Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA NANE
“Unayo nafasi ya kuweza kuyachukua maisha yangu kama ulivyo tishia hapo kwa sababu wewe ni raisi wa nchi ila unapaswa kujiuliza mswali haya, nikifa wananchi wataanza kuniulizia nipo wapi? Watauliza nani kaniua na kwa sababu zipi? Sasa hapo itatafutwa familia yangu na kuulizwa kwa mara ya mwisho nilikutana na nani, unajua watajibu nini? Watasema kwamba nilikutana na mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, mwisho wako utaanzia hapo kwani wataamini wewe ndiye umeniua kwa sababu unahisi kwamba nitakupokonya hiyo nafasi yako. Vipi upo tayari wananchi wajue huo ukatili wako? Unahisi watakuja kukuamini tena na kukufanya uwaongoze? Jibu ni hapana mheshimiwa” mr Apson Limo aliongea kisha akatulia kuacha hayo maneno yakae vyema kwenye kichwa cha raisi huyo kisha akaendelea.

“Kuna swali moja ambalo mimi najiuliza sana, kwanini unaniogopa sana na kuhisi kwamba mimi ni hatari kwako wakati wewe ndiye mwenye madaraka makubwa mheshimiwa? Mimi ni kiongozi wa kawaida tu huenda watu wameniamini kutokana na yale ambayo wameona nayafanya kwa muda mrefu sana. Najua unaweza ukahitaji kuniangusha ila zingatia tu usije ukafanya makosa kwenye hizo harakati zako maana kama wananchi wakijua unaweza ukajikuta kwenye nafasi mbaya sana na hata kama utapita unaweza kupinduliwa. Swali pekee la msingi ambalo unatakiwa kujiuliza ukiwa mwenyewe ni kwamba umewafanyia nini wananchi mpaka wakurudishe tena kwenye hicho kiti ulichopo? Kama hakuna cha maana ulicho kifanya basi nadhani huu ni wakati sahihi kabisa wa wewe kuandaa sababu za msingi pale ambapo wananchi hao watakuwa wanakuuliza maswali kama hayo hadharani, kama utashindwa kuyajibu maana yake utakuwa umejiondoa mwenyewe kwenye hiyo nafasi uliyopo. Nikutakie usiku mwema mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano” Tajiri huyo hakumkopesha raisi wake, alimwambia ukweli wa mambo ulivyo na yale ambayo huenda yangetokea kisha baada ya hapo akatoka humo ndani kwa kuamini kwamba kiongozi wake hakuwa na cha kumfanya kwa sababu kama angemuua basi watu walikuwa wanaenda kujua moja kwa moja kwamba mhusika ni yeye kwa sababu familia yake ilijua kabisa yeye kaitwa Ikulu hivyo raisi alijikuta anabaki tu ndani akiwa mwenye hasira nyingi sana.

Aliipasua kwa kuibamiza meza ambayo ilikuwa ipo pembeni kidogo mwa sehemu ambayo ilikuwepo meza yake kubwa ya mninga ambayo ilitengenezwa kwa ubora wa hali ya juu sana. Mheshimiwa aliambiwa ukweli mtupu kwamba alipaswa kujitafakari sana na kujiuliza kwamba ni kitu gani ambacho alikuwa amewafanyia wananchi mpaka wampe tena nafasi? Hakuwa na jambo la maana sana alilokuwa amelifanya zaidi ya propaganda za mdomoni tu. Hakukuwa na ajira za kueleweka, huduma za kijamii zilikuwa duni sana hususani maeneo ya vijijini, mfumuko wa bei kila sehemu ulikuwa mkubwa sana, uchumi wa nchi ulikuwa kwenye hali isiyo ya kuridhisha, sasa angesimama vipi mbele ya wananchi kuongelea hizo habari?

“Kiongozi kuna jambo ambalo ninapaswa kulifanya?” alikuwa ni mlinzi wake ambaye sauti ya mpasuko wa meza ilimshtua na kumfanya awahi haraka sana kuingia humo ndani ambapo alimkuta mheshimiwa akiwa anapasua pasua vioo huku mkono wake ukiwa unavuja damu basi alimshika na kumtuliza huku akiwa anamuuliza ili kuona kama kuna kitu anaweza kukifanya kwa ajili ya bosi wake.

“Hahahaa hahahaha hahaha yule mjinga kahisi kwamba labda mimi ni mtoto mwenzake sio, anahisi kwamba mimi naweza kutishiwa kirahisi sana namna hiyo? Nitamfanyia kitu kibaya sana mpuuzi yule, nahitaji kukutana na mkuu wa majeshi muda huu” aliongea kwa jaziba sana akiwa anaelekea kwenye kochi kuchukua koti lake lakini mlinzi wake ilimbidi amtulize na kumpelekea bafuni kwanza kumtuliza bosi wake ambaye alikuwa anahema kwa harisa kali mno. Walirudi sebuleni maana mlinzi huyo alimwambia mheshimiwa kwamba kulikuwa na kitu cha kukiongelea hapo.

“Mheshimiwa kuna tatizo”

“Lipi?”

“Inadaiwa kwamba kapteni wa jeshi amekutwa akiwa anaandaa mipango ambayo inadaiwa kwamba alikuwa amepanga kuja kupindua nchi”

“Whaaaaaaaat?” mheshimiwa raisi aliuliza kwa mshangao mkali isivyokuwa kawaida

“Ndiyo mkuu, hilo jambo mkuu wa majeshi alilishtukia mapema sana hivyo amemkamata haraka sana baada ya kupata habari hizo na muda wote alikuwa anakupigia simu lakini simu yako haikuwa ikipokelewa hivyo akaamua kunipigia mimi hapa ili kama unahitaji kuongea na huyo kapteni uongee naye au kama unataka wamuadhibu kwa sheria za jeshi ni wewe tu anasubiri amri yako”

“Safi sana, nilikuwa nawatafuta watu wa namna hii kweli kweli kwenye maisha yangu, nafikiri huyu anaenda kuwa wa mfano kwa kuanza naye nitawashangaza sana wanajeshi kama kuna mwingine alikuwa na huo mpango basi atajutia sana kufikiria hilo jambo” mheshimiwa alitulia kwa muda maana hizo habari ni kama zilikuja wakati mwafaka, wakati ambao alikuwa na hasira sana hivyo akafurahi kuona kuna sehemu ya yeye kutulizia hasira hizo. Ni kama kuna jambo lilimshtua ghafla akamgeukia mlinzi wake

“Inawezekana vipi kapteni kutaka kufanya jambo kama hilo na mkuu wa majeshi asijue?”

“Inawezekana mkuu, unajua mkuu wa majeshi yupo pale juu kupokea taarifa kutoka chini na kuzifanyia maamuzi au kuzipelekea sehemu zingine ambako zitahitajika lakini yeye anakuwa hajui kabisa kinachokuwa kinaendelea huko chini. Sasa kapteni yeye anazipokea moja kwa moja kutoka kwa watu wake wa chini kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba yeye anakuwa na taarifa nyingi zaidi ya mkuu wa majeshi na yeye ndiye ambaye anachagua taarifa zipi za kumpa mkubwa wake, kwa maana hiyo yeye ndiye anajua mambo mengi zaidi hivyo mpaka kufikia hapo ina maanisha kwamba alikuwa amefikia hatua kubwa sana ya mafanikio ya hicho alichokuwa anakifanya”

“Andaa msafara tunaelekea makao makuu ya jeshi wakati huu na mwambie mkuu wa majeshi aandae kabisa sehemu ambayo itatosha watu wa kutosha kuwepo na mtu huyo aandaliwe haraka sana” alitoa amri hiyo akiwa anatoka humo ndani, lilitokea jambo la haraka na yeye alihitaji kulishughulikia haraka sana maana mtu kutishia kumuondoa raisi madarakani lilikuwa ni kosa la uhaini mkubwa sana ambalo adhabu yake ni kifo tu pekee na alitaka kulifanikisha kwa mkono wake mwenyewe iwe ni kama onyo kwa watu wengine ambao walikuwa wana mawazo kama ya huyo kapteni ambaye alitoka kupewa taarifa zake muda mfupi ambao ulikuwa umepita.

Daniel Mpanzi, ndilo lilikuwa jina lake mheshimiwa CDF. Vazi lake likiwa na nyota za kutosha alikuwa ameongozana na makamanda wake wakiwa eneo maalumu kabisa la kupokelea wageni kwenye makao makuu ya jeshi la nchi. Walikuwa hapo kwa ajili ya kumpokea mheshimiwa raisi ambaye alitoa taarifa muda mfupi uliokuwa umepita kwamba sio muda sana angeweza kuingia hapo kukutana na huyo mtu wake ambaye alidaiwa kwamba alitishia kuipindua nchi.

Ndani ya dakika chache msafara huo kutoka Ikulu ulikuwa unaingia ndani ya hilo eneo, alishuka mheshimiwa na walinzi wake huku akipokelewa kwa heshima sana na vijana wake hao ambao wengi kwenye hiyo nafasi aliwaweka yeye mwenyewe.

“Karibu sana mheshimiwa” CDF aliongea huku akiwa anampa mkono bosi wake.

“Asante sana, nahitaji moja kwa moja unipeleke kwa huyo mtu na waambie vijana wako waandae ulingo wa mapambano ambao utawafanya wanajeshi wengi sana kushuhudia pambano hilo ndani ya muda mchache ambao unafuata”

“Sawa mheshimiwa” hakukuwa na maelezo zaidi ya kumpeleka ndani ya chumba ambacho kilikuwa chini sana ya ardhi ambako ndiko alikokuwa amefungwa kapteni huyo ambaye alidaiwa kwamba alikuwa anahitaji kumpindua raisi huyo madarakani.

“Kwenye maisha yangu yote tangu niingie Ikulu kuna watu ambao nimewahi kuwaza kwamba wanaweza kuwa hatari kwa upande wa nafasi yangu japo hawaruhusiwi hata kuwaza kuhusu hilo jambo ila angalau wao wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufanya hilo. Kuna makamu wangu, kuna waziri mkuu, kuna spika wa bunge pamoja na jaji mkuu wa nchi, lakini hapo hapo wanaongezeka watu wawili ambao ni mkurugenzi wa usalama wa taifa bila kumsahau mkuu wa majeshi”

“Hao ndio watu ambao wana nguvu ukinitoa mimi kwa sababu wanaweza kwenda popote na kukutana na yeyote yule hivyo kwa kiasi fulani naweza kusema kwamba kama kusalitiwa basi hawa ndio walitakiwa kuwa watu wa kwanza kabisa kuweza kufanya hivyo lakini kitu cha ajabu kabisa mbwa kama wewe ndo unaanza kuwaza huu ujinga bila kuwaza madhara yake na kama mfugaji wako akikukataa nani atakulisha? Uliwahi kuwaza kwa umakini kabisa hili jambo na halmashauri ya kichwa chako ikafikia uamuzi wa mwisho kabisa wa kuwaza kunisaliti raisi wako ambaye ndiye nasaini hadi mshahara wako?” mheshimiwa alimpa maelezo na kumuuliza swali mwanaume huyo ambaye alikuwa ameketi chini akiegamia nondo ambazo zilikuwa kama kuta za chumba hicho.

Mwanaume huyo alikuwa amechakaa damu kuonyesha kwamba wakati mfupi uliokuwa umepita aliyapitia mateso makubwa sana ambayo yalimfanya achakae kwa damu. Vidole vyake vya mguuni havikuwa na kucha, zilikuwa zinaonekana chini kuonyesha kwamba mtu huyo aling’olewa kucha hizo kwa lazima. Damu ilikuwa bado mbichi sana kwenye vidole vyake, uso wake ambao ulikuwa na hofu kupita kiasi lakini wenye jeuri ndani yake ulikuwa unamwangalia raisi kwa dharau ya aina yake.

“Wewe ni kiongozi dhaifu sana, upo hapo kwa muda tu hata ukiamua kubaki hapo kuna watu ipo siku watakutoa tu” aliongea kwa jeuri mwanaume huyo akiwa ameketi hapo chini, mheshimiwa alitabasamu, mtu huyo alionekana kuwa jeuri sana isivyokuwa kawaida na alikuwa akiwahitaji sana watu wa namna hiyo kwani angewatumia kuweza kutuliza hasira zake ambazo zilikuwa zinamsumbua kwenye kichwa chake.

“Kuna mtu ana kisu kikali hapo?” mheshimiwa aliuliza, lilikuwa ni jambo la haraka sana, alikabidhiwa CDF ambaye moja kwa moja alimpatia raisi mkononi. Mheshimiwa alivua koti lake akiwa na kisu hicho kwenye mkono wake kisha akamsogelea mwanaume huyo ambaye alikuwa ameketi pale chini, aliwapa ishara makamanda ambao walikuwa na mkuu wa majeshi wakamnyanyua mwanaume huyo na kumketisha kwenye kiti kisha wakamfunga kwenye kiti hicho cha chuma vizuri sana kiasi kwamba akawa hana hata uwezo wa kujisogeza sehemu nyingine.

