SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Kama nilivyoandika hapo juu, siwezi kujibu hoja zako kwa sababu hazijakaa katika mpangilio mzuri.

Sorry.
Pole. majibu yangu yote yako kwenye italic, ila pia si lazima ujibu kila nilichosema kwani sio mtihani na bado una kazi kubwa ya kupambana na hoja nyingine humu jukwaani. Unaweza ukajibu post nyingine kwani nazo pia bado zina hoja nzuri tu.
 
igizo limeingia sehemu ya nne
1.Kamati ya PAC kudai Mkataba
2.Kamati ya Mambo ya nje kupewa jukumu la PAC
3.Said Lugumi kutoweka nchini
4.Bunge kudai kilicho takiwa na PAC si mkataba bali Maelezo
5....
5.Mkataba unahusisha chombo cha ulinzi, hauwezi kujadiliwa kwa maslahi ya nchi! I can see another KAGODA is coming
 
upuuzi mtupu. mjiongeze sio kila jambo la kutetea mchana kutwa. kuna mengine ni dhambi na laana.
Ungekuwa ni upuuzi nadhani usingehangaika nao otherwise kama hujitambui! Kwa kukusaidia, upuuzi hupuuzwa.

Kama mimi ninatetea na wewe kwa upande wako unafanya nini kama sio unatetea upande wako mchana kutwa. wewe vipi?

Nadhani huelewi hata mantiki ya ulichokiandika!
 
Aseee inakatisha tamaa sana basi tu!!Hivi sisi Watanzania lini tutaamka?
 
Pole. majibu yangu yote yako kwenye italic, ila pia si lazima ujibu kila nilichosema kwani sio mtihani na bado una kazi kubwa ya kupambana na hoja nyingine humu jukwaani. Unaweza ukajibu post nyingine kwani nazo pia bado zina hoja nzuri tu.
Mimi huwa sina tatizo katika mijadala ya kujenga na siyo mijadala ya kutukanana au kejeli.

Nimekujibu katika msingi wa kiungwana wa sababu nilidhani comment zako niza kiungwana.

Kwa sasa nimeshindwa kuzijibu comment zako kwa sababu zimechanganyikana na comment zangu.

Ziweke katika hali nzuri na nitatoa mtazamo wangu.
 
Kwa kauli hii bunge linapingana na alikisema Mwenyekiti wa PAC kwenye vyombo vya habari.Ni wakati wa kitengo cha habari cha bunge kujitathimini.Wakatafute mahojiano ya Mwenyekiti wa PAC na ITV.
 
Hii nchi bado sana. JPM ana kazi ya ziada. Na sometimes inabidi avae nguo za kijani tu haina jinsi.
Hata hili nahisi atavaa suti ya kijani tu.
 
Sorry siwezi kujibu hoja zako kwa sababu hujazipangilia vizuri!
nilikujibu chini ya aya ulizokuwa unajibu. ila kwa sasa nimejaribu kufuta quote zako nimebakiza majibu yangu kwa quote zako tu. Kama unadhani wangalau italeta mantiki unaweza kutoa pia mtazamo wako, kama bado basi usijali tutakutana tu kwenye mijadala mingi hapa jukwaani wakati tunapiga siasa.
 
Nimemsikia zaidi ya mara moja makamu m/kiti wa hiyo kamati akizungumzia kuletwa mkataba, sasa naona huyu Ndugai kaja na yake. Tutarajie mengi ya ajabu toka kwa huyu spika. Kwanza alipinga kuhusu rushwa kwa wabunge, muda mfupi baadae wakapandishwa kwa pilato, sasa amekuja na hili...
 
