Wanapitia kwa wanawake kwa kua ni wepesi kuhadaika jamani tusiangalie tu swala la jamaa kubaka naamini kua kuna sababu za kutosha tu.
1. Kitendo cha mke wako kutokusikiliza tayari hiyo kwake ni failure maana jamaa alimkatalia Frola kwenda nchi za nje kwa udhamini wa mchungaji wake lakini kihelehele chake akafanikisha kinguvunguvu,tambueni tupo ktk ulimwengu wa utandawazi imagine jamaa kapata taarifa za mkewe kua mahusiano na mchungaji yamekua ya karibu sana AFANYEJE.
2. Kumwacha mme wako na kuzunguka na mchungaji nchi nzima kwa kipindi kirefu Bwana Emmanuel nafasi yake iko wapi?
3. Haya makanisa nahisi kuna kitu hakijakaa sawa maana ktk eneo dogo nnaloishi ndoa nyingi zinayumba maana yanaingiza imani na matendo ambayo siyo wao huambiwa kua chochote kby kitokeacho ni pepo bila kutambua kua elimu ilisisitizwa hata kwy BIBLE, fikiria mtu huyu kakuta remote ya TV yake imebonyezwa na watoto PA IPO kujua ikajiset kwenye option ya Sleep mode yaani inizime baada ya dkk kadhaa mama mtu ametulia kwy sofa lake akiangalia kwaya Mara TV ikajizima na kuanza kukemea Toka shetani haiwezekani TV ijizime yenyewe kuna mkono wa wachawi humu hivyo lack of knowledge imekua majanga sana kwa waafrika wazungu hawana ujinga huu.majitu yaliyoletewa ndo yanajichanganya kiasi cha kuona ndoa haina umuhimu kwy maisha yao, samahani kwa kuwatoa mke kdg ya Mazda.
3. Mambo ya ndani kuyaweka kwenye media kiasi hiki ni upuuzi na inaonyesha pande zote za wazazi ni dhaifu hamuwezi mkaruhusu vitu kama hv kuzagaza, hawa watoto walizaliwa kuwe na limits ktk maamuzi.Flora jutia ujuaji wa kutimsikiliza mmeo tangu mwanzo hili ni jaribu kubwa ktk maisha yako usimkimbie mmeo usimtenge kwa hili mchukie mdg wako aliyekubali kufika nguo Siku ya kwanza.
4. Kingine hawa ndugu huambiwa ukija kwetu utapata Mme wako wa kweli mungu atakuchagulia na unafungishwa ndoa.!!!!!
5. Naomba jamii tuwaseme wanao ropoka juu ya maswala kama haya naona mchangiaji mwingine anasema acha watu wahubiri hats kama wanahubiri Ng'ombe huu ni upuuzi tambueni Uhuru wa kuabudu si hivyo ndo maana hata vitani kuna sheria vinginevyo watu siwangekua wanauana ovyo ovyo tu.