“Kweli upo sahihi kabisa mimi ni raisi dhaifu sana ila ni mimi huyu ambaye nimekufanya wewe uishi vizuri na nakulipa vizuri kwa nafasi ambayo nilikupa mjinga mkubwa wewe wakati nilikuwa nina uwezo wa kumpa hiyo nafasi mtu mwingine na mambo yakafanyika vizuri tu bila uwepo wako. Leo unanikosea heshima kiongozi wako wa nchi huku unamchukulia kawaida hata mkubwa wako wa kazi CDF hapo kwa kuamini kwamba mimi ni dhaifu hivyo hata yeye ni dhaifu kwa sababu aliteuliwa na mimi. Nimesikitishwa sana na hili jambo nilihisi huenda ungeutumia muda huu kuweza kuniomba msamaha ili nione kama naweza kukusamehe lakini ndo kwanza unaleta dharau na jeuri bado mbele yangu mimi, basi sina namna zaidi ya kukufanya ulipe kwa hiyo kauli yako ambayo umeitamka, niamini mimi hiyo kauli unaenda kuijutia sana kwa dakika hizi chache ambazo zinafuatia” mheshimiwa aliongea akiwa mwingi wa tabasamu kwenye uso wake lakini tabasamu hilo halikuashiria hali ya furaha bali hasira na uchungu kwa mtu mwenye cheo cha chini sana kwake kama hicho ambacho yeye ndiye aliye mfanikishia kukipata kumuita yeye dhaifu, alitakiwa kulipa kwa ajili ya hiyo kauli yake ya kijinga ambayo aliweza kuitamka wakati huo.

Mimi sina la ziada ukurasa wa 8 unafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA TISA

Raisi alisogea taratibu na kuchuchumaa shati yake akiwa ameikunja vyema sana ili isipate damu, kisu kikali mno ambacho kilikuwa kinang’aa kikiwa kwenye mkono wake, alikishika vyema sana. Alikizamisha kisu hicho kwenye dole gumba la mguu wa kulia wa kapteni Zola ambalo ndilo lilikuwa jina lake halisi kabisa, alilia kama mtoto mdogo kwa maumivu makali ambayo aliweza kuyapata hapo eneo ambalo muda mfupi kucha iling’olewa bila kutumia ganzi.

“SHiiiiiiiiiiiii!” raisi alimpa ishara mwanaume huyo atulie lakini aliendelea kupiga makelele kitu kilicho pelekea kupokea kofi zito sana kwenye uso wake na kumfanya afumbe macho mpaka pua zake zikawa zinatoa maji maji, uso ulibadilika na kuwa mwekundu sana kwa uzito wa kofi hilo ambalo lilitoka kwenye kiganja cha mheshimiwa raisi.

“Unaanza kuniaibisha sana, muda mfupi hapa umetoka kusema kwamba mimi ndiye mwanaume dhaifu sasa kwanini mwanaume imara kidogo tu hapo unaanza kulia? Mbona hauna misimamo bwana Zola? Nataka nikuonyeshe kwamba kati yangu na hao watu wako ni nani dhaifu sana, nadhani haujawahi kupata bahati ya kunifahamu kwa sababu haukuwa na hiyo nafasi ya kuwa karibu na mimi ila leo utanijua ukiwa hauna namna ya kuweza kuyasaidia maisha yako” mheshimiwa alitamka kwa kumkazia macho mwanaume huyo usoni kisha alikishusha kisu kwa nguvu kwenye hilo dole gumba na kukitawanyisha kidole hicho kwa hasira kitu kilichofanya damu zimrukie mpaka kwenye shati lake safi jeupe.

“Mpuuzi mkubwa wewe, unaruhusu vipi damu yako ilichafue shati langu namna hii? Oooh shiiiiiit!” alitamka kwa hasira akiwa ananyanyuka na kusogea pembeni, baada ya kukikata kidole hicho damu ilikuwa inatoka kwa nguvu sana hivyo iliweza kumrukia hata yeye na kuichafua shati yake na ndiyo sababu alikuwa anamlaumu mwanaume huyo kuruhusu damu itoke sana namna hiyo na kumchafua mheshimiwa. Kwa sababu yeye hakuwa dhaifu alitakiwa kuwa na vitamin K ya kutosha kwenye mwili wake na kuifanya damu igande haraka, kutokuwa na vitamin K ya kutosha ndiko kulimfanya mheshimiwa kuchafuka na hilo lilikuwa ni kosa la Zola, alitakiwa kulijibia vyema.

Wakati huo Zola alikuwa kwenye hali mbaya sana, alikuwa ameangua kilio kikali kwa hayo maumivu, alitamani mtu huyo angeweza hata kumuua lakini sio kufanya kile ambacho alikuwa anakifanya kwa wakati huo lakini nani angeweza kumsaidia na kauli mbovu alizitoa mwenyewe, nani angemsaidia wakati mtu huyo ambaye alikuwa anamfanyia hayo mambo ndiye ambaye alikuwa raisi wa nchi na mwenye kauli ya mwisho kabisa? Hakukuwa na msaada, hata mkuu wa majeshi hakuonyesha kabisa kufurahia jambo hilo japo hakuwa na namna ya kufanya kwani huenda angefanya chochote kibaya basi angepata matatizo makubwa kama ambayo yalikuwa yanamkuta kijana wake huyo ambaye kwa cheo alikuwa mdogo kwake.

Mheshimiwa raisi alisogea mpaka ukutani ambako kulikuwa na box moja kubwa la vifaa, aliivua shati yake na kubakia kifua wazi. Alikuwa mwanaume wa kazi haswa raisi huyo mwili wake ulionekana kukomaa haswa kwa mazoezi hata mkuu wa majeshi na vijana wake walishangaa sana kuona jambo hilo, mtu huyo walizoea kumuona tu akiwa kwenye suti za bei pamoja na nguo za kazini na siku hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza ya yeye kuvua shati mbele yao, mwili ulikuwa umejikata sana, waliogopa mno kwani raisi alionekana kuwa tofauti na vile ambavyo wao walikuwa wakimfikiria kabisa.

Raisi huyo alirudi akiwa ameshika mfuko wa chumvi kwenye mkono wake, aliimwagia karibia yote kwenye kidonda hicho ambacho kilikuwa kinaendelea kumwaga damu. Zola alihisi kama vila anakufa kufa lakini alikuwa hai, alipiga makelele ambayo yalimfanya ajikojolee hapo hapo pua zikiwa zinatoa maji maji mfululizo, alikuwa anahema mithili ya mtu ambaye anataka kufa lakini kifo kinamkataa kabisa.

“Haya mtu imara niambie wewe kufanya hili ilikuwa ni amri ya nani au ulikuwa na nani na nani ambao ulikuwa unataka kuwatumia kutekeleza hili jambo?” mheshimiwa aliongea akiwa anasogeza kiti na kukaa mbele ya mwanaume huyo, kisu ambacho kilikuwa kwenye mkono wake kilikuwa na damu ambazo aliishia kuzifutia kwenye suruali yake ya suti ya gharama sana, watu wote ambao walikuwa humo ndani walikuwa bado wanamshangaa mheshimiwa ni kama hawakuwa wakiamini kwamba huyo ndiye raisi wa nchi yao. Hata CDF alijikuta anaanza kumuogopa sana mwanaume huyo ambaye hakueleweka ni nani haswa maana alionekana kuwa tofauti na vile ambavyo wao walikuwa wanamchukulia.

“Tafadhali nisamehe sana mheshimiwa, nasema ukweli. Huu haukuwa mpango wangu bali ulikuwa mpango wa waziri mkuu mstaafu, mr Oscar” aliongea midomo yake ikiwa inatetemeka mithili ya mtu ambaye alikuwa amepigwa na shoti nyingi sana za umeme tena mfululizo bila hata kupumzika.

“Hahahaha hahahha, yule mzee ndiye alikutuma wewe ufanye haya? Kwa sababu ipi labda na ulikuwa na nani?”

“Alisema tu anataka kukujaza wasiwasi kwa sasa na kukufundisha nini maana ya hofu haswa ili mfanye mazungumzo ya kiume, hivyo akanipa hiyo kazi mimi ila sikuwa na mpango wa kukupindua mheshimiwa” aliongea akiwa ni kama mtu ambaye anajutia sana kwa kile ambacho kilitokea.

“Unajutia?”

“Ndiyo mkuu”

“Kwani kwenye hii nchi raisi ni nani”

“Wewe hapo”

“Sasa unakubalije kazi ya mtu ambaye yupo nje kabisa ya mfumo halafu unasema kwamba haukuwa tayari kunipindua? Unahisi labda kwamba mimi ni mtoto mdogo sana?”

“Hapana mheshimiwa, naomba unisamehe sana tafadhali, nina familia ambayo inanitegemea” mwanaume huyo kwa namna alivyokuwa anatia huruma kama wangekwambia kwamba alikuwa ni kapteni ungekataa kabisa

“Kwani haya ambayo ulitaka kuyafanya, haukujua kama wengine wana familia? Usinipotezee muda wangu ni usiku saivi, nambie huu mpango ulihusika na nani ukiachana na huyo mzee ambaye naenda kumshughulikia baada ya wewe”

“Nilikuwa pekeyangu”

“Hapana, haiwezi kuwa kirahisi hivyo ila kwa sababu umeamua kuwaficha wenzako haina tatizo, wewe utakuwa wa mfano na huko waliko kama wataona basi kuna funzo kubwa sana watalipata kutoka kwako na kile ambacho watakiona mimi nakufanyia wewe hapo nadhani utakuwa na adabu na wakati mwingine utakapo sikia neno raisi likitajwa kwenye maskio yako” mheshimiwa alimaliza na kutoka humo ndani na mlinzi wake kisha akatoka nje kwenda kuvuta sigara yake kwanza kukiweka kichwa chake sawa maana alikuwa kama amevurugwa tayari.

“Mheshimiwa una uhakika na hili ambalo umelifanya? Huoni kama itakuwa ni hatari sana kuuonyesha uhalisia wako hadharani sana namna hii na hawa wote humu ndani wakakuona? Kama inawezekana niwaue.” Aliongea mlinzi wa mheshimiwa raisi akiwa anaamini kwamba watu hao kumuona raisi akiwa kwenye hali kama hiyo kungeleta matatizo mbeleni lakini raisi huyo alikuwa anaendelea kuivuta sigara yake kwa pupa sana, alitabasamu akiwa anaendelea kuufaidi upepo ambao ulikuwa unapuliza hapo akiwa hajali kama walinzi wengi ambao walikuwa maeneo ya karibu na pale walikuwa wanamuona akiwa kwenye hiyo hali.

“Unajua watu wengi huwa hawazijui siri za dunia na watu walio fanikiwa ndiyo maana huwa wanaishia kwenye maisha ambayo hayaeleweki mpaka mwisho wao na huwa na mwisho wenye majuto makubwa kwa sababu ya kuamini kwamba mambo fulani yapo hivi ila baadae wanakuja kuyajua kwamba yapo tofauti. Watu ambao wanayafanya mambo yao kimya kimya na kwa usiri mkubwa sana ndio watu ambao huwa wanapata mafanikio makubwa kwa sababu hata ushindani wao ni mdogo, hiyo ni kutokana na sababu kwamba hauwezi kushindana na mtu ambaye haujui anafanya nini” mheshimiwa alitulia kidogo akavuta funda moja la sigara yake na kuendelea

“Mfano wa hao watu ni mimi hapa, mimi watu hawanijui vizuri ila wanahisi kwamba wananijua ndiyo madhara yake mpaka watoto kama hao wanaanza kuniita dhaifu kitu ambacho sikuwa tayari kukivumilia. Leo nafanya haya ili kwa watakao ona wajue hata namna ya kuniheshimu na siku nyingine wakitaka kufanya kosa kama la huyu mwenzao basi nafsi zao kwanza zijionye moja kwa moja na wasije wakathubutu kufanya ujinga wa namna hiyo” mheshimiwa alipiga funda lingine tena na kujikohoza kidogo.

“Kosa ambalo hata wewe kijana wangu usije ukalifanya kwenye maisha yako ni kuingia kwenye mtego wa kuamini kwamba wewe ni mtu wa mhimu sana kwenye maisha ya mtu fulani. Huu ndio ugonjwa mkubwa sana ambao unawateketeza watu wengi sana hususani vijana wengi mno ambao ni watafutaji, huwa wanafikia hatua wanahisi kwamba bila wao maisha hayawezi kuendelea na hicho ndicho ambacho huwa kinawarahisishia watu wenye akili kufanya mambo yao. Nenda kwenye makampuni mengi sana kuna hatua huwa inafikia mfanyakazi anataka kumvimbia hata bosi wake unakuta anatishia hata kuacha kazi akiamini kwamba bila yeye kazi hazitaenda anasahau kwamba hiyo taasisi ilikuwepo hata kabla yake na kuna watu wengi sana kama yeye na wengine wamemuacha mbali sana wanaitaka nafasi hiyo hiyo, hapo unadhani kinatokea nini? Ndo baadae hao hao huwa wananza kulalamika oooh watu wabaya mara watu wana roho za kikatili, anasahau kabisa kwamba yeye ndiye tatizo kubwa la hayo yote kutokea”

“Hilo ni moja ya makosa ambayo hata baadhi ya vijana wangu huwa wanayafanya, ndiyo sababu hata Pandei Santo nilimpoteza kwenye mazingira ya kutatanisha sana. Nimepitia wasifu wa kijana huyu nimemuona ni mtu ambaye alikuwa amebobea sana kwenye mapigano hivyo nataka nipambane naye muda huu nataka apelekwe ulingoni tena waitwe makamanda wote ambao wana vyeo vikubwa jeshini wamshuhudie mkuu wao wa nchi namna alivyo” alimpa elimu kubwa sana kuhusu maisha na namna ya kuishi na watu mlinzi wake ambaye alikuwa anajulikana kwa jina la Jafarani Msomba ambayo ilimuacha kwenye mshangao mkubwa lakini alitamka kauli ambayo ilimshtua sana mwanaume huyo. Kusema kwamba anataka kupigana na kapteni huyo ambaye aliiasi nchi tena hadharani mbele ya makamanda ilikuwa ni dharau kubwa sana, ni kumkosea heshima mheshimiwa raisi wa chini kama huyo kupigana naye kwa sababu kama angempiga hata ngumi moja tu lilikuwa ni kosa ambalo adhabu yake isingeweza kusameheka abadani.

