Sakata la Mtoto kulawitiwa na Watoto wenzake Arusha:Je sheria inasemaje ?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Kwanza kabisa niombe Jamiiforums wasiunganishe uzi huu na Nyuzi nyingine zinazoelezea kuhusu sakata la Mtoto kulawitiwa Arusha na Kesi yake kufika kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Sote ni mashahidi wa kile kilichoonekana tarehe 10 Mei wakati wa Kliniki ya Haki iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa MKoa Arusha, ambapo dada mmoja ajulikanae kwa JIna la Witness aliopeleka malalamiko yake akidai kuwa mtoto wake kafanyiwa kitendo cha ulawiti lakini alipoenda Polisi Askari hawakumshughulika ipasavyo.

Je wajuzi wa sheria, tunaomba mtusaidie hapo, ni mtoto wa umri wa miaka mingapi, anastahili au hastahili kustakiwa kwa mujibu wa sheria?

Tafadhali sana tunaomba majibu yenu yaambatane na vifungu vya sheria, na kama kuna kesi za mfano,tunaomba mziweke humu au pia katika inbox yangu.

Asante sana.
 
Mtoto wa miaka mitano anajuaje mambo ya mizagamuano? Inaonekana wazazi wake hawajielewi ,watakuwa wamafanya ujinga huku watoto wakiona.
 
Kwanza kabisa niombe Jamiiforums wasiunganishe uzi huu na Nyuzi nyingine zinazoelezea kuhusu sakata la Mtoto kulawitiwa Arusha na Kesi yake kufika kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Sote ni mashahidi wa kile kilichoonekana tarehe 10 Mei wakati wa Kliniki ya Haki iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa MKoa Arusha, ambapo dada mmoja ajulikanae kwa JIna la Witness aliopeleka malalamiko yake akidai kuwa mtoto wake kafanyiwa kitendo cha ulawiti lakini alipoenda Polisi Askari hawakumshughulika ipasavyo
Je wajuzi wa sheria, tunaomba mtusaidie hapo, ni mtoto wa umri wa miaka mingapi, anastahili au hastahili kustakiwa kwa mujibu wa sheria ?
Tafadhali sana tunaomba majibu yenu yaambatane na vifungu vya sheria, na kama kuna kesi za mfano,tunaomba mziweke humu au pia katika inbox yangu.
Asante sana
Mambo kama haya yanapaswa kushughulikiwa na kamati ya maadili na nidhamu ya mtaa.

Viongozi wa mtaa na watendaji hili ni lao

Watoto waonye au wapewe adhabu na wawe chini ya uangalizi kwa muda ili kuhakikisha tabia hizo zinawatoka.
 
Asante sana kwa ushauri huu
 
Je wajuzi wa sheria, tunaomba mtusaidie hapo, ni mtoto wa umri wa miaka mingapi, anastahili au hastahili kustakiwa kwa mujibu wa sheria?
Kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Tanzania (Penal Code), uwajibikaji wa kijinai kwa watoto unategemea umri wa mtoto:​
  1. Kifungu cha 15(1): Mtu chini ya umri wa miaka kumi (10) hawezi kuwajibika kijinai kwa tendo lolote au kutoacha kufanya tendo lolote.​
  2. Kifungu cha 15(2): Mtu chini ya umri wa miaka kumi na mbili (12) hawezi kuwajibika kijinai isipokuwa ikiwa itathibitishwa kwamba alikuwa na uwezo wa kujua kwamba hapaswi kufanya tendo au kutoacha kufanya tendo hilo.​
Screenshot_20240605-182020.jpg

Kifungu cha 15 cha Penal Code
Kwa hiyo, mtoto chini ya miaka kumi hastahili kustakiwa kwa mujibu wa sheria. Kwa mtoto aliye na miaka kumi na kumi na mbili, mahakama itahitaji ushahidi kwamba mtoto alikuwa na uwezo wa kutambua kwamba kitendo alichofanya kilikuwa kinyume cha sheria ili aweze kustakiwa.

View attachment 3009565

Back
Top Bottom