Sakata la mawakala wa mizigo: "Mwanamfalme" amtishia kiongozi mwandamizi wa mawakala 'clearing'

Sakata la mawakala wa mizigo: "Mwanamfalme" amtishia kiongozi mwandamizi wa mawakala 'clearing'

Rizt One njoo ujibu tuhuma huku, usijifiche! Au unasubiri gazeti la JAMHURI likufute kukuhoji?
 
Mkuu mwakyembe anajua haya au mawazoi yake ni urais tuu? Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Kwenye hili Sakata la mawakala hakuna mtu aliyedharaulika na kuonekana Msaliti Kama Mwakyembe .....Mtakumbuka alipoteuliwa mawakala walishherekea...na kumuomba waonane naye ...na kumpokea kwa heshima Kama.......wakikaa naye vikao Vya Siri na wazi Ikiwemo pale Karimjee..Matokeo yake mpambanaji wa ufisadi Mwakyembe ...alipopewa tuhuma na kukuta zinawagusa direct baba,mama na mtoto...akaanza kuwazungusha mawakala kwa ahadi za uwongo......hadi karibuni uzalendo ulipowashinda...kwa kifupi Mwakyembe kwenye hili amekuwa mpenda sifa na media ..tu hajawasaidia kabisa ...
 
Unauliza mwakyembe anajua haya wakati yeye ndio mfichua madudu namba moja bandari! We uko wapi hapa pongezi zote kwake kwa kusafisha bandari wengine wote walichemka!

mimi nalia tu na nchi yangu iliyouzwa kwa wachina ili kumnusuru riz1 alipokamatwa na madawa ya kulevya china. kuna mikataba ya kipuuzi imesainiwa kimya kimya ambayo hata kuivunja uongozi utakapobadirika itakuwa shughuli pevu. hivi ni kwanini vyombo vya habari vya china viliikosa hii habari mapema? maana ingekuwa imeshatolewa kwenye media nchi yetu isingeuzwa kama ilivyofanyika.
 
Unauliza mwakyembe anajua haya wakati yeye ndio mfichua madudu namba moja bandari! We uko wapi hapa pongezi zote kwake kwa kusafisha bandari wengine wote walichemka!

Meno na kucha zangu jamani.....napita njia tuu hapa
 
ila ndugu sisi sijuwi tukovip kuna billion of $ zina safirishwa kila cku kwa macho makavu kahama leo tuonaona tu apo bandarini kuna msemo usemao sokwe haoni ------ yke
 
Tatizo la kuficha ficha vitu ndo linatucost hapa Tanzania. Mgonjwa anaficha ugonjwa wake, mwenye udhaifu anaficha udhaifu wake, hata mwandishi pia anaficha majina?
Anyway, endeleeni kuficha uchi muone kama mtazaa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Meno na kucha zangu jamani.....napita njia tuu hapa
Nasikia jamaa wanasaka wa kumngoa ivyo vitu umu JF ili iwe mfano......................................... maana mumezidi kuwananga
 
Tusubiri itakaposomwa bajeti ya wizara ya fedha tuone wabunge watachangia nini. Maana hili swala ni zito na lilijulikana muda mrefu likawa linapotezewa. Hata sasa hivi vyombo husika havilipi uzito wake. Uchumi wa nchi unahamishiwa kwa vigogo watu tunabaki tunatoa macho tu kama misukule au tumeshikwa na jinamizi.!
 
HABARI MWENDELEZO

BAADHI ya wafanyabiashara katika maduka ya nguo Kariakoo jijini Dar es Salaam wameendelea kulalamika, pamoja na kuelezwa kuwa suala lao la kucheleweshwa mizigo yao Bandarini linashughulikiwa na serikali.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini leo, wamesema 'kuwa hadi sasa hawajui kilichongumzwa kwenye kikao kilichowahusisha Waziri wa Fedha, Mkuu wa Mkoa, Kamishna Mkuu wa TRA, Kamanda wa Kanda Maalum na Mwenyekiti wao wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo'.