“Hapana mheshimiwa siwezi kuruhusu hilo jambo lifanyike kwa sababu hiyo itakuwa ni aibu kubwa sana kwa taifa, watu hawaruhusiwi hata kuigusa nguo yako halafu mtu wa chini kama yule ndiye upigane naye? Hapana mheshimiwa, naichukua nafasi yako hiyo napanda ulingoni mwenyewe kwenda kumchinja huyo mjinga” mlinzi wake alikuwa makini sana kufuata itifaki kwa sababu yeye ndiye ambaye angekuwa matatizoni kama kitu chochote kile kingeweza kumtokea mheshimiwa raisi na hakujua angejibu nini hivyo aliona ni bora yeye akasimamane na kapteni huyo amuulie hapo hapo ulingoni na sio kuruhusu bosi wake kuingia hapo lakini mheshimiwa alimpiga jicho kali sana hivyo hakuwa na namna akapisha njia mheshimiwa akawa anarudi ndani kutoa amri mwanaume huyo apelekwe ulingoni.

Sehemu ya tisa inafika mwisho, panapo majaaliwa tukutane wakati ujao.

Wasalaam,
Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kama wewe ni mpenzi wa simulizi za kipelelezi ambazo ndani yake zimetawaliwa na SIASA CHAFU na namna viongozi wanavyo icheza MICHEZO MICHAFU SANA bila wananchi kujua kwa maslahi yao.....

BASI HII SIMULIZI NI SEHEMU YAKO SAHIHI.....usiplan kuikosa hasa episode moja....hili ni moja kati ya maandiko bora sana ya namna hiyo ya siasa chafu.


Kuna story kali sana
Mpangilio sahihi
Kuna actions za kutisha mno.....

Tuliza akili wakati unasoma kuanzia mwanzo maana baadae utakutana na matukio ambayo kama hukuwa makini mwanzo unaweza ukachanganyikiwa....... utakapo kuja kuambiwa nafsi moja inaishi ndani ya miili ya watu wawili tofauti ....don't panic....

Twende taratibu, utanielewa [emoji996]

Wasalaam,

FEBIANI BABUYA


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KUMI

MASAA SABINI NA MBILI YALIYO PITA (72 HOURS)
Zola, mwanaume hodari sana. Historia yake inaanzia huko wilayani Mbozi kwenye kijiji kijulikanacho kwa jila la Mahenje, pembezoni kabisa mwa milima. Huko ndiko ambako alizaliwa mwanaume huyo na kufanikiwa kupata malezi ya mama yake mzazi tu pekee kwa sababu baba yake aliuawa na wanaume ambao hawakujulikana na kutokana na usalama wa eneo hilo kuwa mdogo hakukuwa hata na ushahidi wa kuwatia nguvuni watuhumiwa wa tukio hilo.

Inadaiwa kwamba baba yake alikuwa ni mpambanaji haswa na alikuwa ameanza kuyapata mafanikio akiwa bado na umri mdogo sana hivyo watu ambao hawakuwa wakihitaji kumuona anapiga hatua hizo wakaamua kumuua mapema. Wakati baba yake anauawa mama yake alikuwa na mimba yake ya miezi saba tu kwa maana hiyo hakuwa hata amezaliwa mwanaume huyo.

Tangu kuzaliwa kwake Zola hakuwahi kumjua baba yake mzazi zaidi ya kusimuliwa tu zile stori zake njema enzi za uhai wake na kumfanya apate nguvu kubwa sana ya kupambana akiamini kwamba atamfurahisha baba yake huko aliko huku akiamini kwamba anamuona kwa kila hatua ambayo anaipiga kwenye maisha yake.

Zola alipambana sana na elimu kwa maana mama yake alimwambia kwamba ndio msaada wake wa pekee ambao umebaki kwenye maisha yake asije akacheza nao kwani ndugu wa baba yake hawakuwa kabisa na muda naye hivyo hakumuacha elimu aende zake akaamua kumshika kisawa sawa. Baada ya kumaliza darasa la saba alifaulu vizuri sana Zola lakini kwa bahati iliyokuwa mbaya sana mama yake mzazi alifariki na kumuacha akiwa mpweke bila msaada wowote ule. Kifo cha mama yake lilikuwa pengo kubwa sana kwake kwani alikosa kabisa msaada wa kumfanya aendelee na masomo ambayo aliamini utakuwa kama ukumbusho kwa mama yake ambaye alimsisitiza mwanae aweze kusoma sana.

Hiyo ilimfanya akose namna zaidi ya kukimbilia jeshini baada ya kusikia nafasi zikitangazwa kuanzia wale ambao walikuwa wamemaliza darasa la saba na kuendelea. Hakuwahi kuipenda kazi hiyo ila ndilo chaguo pekee ambalo lilikuwa kwake hivyo mwanaume huyo akajiunga na jeshi la wananchi la Tanzania kwa mara ya kwanza ambapo alipelekwa JKT Nzovwe, Mbeya. Jitihada zake, nidhamu yake na kujituma kusiko isha kulifanya mwanaume huyo kuhamishiwa mpaka ndani ya kambi ya Msangi iliyopo mkoani Tabora kwa ajili yakuendelea na mafunzo.

Hakuwahi kukata tamaa Zola kwani hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya yeye kuyapatia maisha yake na kuyafanya yawe mepesi kwa kuitumia njia ngumu. Baada ya kupewa mafunzo ya kutosha kwa muda mrefu huku akiwa mstari wa mbele kwenye kila mafunzo, kwenye kila mashindano na kwenye kila mapigano. Kwa mara ya kwanza aliweza kupangwa kwenye kikosi ambacho kilitumwa huko nchini Kongo kwa ajili ya kufanya ukombozi kwa raia ambao walitekwa na kundi la magaidi. Huko kongo sifa zake zilifika mpaka kwa wakubwa kwani ndiye alikuwa mstari wa mbele kabisa mpaka kuhakikisha raia wanarudi wakiwa salama kabisa hivyo hilo lilimfanya awekwe kwenye macho ya uangalizi sana na wakubwa.

Zola alikuwa aseti kubwa sana na mwisho wa siku akachaguliwa kuwa miongozi mwa vijana wachache ambao walipelekwa huko Morogoro kwa ajili ya kuweza kupata mafunzo ya kikomando ambako alinolewa haswa tena zaidi ya sana hususani kwenye swala zima la mapigano ambapo mkono ulikuwa sehemu ya maisha yake, mapigano yakawa kama sanaa kwake mwisho wa siku akaupenda sana mchezo huo kuliko kitu chochote kile.

Zola alikamilisha mafunzo yake na kuapa kulitumikia vazi la nchi yake kwa usahihi kwa namna yoyote ile akiwa tayari hata kufa kwa ajili ya kuhakikisha nchi yake inakuwa salama. Uzalendo wake na kulipenda vazi lake hilo kuliwafurahisha wakubwa ambapo kwa msaada mkubwa sana wa mkuu wa majeshi alipata nafasi kubwa sana ambapo baadae aliteuliwa na kuwa kepteni wa jeshi la wananchi la kujenga taifa akiwa anaifanya kazi kwa karibu sana na CDF. Mwanaume huyo aliifanya kazi yake kwa weledi sana na haki akiamini kwamba alikuwa anamfurahisha mama yake mzazi huko kaburini ambako alikuwepo wakati huo.

Zola licha ya kufanikiwa kwenye maisha yake ya utafutaji, bado hakuwa mshamba sana wa majiji kwa kuwatamani wanawake warembo ambao alikutana nao, tangu akiwa mdogo sana alikuwa na mwanamke mmoja tu huko Mahenje ambaye walikutana shule ya msingi wakaja kupendana vibaya sana, waliahidiana kwamba wangekuwa pamoja kwenye shida na raha kwani hata mwanamke huyo alikuwa ni yatima ambaye alikuwa anaishi kwa mama yake wa kambo aliyekuwa akimtesa sana na mwanamke huyo baba yake mzazi alimuoa kabla ya kupoteza maisha yake hivyo ndiye akabaki msimamizi wa nyumba na mali ambazo aliziacha baba yake mzazi.

Mateso ya mama yake wa kambo baada ya kumaliza shule ya msingi yalimfanya apakimbie nyumbani alipo zaliwa na kwenda kuanza kufanya vibarua na kazi za ndani ambapo baada ya muda alifungua kimgahawa chake huku akiwa anamsubiri Zola ambaye alikuwa jeshini. Subira ikaja kuvuta heri kwa uande wake baada ya zola kufanikiwa jeshini aliamua kwenda kumuoa huyo mwanamke wake ambaye walipendana sana na kuanza kuishi naye ndani ya jiji la Dar es salaam, mumewe akiwa ni mtu mkubwa sana jeshini na Mungu akawajaalia watoto wawili mapacha ambao waliishi nao kwa furaha sana na kuwafanya kuwa moja kati ya familia zenye furaha sana duniani.

MASAA SABINI NA MBILI YA ZOLA.
Siku tatu zilizokuwa zimepita kabla Zola hajakamatwa, alikuwa ametoka ofisini kwake na kuingia nyumbani kwake akiwa amechelewa sana. Baada ya kufika getini alishangaa kuona walinzi wakiwa wanavuja damu huku hawana uhai, aliogopa sana na kukimbilia ndani moja kwa moja ambapo alitafuta kila sehemu lakini hakuona mtu yeyote yule zaidi tu ya kupishana na miili ya walinzi wake zaidi ya kumi ikiwa haina uhai.

Alipata presha ambayo hata yeye kuielezea ingekuwa ni ngumu sana hivyo ikamfanya kukimbilia nje haraka kuweza kuona kama labda upande wa pili wa jengo hilo la kifahari ulikuwa na watu lakini baada ya kufika nje alikutana na wanaume watano wakiwa wanamsubiria yeye afike hapo.

“Ingia kwenye gari tuondoke” mwanaume mmoja alifungua mlango wa gari ambao bila shaka hata yeye alishangaa mbona kama hakuiona gari hiyo wakati anaingia? Akakumbuka kwamba aliingia kwa kasi sana akiwa anawahi ndani ndiyo maana hakuiona gari hiyo.

“Nani kawatuma?”

“Unapoteza muda mr Zola twende ili uiwahi familia yako” mwanaume huyo ni kama alimpandisha hasira sana Zola, alijishika kwenye kiuno chake lakini hakukuta kitu, akagundua kwamba silaha yake aliisahau kwenye gari yake. Alikimbia kwa spidi kali sana kumfuata mwanaume huyo, alidunda chini na kujigeuza kwa sarakasi moja ya haraka sana akamkosa mtu huyo na buti lake likatua kwenye kioo cha gari ambacho kilisambaratika vibaya sana. Aligeuka kwa ngumi kali ambayo ilitua kwenye tumbo La mwanaume huyo na kumfanya agune huku akirudi hatua kadhaa nyuma, hakumuacha atulie, alitishia kama anaenda mwanaume huyo akainama, alipokea buti kali mno kwenye uso wake ambalo lilimpeleka mbali sana.

Zola alikuwa anajiandaa kumkimbilia mwanaume yule ambaye alikuwa amedondokea chini lakini alipigwa mtama mkali wakati anataka kutua chini buti lilikuwa linakuja usawa wake wa uso lakini aliliona hivyo akatumia mikono yake kulipunguza uzito hata hivyo lilimbeba mpaka mbali sana akadunda kwenye ukuta kwa mguu wake na kusimama wima tena.

“Mke wangu na watoto wangu wako wapi?” aliuliza kwa hasira akiwa anasogea kwa jaziba mbele ya mwanaume huyo, hasira zake zilimfanya aende bila balansi yoyote ile hali ambayo ilimfanya kurusha ngumi kwa pupa, alipigwa na ngumi ya mbavu wakati anaguna kusikilizia maumivu mwanaume huyo alimdaka kichwa chake na kukizungusha mara kadhaa na kumfanya Zola kupata kizunguzungu, alivyokuja kuachiwa hakuwa hata na balansi ya kusimama wima alipigwa ngumi nyingi sana kwenye mwili wake kisha akapigwa buti la shingo. Alipata maumivu makali sana akawa anadondoka chini lakini hakupewa huo muda kwani alidakwa na kuchomwa sindano ambayo ilimfanya apoteze fahamu hapo hapo.

Alishtuka baada ya masaa ishirini na manne kupita ambapo kwenye yale masaa sabini na mawili yalikuwa yamebakia masaa arobaini na nane pekee.

“Nipo wapi? Nipo wapi?” alipiga makelele baada ya kutoka kwenye huo usingizi akiwa anahema kwa nguvu sana ila ndio wakati ambao alimwagiwa maji ya baridi sana kwenye mwili wake ambayo yalimfanya ashtuke na kukaa sawa. Aliangalia kila upande wa hicho chumba ambacho alikuwepo, hakuona cha maana zaidi ya wanaume ambao walikuwa na sura mbaya na zilizo komaa haswa.

“Familia yangu iko wapi?” aliuliza kwa wasiwasi sana mazingira hayakuwa rafiki kabisa. Hakuna aliye mjibu zaidi alihisi kama kuna sauti za viatu vya watu zikiwa zinakuja upande wa hicho chumba. Ndipo aliingia mtu ambaye hakuamini kabisa kwamba ni yeye ndiye ambaye alikuwa amefika hapo, alikuwa ni waziri mkuu mstaafu mr Oscar.