Tangu mwanzo tulijua hakuna kitu bali mchezo wa kuigiza tu hapo. Huwezi kulikata tawi ulilokalia wakati chini amekaa simba hata kama umekutana na manyigu humo. Kitwanga hatwangiki
 
PAC wanajipa madaraka ambayo sio yao...hawana mamlaka ya kukagua mikataba bila idhini ya wahusika

Haya ni maajabu ya ulimwengu!! Sasa kama kamati ya bunge haina madaraka ya kuitisha mkataba, ambao dhahiri tena bila chenga wala mawaa ni wa KIFISADI, basi tutegemee washuke MALAIKA mbinguni kuitisha hiyo mikataba. Yaani mtu kavuta mpunga wooote...kazi kafanya kiduuuchu...halafu badala ya kuisapoti kamati ili peas yetu irudi mtu anakuja na kauli kama hizi dah...
 
Mimi huwa sina tatizo katika mijadala ya kujenga na siyo mijadala ya kutukanana au kejeli.

Nimekujibu katika msingi wa kiungwana wa sababu nilidhani comment zako niza kiungwana.

Kwa sasa nimeshindwa kuzijibu comment zako kwa sababu zimechanganyikana na comment zangu.

Ziweke katika hali nzuri na nitatoa mtazamo wangu.
Mkuu tindo kajibu hoja zako vema tu
Ningependa nielewe katika suala hili, nini hasa utetezi wako? Kumbuka tumelizungumza sana hili na rekodi zipo zikibadilika kila baada ya taarifa mpya.

Sasa tuweke rekodi sawa ikiwemo ya kwangu

1. ' Kwa Lugumi lipo jambo linafichwa' nilitoa sababu, naamini serikali inaficha jambo

2. Rekodi yako ni ipi?

Mkuu nchi haijengwi katika utetezi wa uovu. Rais anapoomba ushirikiano kupambana na maouvu anategemea kusikia pande zote. Kitu kinatochotuunganisha ni sisi sote kuwa waathirika wa uouvu uliokithiri nchini.

Labda nikuulize, wale wanaosema lipo tatizo wakalionyesha wamekosea wapi?

Katika hili la Lugumi ukweli tu na si kingine ndicho kinahitajika.

Mnaweza kufanya spinning kama za kashfa nyingi zilizofukiwa katika mazulia kwa udanganyifu huu huu mnaoendelea nao. Mtafanikiwa kwa muda, baada ya hapo ni tatizo

Tunaposikia viongozi wakisema wanapambana na rushwa, hatuangalii macho yao, tunaangali mboni za macho yao kwanini zinatueleza zaidi ya kile kilicho moyoni.

Hili la Lugumi halipo katika macho lipo katika mboni za macho yao , tunaliangalia

Utamaduni wa kuindana na spinning si mgeni, na ni mjinga pekee asiyeelewa hili.

Huu ni utamaduni wa CCM na serikali zake. Utamduni wa rushwa na ufisadi.

Pengine hatutaweza kubadili utamaduni wao katika nyoyo zao ,haituzuii kusema miaka 10 iliyopita inarudi kwa kasi, ari na nguvu mpya. Lugumi imefungua pazia

Tunaanguka kama taifa, na wale waliowekeza matumaini wana maradhi ya moyo.
Bora ya wale walioamini hakuna kipya ni mvinyo ule ule katika chupa mpya

Presha zinawapanda na hasira zinawajaa wakijua kumbe hakuna chochote ni kile kile

Viongozi watawaangaliaje wananchi siku wanapozungumza nao?
Pengine kwa macho, mboni za macho yao zikiwasuta! hawataeleweka, watajawa na hofu.

Hata wakishangiliwa nafsi zao zitawasuta tu, watahisi kuzomewa kwasababu ukweli upo katika nyoyo zao ingawa wanaukana kwa matendo yao!

Wanaukana ukweli kwa udanganyifu , nafsi zao zinajua na zinawasuta!

Bila Lugumi kuwekwa wazi , mboni za macho yao hazitasafishika
 
bunge limechukua nafasi ya mahakama hapo...kuna siku yatakuja majibu hakuna wafanyakazi hewa ulikua ni mfumo mbovu wa kujichanganya tuu tumegundua hayo mapungufu sasa...tutaelewa tuu.
 
Back
Top Bottom