Sakata la mawakala wa mizigo: "Mwanamfalme" amtishia kiongozi mwandamizi wa mawakala 'clearing'

Phillemon Mikael

Platinum Member
Joined
Nov 5, 2006
Posts
10,557
Reaction score
8,673
Wakati hali ya biashara maeneo ya kariakoo imeingia kwenye mgogoro mkubwa ...imedhibitika kuwa chanzo ni kusitishwa shughuli za zile kampuni ya "baba,mama na mtoto"....kampuni hizo zilikuwa zikiwachangisha wafanyabiashara wa kariakoo kiasi cha shilingi milioni 10 hadi 20 ..kadiri ya ukubwa wa kontena ..bila kuzingatia mizigo iliyo ndani...wakati katika hali ya kawaida wafanyabiashara ambao hawatumii kampuni hizo ambazo mizigo yake ilikuwa haikaguliwi ....walikuwa wakilipa wastani wa shilingi milioni 20 hadi 40 kwa kontena.
Kampuni hizo za baba ,mama na mtoto zilikuwa zinalipa kodi milioni 6 hadi 10 kwa kontena ..na kufanya wapate faida ya shilingi milini 10 kwa kila kontena walilokuwa wakitoa kwa kipindi cha miaka takribani sita ambayo wamekuwa wakiliibia taifa .....Kwa wastani kila mwezi kampuni hizo zilikuwa zikitoa Containers 400 hadi 800.......!!!...HII NI WASTANI WA FAIDA YA BILIONI 4 HADI 8 KWA MWEZI KWA MIAKA 6......NA SERIKALI ILIKUWA IKIPOTEZA ZAIDI YA BILIONI 10 KILA MWEZI ...
Imefikia mahali kampuni hizi zimefungua uwakala wa kukusanya mizigo ya wafanyabiashara nchi..huko nje na kufanya consolidation na kukusanya mapato..kinyume cha sheria!!!!

BAADA YA MALALAMIKO KUZIDI WIKI HII TRA WAMEAMUA KUICHUKULIA HATUA KAMPUNI HIZO .......HALI ILIYOSABABISHA TAHARUKI NA KUMFANYA PRINCE AMTISHIE ..KUMNGOA KUCHA KATIBU WA CHAMA CHA MAWAKALA WA MIZIGO NCHINI...AMBAYE TAAYARI AMESHATOA MAELEZO KWA NDUGU ,JAMAA NA MARAFIKI NA MAMLAKA HUSIKA IKIWA KAMA TAHADHARI...KWA KUHOFIA YALIYOWAKUMBA WATU WALIOPINGANA NA KAMPUNI HIZO ...AKIWEMO KAMISHNA MMOJA ALIYEFARIKI KATIKA MAZINGIRA INAYOHISIWA KULISHWA SUMU .......KWA KUIBANA SANA KAMPUNI HIZO WAKATI ZILIPOKUWA ZINAANZA KULIIBIA TAIFA.

KAMPUNI HIZO ZINALAUMIWA KWA KUFANYA MAWAKALA WENGINE WOTE WANAOKARIBIA KUFIKA 400 WALIOPO DAR PEKEE WANAOAJIRI ZAIDI YA WATU 4,000 WASHINDWE KUFANYA BIASHARA ....KWA KUWA BIASHARA ZOTE SASA ZINAFANYA KAMPUNI ZA BABA MAMA MTOTO......

MALALAMIKO YA KARIBUNI YANAYOTOKEA KARIAKOO NI BAADA YA WAFANYABIASHARA WALIOKUWA WAMEMPA TENDA KAMPUNI HIZO ZILIZOWEKEWA NGUMU NA TRA HIVI KARIBUNI ..KUTAKIWA KULIPA BEI HALALI WAKATI TAYARI WALISHALIPA FEDHA KWA KAMPUNI HIZO.




HABARI MWENDELEZO

BAADHI ya wafanyabiashara katika maduka ya nguo Kariakoo jijini Dar es Salaam wameendelea kulalamika, pamoja na kuelezwa kuwa suala lao la kucheleweshwa mizigo yao Bandarini linashughulikiwa na serikali.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini leo, wamesema 'kuwa hadi sasa hawajui kilichongumzwa kwenye kikao kilichowahusisha Waziri wa Fedha, Mkuu wa Mkoa, Kamishna Mkuu wa TRA, Kamanda wa Kanda Maalum na Mwenyekiti wao wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo'.


Mlalamiko yao yote wanayalekeza kwenye Kampuni ya Limited ambayo ndiyo iliyokuwa wakala aliyekuwa akiwaingizia mizigo yao kutoka katika baadhi ya nchi za Asia.


Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Masao alisema wakala huyo ameshindwa kutekeleza makubaliano yao ya awali ya kupakuwa mzigo huo kwa zaidi ya miezi minne sasa hali inayowaweka katika wakati mgumu ambao unawafanya waingie kwenye mgogoro mwingine na taasisi za fedha kwa kushindwa kulipa mikopo waliyokopa.


“Unajua kuna siri ambayo tumeipata tunasikia kuna baadhi ya Kampuni wakati kabla ya Waziri Mwakyembe kupewa Bandari kulikuwa na mchezo kwa baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wakiingiza makontena ya nguo kama vile vitenge lakini wakijidai yamefungasha mzigo kama sidiria, tai, saruji vitu ambavyo kodi yake iko chini wakati wakijua fika wanaibia serikali”alisema Masao.


Masao alisema ugumu wa upakuzi wa mizigo yao iliyokuwa ikiingizwa na kampuni hiyo ulianza mara Waziri wa Uchukuzi, Harryson Mwakyembe alipokabidhiwa waizara hiyo.