“Mheshimiwa ni wewe ndiye umenifanyia haya?”

“Usikuze mambo Zola, familia yako ipo salama na kwa sasa nimeiweka eneo ambalo wataishi kwa amani ila amani hiyo itategemea na utii wako pamoja na wewe kukubali kazi ambayo nahitaji nikupe”

“Unataka nini kwangu?”

“Swali zuri sana. Nahitaji wewe utishie kuanzisha mbio za kumtoa raisi madarakani kwa lazima”

“Whaaaaaat?”

“Nadhani umenisikia vizuri sana”

“Nahisi utakuwa umechanganyikiwa”

“Wewe ndiye ambaye umechanganyikiwa kwa kushindwa kuelewa nacho kimaanisha kwenye maelezo mafupi kama hayo”

“Kama upo kwenye utimamu wako unahisi hicho unacho niambia kinawezekana au kuna mtu anaweza kukifanya kwenye nchi hii?”

“Hilo sitaki kujua na mimi sikulazimishi kwa hilo Zola, ni wewe utaamua kama unaweza kufanya au kama hautaki basi malipo yake itakuwa ni mimi kuiua familia yako maana sasa sitakuwa na uwezo wa kukuvumilia tena mtu ambaye huwezi kuelewa vitu vyepesi kama hivyo”

“Usije ukaigusa familia yangu maana nitakuua”

“Kama ni hivyo basi hauna chaguo zaidi ya kuifanya hii kazi”

“Kwanini unanitoa sadaka kwenye sakata kama hili? Kwanini unahitaji nionekane kwamba mimi ni mwanajeshi wa hovyo sana kwa kuhitaji kuleta machafuko kwenye nchi yangu wakati mimi ndiye ninapaswa kuilinda kwa gharama yoyote ile? Kuna kitu gani haswa ambacho mimi au familia yangu tumewahi kukukosea?”

Zola nini hatima yake? Ukurasa wa kumi unafika mwisho.

Wasalaam.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KUMI NA MOJA
“Zola acha kuniuliza maswali ya kijinga wakati unajua namna siasa inavyo fanya kazi, kwenye siasa haya mambo ya kawaida sana kutoa maisha ya watu fulani ili kukamilisha jambo kubwa mbona inawezekana. Fanya kile nilicho kuagiza ndani ya siku hizi mbili kisha baada ya wewe kulikamilisha hilo tu basi naiachia familia yako” mheshimiwa alimaliza maelezo yake mafupi ambayo ungehisi anatania ila ndivyo alikuwa anamaliza hivyo kisha akanyanyuka ilia toke humo ndani hata Zola aliweza kuachiwa kwa kufunguliwa pale alipokuwa amefungwa.

“Nini sababu ya wewe kuyafanya haya yote na unafaidika na nini kulisaliti taifa lako?”

“Mhhhh unauliza sababu? Ok nahitaji yule raisi atoke Ikulu, nimetafuta sana nafasi ya kuongea naye amegoma kabisa kunisikiliza au kunipa hiyo nafasi hivyo nataka wewe utume ujumbe kwamba nahitaji kuonana naye na anitafute kabla hajachelewa maana kama akitishiwa kupinduliwa lazima atahitaji tu kuonana na mimi na wewe ni miongoni mwa watu wa mhimu sana ndani ya jeshi hivyo atalichukulia hili jambo kwa uzito mkubwa sana. Lakini kingine yule ni raisi dhaifu na mzandiki ambaye pia ni fisadi sana hafai kuendelea kukaa pale Ikulu anatakiwa kutolewa hata kwa lazima”

“Hata kama yupo hivyo kumbuka kawekwa na wananchi pale”

“Wananchi huwa wanampigia kura mtu ambaye anajua zaidi kudanganya na kuwaahidi uongo, hakuna la maana ambalo wanalijua kwenye nchi hii hivyo fanya nilicho kuagiza, na ukikutana naye mwambie ni mimi nimekutuma na nahitaji kuonana naye” mzee huyo alimalzia na kutoka humo ndani akiwa amemuachia mwanaume huyo kazi ngumu sana. Kumpindua raisi lilikuwa ni kosa ambalo hukumu yake ilikuwa ni kifo tu hata kama ulikuwa unatania basi hakuna binadamu ambaye angeweza kukuamini kwa namna yoyote ile. Zola aliwaza sana, aliiangalia sana bendera ya taifa lake ambalo alikuwa analipenda sana lakini angefanya nini na familia yake ilikuwa hatarini? Kama angekataa basi walikuwa wanakufa na aliwajua vizuri wanasiasa hawajawahi kabisa kujali kuhusu maisha ya mwananchi yeyote wala familia yoyote ile zaidi huwa wanaangalia maslahi yao tu pekee.

Wakati mheshimiwa raisi alikuwa anafanya mazungumzo na mlinzi wake nje akiwa anaivuta sigara yake, Zola alikuwa anampa maelezo mkuu wa majeshi sababu haswa ambayo ilimfanya achukue hayo maamuzi ambayo yalimpelekea yeye kukamatwa na kukutana na mheshimiwa raisi. CDF alisikitika sana kwa sababu mwanaume huyo aliyafanya hayo kwa sababu ya kuisaidia familia yake na hakuna ambaye angemwelewa na ukizingatia hata mheshimiwa raisi mwenyewe ndiye ambaye alikuwa ana hasira sana na mtu huyo ambaye alitishia kumtoa kwenye nafasi yake hivyo alikuwa na nafasi ndogo sana ya kupona na asingeweza kabisa kumtetea kwani angejumuishwa naye kwamba alikuwepo kwenye hilo sakata. Ilimuuma sana kwa sababu huyo alikuwa kama kijana wake lakini hakuwa na la kufanya ilibidi kila kitu akiache kwenye mikono ya mheshimiwa raisi ili aweze kufanya kile ambacho kingempendeza yeye mwenyewe.

Mheshimiwa alitoa maelekezo ambayo yalimshangaza kila mtu kwa kudai kwamba anahitaji kupigana na mtu huyo, licha ya mshangao hakuna mtu ambaye alikuwa anaweza kupinga kwani kauli yake ilikuwa ni zaidi ya sheria basi Zola akatolewa na kupelekwa ulingoni ili aweze kupambana na raisi wa nchi yake ili kama anahitaji kumpindua basi aanzie ulingoni kwanza na raisi huyo aliahidi kwamba kama kweli kijana wake huyo ataweza kumdondosha ulingoni atakuwa tayari kumuachia Ikulu na kukubali kupinduliwa. Ni maamuzi ambayo yaliwashtua wengi mno maana makamanda wote wakubwa ambao walikuwa na vyeo vikubwa jeshini waliitwa kuweza kushuhudia pambano kati ya raisi na mwanaume ambaye alitishia kumpindua raisi huyo.

Ulingo ulikuwa unawashangaza wengi sana, hakuna kamanda hata mmoja ambaye alikuwa ana uwezo wa kuongea chochote zaidi ya kila mtu kubaki na mshangao mkubwa baada ya kumuona mheshimiwa raisi akiwa kifua wazi tena damu ikiwa sehemu ya mwili wake. Alikuwa amesimama katikati ya ulingo huku Zola akiwa anaingizwa hapo kwa msaada wa makomando wawili ambao walimshika mikono yake huku na huko kutokana na kidole chake kimoja kukatwa, alikuwa kwenye maumivu makali sana ambayo yalimkosesha imani ya kuweza kusimama na kutembea mwenyewe.

“Huyu mnaye muona mbele yenu ni raisi wa jamhuri ya Muungano lakini ndiye amiri jeshi mkuu wa nchi ya Tanzania lakini huyo kijana ambaye mnamuona anaingizwa katikati ya ulingo ni kapteni wa jeshi la wananchi la kujenga taifa. Huyo anakuwa mwanaume wa kwanza mwenye bahati zaidi duniani kuweza kupigana na mheshimiwa raisi wa nchi yake, huenda hili jambo lilitakiwa kuandikwa kwenye vitabu vya historia ila kwa bahati mbaya sana hili jambo linatakiwa kuishia hapa hapa ndani na kama hata mmoja wenu atajaribu kulifikisha huko nje basi hato iona siku inayo fuatia mbele yake” mheshimiwa aliongea huku akiwa anawanyooshea vidole makamanda hao mmoja baada ya mwingine akiwa katikati ya ulingo ambao uliandaliwa kwa mapambano, alitulia kidogo na kuendelea;

“Jina lake anaitwa kapteni Zola, mwanaume ambaye amewahi kusifiwa sana kwa uadilifui mkubwa na mtu mzalendo ndani ya taifa hili ndiyo sababu akaipata hiyo nafasi lakini kwa bahati iliyokuwa mbaya tamaa ikaingia kwenye kichwa chake akaamua kuhitaji kunipindua ili yeye na wenzake waweze kuishika Ikulu. Nina uhakika kila mmoja wenu anajua sheria za nchi hii na katiba inavyo eleza kuhusu kosa kama hilo ambalo ni ugaidi usio vumilika, anatakiwa kuuawa lakini nimempa nafasi ya kuweza kuyaokoa maisha yake” mheshimiwa alitulia na kumgeukia tena Zola ambaye alikuwa ameachiwa na kusimama vizuri kwa mguu mmoja huku mwingine akiwa ameunyanyua kidogo upande wa mbele mithili ya mtu ambaye alikuwa ananyata ili kidole hicho kisiguse chini.

“Nimempa nafasi ya kupigana na mimi na kama akifanikiwa kunipiga au kumaliza hata dakika mbili akiwa amesimama mbele yangu basi mimi nitamuachia madaraka na kuanzia leo yeye ndiye atakuwa kiongozi mkuu wa taifa hili” mheshimiwa alitamka kama anatania kitu ambacho kilipelekea kila mtu kubaki na mshangao. Raisi alikuwa kama kachanganyikiwa kufanya maamuzi ya kijinga namna hiyo na hawakuelewa kwamba ni kipi hasa ambacho kilikuwa kinafanya anakuwa na michezo ya kitoto namna hiyo, CDF aliwapa ishara ya kuwa watulivu watu hao hawakutakiwa kuongea lolote wala chochote kwani ambaye angeingilia tu alikuwa ananunua kesi kwa kiongozi huyo jambo ambalo lingekuwa ni hatari sana.

“Zola una dakika mbili za kuyaokoa maisha yako, ukifanikiwa kunipiga au kumaliza dakika mbili ukiwa bado una uwezo wa kusimama, mimi nitakuacha wewe na Mr Oscar mfanye mnacho kitaka” mheshimiwa aliongea akiwa anaiweka mikono yake nyuma kabisa kuonyesha alikuwa akimdharau sana mwanaume huyo.

Zola alisita sana kufanya hicho kitu ila hakuwa na namna kwa sababu alikuwa amechelewa sana, hakuwa na chaguo lingine kwani kama angegoma ingekuwa ishara ya kuidharau amri ya raisi hivyo angeendelea kuiweka familia yake kwenye hatari zaidi, maji aliyavulia nguo alitakiwa kuyaoga. Alizikunja ngumi zake kwa hasira sana akiwa anauma meno yake, aliukaza ule mguu ambao kidole chake kilikatwa, spidi aliyokuja nayo alirusha ngumi kali nne mfululizo ila alipiga upepo raisi huyo alipiga magoti na kuteleza wakati ngumi zikipita juu yake Zola akaenda kutua kwenye kamba.

Aligeuka kwa nguvu mwili ukiwa unaitikia kwa namna mifupa ilivyokuwa inakazwa kwani mwanaume huyo aliwahi kupitia mafunzo ya kikomando hivyo alikuwa kamili sana. Round kick ambayo aligeuka nayo alimkosa raisi eneo la shingo lakini kabla ya kutua chini alijigeuza kwa tikitaka safi ambayo uilitua kwenye kifua cha mhesimiwa raisi na kukita hapo kwa nguvu sana kiasi kwamba mheshimiwa huyo alirudi nyuma kama hatua mbili hivi na kama angekuwa mtu dhaifu basi huenda angerushwa nje ya ulingo kabisa.

Raisi aliukunja mkono wake wa kulia, mifupa iliitikia mithili ya mti mkavu unaovunjwa, Zola alikuwa amepata moto sana hata mwili ulikuwa umemchemka mno, alijivuta kumfuata mheshimiwa alipokuwa ila ni kama walizipishanisha hesabu zao. Zola hesabu alizokuwa amezipiga ziliwahiwa mara mbili kwani mheshimiwa naye alijisogeza kwa kasi ambayo ilimshinda Zola kwenda nayo sawa hivyo yeye aliwahiwa, alipokea ngumi nzito ya kifua na kumfanya atapike damu ila hakupumzishwa viganja viwili vilipitishwa kwenye paji lake la uso alibaki amezubaa kama zoba. Akiwa amesimama na kushika kichwa chake ambacho bila shaka kilikuwa na maumivu makali sana alipokea mtama mkali ambapo kabla ya kutua chini alipigwa na ngumi tatu kifuani, palisikika kishindo cha kama kitu kuvunjwa hivi.

