Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Sera ya "Elimu Bure" ilikuja kama mkombozi kwa wazazi wengi wa Kitanzania wenye kipato cha chini. Lengo lilikuwa wazi: kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya msingi ya elimu bila kikwazo cha kifedha. Hata hivyo, uhalisia mtaani na mashuleni kila uchwao unazidi kuthibitisha kuwa, huenda elimu hii si "bure" kama inavyohubiriwa.
Suala la michango shuleni limekuwa ni kizungumkuti kinachowaumiza wazazi, huku kukiwa na mkinzano mkubwa kati ya matamko ya viongozi wa kitaifa na kinachoendelea kwenye ofisi za wakuu wa shule.
Wazazi wanaumia, na mifano iko wazi kila kona ya nchi. Chukulia mfano wa mzazi anayempeleka mwanafunzi kuanza shule; anaambiwa akamilishe mahitaji na michango inayofikia hadi Tsh 300,000/-. Mzazi akiomba muda wa kujipanga, anakataliwa. Hapa mzazi hana pa kusemea, na mamlaka zinazopaswa kusimamia zinaonekana kuwa kimya.
Hali ni tete zaidi kwa shule ambazo zimebuni mifumo ya michango isiyo na ukomo. Mfano hai ulioripotiwa na wazazi ni Shule ya Sekondari Fulwe iliyopo Morogoro Vijijini, ambapo wazazi wanalalamikia utaratibu uliowekwa na uongozi wa shule wa kutoza michango ya "taaluma" ya Tsh 1,000 kila mwezi kwa kila mwanafunzi shule nzima, huku madarasa ya mitihani yakitozwa zaidi ya Tsh 5,000 kila mwezi.
Kila baada ya muda, tunasikia matamko mazito kutoka kwa viongozi. Mwaka 2024, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, alikemea na kusema, "Michango ya ovyo ovyo shuleni ambayo haina maelezo ikome." Mwaka huu wa 2026, Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda, amesisitiza tena, "Ni marufuku kumrudisha mtoto nyumbani kisa mchango."
Pamoja na matamko haya, michango inaendelea. Kwa nini? Jibu linaweza kuwa gumu lakini lipo wazi: Kuna uwezekano mkubwa serikali inafumbia macho (au kubariki kimya kimya) kutokana na ukweli kwamba ruzuku inayoenda mashuleni haitoshelezi.
Fedha za kugharamia elimu bure inavyoonekana zimekuwa hazikidhi mahitaji halisi ya uendeshaji wa shule. Mara nyingi, fedha hizi zinapunguzwa kila uchwao na, baya zaidi, zinaweza kuchelewa kufika shuleni hata kwa miezi mitatu. Katika mazingira haya, walimu wakuu wataendeshaje shule? Wananunuaje chaki? Wanalipiaje bili za maji, umeme, na ulinzi? Kuwabana wazazi inabaki kuwa njia pekee ya kunusuru shule zisifungwe.
Ili kumaliza kabisa kadhia hii, TAMISEMI na Serikali kwa ujumla lazima zikubali kukaa chini na wataalamu wao ili kutatua mzizi wa tatizo badala ya kutoa matamko yasiyo na nguvu za kiutendaji. Yafuatayo ni lazima yafanyike:
Pia Soma:
1. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Fulwe ameanzisha michango ambayo matumizi yake hayajawekwa wazi
2. Shule ya Sekondari Nakake - Wilayani Kyerwa (Kagera) ina michango mingi hadi baadhi ya Watoto wanaacha shule
3. Walimu wa Shule ya Secondary Kijichi – Temeke wana michango mingi sana, Mwanafunzi ambaye hana anachapwa
4. Michango imezidi Shuleni! Mfano, Shule ya Msingi Mikocheni (A) hadi birthday ya Mwalimu Wanafunzi wanachangishwa

- Kuongeza na Kupeleka Ruzuku kwa Wakati: Serikali ifanye tathmini ya mahitaji halisi ya uendeshaji wa shule za serikali. Fedha hizo ziongezwe na kupelekwa kwa wakati bila ucheleweshaji wa miezi kadhaa.
- Kuboresha Maslahi ya Walimu: Mzizi mwingine wa "michango ya ubunifu" mashuleni ni ukosefu wa motisha kwa walimu. Walimu wanaojituma ziada hawana posho. Serikali iongeze mishahara ya walimu na kuweka mifumo rasmi ya motisha (incentives) inayotambulika na kulipwa na serikali yenyewe. Mwalimu anayelipwa vizuri hana haja ya kubuni michango ya "taaluma" kinyume na utaratibu.
- Miongozo Thabiti na inayosimamiwa (Enforcement): Badala ya matamko ya kisiasa, TAMISEMI itoe muongozo unaoeleweka wa nini kinaruhusiwa na nini hakiruhusiwi, na kuchukua hatua kali kwa viongozi wa shule wanaoanzisha michango ya unyonyaji kama ilivyoainishwa hapo juu.