SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

No way.....jamani tuhurumieni hata sisi tumesoma na tuna akili.Tumemsikia msaidizi wa M/kiti live.Tumuogope Mungu...
 
Hiyo issue ngumu kwa mtumbua majipu, anaikimbia kwa njia tofauti, mwenye akili na afahamu
 
Mkuu tindo kajibu hoja zako vema tu
Ningependa nielewe katika suala hili, nini hasa utetezi wako? Kumbuka tumelizungumza sana hili na rekodi zipo zikibadilika kila baada ya taarifa mpya.

Sasa tuweke rekodi sawa ikiwemo ya kwangu

1. ' Kwa Lugumi lipo jambo linafichwa' nilitoa sababu, naamini serikali inaficha jambo

2. Rekodi yako ni ipi?

Mkuu nchi haijengwi katika utetezi wa uovu. Rais anapoomba ushirikiano kupambana na maouvu anategemea kusikia pande zote. Kitu kinatochotuunganisha ni sisi sote kuwa waathirika wa uouvu uliokithiri nchini.

Labda nikuulize, wale wanaosema lipo tatizo wakalionyesha wamekosea wapi?

Katika hili la Lugumi ukweli tu na si kingine ndicho kinahitajika.

Mnaweza kufanya spinning kama za kashfa nyingi zilizofukiwa katika mazulia kwa udanganyifu huu huu mnaoendelea nao. Mtafanikiwa kwa muda, baada ya hapo ni tatizo

Tunaposikia viongozi wakisema wanapambana na rushwa, hatuangalii macho yao, tunaangali mboni za macho yao kwanini zinatueleza zaidi ya kile kilicho moyoni.

Hili la Lugumi halipo katika macho lipo katika mboni za macho yao , tunaliangalia

Utamaduni wa kuindana na spinning si mgeni, na ni mjinga pekee asiyeelewa hili.

Huu ni utamaduni wa CCM na serikali zake. Utamduni wa rushwa na ufisadi.

Pengine hatutaweza kubadili utamaduni wao katika nyoyo zao ,haituzuii kusema miaka 10 iliyopita inarudi kwa kasi, ari na nguvu mpya. Lugumi imefungua pazia

Tunaanguka kama taifa, na wale waliowekeza matumaini wana maradhi ya moyo.
Bora ya wale walioamini hakuna kipya ni mvinyo ule ule katika chupa mpya

Presha zinawapanda na hasira zinawajaa wakijua kumbe hakuna chochote ni kile kile

Watawaangaliaje wananchi siku wanapozungumza nao?

Pengine kwa macho, mboni za macho yao zikiwasuta! hawateleweka, na watajawa na hofu. Hata wakishangiliwa nafsi zao zitawasuta tu, kwamba wanazomewa kwasababu ukweli upo katika nyoyo zao ingawa wanaukana kwa matendo yao!

Ufafanuzi murua sana huu, ngoja tumuone akija kama atakuwa na majibu ya msingi au kupiga siasa.
 
Nilikuwa na Imani na hii serikali ya awamu ya tano. Lkni, kama ni asilimia sasa zinazidi kupungua toka 95% hadi 50%. Ngoja tusubiri kitakachoendelea.


Wakamwambia, "Bwana,Yohana ametutuma kwako tuje tukuulize, Je wewe ni yeye yule tuliokuwa tukimsubiria au tumngoje mtu mwingine?" akawaomba wampatie maji anywe. Naye alipomaliza kunywa, akawatazama, akawajibu akisema....."Kamwambieni Yohana yale mnayo yaona ninyi wenyewe..viwete wanatembea, vipofu wapata kuona tena."HERI MTU YULE ASIYE NA MASHAKA NAMI"

mbarikiwe wana JF
 
Na chama chetu Pendwa CCM ...aiseee

Cha kushangaza hawamkamati hata Lowasa
Mnapotafuta mileage za kitoto kupitia matukio kama haya wengine tulishachoka haya ...hapa tunazungumzia ufisadi ...mkileta uchadema na uccm wenu mnaishia kuwasaidia CCM kuhamisha mjadala na kuanza kuwajadili akina EL , yule mbunge aliyepita wa segerea n.k ...hatuwezi kuwatandika CCM kwa uhakika kama zamani ...tuzungumze ufisadi na jinsi danadana zinavyopigwa ....uvyama ni upuuzi tu ...
 
nilikujibu chini ya aya ulizokuwa unajibu. ila kwa sasa nimejaribu kufuta quote zako nimebakiza majibu yangu kwa quote zako tu. Kama unadhani wangalau italeta mantiki unaweza kutoa pia mtazamo wako, kama bado basi usijali tutakutana tu kwenye mijadala mingi hapa jukwaani wakati tunapiga siasa.
Mbona bado vivyo hivyo.

