SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Hi
Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge yo Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 April, 2016 ililitaka Jeshi Ia Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System). Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo Ia kupotosha umma kutokana na kile kilichoamuliwa na kamati hiyo.

Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 April, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi Ia Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine iliona kuna haja ya kupata maelezo ya kina kwa maandishi katika utekelezaji wa mkataba huo.

Kutokana na haja hiyo, kamati ilimwagiza Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.

Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo yo Ndani tarehe 12 Aprili 2016 kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu yo Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprifi 2016 kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016 kama ilivyoshauriwa na kamati.

Ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016.

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge

DAR ES SALAAM

15 Aprili, 2016.
hivi ndivyo nchi yetu kwenye tv kinachoombwa ni mkataba lakini bunge linaongea vingine lengo ni kuficha kilicho kusudiwa
 
Mtakumbuka tumehoji sana kuhusu Lugumi. Wapo wenzetu MsemajiUkweli wakitetea kwa nguvu zote kuwa hakukuwepo na tatizo. Tulisema ficha ficha ya habari ilieleza mengi zaidi kuliko tuliyokuwa hatuyajui

Soma hapa Utetezi wa Polisi sakata la Lugumi huu hapa | Latest News, Sports, Business, Entertainment, Features, Columnist | IPPMEDIA
Si mpaka kamati ije na majibu...kwa sasa bado ni mapema kutoa hukumu...maana info zilizopo bado ni za 'nasikia...nasikia...' watembelee hivyo vituo waje na ushaidi usio na shaka
 
Si mpaka kamati ije na majibu...kwa sasa bado ni mapema kutoa hukumu...maana info zilizopo bado ni za 'nasikia...nasikia...' watembelee hivyo vituo waje na ushaidi usio na shaka
Yes, nimemsikia Rais akiwa viwanja vya Biafra akisema 'Nanyi Polisi mnatuhumiwa kutumia pesa vibaya, lakini yaliyopita si ndwele tugange yajayo''

Nikikumbuka jinsi viongozi walivyokuwa wanatupiana mpira, mhh anyways

Tusubiri ni suala la muda
 
Yes, nimemsikia Rais akiwa viwanja vya Biafra akisema 'Nanyi Polisi mnatuhumiwa kutumia pesa vibaya, lakini yaliyopita si ndwele tugange yajayo''

mimi pia ninaamini time will tell!

Nikikumbuka jinsi viongozi walivyokuwa wanatupiana mpira, mhh anyways

Tusubiri ni suala la muda
 
Kwa nini Serikali isitoe Mkataba wa Lugumi hadharani?. Kwani kuna tatizo gani?. Naomba jibu.
 
Sakata la Lugumi lahitimishwa bungeni

Haya wale waliodhani sisi ni wajinga Lugumi imezikwa rasmi

Hakuna aliyeona mkataba

Spika kafunga mjadala

Suala limepigwa dana dana hadi kufunikwa, halafu tunaambiwa eti wanapambana rushwa

Tunaambiwa majipu!!! Thubutu!

Hawa watu wamekulia katika mfumo wa kifadi wa CCM, wameona nchi ikitafunwa na uhalaifu unavyoweza kufichwa.

Wamewekwa na mfumo ule ule uliowalea. Wanajaua kashfa zote zinafichwa kwa njia gani

Ni maajabu sana wanaweza kuwa tofauti leo.
Ni wale wale msiwe na matumaini fake, msidhulumu nafsi zenu mkidhani ni mvinyo mpya!

Ni wale wale waliokuwa kimya nchi ikiliwa, leo wanapata wapi sauti za kukemea uovu?
Miaka makumi walikuwa kimya, leo wanasema eti wanakerwa na rushwa na ufisadi!

''Yaliyopita si ndwele tugange yajayo'' mliambiwa

Tanzania Oyee

Hapakazi tu

MsemajiUkweli nyumba kubwa
 
Kwa nini Serikali isitoe Mkataba wa Lugumi hadharani?. Kwani kuna tatizo gani?. Naomba jibu.
Mmeshaambiwa "yaliyopita si ndwele, tugange yajayo"! Sasa mnataka nini tena? Hebu acheni "uchochezi" wenu......ebo! Nyinyi 'hamna haki ya kuihoji serikali yenu takatifu nje ya bunge'.....umeelewa?😀😀😀😀😀
 
Sakata la Lugumi lahitimishwa bungeni

Haya wale waliodhani sisi ni wajinga Lugumi imezikwa rasmi

Hakuna aliyeona mkataba

Spika kafunga mjadala

Suala limepigwa dana dana hadi kufunikwa, halafu tunaambiwa eti wanapambana rushwa. Tunaambiwa majipu!!! Thubutu!

Hawa watu wamekulia katika mfumo wa kifadi wa CCM, wameona nchi ikitafunwa na jinsi ya jinsi uhalaifu unavyoweza kufichwa. Wamewekwa na mfumo ule ule uliowalea.

Ni maajbu sana wanaweza kuwa tofauti na mzazi wao.

Ni wale wale waliokuwa kimya nchi ikiliwa, leo wanapata wapi sauti za kukemea uovu?

Miaka 20 walikuwa kimya, waacheni waendelee na kazi yao

Hawa ni CCM wasiwadanganye, ''Yaliyopita si ndwele tugange yajayo'' mliambiwa

Tanzania Oyee

Hapakazi tu
halafu unasikia kuanzisha mahakama ya 'walaji' itawafunga nani kama mambo yanazima kama mshumaa...
 
halafu unasikia kuanzisha mahakama ya 'walaji' itawafunga nani kama mambo yanazima kama mshumaa...
Tuliona kuanzia mwanzo dana dana, tukajua hapa kunafichwa kitu. Sasa taarifa kama imetoka tuelezwe mkataba ulikuwaje, na nani alitangaza tenda, tenda ilisimamiwaje n.k.

Kuna gazeti lilisema mzabuni alipatikana ! hatujui alishindanishwa na nani

Leo watu wanamatumaini kweli kweli, mahakama ya mafisadi, majipu n.k.
Msitese nafasi zenu ni wale wale

Escrow, Richmond, Memeremeta, Tangold, EPA, Dowans, Nyumba za serikali!
Yaliishaje! Ni wale wale, mkiona jipu ni kuwapa matumaini feki.

Ni wale wale walioficha uovu miaka nenda rudi, hawawezi kuwa tofauti!
Hawakuwahi kukemea uovu. leo wanaanzia wapi kukemea! hawana experience

Mjadala wa Lugumi sasa umefungwa.

Watu wajadili maendeleo na si siasa kila siku.

Watu wasikwamishe serikali katika jitihada za kuleta maendeleo. Ni wakati wa kazi tu

Tanzania Hoyeeeeee

#Hapakazi
 
Hatutaki taarifa fupifupi ijengwe tabia ya kununua muda tv ya taifa na jambo lichambuliwe kiundani,hii mambo ya kuelezea jambo zito kwa sentensi mbilitatu Ni kutuvuruga akili. Nendeni kwenye tv au redio jopo Zima na huyo mwenyejina tutawauliza na maswali huko.We don't need narrations in vast issues
 
kinya30062016-jpg.361604
 
Kama mgeni wa nchi hii ndio utayashangaa hayo!
 
Back
Top Bottom