Sakata la Mpina na Waziri Bashe, nilivyoelewa kwa Lugha Rahisi

Hii ndio Point kubwa kabisa inayotakiwa kujibiwa na walio upande wa Supika 🙄😳
 
Hasara gani ?! Serikali imetoa pesa kununua au ?! Hebu mtaalamu tuambie hiyo hasara ..
Hasara ya Ubaguzi, uendele, kutozingatiwa vigezo na Taratibu, kutokuwepo Kwa usawa. Hivyo kunaweza kusababisha mahusiano Mabaya kati ya aliyependelewa dhidi ya aliye na juhudi mwishowe ndio haya tunayosema momonyoko wa maadili.
 
Nadhani Mpina kuna kitu kagundua kwamba angeenda kwenye kamati angezimwa mdomo kwa kuambiwa yamkini ushahidi una makosa hivyo siyo wa halali ndio mana ameona aulipue kwanza mbele ya kadamnasi ujulikane. Amecheza kete nzuri hapo
Basi acha akapambane na kanuni za bunge kuhusu ushahidi.
 
Sawa mimi nimekiri sijui ni hasara gani wewe mtaalamu nifahamishe serikali imepata hasara ipi ?!
Serikali inapojihusisha katika rushwa, kwani hujui kuwa ni hasara? Kodi inayopoteza hujui kuwa ni hasara?
 
Sawa.

Wewe usiye Kondoo. Na mwenye Ujasiri wa Simba, chonde tuongoze sisi Kondoo ili kuwafurumisha Hawa mumiani waliogeuza Nchi yetu kuwa ni Miliki Yao...
Siwezi kuongoza 'kondoo'. Ondoeni hizo fikra potofu kwanza vichwani mwenu.
 
Luhaga Mpina hakwenda kwenye 'media' kwa bahati mbaya; alijuwa alichokuwa akifanya.

Taarifa imekwisha wafikia wananchi, spika hana tena namna ya kuichakachua hiyo taarifa.
Uko sahihi sana
 
Luhaga Mpina ana hoja. Ni kweli kuwa upungufu wa sukari ulikuwepo lakini ni kweli pia kuwa kulikuwa na utapeli mkubwa kwenye kuruhusu uagizaji wa dharura. Sasa yeye Mpina anachohoji ni huo utapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…