(individual, taasis, NGOs) etc kuwa na huru kujadili mambo ya kitaifa na kwa uwazi zaidi hili ni jambo jema kwa serikali....
Awamu ya nne iliweka wazir marosoroso ya Auditor General reports kwa mahesabu ya serikali kwa ajili ya wananchi wafahamu na viongozi husika wafuatilie.
Jamaa wamebadilisha sheria ya rushwa,,, na sasa sio sheria ya bribery bali ya corruptions,,, hii imesababisha at least hata kwenye CCM watu wamekemewa au imeonekana sio jambo tena la kawaida...
Takrima is out!
Naomba kuendelea kuelemishwa maana nadhani kama ni Ben abebe mzigo wako na kama ni Jakaya pia abebe mzigo wake
Nadhani Kilitime unajaribu kutetea japo hata MBINU ZA KUTETEA ZINAKUSHINDA. NI AIBU KUHUSISHA BUZWAGI, RICHMOND na awamu zilizopita. Unaweza kuhusisha suala la BoT na awamu zilizopita lakini awamu ya nne imechukua hatua gani? Hapo utabaini kwamba kwa kipindi cha miaka miwili tu 2006-2007 kiasi cha fedha kilichopotea serikalini ni kikubwa mno na kwa mwendo huo wa KASI MPYA baada ya miaka kumi (kama tukijaaliwa) itakua ni BALAAAAAA KUBWA na nchi itakua haitawaliki. Kinachofanyika ni kusema na kukemea ili wahusika wachukuliwe hatua na ili wasitokee wengine wakaendelea kuchota wakijua HAWATAGUSWA. Hivi kampuni zinazotajwa kuchota fedha za BoT ni za watu wa awamu na tatu ama ya pili?
Unapozungumzia Mkataba wa Buzwagi hauna tatizo, bali tatizo ni sheria,, hivi JK aliposema wanarekebisha kwanza ndio wasaini mikataba, aliteleza ulimi ama alijua TUTASAHAU?
Unapozungumzia UKAME NA TATIZO LA UMEME, hivi kwako pakitokea tatizo unaruhusu familia yako ikafanye uhalifu? NAdhani hakuna UHALALISHWAJI WA UKIUKWAJI WA TARATIBU NA UHALIFU MWINGINE WOWOTE KWA SABABU ZA UHARAKA. Hata VIBAKA WA KARIAKOO WANAKUFANYA UWE NA WASIWASI NA HARAKA ILI WAKUPORE, HIVI UHARAKA WA RICHMOND, umeme umeanza kuzalishwa lini?