Zola alijigongesha kwenye kamba ambazo zilikuwa pembezoni mwa huo ulingo akarudi tena alikotokea ambapo alishikwa ubavuni, mbavu ilivunjwa na mkono mmoja kisha akapigwa na kiganja kwenye bega lake, alipiga magoti huku akiunguruma kama simba jike ambalo limekosa chakula. Kilikuwa ni kipigo cha kikatili sana na cha kutisha ambacho kilimfanya kila aliyekuwa anaangalia afumbe macho yake, watu hawakuwa wakiamini kwamba huyo ndiye raisi wa nchi yao ambaye pengine walikuwa wakimchukulia poa sana kwenye kila kitu. Zola alihitaji kunyanyuka lakini alishindwa, alikuwa akitapika damu nyingi sana kwenye mdomo wake alidondoka na kulala chini akiwa anahema kwa shida na mikono yake ameiweka kichwani kwa maana kichwa kilikuwa kwenye maumivu makali isivokuwa kawaida. Raisi aliwapa ishara wale makomando ambao walikuwa wamemleta wamnyanyue na kumshikilia huku akiwa anaiangalia saa yake, alikuwa ametumia dakika moja na sekunde thelathini, alitabasamu. Mwanaume huyo alinyanyuliwa na kushikwa huku na huko kisha yeye akawa katikati.

“Amejitahidi sana kuweza kumaliza dakika moja na nusu hivyo mtihani amefeli maana nilimpa dakika mbili. Najua huenda kuna wengine miongoni mwenu mliwahi kuwaza au kuwa na akili kama za huyu mwenzenu ila kama uliwahi kuliwaza hilo shukuru MUNGU mimi sijakupata kwa maana malipo yake ni kifo na sina msamaha juu ya hilo. Huyu anakuwa mfano kwenu na ole wake nije nimjue mwingine kwamba ana mipango ya chini chini kuhusu mimi, mimi ni raisi wa nchi ambaye nina uwezo wa kupata taarifa za taifa zima ndani masaa ishirini na manne tu hivyo msihisi sijui mambo ambayo yanendelea ndani ya nchi hii na kama mnawaza hivyo basi mtakuwa mnafanya makosa makubwa sana” mheshimiwa aliongea kwa sauti ambayo alikuwa ana uhakika kwamba kila mtu alikuwa akimsikia vizuri kisha aliitoa bastola kwenye kiuno chake na kumlenga Zola kichwani, alimpiga risasi sita kitu kilicho pelekea kichwa hicho kupasuka vibaya sana na damu kuwadondokea wale makomando. Boniphace Walawala aliitupa bastola hiyo chini na kuondoka hilo eneo akiacha maswali mengi sana na hofu kubwa kwa makamanda wake wa jeshi ambapo hawakumuelewa na hawakujua raisi wao alikuwa ni nani hasa.


Mr Apson Limo tangu akutane na raisi wa nchi yake hakuwa sawa, japo aliongea kijasiri sana mbele yake ila bado nafsi yake ilikosa kabisa Amani na kumfanya kuwa mtu mwenye mawazo kwa sababu alijua yule ni mkuu wa nchi mpaka wakati huo hivyo angeweza kufanya jambo lolote lile hususani kwenye familia yake na wakapata matatizo. Usingizi haukuwa sehemu yake usiku huo, alikuwa amekaa nje pekeyake karibu na bustani yake ya maua akiwa amejiinamia mawazo yakiwa mbali sana.

Mkewe alikurupuka usiku wa manane na kushtuka baada ya kuona kitandani yupo mwenyewe na mumewe hayupo. Aliangaza kila upande lakini hakuona mtu ikamlazimu kusogee kwenye saa ili kujua kama labda ni mapema kumeshakucha lakini alishangaa baada ya kuona ni saa nane ya usiku akawa na mashaka sana kwenye moyo wake. Alinyanyuka na kuelekea kwenye maktaba ya mumewe napo huko hakuona mtu yeyote basi akatoka nje ambako alikuwa anawaona tu walinzi wakiwa wanazunguka lakini hakumuona mumewe hivyo akalazimika kuzunguka upande wa nyuma ambako kulikuwa na bustani nzuri sana ya maua ndipo alipo muona mtu kwa mbali akiwa amejiinamia chini, alisikitika na kumuonea sana huruma baba wa watoto wake. Alisogea na kukaa pembeni huku akiwa anamwangalia mumewe kwa huruma sana

“Ni usiku sana saivi unatakiwa uweze kulala. Unajua kabisa mimi siwezi kulala mwenyewe kitandani, kumbato lako huwa ni mhimu sana kwangu na ndiyo maana nimeshindwa kabisa kupata usingizi. Nini shida baba angu?” Alibahatika kupata mke bora sana na ambaye alikuwa akimjali sana, aliuinua uso wake na kumwangalia mkewe kwa huruma sana maana hata macho yake yaliongea juu ya jambo hilo.

Hadithi hii nzuri ya wapendanao inatuhitimishia ukurasa wa kumi na moja. Panapo majaaliwa tukutane wakati mwingine.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kama unataka kuyapata maandiko yangu yote ya kipelelezi. Haya hapa[emoji116]

1. GEREZA LA HAZWA......5000 FULL

2. ULIMWENGU WA WATU WABAYA......3500 FULL

3. I WANT TO DIE JUDGE....... 3500 FULL

4. INNOCENT KILLER (THE REVENGE).....5000 FULL

5. NYARAKA NUMBER 72 (DOCUMENT NUMBER 72)......4000 FULL

6. ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD).....5000 FULL (4000 KWA ILIPO ISHIA)

7. JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)....5000 . KUNA SPECIAL OFA KWA LEO TU NI 3500 (LEO TAREHE 14, JANUARY 2024 TU)


Short stories (hizi utachagua unayo itaka wewe, ukinunua moja ya juu hapo short story unapewa free tu kupooza kichwa.

8. MIMI NAITWA GAMA

9. ABELA NDIYE MUUAJI

10. NILIUA KWA SABABU YA KUKULINDA "NITAKUUA DAVINA"

11. NAFSI YANGU-MAUTI YANGU)

12. MASAA 840 YA BINTI WA RAISI (35 DAY-Z)

13. HATIMA YA UJINGA WAKE

14. COLLEGE ROMANCE


Namba za malipo.

0745982347 (M-PESA)

0621567672 (HALO-PESA)......WhatsApp number

0714581046 (TIGO-PESA?

Zote jina moja FEBIANI BABUYA.View attachment 2871419View attachment 2871420View attachment 2871421View attachment 2871424View attachment 2871422View attachment 2871423
FB_IMG_1704861903330.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hii story naona imepotezewa though ni one of the best....


Ngoja niachane nayo.


Tutaisoma JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY) instead.
JamiiForums1269194562.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KUMI NA MBILI
“Naomba unisamehe sana kwa kuwa na mume kama mimi, hata watoto wangu wanatakiwa kunisamehe sana mimi kuwa baba yao. Kuna muda unafika nawaza sana kwamba huenda ningekuwa mbali na haya maisha ningekuwa mtu mwenye furaha sana na familia yangu ila naiona furaha ikififia kila saa moja linavyokuwa linasogea mbele, hali hii inanifanya naogopa sana” Alitulia akiwa anamwangalia mkewe bado kisha akaendelea.

“Kwa sasa nahitaji Tommy arudi, nahitaji wanangu wote niwe nao karibu huenda nitaweza kuwalinda, huko aliko sijui hata kama kuna usalama wa kutosha. Namhitaji mwanangu niwe namuona sitaki jambo lolote baya liweze kumtokea huko aliko maana sitaweza kujisamehe kamwe” Alitamka kauli ambazo zilikuwa ni nzito sana mbele ya mkewe kiasi kwamba mkewe alibaki anamshangaa tu asielewe mwanaume huyo alikuwa amekumbwa na nini hasa kwa kipindi hicho kwani alikuwa anaongea kama mtu ambaye anataka kuacha usia kabla ya kuondoka jumla.

“Baba Patrina unamaanisha nini kuongea maneno mazito kama hayo?”
“Nisikilize mke wangu, najua wewe ni mke bora sana kwangu, najua wewe ni mama bora sana kwa wanangu na sina mashaka na wewe kabisa hata ikija kutokea siku sipo utaiendesha vizuri sana hii familia, huwa nakuona wewe kama ni mimi mwingine hivyo nakuamini sana mke wangu”

“Una maanisha nini kuniambia hivyo?” Mkewe aliuliza kwa ukali huku machozi yakiwa yanaanza kumtoka kwenye uso wake, maneno ambayo mumewe alikuwa anamtamkia hapo hadharani hayakuwa mazuri sana, yalikuwa ni maneno ya kuogofya na kuitisha nafsi yake na hakuelewa mwanaume huyo alikuwa amekumbwa na nini haswa kwenye nafsi yake.

“Kuingia kwenye siasa ndiyo maamuzi ya hovyo zaidi mimi kuweza kuyafanya, ni maamuzi ambayo naona siku moja yanaweza kunitokea puani na kunifanya nijutie kwenye maisha yangu yote. Wenye nchi yao wanaihitaji hii nafasi niliyo nayo niiachie na nijiweke mbali na siasa kwa kigezo cha kunitaka hata niumwe ili wananchi wakose hoja, hata mheshimiwa raisi naye anahitaji nitoke kwenye hii nafasi kwani anahisi mimi ndiye nitamletea shida huku akitishia hata kunidhuru hata mimi maana yake familia yangu inaweza kutumika kama udhaifu wangu hivyo haipo salama tena. Naogopa sana mke wangu” Mwanaume aliongea kwa uchungu sana mbele ya mkewe ili aelewe kwamba ni kwanini alikuwa hawezi hata kuupata usingizi usiku wa siku hiyo. Hata mkewe alichoka, midomo ilibaki inatetemeka tu hakuwa na la kufanya, michezo ya siasa aliijua vizuri, maisha ya watu yalikuwa yakitolewa sadaka na hakuna mtu ambaye alikuwa na muda hata wa kujali, watu walikuwa wanauawa lakini kila mtu alikuwa anaangalia maslahi yake binafsi tu.

“Mimi nipo tayari kuishi maisha yoyote yale na wewe, mimi nipo tayari kuishi popote pale na wewe ila sipo tayari kuona hii hali inakukuta ukiwa hivi, sitaki uwe mnyonge sana namna hiyo wakati wewe ndiye baba wa familia. Wanao wanajua kwamba wana baba jasiri sana na shupavu mno sasa wakiona unafikia hatua ya kukata tamaa namna hii utawavunja moyo sana na watakata tamaa. Wewe ni mwanaume ambaye kukuchagua ndilo jambo bora zaidi kuwahi kulifanya kwenye maisha yangu, maisha yako hayalindwi na mtu bali Mungu tu. Dunia tuliyopo haitupi uhakika wa kuishi kwa amani kwa sababu tulizaliwa kuteseka mpaka siku tufe ndipo tukapumzike hata maandiko ynasema hivyo, mimi nitakuwa bega kwa bega na wewe na nitakuwa mtu wa kwanza kwenda kukupigia kura, hao wanataka kukukatisha tamaa juu ya ndoto zako ambazo wananchi wako wanazitamani ziweze kuwaletea mabadiliko makubwa. Kapambane kamanda wangu mkeo mimi nakupenda sana na nina imani wewe utakuwa mshindi kwa namna yoyote ile” Familia ndiyo nguvu ya kwanza ya mwanaume mpambanaji na ndicho kitu ambacho alikuwa anakiishi Mr Apson Limo, mwanaume ambaye akili yake ilikuwa inategemewa na watanzania kuleta ukombozi, alifikia hatua akawa amekata kabisa tamaa ya maisha lakini mkewe kipenzi alikuwa naye karibu muda wote kumpa faraja.

Maneno ya mkewe yalimpa nguvu sana, hakutakiwa kudhoofika kwa kauli za watu ambao walikuwa wanamtishia ili kumtoa kwenye njia yake bali alitakiwa kuwaonyesha kwamba yeye hakuwa mnyonge hata kidogo, alikuwa ni mwanaume aliye kamili ambaye angeibeba nchi kwenye mabega yake. Alinyanyuka na kumkumbatia mkewe kwa nguvu sana akiwa anacheka mno, mkewe alikuwa amempa tumaini jipya kwenye moyo wake ambalo lilikuwa kama limechochea kasi ya uwakaji wa moto ndani yake, alimpiga mabusu mengi sana mkewe kisha akambeba kwenda naye kitandani ambako waliyamaliza kikubwa zaidi huku wakiwa na matumaini mapya ya maisha.

Saa saba usiku wakati watu wenye pesa wakiwa wanaendelea kuzitumia pesa zao kwenye kumbi za starehe huku maskini wakiwa wanaumiza kichwa kwa kuihofia kesho yao ambayo ilikuwa inakaribia kwa kasi sana na kuwafanya waisogelee siku nyingine ya kuendelea kuteseka. Baharini wanaume wawili wazito walikuwa wamekutana ili kufanya mazungumzo ya kiume haswa na ndiyo maana walichagua eneo hilo ambalo waliamini kwamba lilikuwa salama sana kwa upande wao.

Raisi wa nchi ya Tanzania Boniphace Walawala alikuwa amekutana na mr Oscar ambaye alikuwa ni waziri mkuu mstaafu wa nchi ya Tanzania, wanaume hao walikuwa na mazungumzo mazito sana ikiwa ni mpango wa Mr Oscar baada ya kuhitaji kukutana na huyo mwanaume kwa muda mrefu sana lakini ilikuwa ikishindikana kabisa kutokana na mheshimiwa raisi kuupuuzia wito wa kigogo huyo mpaka pale alipoamua kutishia kuipindua nchi kupitia kapteni wa jeshi.

