Kanuni uliyoitaja ni hii hapa..!!
View attachment 3277231
Hakuna cha maana kinachobebwa na kanu kwenye kughairisha ile mechi. Ni usimba tu. Na ndiyo maana Karia anajiropokesha kwenye vyombo vya habari na kutoa kauli zake bila vikao.
Hebu tuijadili hii kanuni uliyoweka hasa kifungu 1.3.
Kifungu 1.3 kinasema kuwa " sababu ya dharula au/ na yenye msingi itakayokubaliwa na TFF"
Sasa kwa kuwa Sheria ni jambo linalotumia fasihi andishi kwenye kuielewa, basi hebu tuichambue hiyo Sheria kiuandishi.
Kufungu hicho cha kanuni ya 3 kifungu kidogo 1.3 kinamaanisha kuwa dharula ama sababu ya msingi itakayokubaliwa na TFF mechi inaweza kuahirishwa.
Dharula ni kwamba haikutarajiwa kuwa Simba itakwenda kufanya mazoezi yake ya mwisho ambayo ni haki yao Kwa mujibu wa kanuni ya 17.
Ni dharula pia kwa kuwa vurugu walizofanyiwa Simba pamoja na kuzuiwa kuingia uwanjani Mkapa, ni mambo ambayo hayakutarajiwa.
Kwa mujibu ya kanuni hiyo, sababu ya msingi itakayokubaliwa na TFF inaweza kuahirisha mechi. Sasa sababu ya msingi ni ipi.
Kwenye mambo ya Sheria Kuna msemo kwamba " si tu haki inatakiwa itendeke, bali pia inatakiwa ionekane inatendeka".
Kwa ivo ili kutenda haki Kwa Simba ambao walikuwa wameandika barua rasmi ya kulalamika kwa bodi ya ligi, ni lazima vielelezo vipatikane. Kumbuka tukio lenyewe lilitokea usiku.
Kwa ivo sababu ya msingi iliyotolewa na bodi ya ligi Kwa TFF na kukubaliwa, ni kwamba muda wa kupata vielelezo kabla ya mechi kuchezwa ni mdogo hivyo wakaona ni heri mechi iahirishwe.