SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Kwanza naomba uelewe kuwa Aeshi siyo mwenyekiti wa PAC.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Mwenyekiti wa PAC na LAAC lazima atoke kambi ya Upinzani. Wapinzani walikataa kushiriki uchaguzi wa PAC na LAAC kwa madai kuwa wajumbe walioteuliwa kutoka kambi ya upinzani hawana uwezo. kwa lugha nyingine, kambi ya upinzani haiwaamini wajumbe wa PAC.

Pili, hakuna sehemu ambayo Rais Magufuli alisema ataweza kutumbua majipu yote lakini vile vile huwezi kutaka Rais Magufuli atumbue pia majipu ambayo hayajaiva na kama akifanya hivyo, kuna wengine watakuja hapa wanadai Rais anakurupuka.
Nimekutukania kiungo cha mamako
 
Unawezaje kuomba maelezo ya mkataba, bila mkataba wenyewe?

Au kwa mfano rahisi,
unawezaje kuomba harufu ya chakula badala ya chakula chenyewe?

Hii taarifa kwa Umma imeandikwa kwa Ku panic.
Wanataka maelezo ya kina bila kuwa na 'ground' ya maelezo
Hawahitaji mkataba, wanataka mtu atakaytoa maelezo meengi ya kina bila kujua anafikiaje kina.

Hili la Lugumi kadri linavyosonga mbele linakuwa na mvuto, wanaingia waliomo na wasiokuwemo. Taarifa ya bunge inazidi kutia ukakasi na kuleta maswali zaidi
 
Ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016.
Ni kitu hicho hicho tu, hapo ni mchezo wa maneno tu. Utapewaje maelezo kuhusu mkataba ulivyotekelezwa bila ya kujua kilichotakiwa kutekelezwa? Hakukuwa na haja ya hili tamko, labda lengo ni kupunguza joto la ishu yenyewe
 
PAC wanajipa madaraka ambayo sio yao...hawana mamlaka ya kukagua mikataba bila idhini ya wahusika
Wahusika ni akina nani sasa ambao inabidi waidhinishe? Ina maana hata wawakilishi wa wananchi kama wabunge hawaruhusiwi kuona mikataba!!
 
ccm chama cha majipu. nchi hii haiwezi kusonga mbele bila ya kuiweka ccm pembeni. hawa ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo na ndio maana watanzania wamekata tamaa ata ya kufanya kazi. kwa mtindo huu ile report ya 71% hawafanyi kazi itaongezeka zaidi.
 
Hakuwezi kuwa na maelezo ya kina bila ya msingi wa maelezo ya kina. Msingi wenyewe ndio huo mkataba.

Hapa wenzetu husema "I smell a rat here". Yaani unataka uone performance ya kina ya mkataba, mradi etc bila kujua mkataba au mradi unasema nini? Goals, objectives, schedules and other contractual issues. Utafanyaje ufuatiliaji au tathmini? Kama ni kweli basi hata kamati yenyewe na bunge inamatatizo. Lakini siamini kama wabunge hao wako weupe kiasi hicho. Kwa hiyo kama nikweli naamini kuna kinachofichwa. Ulichosummarise ni 100% sawa tunafanywa wajinga na pia wapumbavu.
 
Ngoja nisubiri nisimhukumu mapema Magufuli....
 
Wanaotumbuliwa ni wafanyakazi tu. Wanaoba mabilion nikazi kuwatumbuwa.
 
Makosa si hayo tu bali pia kuna maneno mengi katikati ya sentensi yameanza kwa herufi kubwa bila sababu za msingi na kinyume cha kanuni zs kawaida kabisa za uandishi. Kama kweli imetoka ofisi ya bunge ni aibu!QUOTE="msem, post: 15894868, member: 337697"]Siko katika position ya kujua kama bandiko hili ni la kweli au sio la kweli(mtandaoni lolote linawezekana,ila kuna spelling mistakes hapo ambazo zinashusha status ya thread yenyewe:
1.yo hesabu=ya hesabu (paragraph ya kwanza)
2.mambo yo ndani=mambo ya ndani (paragraph ya nne)[/QUOTE]
 
Kwanza naomba uelewe kuwa Aeshi siyo mwenyekiti wa PAC.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Mwenyekiti wa PAC na LAAC lazima atoke kambi ya Upinzani. Wapinzani walikataa kushiriki uchaguzi wa PAC na LAAC kwa madai kuwa wajumbe walioteuliwa kutoka kambi ya upinzani hawana uwezo. kwa lugha nyingine, kambi ya upinzani haiwaamini wajumbe wa PAC.