Wanaume hao walikuwa wameandaa boti moja ya kifahari sana ambayo ilikuwa na ulinzi wa kutosha, humo ndimo walimo kutania kwa ajili ya hicho kikao chao ambacho kila mtu alikuwa ana msongo sana na mwenzake. Mezani kulikuwa na vinywaji ghali sana ambavyo waliendelea kuvishushia taratibu baada ya kukutana kabla ya kuyaanza mazungumzo yao.

“Kuna kitu gani ambacho ulikisahau kwenye siasa na hukukifanya kipindi ambacho wewe ulikuwa waziri mkuu?” raisi alimuuliza mwanaume huyo huku akiwa anashushia glass ya wine kwenye kinywa chake.
“Kwenye siasa naweza kusema kwamba nilisahau kila kitu kwa sababu siasa kila siku inabadilika, kila siku inakuja na vitu vipya na watu wapya vile vile kwahiyo kusema niliondoka na kila kitu nadhani utakuwa ni uongo” mr Oscar alijibu huku naye akishushia wine yake.
“Unajua nimeacha mambo mengi sana mpaka nakuja kukutana na wewe hapa? Ulicho kifanya nitashughulika nacho baadae ila kwa sasa naomba uniambie kwamba unataka nini hasa kutoka kwangu?” raisi alikuwa anaongea kiwepesi sana ila macho yake yalikuwa yakizungumza kwa hasira ambazo alikuwa nazo juu ya huyo mtu ambaye alikuwa mbele yake.

“Mimi nataka jambo dogo sana kutoka kwako mheshimiwa, nahitaji ukubali kuyaachia madaraka kisha hiyo nafasi apewe yule kijana mr Mafupa”
“Hiyo ndiyo sababu iliyokufanya uhangaike mpaka kumtuma yule kijana atishie kunipindua madarakani?”
“Hivyo ndivyo ambavyo siasa inafanya kazi mheshimiwa raisi”
“Mhhhhh hivi una familia labda?”
“Usiniambie kwamba unajaribu kunitisha mheshimiwa?”
“Swali langu ni rahisi sana kama utaamua kulielewa ila ni gumu sana kama utaamua kuleta ufahari wa kulijibu. Una uhakika kabisa kichwa chako kina akili za kutosha mpaka ukawaza kufanya jambo la kijinga sana namna ile? Unaweza ukanipa sababu ambayo itanishawishi nisikuue?” mheshimiwa aliongea kwa sauti nzito sana huku akiitoa sigara yake na kuiwasha kisha moshi akaupulizia usoni kwa waziri huyo mstaafu.

“Huenda natakiwa kukuheshimu kwa sababu wewe ni raisi wangu ila unatakiwa kuwa na kumbukumbu nzuri kwamba kwenye siasa umenikuta na huenda kuna mengi sana ambayo umejifunza kutoka kwangu. Hii nchi mimi naijua kuliko wewe, hawa wananchi mimi nawajua kuliko wewe lakini kikubwa zaidi ni kwamba mimi ni miongoni mwa wale waasisi wa hiki chama ambacho wewe ndiye unaye kiongoza. Mimi nakijua hiki chama hata mara tano ya unavyo kijua wewe, nawajua watu wengi sana kuliko unavyo wajua wewe lakini mimi ni mtu mwenye nguvu sana kwenye hiki chama kuliko mtu yeyote yule hivyo naweza kukutoa hapo muda wowote ule kuanzia sasa hata kwa lazima ila nimeamua kutumia ustaarabu na kukuomba ukubali kuachana na hiyo nafasi kwa amani ila kama utaamua kuhitaji nitumie nguvu sawa nitafanya hivyo” walikuwa ni mafahari wawili ambao walikuwa wanaonyeshana jeuri, waziri huyo alijihisi kwamba yeye ndiye ambaye alikuwa mtu wa mhimu zaidi kuliko hata raisi wa nchi hivyo jambo hilo lilimpa nguvu na kiburi kikubwa sana kiasi kwamba akawa anaongea na raisi wake mithili ya kijakazi wake.

“Kuwa wa kwanza haimaanishi kwamba ndio kuwa sahihi hivyo kuwa muasisi haimaanishi wewe unajua kila kitu kwa sababu haujawahi kupata hata nafasi ya kukaa Ikulu hivyo wewe ulikuwa mbwa kama mbwa wengine tu ambao walikuwa wanatumwa. Ulicho kifanya nimekipokea kwa uzito wake ila sitakuua nakuacha hai, sikuachi hai kwa sababu unafaa kuishi hapana ila nataka ushuhudie kitu ambacho kinatokea. Niamini mimi baada ya wewe kushuhudia hilo nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe. Najua huyo bwana mdogo atakuwa alikushawishi na kukupa ahadi ya kukurudishia mali zako zote ambazo zipo chini ya serikali ndiyo maana ukakubali kumsaidia ila kwa bahati mbaya unacheza na mtu ambaye siyo kipimo chako. Mr Oscar hili nitaliacha lipite mpaka pale ambapo jambo hili litaisha kisha nitakuthibitishia kwamba wewe ni mtu dhaifu sana na hizo nguvu ambazo unasema kwamba unazo hauna na mimi ndiye ninaye amua kwamba nikuue lini au uendelee kuishi. Kama una jambo lingine niambie haraka sana nina dakika tano za kuweza kukaa hapa na wewe” mwanaume wa shoka ambaye ndiye alikuwa raisi alimjibu kijasiri kigogo huyo kumthibitishia kwamba yeye si kitu mbele yake.

“Una uhakika utakaa Ikulu tena? Una imani na watu ambao wanakuzunguka na unafanya nao kazi? Bwana mdogo utajutia sana kuikataa nafasi hii ambayo nimekupa leo ufanye maamuzi kwa amani ukaikataa. Likumbuke sana hilo”

“Mhhhhhhhh mhhhhhhhhhh mimi ndiye ambaye natakiwa kukupa wewe pole kwa sababu unahitaji kushindana na mkubwa wako wa nchi, yaani unapambana na mtu ambaye hata haumjui vizuri ni nani na yupoje. Siku ambayo utakuja kunifahamu ni siku ambayo hautakuwa na maisha tena, kumbuka mimi ni raisi wako, mimi ni bosi wako ninaweza kufanya lolote hata leo ukaishia kufungwa au kuuawa ila nakuacha hai, nakuacha hai kwa sababu……” alitaka kuongea lakini alisita kidogo

“Nataka uwe mtu wa mwisho kufa baada ya kuujua ukweli ila usisahau una binti mrembo sana ambaye umemficha kwa sasa. Sio hilo tu pili una mwanamke mrembo sana ambaye kwa mzee kama wewe hakufai kabisa, utashuhudia kwa macho yako nikiwa nafanya mapenzi na mwanao na yule mwanamke wako hahahhahhahahah hapo ndipo utaelewa watu ambao unahitaji kushindana nao wapoje” hilo ni jambo ambalo lilimshtua sana mr Oscar, kuna mambo ambayo yalikuwa ni siri yake yeye hususani kuhusu uwepo wa binti yake bila kumsahau huyo mrembo ambaye ndiye alikuwa kimada wake, sasa raisi alijuaje kuhusu hayo? Aliichomoa bastola na kumyooshea raisi kichwani wakati amenyanyuka na kuanza kutoka humo ndani.

“Nitakuua mshenzi mkubwa wewe” alitamka kwa hasira sana lakini mwanaume huyo hakumkopesha, alimgeukia na kumwangalia kwa msisitizo sana
“Usisahau kwamba aliyepo mbele yako ni nani, unamnyooshea bunduki raisi wa nchi yako? Kama unahisi unaweza achia hiyo risasi yako nikuone unavyo jua kulenga. Kwenye hizi vita unapo taka kushindana na watu wakubwa jambo la kwanza hakikisha hauna kitu ambacho kinaweza kuwa udhaifu mkubwa kwako kwa sababu unaweza ukajuta baadae na kuwalaumu watu. Nikutakie usiku mwema mr Oscar, ni matumaini yangu umeyafurahia mazungumzo yetu hivyo natarajia tutakutana wakati mwingine hivi karibuni” dawa ya jeuri ni kiburi hicho ndicho alicho kutana nacho mr Oscar, alihisi kwamba huenda yeye ndiye ambaye alikuwa na akili sana ila wanadamu walimuonyesha kwamba yeye kwenye huo mchezo bado alikuwa kinda sana na alitakiwa kabisa kutulia kwani madhara yake huenda asingeweza kuyahimili. Mheshimiwa alitoka mpaka nje kabisa ya boti hiyo ambayo ilikuwa inatembea, kuna boti nyingine ya kifahari ambayo ilikuwa inamsubiri hapo alipanda na kutoweka hilo eneo huku akimuacha mwenzake kwenye sitofahamu isiyo na mwelekeo wowote ule.

Ukurasa wa kumi na mbili unafika mwisho, panapo majaaliwa tukutane wakati ujao.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KUMI NA TATU
Patrina alikuwa kwenye kampuni yake kubwa ambayo ilikuwa ikijihusisha na mambo ya urembo, ni kampuni ambayo ilikuwa inafanya vizuri sana sokoni kwa sababu wateja walikuwa wanakipata kile ambacho walikuwa wanakitegemea kutoka kwake. Baba yake alikuwa anajivunia sana mwanae huyo kuwa mtoto wake wa kwanza kwani alikuwa ni mfano mzuri sana kwa wadogo zake wengine ukiacha Tommy ambaye alidaiwa kuwa na akili ambazo hazikuwa za kawaida.

Mwanadada huyo alikuwa ana hamu kubwa sana hilo sakata la uchaguzi liweze kuisha haraka kwani alikuwa ameahidiwa na baba yake kwamba jambo hilo likiisha basi baba yake atamfungulia kampuni kubwa zaidi ya urembo ambayo huenda ikawa ndiyo kampuni bora na ya kisasa zaidi ndani ya bara zima la Afrika. Alikuwa kwenye ofisi yake akiwa amependeza sana anaangalia kila kona ya chumba hicho ambacho kilikuwa kimepambwa sana.

Macho yake yaliishia kwenye simu akiwa anaangalia picha ambazo alikuwa amepiga na mwanaume ambaye alimpenda sana, hakuwa mwingine bali Remsi ambaye alimuahidi kwamba jambo hilo litakapo isha basi ataenda kumvesha peta wakati anajitambulisha kwa wazazi wake. Akiwa anaendelea kutabasamu huku akiunyonga nyonga mwili wake simu yake ya mezani ilianza kuita kwa fujo sana hivyo akaipokea haraka.

Simu hiyo ilimpa tabasamu sana, akamwambia katibu wake amruhusu mtu huyo ambaye alifika kumuona haraka sana aweze kuingia humo ndani. Alikuwa mpenzi wake ndiye ambaye alikuwa amefanikiwa kuingia hapo, alimkimbilia na kumkumbatia kwa mahaba mazito ambayo yalijionyesha waziwazi kwenye macho yake. Hawakuongea kwa maneno bali vitendo vilijionyesha, bwana huyo alimbeba na kuupush mlango ambao ulikuwa pembeni, huku kulikuwa na chumba kikubwa sana cha kupumzikia.

Waliamua kuisahau dunia kwa muda na kusahau kwamba ulikuwa ni muda wa kazi, walifanya mapenzi mfululizo kwa saa zima wakiwa hawana nguo hata moja kwenye miili yao na ndipo baada ya kumaliza walipo lishtukia jambo hilo.
“Mhhhhh utakuja uniue bure wewe mwanaume uwe unanipa hata muda napumua”
“Nifaidi nikiwa bado nipo hai”
“Ok, kuna shida gani imekuleta hapa? Maana sio kawaida yako wewe kunifuata kazini tena bila taarifa”
“Yes, upo sahihi. Nimekuja hapa kwa lengo moja tu, unajua siku moja natamani sana niweze kufanya surprise nyumbani kwenu ila bahati mbaya sana sijui hata ratiba zenu zipoje kuanzia ndugu zako, wazazi wako hata shemeji zangu pia” mwanaume huyo aliulizwa swali ambalo kwa mtu ambaye alikuwa timamu alitakiwa kumhoji sana ila kwa sababu ya mapenzi kumtia upofu Patrina alihisi huenda ni moja ya njia za upendo mpaka mwanaume huyo akawa anahitaji kuijua familia yake vizuri hivyo kwake aliona kama ni bahati na hakuona kama kuna tatizo lolote.
“Sasa kumbe ni hilo tu? Si ungeniambia hata kwenye simu” aliongea akicheka kisha akasogea kwenye droo moja kubwa ambapo alitoa notebook na kumkabidhi bwana huyo

“Humo ipo ratiba nzima ya familia yetu yote kasoro mdogo wangu wa kiume tu ambaye yupo nje ya nchi”
“Haujawahi kunipa maelezo ya kutosha kuhusu huyo shemeji yangu ambaye yupo nje ya nchi”
“Unataka kumfahamu kwani?”
“Ndiyo”
“Huyo huwa sioni kama ni mtanzania halisi maana ameutumia muda mwingi wa maisha yake akiwa nje huko. Ni mtu mwenye akili ambazo ni wanadamu wachache sana wanapata bahati ya kuwa nazo, yaani namaanisha kwamba ana uwezo mkubwa mno ambao sio wa kawaida kwa wanadamu. Amesoma sana na kwa sasa amemaliza hivyo muda wowote ule anatarajia kurudi nchini”

“Naweza kumuona hata kwa picha?” Patrina hakujibu kitu aligeukia juu ya kabati, hapo palikuwa na picha kubwa sana ya watu wawili ambao walifanana sana wakiwa ndani ya suti za bei ghali mno. Mwanaume huyo baada ya kuiona picha hiyo aliiangalia kwa umakini mno ni kama kuna kitu alikuwa anahitaji kukidadisi kisha akatikisa kichwa kuonyesha kwamba alikuwa ameridhika na jibu ambalo alipewa.
“Nafikiri nitakupigia simu mimi ngoja niwahi kwenye majukumu mengine”
“Unataka kuondoka mara hii tena?”
“Ndiyo”
“Hata haujanifurahisha kabisa”
“Nilikumisi tu ndio maana nikataka nije kufanya mapenzi na wewe kisha niendelee na ratiba zangu zingine” mwanaume huyo alidanganya na kumbusu mwanamke huyo mdomoni ambapo alibaki anajichekesha tu huku mwamba akiwa anaishia mlangoni. Binti hakujua kwamba kutoa siri za familia alikuwa anaiweka familia yake kwenye hatari kubwa sana.