Jaribu kupitia tena kama unataka nijibu hoja zako.
 
Ni dhahiri Ndugai anataka kuligeuza bunge kama pango la kufichia mafisadi! Hii ni aibu
 
PUMBAVU KATIBU WA BUNGE!!

Ujinga huu waelezeni CCM std 7 failure. Magazeti yamepiga simu , yameoji yaliojiri na wahusika kukiri kuombwa Mkataba, na waulete ndani ya siku 3!! kupitia Ofisi ya Bunge.
Narudia tena!!

Bunge nalo limegeuka uchi wa Bumbuzi!! Uko nje nje!!

Mkuu taratibu Mod wanaweza kukulima ban,kifupi viongozi wa nchi hii wana raha sana hasa aina ya wananchi wanao waongoza.Mtu mmoja au zaidi anaweza kuchota fedha za walipa kodi na asiguswe na yeyote yule..Tulishazisikia kauli zao za kejeli kwa wananchi "Hivi ni vijisenti tu"
"Milioni kumi ni pesa za mboga tu"

Na Watanzania wametulia tuli,wachache wenye uthubutu wanaishia kukemea tu ...Leo Bunge linalotakiwa kuwatetea wananchi limekuwa ni chombo cha kula na wanyang'anyi sahani moja!?
 
Sasa mbona ile taarifa ya magazeti ambayo haikukanushwa kuwa walipelekewa akina Adadi Rajabu iliongelea mkataba na sio maelezo ya utekelezaji wa mkataba!?
Tuweni wakweli tupunguze laana na dharau kwa nchi yetu na wananchi wake nje ya mipaka na hata ndani.
Kama mtu kakuibia na huwezi kumfanya lolote kwa nini asikudhalau kukudhihaki na hata kukudunda
 
PAC wanajipa madaraka ambayo sio yao...hawana mamlaka ya kukagua mikataba bila idhini ya wahusika
Wanataka maelezo ( kwa maandishi ) kuhusu utekelezaji wa mkataba na si kukagua mkataba wenyewe. Kwa lugha nyingine utekelezaji wa mkataba ndo mkataba wenyewe ndugu yangu
 
Double standards at its best.

Wengine wanafukuzwa na kusimamishwa papo hapo tena kwa ziara za kushtukiza wakati wengine wanaombwa kwa kupewa muda wa kutosha kupeleka mikataba.

Mimi naamini JPM kama ataendelea na hizi double standards basi hataisaidia hii nchi. Kama ameamua kuisiadia hii nchi ni lazima kwanza asimpendelee wala kumuonea yeyote ili ile 'mindset' anayodai haijabadilika ubadilike.
 
Kama kweli taarifa hii imetolewa na bunge basi ni vyema makamu mwenyekiti wa kamati ya PAC akaenda kwenye tv station kuomba radhi. Kwa sababu ktk luninga tuliona wote Aeshi akiongea tena kwa kituo. Mbona bunge la Ndugai linaanza kuonyesha udhaifu mkubwa mapema hivi kweli litaweza kuisimamia serikali.
Mkuu,watu waliyasema haya kitambo.Mafisadi wa nchi hii hawaguswi kiurahisi
 
serekali ya maigizo na series. kwa mwenye akili hawezi kuwa na matumaini nayo wala kushabikia.
 
NAOMBA TUMWESHIMU MUNGU RANGI NYEUPE IBAKI KUWA NYEUPE. UKIPEWA HESHIMA NA MUNGU KUJUA HII RANGI NI NYEUPE NA WEWE UKASENA NI BLUU UNAONYESHA KUTOMTHAMINI MUNGU ALIYEKUPA NEEMA YA KUWA NA UFAHAMU. USHAURI WANGU NI HUU MSIWAHESHIMU WANADAMU KWA KUWAFURAHISHA KWA YALE WANAYOYAPENDA HALI MKIJUA SIO NA HIVYO MKAMDHARAU MUNGU. BARIKIWA.
 
Back
Top Bottom