BONGE BONGE
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 3,722
- 2,110
....kuna wakati natamani kuishi mwezini, kumbe Tanzania wote ni malofa na mafala!!!!!
Hii post nimeipata unaweza kuisoma. lugumiHOJA INAYOTAWALA SASA HIVI NI JUU YA KAMPUNI ZILIZOINGIA MKATABA NA POLICE: KINA NANI WAMILIKI! HII NDIYO HOJA. WAO WAUPELEKE HATA KAMATI YA AFYA AU MICHEZO. TUNACHOTAKA HUO MKATABA UWEKWE HADHARANI.
Well said Mkuu[emoji111] . Massage sent[emoji106]Halafu nani alisema Magu anaweza kutumbua kila jipu? !
Nasubiria pale daktari wa majipu atakaposhindwa kutumbua jipu la standard seven.
Aliyesema Magu anaweza kutumbua kila jipu ni anayewalipa mawaziri mishahara ya uwaziri na ubunge na kuwapa gari la uwaziri na jingine la ubunge huku akizuwia watumishi hewa na wale wanaopokea mshahara zaidi ya mmoja.Mimi naamini maneno ya Aeshi (?) M/kiti wa PAC niliyemsikia kwa masikio yangu na niliyemuona kwa macho yangu akiongea ITV.
Kamwe sitaamini hili tamko lindana la ofisi ya Bunge. Halafu nani alisema Magu anaweza kutumbua kila jipu? !
Mbona tupo pamoja mkuu, kuanzia mwanzo hoja yangu ni kuwa kificho cha nini? Ninashangaa unasubiri ukweli, utaupata wapi ikiwa ilichukua 7 kutafuta faili na sasa yanazuka mengine kama haya ya bunge? Ukweli upi unaousubiri ikiwa mwenyekiti PAC aliomba mkatab, Mwenyekiti ulinzi na usalama akakiri kuupata, Bunge linasema kinachotakiwa ni maelezo ya kina. Ukweli upi tena na utaupata wapi?
Hakuna mahali nimeweka hitimisho la suala hili, hata hivyo ubabaishaji umezua hisia kwa jamii na ni haki ukizingatia serikali inasema hili, bunge linasema kile kamati hazijulikani zinafanya kazi gani, bunge halijui kamati zimeomba nini
Hoja hapa ni kuwa wanaficha ukweli, ndio maana tunawaangalia kupitia mboni za macho na kujiuliza, ndio hawa wanaosema wanapambana kweli?
Ukweli utapatikana wapi katika ubabaishaji uliopo?
Rekodi zinaonyesha ukibadili mwelekeo kila taarifa inapokuja! katika hali hiyo unaupta wapi ukweli? Ni upi unaoufuata!
NIMEISOMA. NA HAYO NDIYO PAC WANAPASWA KUWEKA WAZI. SIYO HILI LA NANI KAUOMBA NA NANI HAKUUOMBA MKATABA!Hii post nimeipata unaweza kuisoma. lugumi
Mkuu hapa kuna hoja mbili. Kwanza, lazima wananchi wawezeshwe kupata ukweli wa tukio zima ili kupitia wanasheria waweze kubaini kama kuna tatizoMkuu samahani nnaomba utusaidie hapa ,kama hali ndio hii wananchi wanayo nafasi gani kisheria katika hili ukizingatia walio ibiwa ni wao!?
Mungu was mbinguni shuka uwasaidie watanzania. Tumeweka mijambazi yenye nguvu na akili madaraka. Halafu yanaigiza na kututaka tuyashangilie eti majipu!! Majipu?!!!stupid baada ya kumtorosha agent was wizi yanatuzuga kijingaaaaa!!!!! Chama cha majambazi awamu ya tank no hatari ya karne.Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge yo Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 April, 2016 ililitaka Jeshi Ia Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System). Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo Ia kupotosha umma kutokana na kile kilichoamuliwa na kamati hiyo.
Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 April, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi Ia Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine iliona kuna haja ya kupata maelezo ya kina kwa maandishi katika utekelezaji wa mkataba huo.
Kutokana na haja hiyo, kamati ilimwagiza Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.
Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo yo Ndani tarehe 12 Aprili 2016 kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu yo Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprifi 2016 kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016 kama ilivyoshauriwa na kamati.
Ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
15 Aprili, 2016.