DOKEZO Sakata la Mount Meru Millers kuchakata mafuta ya kupikia kwa kutumia sumu/ chemical badala ya alizeti serikali mko wapi

DOKEZO Sakata la Mount Meru Millers kuchakata mafuta ya kupikia kwa kutumia sumu/ chemical badala ya alizeti serikali mko wapi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Hawa ndo watengenezaji wa Singida oil na Sunola ambazo zinatengenezwa kwa chemical na sio alizeti kama tunavyoaminishwa.

Nimeitoa huko twitter hii post naona inasambaa kwa kasi ya upepo.

ALERT [emoji599] [emoji599] [emoji599]

mount meru millers wana brand ya singida oil na sunola ambayo yote wanasema yanatokana na pure sunflower.

lakini ukweli ni kwamba Brand ya singida oil sio pure sunflower oil ,ni mafuta wanayotengeneza kutokana na mashudu/takataka ya alizeti ambayo inachakatwa pamoja na kemikali aina ya hexane .Baada ya kuchakatwa na hiyo kemikali ya hexane inapatikana mchanganyiko wa kimiminika ambacho ni crude oil pamoja na hexane.

Ambapo baada ya hapo inafanyiwa chemical process ya kutenganisha crude oil na hexane ,ili kuweza kuruhusu crude oil kwenda kusafishwa na kua salama kwenye process kama water demagation , saponification and colour removing... [emoji24][emoji24]

Lakini kwa bahati mbaya kiwandani hapo wanakuwa hawafanikiwi kuondoa kemikali yote ya hexane ambayo ni hatari kwa afya ya mtumiaji na wanapaki mafuta hivo hivo ikiwa na mchanganyiko wa kemikali hiyo [emoji22][emoji22]

Ndo maana ukitumia mafuta ya singida oil lazima ladha yake iwe chungu hapo ndipo unapoionja hexane

Tanzania Police Force na TBS tanzania hii kitu ni hatari kwa afya ya binadamu hatua za haraka zichukuliwe ili kulionoa taifa letu.

1663249472139.jpg
 
Mi sijui lakini mafuta ya sunola yakiisha dumu lake likikaa muda yale mabaki ya mafuta yanakua kama gundi au nta hivi sijui kwakweli ila mm nimeacha siku hizi natumia mafuta ya mashine za mtaani ila nayo kuna muda sijui wanasagiq nini mtumbo yanavuruga hatari. Mungu tuu atusaidie
 
Aliyepost huko Twitter una uhakika sio moja ya washindani wa huyu anayetuhumiwa? Au chawa wake? Nadhani kuna TBS wafanye kazi yao
 
Aliyepost huko Twitter una uhakika sio moja ya washindani wa huyu anayetuhumiwa? Au chawa wake? Nadhani kuna TBS wafanye kazi yao
Ndio amewaomba TBS wachukue hatua mkuu
 
Pole ndugu yangu:
Kwenye usindikaji wa mafuta ya kula yanayotokana na mbegu, matumizi ya dawa jamii ya hexane ni matumizi ya kawaida - Solvent exytraction.

Ndiyo maana kuna wingu kubwa la ununuzi wa mashudu na kupelekwa Kenya na China . Mashudu haya ni kwaajilii ya second refinery kwa njia ya kemikali , hii inachocjhewa na kuwa for ages tumekuwa tukitumia mashine za kukamua mafuta ya alizeti zenye poor mechanical efficiency na hivyo kuacha mafuta mengi kwenye mashudu.

Kwa taarifa yako, mafuta yaliyopatikana na nji9a hii ni bora zaidi kwa kuwa Hexane huondolewa kwenye mafuta kwa njia ya STEAMING ambapo process hii ni sawa na kuua ndege wawili kwa jiwe moja kwakukwa huondoa pia ALKALOID ambayo ni sumu kwa mlaji.
 
Mi sijui lakini mafuta ya sunola yakiisha dumu lake likikaa muda juani yale mabaki ya mafuta yanakua kama gundi au nta hivi sijui kwakweli ila mm nimeacha siku hizi natumia mafuta ya mashine za mtaani ila nayo kuna muda sijui wanasagiq nini mtumbo yanavuruga hatari. Mungu tuu atusaidie
Asante, umeshasema hujui..
 
Aliyepost huko Twitter una uhakika sio moja ya washindani wa huyu anayetuhumiwa? Au chawa wake? Nadhani kuna TBS wafanye kazi yao
Sasa tbs watafanyaje Kaz Bila kupata Taarifa Kama hizi?

Hata Kama sio za kwel lakn uchunguz ufanyike tuupate ukweli

Kuwe na maabara huru kwa ajili ya uchunguzi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ukitaka mafuta yatengenezweje? Kutokujua ndiko kunakusumbua. Unachafua biashara ya watu kwa kutokujituma kujua hiyo process.
Acha ujinga.
Aache ujinga kivipi? Ameeleza kuwa mafuta ya Sunola yametokana na mashudu (takataka) badala ya alizeti halisi, HUJALIPINGA

Ameeleza kuhusu kemikali ya HEXANE kuchanganywa na hayo makapi, HUJAPINGA

Unasema anataka mafuta yatengenezwaje? Kama huko ulikoeleza ndio namna ya utengenezaji mafuta (kimtazamo wako) anachafuaje Biashara ya watu? Mpinge kwa hoja na sio kwa upana tu (general)
 
Mkuu, nakuomba usome Post#11, nimefafanua namna ambavyo wakenya na wachina wanavyonunua mashudu kwa wingi kwa ajili ya kwenda kukamua mafuta kutoka katika mashudu. mafuta yanayobaki katika mashudu ni mafuta safi na ukizingatia kuwa mashine zetu zinaacha mafuta mengi katika mashudu
 
Back
Top Bottom