Pili, hakuna sehemu ambayo Rais Magufuli alisema ataweza kutumbua majipu yote lakini vile vile huwezi kutaka Rais Magufuli atumbue pia majipu ambayo hayajaiva na kama akifanya hivyo, kuna wengine watakuja hapa wanadai Rais anakurupuka.

Aeshi ndie Kaimu mwenyekiti mpaka hapo atakapopatikana huyo mwenye kiti kwa hiyo ndie msemaji mkuu wa kamati kwa sasa. Hatutegemei adanganye kuhusu hili.
Hiyo sehemu ya pili nakuunga mkono. Raisi pia anahitaji muda issue itue kwake na aifanyie uchunguzi.
Ni tegemeo langu kuwa kwenye hili nalo atalifanyia kazi na kuchukua uamuzi ufaao na hata lipotezea hasa kama matamshi ya bunge ndio hayo ya ajabu ajabu-wanataka watathmini bila kuwa na taarifa kamili ya kinachotathminiwa.
 
Kwanza nikupongeze kwa kujitahidi kujibu kwa busara japo najua kwa hili sakata limekushuka.
Unaposema limenishuka unakuwa na maana gani?

Kwani mimi ni Bunge, LUGUMI au ninamiliki Polisi.

Hivi kama isingekuwa Bunge unadhani hii suala lingekuwa kwenye media kwa sasa au hufahamu muda ambao CAG alitoa repoti ya mwaka 2013/14?

Umewahi kujiuliza kwa nini PAC iliyopita haikulishikia bango hili suala wakati wanapitia mahesabu ya mwaka 2013/14?

Halafu kwa mambo ya kitoto hivi ndio eti watu wanaaminisha wananchi kwamba nchi hii haitegemei misaada na itakuwa nchi ya viwanda!!
Ni haki yako kudhani kuwa taifa litaishi milele kwa kutegemea misaada!

Hakuna mtu aliyesema nchi haitegemei misaada. Ninasema misaada isiwe ni fimbo au kichaka kupitishia ajenda zilizojificha.

Wewe unadhani taifa litaishi katika maisha yote kwa kutegemea misaada?
Kweli unaweza kusimama mbele ya hadhara ukahubiri nchi kuwa ya viwanda huku ukipindisha ukweli wa wazi kiasi hiki!!?
Yes, nchi inaweza kuwa ya viwanda kwa sababu hili sio suala jipya. Tanzania ilishawahi kuwa na viwanda vingi tu.
Yaani hata ile imani haba niliyoanza kuipata kwa hili debe mlilokuwa mkiipigia serekali hii ya Magufuli imefutika rasmi kwa tangazo la utumbo kama huo.
Hulazimishwi kuwa na imani kwa Rais Magufuli kwa sababu hukulazimisha hata kuwa na imani haba unayodai uliyokuwa nayo.

Kwani unasubiri kupigiwa debe ndio uwe na imani na utendaji wa Rais Magufuli.

Labda nikuulize, kwa sasa una imani na nani ambaye ni bora kuliko Rais Magufuli?
Ila si mbaya endeleeni kudanganya wananchi kwamba mnapambana na ufisadi huku mkiwachombeza na matumaini hewa ya viwanda huku kukiwa hakuna mpango wala dalili za dhahiri la hilo kutokea zaidi ya kupiga siasa.

CC: Humphrey Polepole, mzee mwanakijiji
Huo unaodhani ni uwongo inawezekana ni fikra zako na wengine ninaamini wana fikra tofauti.

Nani unadhani angepambana na ufisadi zaidi ya anachokifanya Rais Magufuli?

Nimalizie kwa kusema, We are at war with the army we have (Rais Magufuli), not the army you might want or wish to have at your irrational thoughts and ideas![/QUOTE][/QUOTE]
 
