Sakata la mabasi na malori bado bichi.. Halihitaji maamuzi ya zimamoto

Sakata la mabasi na malori bado bichi.. Halihitaji maamuzi ya zimamoto

Stand ya Mbezi ni ndogo kuweza kuhudumia wasafiri wote nchini
Aliyedesign Ile stand sijui alikuwa na akilia gani, kale ka stand ni kadogo mno, space imebana Sana, yaani Abria mnajazana hapo magari kupishana ni mtihani mno
 
Stand ya Mbezi ni ndogo kuweza kuhudumia wasafiri wote nchini.. Lakini pamoja na udogo wake haijazingatia mambo mengi ya msingi
Huduma nyingine za usafiri kama daladala zilipaswa kuwepo hapo hapo
Ukishuka pale ukiwa na begi zito cha Moto unakuta, kwa kuwa stand iliamuriwa kujengwa nje ya Mji, basi Eneo ulipaswa kuwa kubwa la kutosha kuwe na Feeders roads in and out za Mkoa na za Mjini.

Ndio Maana Ubungo ilikuwa nzuri na rahisi
 
On serious speaking...! Tanganyika inapitia kipindi kigumu mno! ILA yana mwisho..!
Mwisho wake siuoni kwa hizi siasa za kila mmoja anataka aonekane anafanya jambo zuri, akifanya mwenzake hata kama ni zuri atapinga na kuongea kupotosha kisa tu sifa zitakuwa za yule si zake. Akija kushika yeye madaraka kizuri alichoanzisha mwenzake, atakiacha au kukisiliba matope aje kuanzisha chake

Watu wanapambania kujenga legacy zao kuliko taifa.



Tutasubiri sana
 
Swala la mipango miji tulishafeli miaka mingi, hakuna kurudi nyuma.😭
Swala sio mipango miji, suala ni utekelezaji wa hiyo mipango miji.Ramani zipo, miongozo ipo:Watwndaji wenye kufuata hawapo...Ndo maana open spaces zinaisha zote, watu wanalalamika, lkn kimya.Mfano watu wamelalamikia biafra pale-lkn ndo kwanza show rooms zinatililika
 
Haya mambo yamekaa shaghala baghala mpaka basi. Kila upande ukisikiliza hoja zao unaona kabisa zina mantiki! Yaani kumwambia abiria atoke Kigamboni au Chanika, aje mpaka stendi ya Mbezi kupanda basi isiku huku kukiwa hakuna usafiri wa uhakika na nafuu wa kumfikisha; na wenyewe ni usumbufu!

Wakati huo huo unakuta kuna mabasi yalikuwa yanafuka mpaka huko Kigambo ma Chanika kuwachukua/kuwafikisha hao abiria!! Ni hivyo hivyo kwa abiria wanaopandia Shekilango na wenyewe walipunguziwa usumbufu kwa sehemu kubwa!

Serikali inatakiwa iache ubabe, na badala yake itafute njia sahihi za kuondokana na huu mzozo. Wasilasimishe wamiliki na abiria kutumia stendi ya Mbezi, huku kukiwa hakuna miundombinu rahisi, nafuu na ya kisasa ya kuwasaidia abiria kufika/kutoka huko Mbezi kwa wakati.
 
Mtu anaekuja na porojo za stendi ya MAGUFULI ni ndogo

Namuona poyoyo wa grade A+ hivi nani kasema hiyo stand n ndogo?

Mnataka mgeuze STAND kuwa PARKING kama mabus ni kupakia na kuondoka iyo stand udogo wake unatokea wapi?

Pakia/Shusha abiria ondoa gari peleka kalaze unapolaza bus lako asubuhi lete gari...

Hiyo ni stand na wala sio PARKING ya MABUS kama ambavyo mnaoleta hoja za stand ni ndogo.

Kero kubwa ya MAGUFULI ni ofisi za kukatia ticket hazionekani

Mtu ukifika maduka ya nnje yote wamepewa vinyozi na mawakala wa pesa na wauza maduka wengine, mgeni kuingia ndani atafute ofisi za bus flan inachosha ki ukweli... frem za nnje zote wangepewa wenye mabus na sio wafanyabiashara wengine shida stand imegeuka sehemu ya watu kujilia kodi za kila mwezi.

Watu wana frem wameweka kamishen zao za juu kila mwezi hela zinaingia...

STAND YA MABUS ya MAGUFULI INATOSHA PELEKENI MABUS NDANI.

ABIRIA NA NYIE ACHENI UVIVU, MNALALAMIKA ni mbali kwani mnasafiri kila siku? Wanaotumia airport nao wasemeje???
Hizo frem za maduka ni maslahi ya wanaoiongoza stendi kwa sasa, na ni baada ya kuona basi hazifungui ofisi ndio maana wakajibinafsishia hizo sehemu, kweli kabisa kila mwenye basi anapashwa kuwa na maegesho/karakana ya kuyahifadhi/matengenezo magari yake Stendi ni mahala pa kupakia na kutoka mara moja. Ukiingia kule chini stendi utakuta kuna maduka ya wauzaji oil na mabasi yanatengenezwa huko huko. jambo la hatari ni lengo lilikuwa nini na kwanini tulishindwa kulifwata na kwanini tuanze mbio mbio kwa sasa.
 
Back
Top Bottom