Mlalamiko yao yote wanayalekeza kwenye Kampuni ya Limited ambayo ndiyo iliyokuwa wakala aliyekuwa akiwaingizia mizigo yao kutoka katika baadhi ya nchi za Asia.


Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Masao alisema wakala huyo ameshindwa kutekeleza makubaliano yao ya awali ya kupakuwa mzigo huo kwa zaidi ya miezi minne sasa hali inayowaweka katika wakati mgumu ambao unawafanya waingie kwenye mgogoro mwingine na taasisi za fedha kwa kushindwa kulipa mikopo waliyokopa.


“Unajua kuna siri ambayo tumeipata tunasikia kuna baadhi ya Kampuni wakati kabla ya Waziri Mwakyembe kupewa Bandari kulikuwa na mchezo kwa baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wakiingiza makontena ya nguo kama vile vitenge lakini wakijidai yamefungasha mzigo kama sidiria, tai, saruji vitu ambavyo kodi yake iko chini wakati wakijua fika wanaibia serikali”alisema Masao.



Masao alisema ugumu wa upakuzi wa mizigo yao iliyokuwa ikiingizwa na kampuni hiyo ulianza mara Waziri wa Uchukuzi, Harryson Mwakyembe alipokabidhiwa waizara hiyo.


Alisema waziri huyo ambaye kutokana na dhamana aliyopewa ilimfanya aweze kubadili uongozi wa Bandari ambao ulikuwa ukidaiwa kujihusisha kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara katika kukwepa kodi.


Mwenyekiti wa Umoja huo, Mathias Makoi, akitolea ufafanuzi malalamiko ya wafanyabiashara hao, kwanza alikiri kukwama kwa makontena hayo Bandarini.


Hata hivyo, alisema katika kumaliza tatizo hilo hivi sasa wako kwenye mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mkurugenzi TRA ambapo mazungumzo hayo yamefikia hatua nzuri.


“Hivi sasa mazungumzo hayo yanaendelea na suala hilo liko kwa mkuu wa mkoa na Kamanda wa Polisi bila ya kufafanua.


“Hapa lilipo tumefikia panatosha na wala hatutaki liandikwe tena kwenye vyombo vya habari, na hatutaki kuyavuruga mazungumzo hayo”alisema Makoi.


Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Limited aliyejitambulisha kwa jina la Haleem, alikubali kuchelewa kwa mizigo hiyo lakini kilichosababisha hali hiyo ni mabadiliko ya viwango vya kodi ambavyo hivi sasa vimepanda ukilinganisha na awali.


“Kodi imeongezeka, fikiria kama mwanzo ulikuwa ukilipa sh 2000 ghafla unaambiwa ulipe sh 5000 ni lazima kwanza uanze kujipanga upya hata hvyo tunajadiliana na wafanyabiashara hao kuona ni jinsi gani tunaitoa mizigo hiyo”alisema.


Kuhusu kikao cha Waziri Dk. Mgimwa, Kamishna wa TRA, Mkuu wa Koa Sadik, Kova pamoja na Mawakala, kilikuwa ni kwa ajili ya kujadili jinsi ya kuboresha utendaji ambao wanadhani utachochea kasi ya upakuaji wa mizigo bandarini hapo na si kujadili makontena yake kama ilivyodaiwa na baadhi ya wafanyabiashara
ukifuatilia habari za magazetini jana juu ya hili sakati ni kuwa hakuna kodi iliyopanda tangia mwezi wa saba mwaka jana na hata percentage wanazochage ni zile zile na hizi ni kauli za kujinusuru inavyoonekana. Kuna watu wengi wamepoteza mizigo iliyo chini ya TRA kwa makosa madogo madogo sana lakini hawa jamaa ni wazi wana nguvu kubwa ya ushawisi maana wanapewa nafasi za majadiliano wakati sheria ziko wazi.
Kuna majina ambayo naanza kuyaona kama yalivyowekewa red yanayoonyesha wazi kuwa hili suala litaisha juu kwa juu. Ngoja tusubiri na tutaona

 
Udaku jazz band: hivi wewe Mikael P Aweda pale mlimani ulisomea umbea; porojo na udaku? siasa imekushinda naona umejikita kwenye majungu hata unachokiandika unakielewa mwenyewe hizi njaa mmekosa namna nyingine ya kuzitibia?

