SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Sijui nichangie nini,mana hapa tunatafutwa sana tunaopinga ufisadi wenyewe
 
Usihoji haya ni masuala ya usalama wa taifa tehteh
Nchi itatetereka
 
 
Siko katika position ya kujua kama bandiko hili ni la kweli au sio la kweli(mtandaoni lolote linawezekana,ila kuna spelling mistakes hapo ambazo zinashusha status ya thread yenyewe:
1.yo hesabu=ya hesabu (paragraph ya kwanza)
2.mambo yo ndani=mambo ya ndani (paragraph ya nne)
 
Bunge lenye meno kibogoyo tumemsikia Aishi siku tatu mfululizo akitolea maelezo mkataba upelekwe ha ha magufuli chali hawezi kutumbua jipu la katikati ya matako
Hahaaaaaa, duh .....
 
Sasa napata picha, ni kwa nini Bunge limekataa kuonyeshwa LIVE.

Kama hata Katibu wa Bunge ameshinikizwa kutoa Press release ya kumkingia kifua UNTOUCHABLE Lugumi, basi mjue aliye nyuma ya Lugum siyo mtu mdogo bali ni kigogo mkubwa kabisa ambaye ana impunity, ambapo hawezi kushitakiwa na mahakama yoyote hapa nchini.
 
Mbona ukanushaji huu umekawia sana? Si bure!
Halafu umelenga kusingizia vyombo vya habari

Ukanushaji umechelewa kwasababu walikuwa 'maabara' wakitafuta namna ya kutoka

Umesahau watuhumiwa wa rushwa walivyoitwa 'mabadiliko ya kawaida' na Spika
Nchi hii wamezoe kuishi kwa uongo , udanganyifu ulaghai. Hizi ni tamaduni zao lakini Lugumi ita define kila kitakachokuja

Spika kimya, katibu wa bunge kimya! Lugumi ngoma nzito bwana!!!

Ni kuficha ukweli tu. Huwezi kupata maelezo bila kuwa na mkataba.
Hata uongo sasa unakuwa tatizo nchini na mafundi wanafilisika !

LUGUMI na Serikali ya awamu ya tano ni pacha, na wataishi nalo hili kila asubuhi
 
Hivi serikali na bunge la Tanzania vinamlinda nani ? ni nani hasa anayewekewa uzio ili mkataba wake usionwe na mamlaka halali za nchi hii ? haya yanafanyika kwa faida ya nani ?
 
Hakuwezi kuwa na maelezo ya kina bila ya msingi wa maelezo ya kina. Msingi wenyewe ndio huo mkataba.

dah! we acha tu, sijui kwa nini tunakubali kuongozwa na watu ambao capacity yao ya kufikiri ndio hii.
 
Mkuu, nimesema huko nyuma kuwa filimbi zimekuwa nyingi sana kuhusiana na hili suala kiasi kwamba hata ukweli kwa sasa haujulikana ni upi.

Mbaya zaidi bunge letu limejaa wala rushwa na kwa msingi huo, ni vigumu sana kupata ukweli.

Waandishi wa habari pia wanatanguliza matumbo yao badala ya maadili ya kazi zao.
 
jipu limegeuka jiwe kudadeki ! usaha hamna , damu hamna !
 
 

Attachments

nguvu zote zimeniishia yaani mbuge Aeshi tumuone kwa macho yetu akidai performance report ya mkataba pamoja na nakala ya mkataba leo mseme huo ni uzushi kweli hili sakata ni jipu lililokaa sehemu mbaya ukilitumbua hakika utakufa na lugumi ni kampuni toka sayari ya mars
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…