Siku zilikimbia sana na majuma kalikatika huku harakati za maisha zikiwa zinaendelea kama kawaida lakini pia maandalizi ya uchaguzi yalikuwa yanaenda kwa kasi isiyokuwa ya kawaida watu wakizidi kuliongelea suala hilo kwa umakini lakini matumbo joto yalikuwa yanaendelea kuwapata wale wagombea hususani wote ambao hawakuwa na imani sana na nafasi zao. Rushwa ilikuwa inatembea kila sehemu watu wakiendelea kujitengea watu wao ili unapofika wakati wa uchaguzi wawe sehemu salama zaidi za kuweza kuwafanya waingie sehemu ambazo walizitaka lakini pia mauaji hayakuisha kwa wale ambao walionekana kuwa kikwazo kwenye maslahi ya watu fulani.

Mitaa ilikuwa inachafuka kwa vurugu za wapinzani mtaani kila mtu akimtambia mwenzake, chama hiki kikitamba na kwamba ndicho kilipaswa kuiongoza nchi na chama kingine hivyo hivyo lakini pia mauaji ya wananchi hayakuisha baadhi ya maeneo huku polisi wakibebeshwa msalaba kama ilivyo kawaida kwani watu hao wakifanya mema huwa hawaonekani kabisa ila siku wakifanya mabaya basi kila mtu ni lazima aweze kuyaona na walisha amua kuzikubali lawama hizo kwani ni moja ya sehemu ya majukumu yao.

Mitandao ya kijamii pia haikuwa nyuma kwa sababu ilitumika kama sehemu ya kufikisha ujumbe kwa watu wengi tena kwa haraka zaidi hivyo ilitumika sana japo matumizi yake mengi yalikuwa kwa ubaya na sio kwa wema maana viongozi badala ya kuitumia kusambaza sera zao ni namna gani wangeweza kuileta Tanzania iliyokuwa bora zaidi wao walikuwa wakiitumia kutukanana, kupigana majungu na kukashfiana kitu ambacho kilikuwa kinaendelea kuzua taharuki juu ya hatima ya nchi kwa maana watu wengi hawakuwa wakiona kama watu hao wanafaa kuiongoza nchi kwa sababu hawakuwa na maono yoyote juu ya Tanzania ijayo zaidi ya kubeba visasi moyoni na tamaa ya madaraka.

Huo ndio wakati ambao wananchi walianza kumkimbilia Apson Limo, mwanaume pekee ambaye alikuwa ana uwezo wa kuutuliza umati wa mamilioni ya watu kwa kauli yake moja tu pekee. Ni tajiri ambaye alijitolea kila alicho nacho kuweza kuwasaidia wananchi, ni kiongozi ambaye alikuwa amebeba maono makubwa sana juu ya baadae ya nchi ya Tanzania, ni kiongozi ambaye hakuwa na muda wa kutoa lugha chafu kuhusu viongozi wengine zaidi zaidi alikuwa anatengeneza hoja za namna watanzania wanayo paswa kuyafanya ili kuweza kushirikiana na viongozi wao kuitengeneza nchi yao.

Hilo jambo lilimtofautisha sana na wenzake wote hivyo wananchi nchi nzima walikuwa wanaliimba jina lake kila sehemu, kila kona ungekutana na mabango yake watu wakimuimba kama shujaa wao na kwa namna yoyote ile walikuwa wanamuweka Ikulu bila kipingamizi kwani waliamini kwamba ndiye alikuwa mkombozi wa taifa lao. Usiku akiwa ameketi nyumbani kwake na familia wakiwa wanaangalia taarifa ya habari na namna watu walivyokuwa wanamhitaji, getini kwake alifika mtuma ujumbe mmoja ambaye aliacha ujumbe kwenye bahasha hapo.

Ujumbe huo ulikuwa unamtaka aweze kujiengua kwenye hiyo nafasi ambayo yupo haraka sana na mpaka kesho mchana awe ameliweka hilo jambo hadharani kwa usalama wake na wa familia yake. Ujumbe huo uliandikwa kwa maandishi makubwa huku ukiwa umesindikizwa na sahihi ambayo ilipigwa kwa kutumia damu. Alikuwa amesha amua kuyafuata maamuzi yake hivyo hakuwa na muda wa kurudi nyuma, aliichukua karatasi hiyo na kwenda kuichoma moto, kwa wakati huo alikuwa na moto sana kwenye moyo wake, alikuwa anajiona kama ni raisi wa nchi tayari na alikuwa tayari kuwapeleka watanzania kwenye nchi ya ahadi.

Asubuhi na mapema kulikucha salama na masaa yakawa yanaenda kwa kasi sana mpaka mheshimiwa aliporudi nyumbani jioni baada ya kupigiwa simu ya ghafla na mke wake. Simu hiyo ilimshtua sana ndiyo maana aliamua kuwahi kwa sababu hakuwa na namna maana aliambiwa kwamba nyumbani hakukuwa kwema kabisa, kulikuwa na hali ya hatari isivyokuwa kawaida.

Alipofika nyumbani kwake ndipo aligundua kwamba binti yake Latifa hakuwepo, alimuuliza mkewe kama mwanae yuko wapi? Mama huyo alijibu akiwa analia kwamba walimu walidai aliondoka shuleni na walinzi wake kama siku zote mapema sana lakini kitu cha ajabu mtoto huyo hakuwa amefika nyumbani. Mzee Limo alichanganyikiwa, alikuwa anampenda sana kifunga mimba wake. Aliamua kuitrack ile gari ambayo mwanae alikuwa anapelekwa nayo shule, gari hiyo ilionekana kuwepo pembezoni mwa bahari hivyo alitoka nje haraka na mkewe na walinzi wake na kuelekea huko baharini lakini kitu ambacho alikutana nacho huko kilimtisha na kilimshangaza sana.

Walinzi wanne wa mwanae walikuwa wameuawa kikatili sana ndani ya hari hiyo huku mwanae huyo akiwa haonekani humo ndani, mkewe alianza kuangua kilio ikamlazimu yeye aanze kumbembeleza wakati mama huyo akiwa analia na kudai kwamba anamtaka mwanae, yaani hataki kitu chochote kile kwenye maisha yake zaidi ya huyo mwanae wa mwisho ambaye ndiye alikuwa roho yake, alimpenda mno. Lakini bwana Limo kwa muda huo hakuwa na cha kufanya maana hata yeye hakuwa na taarifa zozote juu ya wapi alipo mwanae, mwanaume macho yake yalijawa na mfadhaiko usio wa kawaida, siasa ilianza kumtokea puani.

Mheshimiwa Apson Limo akiwa anaendelea kuangaza macho yake kwenye hiyo gari alihisi kama vile kulikuwa na ujumbe kwenye kikaratasi ambacho kilipachikwa kwenye usukani hivyo ikamlazimu kukichomoa ili aweze kujua kimeandikwa nini, kweli alikutana na ujumbe ambao uliandikwa kwa wino uliokolezwa sana, ujumbe ulisomeka;

“NIMEKUPA MUDA MWINGI SANA WA KUWEZA KUJITAFAKARI ILA KWA BAHATI MBAYA UMEWEZA KUDHARAU MAELEZO YANGU, NIKAKUONGEZA SIKU NYINGINE YA JANA BADO UKANIONA KAMA MIMI NI MTOTO MWENZAKO. SASA NATAKA NIKWAMBIE MWANAO NIPO NAYE KWENYE MKONO WANGU NA KAMA UKIJARIBU KUPIGA MAKELELE POPOTE BASI HUWEZI KUMPATA AKIWA HAI. KESHO SAA MOJA KAMILI ASUBUHI UENDE PALE MBAGALA UTULIE UTAPEWA UTARATIBU SEHEMU YA KWENDA KUMKUTIA MWANAO” Ujumbe ambao ulikuwa na vitisho na mkanganyiko mkubwa ulikuwa umeishia hapo, alipewa onyo akajifanya mjanja sasa wanaume walikuwa wanamuonya kwa vitendo. Alijikuta akiukunja ujumbe huo kwa hasira sana huku akipasua kioo cha gari kwa mkono wake ambao ulianza kutoa damu lakini hakujali.

Aliwataka walinzi wake wambebe mkewe waondoke naye hilo eneo haraka sana kisha waishughulikie miili hiyo kabla jambo hilo halijafika kwenye mikono ya polisi maana ingekuwa ni hatari sana kwa sababu gari ambayo ilitumika ilikuwa ni yakwake yeye. Mkewe hakukubali alikuwa akimvuta vuta mumewe huku akimtaka mwanae na kama isingekuwa hivyo basi walitakiwa kwenda kituoni kuripoti habari hiyo lakini mumewe alitikisa kichwa kuonyesha kupingana na kauli ya mkewe.

Tukutane sehemu inayofuata ya kumi na nne, ya kumi na tatu inafika mwisho.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KUMI NA NNE
Una maanisha nini kunigomea kwenda polisi? Ole wako nisimpate mwanangu, sitakusamehe kamwe” mwanamke huyo aliongea kwa hasira sana lakini hata hivyo alipandishwa kwenye gari nyingine na walinzi wakatangulia naye nyumbani huku Apson akiwa amebaki ameduwaa hapo, alikaa chini kwenye mchanga akiwa na mawazo sana. Mkewe alikuwa anamlaumu yeye utadhani yeye ndiye ambaye alimteka mwanae au yeye ndiye ambaye alipenda hali kama hiyo iweze kutokea ila aliamua kukubali kwani mwanaume malipo yake ni kuzikubali lawama hata kama jambo hajalifanya yeye.;

“Pole sana mzee, najisikia vibaya sana umefanyika uzembe wa kumlinda princess Latifa” aliongea mlinzi wake wa karibu sana huku akiwa anampa kitambaa cha kujifutia maana licha ya upepo mkali wa hapo baharini mzee huyo alikuwa anatokwa na jasho sana ambalo ni wazi lilionyesha kwamba alikuwa kwenye hofu na wasiwasi mkubwa sana. Alikipokea kitambaa hicho na kujifutia nacho usoni huku akimeza mate kwa taabu sana.

“Sio makosa yako, hata kama mwanangu angekuwa analindwa na nani bado wangemteka tu wakiamua. Kama anauawa hata raisi ambaye yupo madarakani unahisi itashindikana kwa mtu wa kawaida? Siasa ni mchezo mchafu sana, siasa inayatoa maisha ya watu, siasa kwa sasa haipo kwa ajili ya kusaidia watu bali kuwakomoa watu. Najisikia vibaya sana nimeshindwa kumsaidia mwanangu, najisikia uchungu nimemsababishia malaika wangu mateso makubwa namna hii ambapo sijui huko aliko amekula nini maana huwa hawezi kula bila kumuona mama yake. Najiona baba wa hivyo sana kwa kushindwa kuilinda familia yangu mwenyewe” mwanaume huyo aliongea kwa uchungu sana mpaka chozi lilimshuka kwenye macho yake, alipanda kwenye gari na kuhitaji watu hao watoke hapo kwenda nyumbani ila kabla hajandoka mlinzi wake alimuuliza swali lingine

“Mzee ni kweli tunaenda kukaa kimya mpaka hiyo kesho?”
“Hii michezo ipi hivi, hapa nikisema natumia hasira basi mwanangu naenda kumkosa kitu ambacho siwezi kukiruhusu nikifanye. Nitasubiri mpaka hiyo kesho asubuhi nione wananipa maagizo gani ya kuyafuata” alikuwa amejikatia tamaa tayari, hakuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri kuambiwa ambacho kingefuatia.

Asubuhi na mapema kulikucha kama ilivyo kawaida, na muda huo alikuwa amefika tayari huko ambako aliitwa lakini mkewe hakukubali ilibidi waende wote huku bosi huyo akiwa amemuahidi mkewe kwamba mwanae wangempata akiwa hai. Wakiwa hilo eneo alipokea ujumbe na kuelekezwa kusogea mpaka lilipo moja ya jalala kubwa sana ndani ya Mbagala. Hawakuwa mbali sana hivyo ikawabidi wasogee eneo hilo huku watu wakiwa wanashangaa kumuona kiongozi ambaye walikuwa wanampenda sana akiwa mtaani, lakini licha ya hayo yote yeye hakuwa na muda nao bali alikuwa anakimbilia kwenye hilo jalala ambalo alikuwa ameagizwa.

Walichokutana nacho ni kilio kwa baadhi ya wamama ambao hawakuwa na roho ngumu ya uvumilivu, hata yeye alijikuta anasimama ghafla sana, alitoa ishara ya mkono kwa mlinzi wake, alielewa hivyo alimbeba mke wa bosi wake haraka sana na kwenda kumfungia kwenye gari kwani hakutakiwa kukiona hicho ambacho alikuwa amekiona tajiri huyo. Kwenye hilo jalala watu walikuwa wamezunguka baada ya mtoto mmoja wa mtaani kukutana na mfuko wenye damu wakati akiwa anatafuta mabaki ya vyakula asubuhi hiyo. Hiyo hali ilimfanya apige mekelele sana ya kuomba msaada na ndipo watu walipo anza kujazana ndani ya hilo eneo.