Alisema waziri huyo ambaye kutokana na dhamana aliyopewa ilimfanya aweze kubadili uongozi wa Bandari ambao ulikuwa ukidaiwa kujihusisha kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara katika kukwepa kodi.


Mwenyekiti wa Umoja huo, Mathias Makoi, akitolea ufafanuzi malalamiko ya wafanyabiashara hao, kwanza alikiri kukwama kwa makontena hayo Bandarini.


Hata hivyo, alisema katika kumaliza tatizo hilo hivi sasa wako kwenye mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mkurugenzi TRA ambapo mazungumzo hayo yamefikia hatua nzuri.


“Hivi sasa mazungumzo hayo yanaendelea na suala hilo liko kwa mkuu wa mkoa na Kamanda wa Polisi bila ya kufafanua.


“Hapa lilipo tumefikia panatosha na wala hatutaki liandikwe tena kwenye vyombo vya habari, na hatutaki kuyavuruga mazungumzo hayo”alisema Makoi.


Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Limited aliyejitambulisha kwa jina la Haleem, alikubali kuchelewa kwa mizigo hiyo lakini kilichosababisha hali hiyo ni mabadiliko ya viwango vya kodi ambavyo hivi sasa vimepanda ukilinganisha na awali.


“Kodi imeongezeka, fikiria kama mwanzo ulikuwa ukilipa sh 2000 ghafla unaambiwa ulipe sh 5000 ni lazima kwanza uanze kujipanga upya hata hvyo tunajadiliana na wafanyabiashara hao kuona ni jinsi gani tunaitoa mizigo hiyo”alisema.


Kuhusu kikao cha Waziri Dk. Mgimwa, Kamishna wa TRA, Mkuu wa Koa Sadik, Kova pamoja na Mawakala, kilikuwa ni kwa ajili ya kujadili jinsi ya kuboresha utendaji ambao wanadhani utachochea kasi ya upakuaji wa mizigo bandarini hapo na si kujadili makontena yake kama ilivyodaiwa na baadhi ya wafanyabiashara
 
Weka wazi mkuu, unafichaficha nini? Mwanamfalme nani?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

R1 mtoto wa bwana dhaifu chini ya kivuli cha ile kampuni ya mwarabu aliyeua mtu Kariakoo kwa kumpiga risasi na kesi ikaisha hivi hivi.
 
Good! Sasa jee! Unajuwa ndugu watu wanatumia vyeo vya ndugu zao, baba zao kufisadi nchi hii. Huyo mbona anaonekana njoo kwa hawa wa chini sasa kama makatibu wakuu ndiyo usiseme! Tanzania hii!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Lakini yana mwisho. Remember even the longest hour is sixty minutes.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Unaficha ficha wkati hili linajulikana wazi. Kampuni hiyo inaitwa Silent Haulage na inaongozwa na Ghalib. Offcourse Riz one na Mshua na wenye share jamaa anasimamia. Wamewaibia sana Watanzania hawa kwa kufanya under declaration na false declaration ya mizigo wLiyokuw wanaingiza na mizigo yao ilikuwa haikaguliwi. Tulioenda China na kuleta mizigo tunajua jinsi ambavyo mizigo ilivhokuwa inatoka mapema.

Suala hili linatakiwa lisiishie hapo tu, maafisa wa TRA wanatakiwa kuwajibishwa kwa kutofanya ukaguzi wa mizigo inapoingia ili kuthaminisha kodi sahihi ya kulipa.

Hii nchi haiishi vituko.
 
Kampuni hizo zilikuwa chini ya HOME SHOPING CENTRE walikuwa mstari wa mbele kusaidia wahanga wa mafuriko wakifanya ile SCR
 
Ndugu zangu hawa jamaa wameitafuna hii nchi kwa
muda mrefu sana na kabla ya Dar mwaka 2003 walikuwa wanautumia mpaka wa Holili na hasa bandari ya Mombasa na baada ya kuiba vya kutosha na mpaka wa holili kustukiwa waliamua kurudi dar na kuitafuta network ya
 
usishangae kuambiwa huyo aliezuia makontena hana akili nzuri, hivyo yupo mhimbili amelazwa kwa magonjwa ya akili..!!!
 
Ndugu zangu hawa jamaa wameitafuna hii nchi kwa
muda mrefu sana na kabla ya Dar mwaka 2003 walikuwa wanautumia mpaka wa Holili na hasa bandari ya Mombasa na baada ya kuiba vya kutosha na mpaka wa holili kustukiwa waliamua kurudi dar na kuitafuta network ya baba mama na mtoto na ndo utendaji ukanoga
kiukweli hilo pakacha limeshavuja na hakuna nafuu yoyote kwa mchukuzi. huyu jamaa ana akili nyingi kama nyoka ana kampuni za uwakala wa kutoa mizigo zaidi ya tano na hakuna yenye jina lake na pia ana mtandao mkubwa sana anawatumia wabongo na warabu wenzie wenye njaa kama vivuli ktk hizo kampuni na zaidi ukienda ofcn kwake wanaofanya declaration na documentation ni watoto wa watumishi wa TRA na wafanyakazi wa Tra waliofukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali huwapokea oficn kwake hapo samora palipokuwa masjala kuu ya magari zaman amechukua floor nzima
 
Mkuu mwakyembe anajua haya au mawazoi yake ni urais tuu?


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Home shopping centre ngoma inogile .........
 
Unauliza mwakyembe anajua haya wakati yeye ndio mfichua madudu namba moja bandari! We uko wapi hapa pongezi zote kwake kwa kusafisha bandari wengine wote walichemka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…