Sakata la Mtoto wa Rose Nungu (MunaLove), Linaumiza Sana Moyo

Sakata la Mtoto wa Rose Nungu (MunaLove), Linaumiza Sana Moyo

Hivi kugombania maiti kuna maana gani? Kwani maiti ikizikwa popote kuna shida? Wekeni misiba hata mitatu mpate rambirambi zenu kama ndizo zinawaliza.
Hata mimi huwa nashangaa sana...
kama anazikwa tz hakuna noma
labda angekuwa anazikwa Kenya....
 
Mkeo ushampa adhabu hizo au?[emoji3][emoji16][emoji16][emoji23][emoji16][emoji16][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23]
Alafu ww ndio umekoment pale juu unasema wanaume wa Jf .......
una bahati kweli ww ningeikuta ile koment yako......
ningekuchapa juu juuu
 
Wanaume wa Dar wash.nz kweli wanachapiwa weee
wanaibuka siku za misiba!!!!?
Itabidi tuanzishe crash program ya kuwajenga....
acha nibaki huku ughaibuni.....
 
Kazi kwelikweli, mnamtesa marehemu
Acha imani potufu mkuu, marehemu anatesekaje kwa mfano?? Mtu akisha kufa anakuwa amekufa na hajui lolote, hasikii chochote, haoni chochote, hahisi chochote, unabakia mwili tu ambao unaoza taratibu. Hiyo ndiyo maana ya kufa, ukifa unakuwa haupo kabisa.

Maiti hata ikichomwa moto, ikitupwa baharini, ikiliwa na fisi, ikizikwa kwa heshima au ikizikwa kwa dharau; haisaidii kitu wala haibadilishi kitu. Ukifa umekufa, you are gone, finished!
 
Mtoto Patrick ameshatangulia mbele za haki lakini huku nyuma, moto unawaka. Mama yake, Muna Love amesababisha kizaazaa kabla hata mwanaye hajapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele, machozi jasho na damu vinachuruzika.

Muna anadai mtoto ni wa Casto Dickson, yule mtangazaji wa Siz Kitaa (Clouds), Casto anadai mtoto ni wake lakini upande wa pili, yupo baba halisi, Peter Zacharia ambaye anavyo vithibitisho vyote vya kisheria kwamba Patrick ni mwanaye.

Muna anataka yeye ndiye achague wapi anamzika mwanaye, Zacharia anadai yeye ndiyo baba halisi wa mtoto kwa hiyo ndiye atakayechagua wapi pa kumzika mwanaye na azikweje. Muna anasisitiza kwamba mtoto ni wake na msiba ni wake kwa hiyo yeye ndiye atakayemzika mwanaye.

Kuna misiba miwili kwa maiti ya mtoto Patrick, Muna ameweka msiba nyumbani kwake, Zacharia pia ameweka msiba nyumbani kwake. Waombolezaji wamechanganyikiwa, hawaelewi waende kwa Muna au kwa Zacharia.

Zacharia anasema mwanaye akizikwa bila ridhaa yake, yupo tayari hata kufuata sheria ili mwanaye akafukuliwe na azikwe anapopataka yeye, kwa sababu yeye ndiye baba halisi. Anavyo vithibitisho, kikiwemo cheti cha ndoa na Muna na anaeleza kwamba hajawahi kumuacha mkewe huyo, ile yeye ndiye aliyekimbia nyumbani kwao, mtoto akiwa na miaka mitatu.

Nini hatma ya malaika Patric ambaye maskini ya Mungu hana hatia katika hili? Maiti yake inagombewa na kuna hatari akizikwa kabla ya hizi tofauti hazijapatiwa ufumbuzi, mwili wake utafukuliwa na kuzikwa upya.

Yajayo yanahuzunisha sana!


Habari zaidi, soma=>TANZIA: Mtoto wa Munalove Patrick Peter Zacharia Komu almaarufu Partsmartboy Afariki dunia

Haya ndio madhara ya kuwa na mke MALAYA SANA.
 
Jamani wanaume zetu mmepanic sana msitutukane sana,wanawake wazuri wa kuoa bado wapo including me,alichokifanya muna hakikubaliki ila msitutukane wote jamani
pole lakini mimi hili suala linaendelea upande wangu mpaka sasa yaani nashukuru sikuua au kufanya ubaya mwingine.
 
pole lakini mimi hili suala linaendelea upande wangu mpaka sasa yaani nashukuru sikuua au kufanya ubaya mwingine.
pole ila mda ni tiba nzuri utakuwa sawa tu mke umemuaacha au?
 
Back
Top Bottom