Sakata la RC Malima na Mkurugenzi Mwanza halina tofauti na wale wauguzi kubishania vifaa tiba feki

Sakata la RC Malima na Mkurugenzi Mwanza halina tofauti na wale wauguzi kubishania vifaa tiba feki

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kuna tuhuma nzito zimetangazwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza

RC Adam Malima ameonekana akimtuhumu Mkurugenzi wa jiji kuhusika na utapeli wa kuuza viwanja viwili vyenye thamani ya Bilioni moja!
Hii ni taharuki na tuhuma nzito sana!

Ukitafakali kwa kina jambo hili linaibua maswali mengi sana yasiyo na majibu!

Vyeo hivi vya Mkurugenzi na RC vina mgongano mkubwa sana wa kimaslahi, nashauri viandaliwe utaratibu mwingine ikiwezekana cheo kimoja kifutwe ili kuondoa mgongano wa maslahi kwasababu!

Wakurugenzi ni wasimamizi wakuu wa watendaji katika eneo husika! Wakurugenzi ndiyo wenye wataalamu katika eneo husika, wakurugenzi ndiyo mikono ya serikali na vitendea kazi!,wakurugenzi siyo mwanasiasa ingawa wanatoka kwenye chama cha siasa!

Tofauti kubwa iliyopo kwa RC&DC ni hivi!

RC/DC ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika eneo, ni Icon ya serikali hasa kwenye masuala ya Kiitifaki (protocol)! Ni auxiliary leader katika eneo! Mikono yake mikubwa ni Polisi peke yake! Kwasababu wataalam mpaka migambo wote ni wa wakurugenzi!

Yaani RC/DC akitaka kula peke yake ni kwenye madili haramu ya kipolisi!

Nje ya hapo RC na DC hawezi kula bila mikono na baraka ya Mkurugenzi! Maana mambo yote ya dokomenti yako chini ya Mkurugenzi!

Hivyo tukirudi kwenye sakata la Mwanza!
HAKUNA MWEMA PALE lakini SHIDA Ni ule ulaji UMELIWAJE!

Mkurugenzi anaweza kutusua dili peke yake na likaisha bila msaada wa RC/DC
Na hili ndiyo maana wakurugenzi wanaonekana ni wabaya kila siku!

Mkurugenzi siyo mwanasiasa bali ni mtaalam! Hivyo kula yake haihitaji blaah blaah na makamera!

Kosa lililotokea Mwanza ni Mkurugenzi kula peke yake!

Na kama TAMISEMI ikikurupuka katika mgogoro huu tutarajie watapokea migogoro mingine mingi kutoka kwa RC na ma DC inchi NZIMA!

UKIONA ENEO HALINA MGOGORO UJUE MKURUGENZI NA RC/DC WANAKULA SAHANI MOJA!

Hakuna Eneo ambalo Halina upigaji! Wote wezi tu sema wanazungukana!
 
Tunazungumzia sakata hili la Mwanza! Hakuna utapeli Bali kuna MTU kanyimwa mgao!
Kunyimwa mgao kunaambatana na "...yeye ni nani?" Kumbuka Waziri wa ardhi ni Mbunge wa huko
 
Hajafinyiwa, mkurugenzi kamtosa, nina jamaa yangu afisa ardhi mkoa fulani..... chemistry yao inaunganisha Yeye-Mkurugenzi-RC ,wamepiga sana hela za wanaoanzisha sheli.
Wanazi piga sana, sema ma RC/DC huwa hawariziki wakimegewa mgao !

Sakata la Mwanza Malima alizingua! Akiamini mzigo ni mwingi kumbe kambuzi kalikuwa kadogo
 
Back
Top Bottom