Chama
Gongo la mboto DSM
CC Ritz
 
Last edited by a moderator:
Udaku jazz band: hivi wewe Mikael P Aweda pale mlimani ulisomea umbea; porojo na udaku? siasa imekushinda naona umejikita kwenye majungu hata unachokiandika unakielewa mwenyewe hizi njaa mmekosa namna nyingine ya kuzitibia?

Chama
Gongo la mboto DSM
CC Ritz

Mikael huyu umemshika Masaburi!
 
Udaku jazz band: hivi wewe Mikael P Aweda pale mlimani ulisomea umbea; porojo na udaku? siasa imekushinda naona umejikita kwenye majungu hata unachokiandika unakielewa mwenyewe hizi njaa mmekosa namna nyingine ya kuzitibia?

Chama
Gongo la mboto DSM
CC Ritz

942515_617153594963121_1994579558_n.jpg


Tunasubiri maisha bora acheni kujineemesha na keki ya Taifa wenyewe
 
wakisimama kwenye majukwaa ni "hakuna mbadala wa amani" nyuma ya apazia wanapora tuwaombee yawakute yaliyomkuta gadafi na familia yake
 
Rushwa na ufisadi vimeota mizizi kiasi kwamba sijaona bado mwanasiasa Tanzania atakayeweza kuzitokomeza peke yake.

Wenye uwezo wa kutokomeza rushwa na ufisadi siyo wanasiasa bali ni wananchi peke yao. Mpaka hapo wananchi watakapoona na kuguswa na madhara ya rushwa na ufisadi ndipo watakapopata msukumo wa kupambana nayo. Kwa sasa wananchi wamewaachia hiyo kazi wanasiasa peke yao kwa vile wanasiasa kwa kutaka kupewa kura, wanajinadhibisha na kujipiga kifua juu ya majukwaa ya kisiasa kama wataweza kuyaondoa haya madudu nchini.

Wananchi wako HAPPY kabisa kulipa undervalued fees kwa import wanayoifanya au kulipa rushwa ili wapate huduma kwa haraka bila kujiuliza madhara yake kwa Taifa. Hii inatokana na fikra au mtazamo kwamba, swala la mapambano ya rushwa na ufisadi haliwahusu wao.

Ukisoma mabandiko hapa, utagundua kuwa, hizi kampuni watu walizijua muda mrefu kama zinaibia taifa pesa na wengine wameisha fanya nazo biashara ya kuliibia taifa pesa lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kunyosha kidole.

Ukosefu wa investigative journalist Tanzania nako kunachangia sana kuendelea kuwepo rushwa na ufisadi wa waziwazi. Kwa habari za udaku tunaongoza.

Kwani kazi ya kupambana na ufisadi na ruswa bandarini niya Mh. Mwakyembe peke yake?.
 
Alisema waziri huyo ambaye kutokana na dhamana aliyopewa ilimfanya aweze kubadili uongozi wa Bandari ambao ulikuwa ukidaiwa kujihusisha kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara katika kukwepa kodi.

Bandari wanatoza kitu kinaitwa port charges na sio kodi, masuala ya kodi yanasimamiwa na TRA. Mwakyembe ni waziri wa uchukuzi hasimamimi kodi masuala ya kodi yapo chini ya Wizara ya Fedha.

Hivi ninyi Bavicha kila uchao mnazusha uongo na ku spin mambo ambayo hata darasa la saba hawezi kuyakubali.
 
usishangae kuambiwa huyo aliezuia makontena hana akili nzuri, hivyo yupo mhimbili amelazwa kwa magonjwa ya akili..!!!

Duh! Hii nayo Kali, umenikumbusha afande Advera Senso
 
Back
Top Bottom