Mbona tupo pamoja mkuu, kuanzia mwanzo hoja yangu ni kuwa kificho cha nini? Ninashangaa unasubiri ukweli, utaupata wapi ikiwa ilichukua 7 kutafuta faili na sasa yanazuka mengine kama haya ya bunge? Ukweli upi unaousubiri ikiwa mwenyekiti PAC aliomba mkatab, Mwenyekiti ulinzi na usalama akakiri kuupata, Bunge linasema kinachotakiwa ni maelezo ya kina. Ukweli upi tena na utaupata wapi?
Nimekupa mfano wa Hati ya Muungano kama benchmark yangu katika siasa za Tanzania.
Tuliwahi kuambia hivi hivi kama unachokisema kuwa tunasubiri ukweli wa nini wakati hakuna Hati ya Muungano. At the end of the day, Hati ya Muungano ikatolewa na serikali. Kwa mantiki hii, nimejifunza kusubiri ukweli kwa sababu ukweli haufichwi bali hucheleweshwa tu.
Hakuna mahali nimeweka hitimisho la suala hili, hata hivyo ubabaishaji umezua hisia kwa jamii na ni haki ukizingatia serikali inasema hili, bunge linasema kile kamati hazijulikani zinafanya kazi gani, bunge halijui kamati zimeomba nini
Maandiko yako mengi ya nyuma yanatoa angalizo kuwa umeishaelewa ukweli wa suala hili ila unataka kuudhihirishia ulimwengu kuwa ulichokisema ni kweli.
Hutaki kuangalia picha nzima kuanzia Polisi, Bunge na vyombo vya habari. Kwako kila kinachoandikwa na vyombo vya habari ni kweli kama vile hivi vyombo vyetu vya habari nivya kuamini.
Hakuna tamko rasmi la polisi kupitia press conference kuhusiana na suala hili. Tamko la Polisi lingetufanya kuelewa upande wa Polisi. Tunasoma tu habari kwenye magazeti zikisema fulani amesema hivi au vile mbaya zaidi habari hizi zinakinzana.
Kwa sasa tumepata Tamko rasmi la Bunge. Ninasubiri Tamko rasmi la Polisi.
Hoja hapa ni kuwa wanaficha ukweli, ndio maana tunawaangalia kupitia mboni za macho na kujiuliza, ndio hawa wanaosema wanapambana kweli?
Naomba uelewe kuwa Ukweli huwa haufichwi bali unacheleweshwa.
Una maana gani unaposema ''ndio hawa wanaosema wanapambana kweli'' Una maana bunge au Polisi?
Ukweli utapatikana wapi katika ubabaishaji uliopo?
Rekodi zinaonyesha ukibadili mwelekeo kila taarifa inapokuja! katika hali hiyo unaupta wapi ukweli? Ni upi unaoufuata!
Ninaamini ukweli utapatikana lakini inawezekana siyo kwenye muda unaodhani wewe ni mwafaka.
Mimi ninausubiri ukweli ili nipitishe hukumu yangu.