Kuhusu kauli ya Mnyika namuunga mkono na ndio maana hata mimi nilileta huu uzi hapa chini:
Hoja ya kurudisha Bungeni sakata la Richmond iende sambamba na kuondoa kinga ya Rais
Ukweli ni kwamba ukipitia taarifa ya kamati ya Mwakyembe mwanzo mwisho huwezi kuamini kuwa yote yale yalifanyika bila bwana fulanj kujua.Ni mwendawazimu pekee ndio atakaeamini hivyo.
Mtu mwenye akili lazima ujiulize maswali haya 9 yafuatayo hapa chini:
1.Kwanini Lowassa hakuhojiwa?
2.Lowassa angehojiwa na katika kujittetea unadhani angemtaja nani?
3.Na kama angetaja mtu/watu katika kujitetea,unadhani angetaja wa chini yake tu bila kumtaja bwana fulani?
4.Je,unadhani Mwakyembe na kamati yake hawakujua hatari ya kumuhoji Lowassa?
5.Kama wangemuhoji Lowassa, unadhani Mwakyembe na timu yake walikuwa tayari kumtaja(kumu-implicate) mh.sana wa wakati huo katika taarifa yao walioiwasilisha Bungeni?
6.Wangemtaja mh.sana wa wakati huo katika ripoti yao,unadhani nini kingefuata?
7.Unadhani Lowassa nae angeweza kueleza kila kitu mbele ya Bunge kabla ya kujiuzulu?
8.Na yeye kama angeeleza ukweli wote anaoujua,unadhani nini kingefuata?
9.Unadhani angeondoka Lowassa peke yake bila fulani kuingia matatani?
Haya mambo yanawezekana tu katika nchi za wenzetu na sio huku kwetu tunakowaona kina fulani kama miungu watu.
Tuache kupotezeana muda na kudanganyana.