Sakata la Sabaya tusilipime kwa yeye kufikishwa Mahakamani

Sakata la Sabaya tusilipime kwa yeye kufikishwa Mahakamani

Wacha pressure mjomba, ushahidi uko wa kila aina (video & audio) hata ukitaka kupeleka mashahidi physically mahakamani wapo wakutosha, wengine walipigwa, wakaporwa mali zao madukani, wakatoa huduma Sabaya hakulipa, hata kama wanasheria wa serikali hushindwa kesi kizembe ila sio kwa hii ya Sabaya, wakishindwa wafukuzwe kazi wote.
 
Kwahiyo tayari una HUKUMU yako kichwani?

Ikitokea ikawa tofauti na unavyotaka utaanza kujambajamba.

Hivi wafuasi wa Mbowe mna akili timamu kweli ?
Aliyofanya yana tofauti gani na aliyoyafanya Bashite?Mbona Bashite haguswi?
 
Na vipi Sabaya akiamua kuweka kila kitu hadharani in case alikuwa anatumika?
Htaa kama kutumika hakuna kiongozi ambae atakutuma ukalawiti watu.

Hakuna kiongozi atakutuma ukaibe wake za watu. Hakuna kiongozi mpumbavu huyo.

Hakuna kiongpzi atakutuma uende baa kunywa alafu usilipe uache bili na madeni kibao.

Hakuna kiongpzi atakutuma ukatafute alipo lala nandy kisha utake kulala nae kwa nguvu,hakuna kiongozi huyo.

Hakuna kiongozi atakayekutuma kufanya uchafu huu yeye afaidike na lipi.

Msije sema magufuli kamtuma,kama alikubali kutekeleza basi acha yeye awajibishwe na sio kweli kwamba yote ambayo kafanya alitumwa huo ni uongo.

Pengine anashtakiwa kwa mashtaka ambayo watu wengine waathirika wana ushahidi nayo

Hizi tuhuma zinamkabili ndugu sababya,msitake kumtetea ionekane kqamba alitumwa,hata kama alitumwa sio kwa vyote mengine ni ajenda zake mwenyewe tu
 
kundi rahisi zaidi kulidanganya ni kundi la watu waliokata tamaa.
 
Aliyofanya yana tofauti gani na aliyoyafanya Bashite?Mbona Bashite haguswi?
Kamguse wewe. Mtu yuko mtaani hana madaraka yoyote mnaogopa nini kumshtaki.

Angekuwa analelewa na wenye madaraka tungelaumu.
 
Hili sakata lina shuhuda nyingi sana dhidi ya Ole
Kama ni za kweli amevuruga na hachomoki.... kama zimetengenezwa kuna watu wataamia
Muda utasema
Kumbuka iliwahi daiwa kuwa alikuwa anakusanya noti kwa ajili ya shughuli za chama fulani.
 
Zee la malalamiko uchwara. Hujui hata unalalamika nini maana unalalamikia kila kitu.

Aliyekuroga kakuweza kikamilifu.
Hivi ile barua iliyosambaa mitandaoni ilisomeka kuwa alikuwa anakusanya noti kwa ajili ya shughuli za chama gani?
 
Sabaya kupelekwa mahakamani ni jambo moja, na kitachojiri mahakamani, ni jambo lingine na ambalo ndio la msingi zaidi. Hivyo, tujipe muda badala ya kufurahia kuwa haki imetendeka.

Kumbukeni: Zimwi likujualo, halikuli likakwisha.

Mwisho, tujiulize Sabaya aliyatenda haya bila kuwa na baraka za mtu au watu fulani?Na hao TAKUKURU watakuwa tayari kuwasilisha ushawishi au maelezo yatayohusisha waliokuwa wanamtuma(kama alikuwa anatumwa))?

Na vipi Sabaya akiamua kuweka kila kitu hadharani in case alikuwa anatumika?

Nitakuwa wa mwisho kuamini aliyatenda haya pasipo vyombo vya dola vilivyodhibiti ujambazi kuyajua..

Time will tell.
Umenena vyema kaka, tungoje mwisho wake kwanza, its too early kusema kitu kwa sasa
 


Akamvulie na jaji miwani....
 
Trump yupi unayemwongelea ? Huyo ni mhalifu kama walivyo wahalifu wengine,hakuna cha support hapa mkuu ! jinai kama ipo basi itakula kwa aliye tenda hiyo jinai
Kama kweli watz tunampango wa kuendelea na amani yetu,huyu bwana tuachane nae coz naona suport aliyonayo mitaani ni km trump
 
Hivi ile barua iliyosambaa mitandaoni ilisomeka kuwa alikuwa anakusanya noti kwa ajili ya shughuli za chama gani?
Wewe ni taahira, kwahiyo sasa hivi anashtakiwa na serikali ya chama gani ?

Barua mtu yeyote anaweza kuandika na kusambaza mtandaoni. Kama ni kosa genuine hiyo barua iwe ushahidi mahakamani na siyo kusambazwa kwa makamanda uchwara.
 
Sabaya akichomoa hii hatakaa arudie upuuzi wake
Hawezi kuchomoka kwenye mashtaka yote hayo, labda ya ubakaji na ulawiti yanayohitaji ushahidi kama picha za video au manii na nywele za sirini, japo pia ushahidi wa kimazingira unaweza kumtia hatiani kutokana na hoja zitakazotolewa na upande wa mashtaka.

Lakini hayo mashtaka ya kupiga watu, kuhudumiwa na kutolipa, kuchukua wake za watu mbele ya waume zao that's kidnapping wengi waliona, kazi anayo.
 
Wewe ni taahira, kwahiyo sasa hivi anashtakiwa na serikali ya chama gani ?

Barua mtu yeyote anaweza kuandika na kusambaza mtandaoni. Kama ni kosa genuine hiyo barua iwe ushahidi mahakamani na siyo kusambazwa kwa makamanda uchwara.
We tukana tu ila habari ndio hio.
 
Back
Top Bottom