MFIKISHIENI JPM..
By Malisa GJ,
Kwa moyo wa dhati kbs nampongeza Rais Magufuli ktk jitihada zake za kubana matumizi. Lakini nina mambo mawili ya kumshauri;
#MOSI;
Kubana matumizi bila kubuni vyanzo vipya vya mapato ni kazi bure. Kama atawanyima madereva safari za Dodoma, akapunguza posho za watumishi Lakini bado tukaendelea kupewa 04% kwenye madini na 09% kwenye gesi ni kazi bure.
Kama atapunguza mishahara ya watumishi, atazuia safari za nje, ataondoa sijui semina na warsha serikalini lakini akafumbia macho "mbio za mwenge" naona ni kazi bure pia.
Namshauri badala ya kulazimisha malaika waishi kama mashetani, ni vizuri ajitahidi kuwafanya hao mashetani (watanzania maskini) waishi kama malaika. Falsafa ya kufanana si kumfilisi tajiri ili awe maskini kama wewe, bali kumsaidia maskini apande na kufanana na tajiri.
Kama kipato hakitoshi kwenye familia dawa sio kubana matumizi na kulazimisha watoto wale dagaa kila siku, dawa ni kuwajibika zaidi na kutafuta njia mbadala ya kukuza kipato ili watoto waweze kubadilisha mboga.
#PILI;
Napenda kumuuliza JPM anapata wapi ujasiri wa kuwakemea watumishi wenye mishahara miwili (au zaidi) wakati mawaziri wake wote wana mishahara miwili? Mawaziri wote wana mshahara wa uwaziri na wa ubunge. Wana posho za uwaziri na za ubunge. Wengine ni wajumbe wa bodi za taasisi mbalimbali huko nako wana posho. Bado posho za kamati za bunge.!
Waziri ana "shangingi" la uwaziri, ana "shangingi" la Ubunge. Ana hela ya mafuta ya ubunge (lita 1000 kila mwezi kwa wabunge wa majimbo), ana hela ya mafuta kama Waziri. Mawaziri ni majipu makubwa zaidi kuliko hao watumishi wenye mishahara miwili.
Nashauri anza na mawaziri kwanza. Wapokee mshahara mmoja tu, posho moja tu, gari moja tu. Asiyetaka ajiuzulu.
Rasimu ya Warioba ilizuia Waziri kuwa Mbunge. Lengo lilikua kupunguza mgongano wa kimaslahi kati ya bunge na serikali, lakini pia kuwaondolea Mawaziri mishahara na posho mbilimbili. Lakini CCM kusikia posho mbilimbili na mishahara miwili-miwili inafutwa wakaitupilia mbali rasimu ya Warioba.
Sasa Mheshimiwa Rais umeacha kuwaona hao unakuja kuhangaika na Mwalimu wa shule ya msingi Vigwaza darasa la 3B anayepokea mishahara miwili ambayo jumla yake haifiki hata posho ya waziri kwa siku moja? U cant be serious brother.
Anza na Mwenge, then futa mikataba yote ya kinyonyaji kama mikataba ya madini na gesi, then pandisha mishahara kwa watumishi wa umma, kisha punguza kiwango cha PAYE kwny mishahara, kisha boresha mazingira ya kazi kwa watumishi, halafu rudisha upya bunge la Katiba na rasimu ya Warioba, ndo uje kwenye mishahara miwili. Na ukifika hapa anza na mawaziri.
Mawaziri wako ndio mabingwa wa kupokea mishahara miwili. Wabane wao kwanza ili waliopo chini washtuke na kuchukua hatua.
Lakini kukimbizana na watumishi wanaojilipa mishahara miwili wakati mawaziri wako wote wana mishahara miwili itz worthless. Ni sawa na kumshangaa mtoto wa jirani yako kunywa "Castle lite" wakati mwanao kalowea kwenye "viroba" na "chang'aa".!!
Malisa GJ.!
 
Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge yo Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 April, 2016 ililitaka Jeshi Ia Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System). Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo Ia kupotosha umma kutokana na kile kilichoamuliwa na kamati hiyo.

Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 April, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi Ia Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine iliona kuna haja ya kupata maelezo ya kina kwa maandishi katika utekelezaji wa mkataba huo.

Kutokana na haja hiyo, kamati ilimwagiza Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.

Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo yo Ndani tarehe 12 Aprili 2016 kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu yo Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprifi 2016 kabla yo tarehe 18 Aprili, 2016 kama ilivyoshauriwa na kamati.

Ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016.

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge

DAR ES SALAAM

15 Aprili, 2016.
Mkiwa waongo muwe na kumbukumbu. Haeshi Hilaly aliongea na kuoneshwa katika television mbalimbali katika taarifa zao za habari,jioni ya siku hiyo.
Ni UPUMBAVU kuendelea kudhani Watanzania ni Walewale wa kudanganywa siku zote.
Kama nanyi hapo Dodoma Akili zimedumaa kwa kula Viwavi, ni heri mkakaa kimya kuliko kutudanganya sisi ambao ndio waajiri wenu!
 
Back
Top Bottom