Sakata la RC Malima na Mkurugenzi Mwanza halina tofauti na wale wauguzi kubishania vifaa tiba feki

Sakata la RC Malima na Mkurugenzi Mwanza halina tofauti na wale wauguzi kubishania vifaa tiba feki

Tofautisha serikali na mtu binafsi, serikali ikiamua kuvaana na wewe, inakuvaa kama taasisi, na haitakuachia kirahisi, Sabaya unamuona, alitegemea ulinzi wa mtu binafsi, sio taasisi, na ili ulindwe na taasisi fata matakwa na maslahi ya nchi, sio vitumbo vyenu hivyo vimejaa vibambara na viporo vya ugali wa mtama.

Anayelalamika hapo ni serikali, Malima ni kisemeo tu Cha serikali, anaongea kwa niaba ya hao wananchi wanaokaa Jiji la mwanza, I mean, ni wananchi ndio wamesema mmeuza kiwanja Chao wakati waliwapa mkitunze, na wao wamekitunza kwa miaka dahari, wamepita wakurugenzi na maafisa ardhi wangapi hapo? Walikuwa wajinga kukiacha nyie ndio mna akili? Hata kufanya Public Private partnership mlishindwa? Shnz typ

Hivyo viwanja Wana mwanza unaowaona hapo mjini ndio wamiliki, sio nyie mliokaa hapo kwenye hizo ofisi
Inaonekana Kuna jamaa la lake zone, lilikupelekea Moto halafu likakataa kukulipa. Unavuja tu
 
Huyu mpuuzi analelewa kila siku kwani yeye nani nchi hii.

Inachosha kuandelea kumsikia huyu mjinga.

To hell witj kikwete na huruma za alichomfanyia baba yake.

Baba yake ndio aliiba pesa za serikali na kufunga akaunti zake haikuwa dhambi.
Wanamuita jembe
 
Toka lini Bakari Malima akawa RC!
Usijali mwandishi kutohoa jina, jali mantiki na uzito wa hoja!

Hivi jina la msikitini la Malima anaitwa nani, maana babake naye alikuwa akitumia jina lake la uji la Kighoma!
 
Unajua RC ni boss wa DED? Unajua kikatiba RC ni Rais wa Mkoa?
Hilo linajulikana!

Kinachoongelewa hapa ni mambo yao ya madili na namna vyeo vyao hivyo vinavyosigana!

Nani ni nani kwa mwenzake, maana wote ni wateule wa Rais.

Kama Rc ni Rais wa Mkoa kashindwaje kumwadabisha moja kwa moja DED mpaka abembeleze ngazi za uteuzi, ushasikia Rais anaziomba ngazi za uteuzi?
 
Hilo linajulikana!

Kinachoongelewa hapa ni mambo yao ya madili na namna vyeo vyao hivyo vinavyosigana!

Nani ni nani kwa mwenzake, maana wote ni wateule wa Rais.

Kama Rc ni Rais wa Mkoa kashindwaje kumwadabisha moja kwa moja DED mpaka abembeleze ngazi za uteuzi, ushasikia Rais anaziomba ngazi za uteuzi?
Wewe hujui kaa kimya! Unaposikia Rais amemtumbua mtu, lazima sheria na michakato ya kumfukuza ifanyike ndipo aondoke Ofisini. Rais hawezi kumfukuza kazi mfano mwalimu wa shule ya msingi na hapo hapo akaondoka, lazima mamlaka yake ya nidhamu ihusike. Unless yeye Rais ni mamlaka ya nidhamu ya huyo mtu hata kama ni presidential appointee
 
Kuna tuhuma nzito zimetangazwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza

RC Adam Malima ameonekana akimtuhumu Mkurugenzi wa jiji kuhusika na utapeli wa kuuza viwanja viwili vyenye thamani ya Bilioni moja!
Hii ni taharuki na tuhuma nzito sana!

Ukitafakali kwa kina jambo hili linaibua maswali mengi sana yasiyo na majibu!

Vyeo hivi vya Mkurugenzi na RC vina mgongano mkubwa sana wa kimaslahi, nashauri viandaliwe utaratibu mwingine ikiwezekana cheo kimoja kifutwe ili kuondoa mgongano wa maslahi kwasababu!

Wakurugenzi ni wasimamizi wakuu wa watendaji katika eneo husika! Wakurugenzi ndiyo wenye wataalamu katika eneo husika, wakurugenzi ndiyo mikono ya serikali na vitendea kazi!,wakurugenzi siyo mwanasiasa ingawa wanatoka kwenye chama cha siasa!

Tofauti kubwa iliyopo kwa RC&DC ni hivi!

RC/DC ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika eneo, ni Icon ya serikali hasa kwenye masuala ya Kiitifaki (protocol)! Ni auxiliary leader katika eneo! Mikono yake mikubwa ni Polisi peke yake! Kwasababu wataalam mpaka migambo wote ni wa wakurugenzi!

Yaani RC/DC akitaka kula peke yake ni kwenye madili haramu ya kipolisi!

Nje ya hapo RC na DC hawezi kula bila mikono na baraka ya Mkurugenzi! Maana mambo yote ya dokomenti yako chini ya Mkurugenzi!

Hivyo tukirudi kwenye sakata la Mwanza!
HAKUNA MWEMA PALE lakini SHIDA Ni ule ulaji UMELIWAJE!

Mkurugenzi anaweza kutusua dili peke yake na likaisha bila msaada wa RC/DC
Na hili ndiyo maana wakurugenzi wanaonekana ni wabaya kila siku!

Mkurugenzi siyo mwanasiasa bali ni mtaalam! Hivyo kula yake haihitaji blaah blaah na makamera!

Kosa lililotokea Mwanza ni Mkurugenzi kula peke yake!

Na kama TAMISEMI ikikurupuka katika mgogoro huu tutarajie watapokea migogoro mingine mingi kutoka kwa RC na ma DC inchi NZIMA!

UKIONA ENEO HALINA MGOGORO UJUE MKURUGENZI NA RC/DC WANAKULA SAHANI MOJA!

Hakuna Eneo ambalo Halina upigaji! Wote wezi tu sema wanazungukana!
Mda huo RAS anakuwa Yuko wapi? Kwanza RAS angepewa meno ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi yeyote.
 
Wewe hujui kaa kimya! Unaposikia Rais amemtumbua mtu, lazima sheria na michakato ya kumfukuza ifanyike ndipo aondoke Ofisini. Rais hawezi kumfukuza kazi mfano mwalimu wa shule ya msingi na hapo hapo akaondoka, lazima mamlaka yake ya nidhamu ihusike. Unless yeye Rais ni mamlaka ya nidhamu ya huyo mtu hata kama ni presidential appointee
Kwa kweli sijui, ngoja ninyamaze mkuu.
 
Back
Top Bottom