SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge yo Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 April, 2016 ililitaka Jeshi Ia Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System). Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo Ia kupotosha umma kutokana na kile kilichoamuliwa na kamati hiyo.

Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 April, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi Ia Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine iliona kuna haja ya kupata maelezo ya kina kwa maandishi katika utekelezaji wa mkataba huo.

Kutokana na haja hiyo, kamati ilimwagiza Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.

Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo yo Ndani tarehe 12 Aprili 2016 kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu yo Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprifi 2016 kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016 kama ilivyoshauriwa na kamati.

Ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016.

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge

DAR ES SALAAM

15 Aprili, 2016.
Jambo hili ni gumu maana litaanika wakubwa...wahusika wa wizi huu ni viongozi wakubwa...baada ya kuzima swala hili usitarajie kwamba kutakuwa na vita dhidi ya ufisadi nchini. wahusika wakuu ni wakina Rizi 1 na viongozi waandamizi wakuu wa ccm na serikali yake. wanahaha kuzima swala hili kwa gharama yoyote ile..January yumo na wengine wengi tu.
hilo ni cha mtoto lakini likiwekwa wazi litaibua jambo kubwa lililojificha nyuma kwa hiyo kuna kila aina ya juhudi kuzima swala hili...Magufuli na timu yake ya watu wachache anataka lishughulikiwe lakini hawataki maana jeshi la polisi pia litaingia kwenye kashfa kubwa na kudhalilisha vyombo vya usalama kimataifa.
 
PAC wanajipa madaraka ambayo sio yao...hawana mamlaka ya kukagua mikataba bila idhini ya wahusika
Nguvu kubwa unayoitumia kutetea Ufisadi huu, ni afadhali ungeitumia kwenda shule kidogo kwani wewe ni KILAZA WA KUTUPWA.
Kawadanganyeni Dodoma ambao Akili zao zimedumaa kwa kula viwavi, au nendeni Lindi ambako wanakula mbilimbi!
 
Hahahaaa sinema limefika patamu halafu umeme unataka kukatika
 


Tujikumbushe kauli ya PAC juu ya hili sakata la Lugumi.Ukiisikiliza habari hii utaona kabisa Makamu Mwenyekiti wa PAC na Mbunge wa S'wanga Mjini anasisitiza kabisa kuwa wao walichoomba ni "Mkataba na Nyaraka mbalimbali" zinazohusiana na mkataba huo

Lakini leo ofisi ya Bulahi Ndugai inasema kuwa Kamati ya Bunge haikuihitaji mkataba bali "maelezo ya kina",sasa hayo maelezo ya kina watayajuaje bila kuuona mkataba?

Na ukimsikiliza Haeshi ni kuwa hiyo ni siku ya pili wanasubilia Jeshi la Polisi liwasilishe mkataba huo lakin hawaonekani,na zaidi mpaka muda umepita wa kazi jamaa hawajafika,kamati ikaamua kuongeza muda hawakufika na baadae kamati ikatoa "Siku Tatu zaidi" na bado mkataba haukwenda.

Kweli hizi sarakasi zinaanza kutuondolea imani kuwa kuna wengine "hawatumbuliki"...Lakini tutoe muda,tungoje na kusubiri.Kila jambo na wakati wake,ama hakika kuna mengine yamekaa pabaya,hayatumbuliki wala kutumbuliwa.Tumuombee Rais wetu,ana kazi nzito sana sana.

Haya ya kampuni ya Lugumi na Sarakasi za Bunge la Bulahi Ndugai yanatukumbusha kujenga "mfumo imara" na sio "Mtu imara",na mfumo imara huanza kwa kuwa na katiba imara.Tuendelee kumuombea Rais wetu atambue umuhimu wa katiba mpya yenye maslahi kwa wananchi.
 
Afadhali wametoa ufafanuzi, ingawa unawachanganya zaidi wananchi...maelezo ya kina ya utekelezaji wa mkataba ambao haujauona au kufahamu yaliyomo!
 
Nchi hii ni full maigizo. Alietuhumiwa na kufikishwa kizimbani kwa kumuita raisi BWEGE kafikishwa mahakamani akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wapatao 6 wakiwa na silaha za kivita. ila alietapeli na kuitia serekali hasara ya bill 34 bwana lugumi yupo ulaya anakula kuku kwa mrija.
 
Nimekutukania kiungo cha mamako
Ulichofanya ni kusumbua fikra yako kwa sababu mimi sikufahamu na sina muda wa kutaka kukufahamu.

Ni mtu mjinga au mpumbavu anayemtukana mtu ambaye hamfahamu na kwa maana hiyo inawezekana na wewe uko katika kundi hilo!
 
Ulichofanya ni kusumbua fikra yako kwa sababu mimi sikufahamu na sina muda wa kutaka kukufahamu.

Ni mtu mjinga au mpumbavu anayemtukana mtu ambaye hamfahamu na kwa maana hiyo inawezekana na wewe uko katika kundi hilo!
Nimekudharau kabisa. ww ni bure bora angezalowa panya kuliko ww.
 
Ni ngumu sana kupambana na ufisadi kwa dhati ukiwa ndani ya ccm. Utajikuta unawaguss watoto wa marais wastaafu na ndugu na jamaa za watu wazito kwenye chama chako. Hspo utafanyaje? Itabidi upotezee tu! Au unaweza kukata tawi la mti uliokalia? Mh Magufuli anadhani msfisadi ni watumishi wa umma kumbe hawa hawana ubavu wa kufanya ufisadi bila kuhusisha wanasiasa viongozi wakubwa serikalini.
Halafu mara nyingi ambao wamekuwa wanafanya ufisadi mkubwa wanamega fungu kubwa tu kusaidia chama wakati wa kampeni. Je utawatumbuaje?
 
Ni ngumu sana kupambana na ufisadi kwa dhati ukiwa ndani ya ccm. Utajikuta unawaguss watoto wa marais wastaafu na ndugu na jamaa za watu wazito kwenye chama chako. Hspo utafanyaje? Itabidi upotezee tu! Au unaweza kukata tawi la mti uliokalia? Mh Magufuli anadhani msfisadi ni watumishi wa umma kumbe hawa hawana ubavu wa kufanya ufisadi bila kuhusisha wanasiasa viongozi wakubwa serikalini.
Halafu mara nyingi ambao wamekuwa wanafanya ufisadi mkubwa wanamega fungu kubwa tu kusaidia chama wakati wa kampeni. Je utawatumbuaje?
Maneno kuntu mkuu.
 
Mheshimiwa Rais akiliacha hili lipite, haitakuwa na maana ya kutumbua wengine, na kuacha wengine.
 
Mheshimiwa Rais akiliacha hili lipite, haitakuwa na maana ya kutumbua wengine, na kuacha wengine.
sawa kabisa kama mtumishi alikosea lazima atumbuliwe hakuna maana ya kujificha kwenye kivuli cha dini ndio justification ya kuguswa.
 
Back
Top Bottom