Walicho kiona hapo kilikuwa kinatisha sana, ulikutwa mwili wa mtoto huku ukiwa hauna kichwa, yaani ni kwamba mtoto huyo hakuwa hai. Na huyo alikuwa ni binti wa damu kabisa wa Apson Limo, aliyekuwa akijulikana kwa jila la Latifa. Baada ya kuona nguo za shule za yule mtoto na viatu vyake mguuni ndio muda ambao alimzuia mkewe asisogelee hilo eneo kwani alijua asingeweza kuhimili. Mwanae wa mwisho wa damu alikuwa ameuawa huku kichwa kikiwa kimekatwa na hakikujulikana kwamba kilikuwa wapi. Alijikuta anaishiwa nguvu na kukaa chini, sehemu hiyo ilikuwa ni chafu sana ila hata hakujali, bado hakuwa akiamini kwamba kipenzi chake alikuwa ameuliwa kikatili sana namna hiyo na wanadamu tena wakiwa wamefanya udhalilishaji wa kuondoka na kichwa chake. Machozi yalianza kushuka taratibu kwenye mashavu ya kipenzi cha watanzania Apson Limo.

Kama lilivyokuwa kusudio la muuaji wa huyo mtoto kama ni kumdhoofisha mr Apson Limo basi alifanikiwa kwa asilimia zote miamoja kwani alilegea sana mzee huyo, hakuwa na hamu ya ulimwengu wala kufanya jambo lolote lile kwenye huu ulimwengu nafsi yake ikawa inamsuta na kuhisi yeye ndiye ambaye alikuwa chanzo kikuuu cha hayo mambo yote ambayo yalikuwa yametokea. Akiwa hapo chini ni mambo mengi sana yalikuwa yanazunguka kwenye kichwa chake huku chozi likiwa linamshuka taratibu.

Alihisi huenda jambo hilo halikuwa limetokea kweli bali zilikuwa ni fikra zake tu za ndotoni na kama angeamka angemuona mwanae ila hakukuwa na ndoto yoyote ilikuwa ni asubuhi ya mapema sana hivyo kilichokuwa kinaendelea hapo ulikuwa ni uhalisia wenyewe bila chenga. Alikuwa anawaza ataanzia wapi kumwambia mkewe, ataanzia wapi kuyajibu maswali ya mkewe na atamuelewaje ikiwa alimuahidi kwamba angemrudisha mtoto akiwa hai nyumbani, alijiona dunia nzima ameibeba yeye kwenye kichwa chake, alipiga makelele makubwa sana kwa uchungu kiasi kwamba hata udenda ulianza kumtoka mdomoni.

Watu wengi sana ambao walikuwa hilo eneo walikuwa wanamuonea huruma sana mheshimiwa, alikuwa ni baba bora sana lakini alishindwa kuilinda familia yake kwa sababu ya kitu kinacho itwa siasa. Hata polisi wakati wanafika hilo eneo hakuwaona kwa sababu ya mawazo ambayo alikuwa nayo, waandishi wa habari nao hawakuwa mbali japo walizuiliwa kuchukua matukio ambayo hayakuwa salama na polisi ambao kwa kiwango kikubwa ndio ambao walishughulika na ule mwili kiasi kwamba wakawa wameondoka nao kwa ajili ya uchunguzi.

Apson Limo alikaa pale chini kwa saa zima huku asisikie hata zile pole za mapolisi ambao walikuwa wanamheshimu sana kwa sababu walihisi mtu huyo anaweza kuingia Ikulu sasa kama ukicheza naye vibaya ungejikuta nje ya mfumo hata hivyo alikuwa amewahi kuwa waziri bila kusahau kwamba alikuwa ni tajiri mkubwa sana ilikuwa ni lazima wamheshimu sana. Ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa kwani salamu hizo ziliishia kuwa kama kelele tu kwa upande wake maana hakumsikia mtu yeyote yule zaidi ya mlinzi wake ambaye alikuwa yupo pembeni yake na walinzi wengine akimwangalia boisi wake kwa uchungu sana. Baada ya saa zima kupita mzee huyo alinyanyuka na kumpa ishara mlinzi wake mkuu huyo amfuate waweze kuondoka hilo eneo.

“Bosi na kuhusu mama inakuwaje? Maana tumemfungia kwenye ile gari ambayo hawezi kuona chochote nje hivyo hakuna anacho kijua ambacho kinaendelea” mlinzi wake aliuliza kwa misingi ya kwamba ilikuwa ni vyema mkewe aweze kupewa taarifa maana ilikuwa ni haki yake kuweza kujua, mzee huyo alimpiga piga mgongoni mlinzi wake huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana kwa sababu jambo la kumwambia mkewe lilikuwa juu yake na hakujua angeanzia wapi na wangeishia wapi ila hakuwa na namna ikamlazimu kwenye kwenye ile gari na kuifungua kisha akaingia ndani ambako mkewe alimfululiza na maswali mengi na kauli za kuhitaji kumuona mwanae.

Mkewe baada ya kupokea zile taarifa ambazo hakuwa tayari kuzipokea na hata kama alijua kwamba jambo hilo lingetokea siku moja basi hakujua kama ingekuwa ni mapema hivyo kwa mwanae. Alizimia pale pale huku mwili wake ukiwa umelowa kwa jasho kiasi cha kuifanya hali yake iwe mbaya sana, zile taarifa kwake zilikuwa mbaya sana na hakuweza kuzihimili basi ikabidi mpango ubadilike badala ya kwenda nyumbani ikawalazimu kwenda hospitali na msafara huo haraka sana ili kujua hatima ya hali ya mkewe kwani alikuwa anazidi kuchanganyikiwa Apson Limo huku watanzania wengi sana wakiwa sambamba naye kwenye kipindi hicho kigumu maana taarifa zilianza kusambaa kwenye mitandao kwa kasi sana.

Baada ya kufika hospitali mkewe aliingizwa kwnye vyumba vya watu mahututi sana kwani hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya kiasi kwamba mzee huyo alizidi kuchanganyikiwa mpaka akawa hana hata uwezo wa kutembea vyema akawa anatembea kwa nguvu za mlinzi wake ambaye alikuwa amemshika mkono. Mzee huyo alikaa kwenye benchi la hapo hospitali huku nje kukiwa na mamia ya watu ambao walikuwa wamekuja kumpa pole kiongozi wao lakini hata nguvu za kusimama hapo hakuwa nazo ikamlazimu kukaa chini na kuegamia ukuta akiwa amepoteza matumaini kwenye uso wake.

Aliitoa simu yake na kuipiga kwenda kwenye namba ya mwanae wa kiume Tommy, simu hiyo iliita kwa muda mfupi sana na kupokelewa mithili ya kwamba hata mtu wa pili alikuwa anaisubiri kwa hamu sana hiyo simu.
“I need you back home son, urudi muda huu, nenda uwanja wa ndege upande ndege. Nakuhitaji haraka sana, sipo tayari kumpoteza mwanangu mwingine, hakikisha unarudi leo kwa gharama yoyote ile” mzee huyo aliongea akiwa anashusha machozi tena yale machozi ya uchungu kisha akaibamiza simu hiyo chini ambayo ilipasuka. Aliogopa sana kwamba huenda hata huyo mwanae pekee wa kiume alikuwa kwenye hatari kubwa na ukizingatia maadui zake wengi walijua hapo ndipo jicho lake lilipo hivyo alimtaka aweze kurejea nyumbani ili aweze kuwalinda wote kwa pamoja.

“Nawahitaji wanangu wote wanne wawe nyumbani, saivi nyumbani yupo mmoja tu ambaye ndiye alimtangulia ziwa Latifa, dada yao mwingine anaishi shuleni hivyo afuatwe haraka sana Tommy atakuwa hapa jioni au usiku na Linda namhitaji haraka sana naye awepo nyumbani”

“Sawa bosi tutafanya hivyo lakini princes Linda mpaka sasa hakuna taarifa ya mawasiliano yake ambayo inapatikana maana tumemfuatilia hata ofisini kwake hayupo tukahisi labda kuna sehemu yupo hata simu yake imezimwa hivyo tumehisi labda yupo kwenye faragha zake akiisikia tu hii habari anaweza kuja nyumbani”
“Whaaaaaaat?”
“Ndiyo mzee hapatikani maana hata simu yake tumeitrack sana lakini haipo hewani”
“Kwanini haujaniambia hili jambo?” mzee huyo aliuliza kwa ghadhabu sana akionyesha wazi alikuwa anazidi kuchanganyikiwa
“Nisingekwambia ukiwa kwenye hali kama hiyo mzee, nakuahidi tutampata tu na kama ikifika mchana hajapatikana basi tunaanza kumtafuta kila kona ya nchi hii mpaka tumpate”
“Hakikisha unamleta mwanangu nyumbani kwa gharama yoyote ile maana sitakusamehe juu ya hilo kama ukishindwa” alikuwa anaongea huku akiwa amemkunja kola la shati mlinzi wake huyo kwa uchungu ungehisi kwamba mlinzi huyo ndiye ambaye alikuwa amefanya hayo mambo yote.

Hakukuwa na namna zaidi ya kuwakusanya walinzi wote wa mzee huyo na kuwasambaza maeneo mbalimbali ili kuhakikisha kwamba binti huyo anapatikana. Msako ulianzia ndani ya ofisi yake kubwa ya urembo ambako huko walikutana na taarifa za kushangaza kwani zilikuwa zimepita siku mbili bila binti huyo kuonekana ofisini kwake kitu ambacho kiliwashtua sana basi ikabidi waingie ndani ya ofisi yake ila hawakukutana na kitu chochote kile zaidi ya simu yake ambayo ndiyo alikuwa anaitumia tena ikiwa imezimwa, hilo likawapa sana shaka watu hao na kujiuliza mara mbili mbili juu ya jambo hilo.

Kilichofuatia iliwalazimu kwenda kuangalia cctv kamera za jengo hilo, walifanikiwa kumuona mara ya mwisho akiwa anatoka akiwa mwenye furaha lakini mwenye haraka sana. Safari yake iliishia kwenye parking ya magari ambako kulikuwa na gari moja ambayo ilikuwa ikimsubiri japo mtu ambaye alikuwa ndani ya hiyo gari alikuwa haonekani maana gari ilikuwa na rangi nyeusi na mtu huyo hakufanikiwa kutoka nje ili sura yake ionekane waziwazi.


Je ni kweli kwamba bidada amepotea hivi hivi? Ukurasa wa kumi na nne unafika mwisho, tukutane ndani ya kurasa zinazo fuata.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KUMI NA NNE
Una maanisha nini kunigomea kwenda polisi? Ole wako nisimpate mwanangu, sitakusamehe kamwe” mwanamke huyo aliongea kwa hasira sana lakini hata hivyo alipandishwa kwenye gari nyingine na walinzi wakatangulia naye nyumbani huku Apson akiwa amebaki ameduwaa hapo, alikaa chini kwenye mchanga akiwa na mawazo sana. Mkewe alikuwa anamlaumu yeye utadhani yeye ndiye ambaye alimteka mwanae au yeye ndiye ambaye alipenda hali kama hiyo iweze kutokea ila aliamua kukubali kwani mwanaume malipo yake ni kuzikubali lawama hata kama jambo hajalifanya yeye.;

“Pole sana mzee, najisikia vibaya sana umefanyika uzembe wa kumlinda princess Latifa” aliongea mlinzi wake wa karibu sana huku akiwa anampa kitambaa cha kujifutia maana licha ya upepo mkali wa hapo baharini mzee huyo alikuwa anatokwa na jasho sana ambalo ni wazi lilionyesha kwamba alikuwa kwenye hofu na wasiwasi mkubwa sana. Alikipokea kitambaa hicho na kujifutia nacho usoni huku akimeza mate kwa taabu sana.

“Sio makosa yako, hata kama mwanangu angekuwa analindwa na nani bado wangemteka tu wakiamua. Kama anauawa hata raisi ambaye yupo madarakani unahisi itashindikana kwa mtu wa kawaida? Siasa ni mchezo mchafu sana, siasa inayatoa maisha ya watu, siasa kwa sasa haipo kwa ajili ya kusaidia watu bali kuwakomoa watu. Najisikia vibaya sana nimeshindwa kumsaidia mwanangu, najisikia uchungu nimemsababishia malaika wangu mateso makubwa namna hii ambapo sijui huko aliko amekula nini maana huwa hawezi kula bila kumuona mama yake. Najiona baba wa hivyo sana kwa kushindwa kuilinda familia yangu mwenyewe” mwanaume huyo aliongea kwa uchungu sana mpaka chozi lilimshuka kwenye macho yake, alipanda kwenye gari na kuhitaji watu hao watoke hapo kwenda nyumbani ila kabla hajandoka mlinzi wake alimuuliza swali lingine

“Mzee ni kweli tunaenda kukaa kimya mpaka hiyo kesho?”
“Hii michezo ipi hivi, hapa nikisema natumia hasira basi mwanangu naenda kumkosa kitu ambacho siwezi kukiruhusu nikifanye. Nitasubiri mpaka hiyo kesho asubuhi nione wananipa maagizo gani ya kuyafuata” alikuwa amejikatia tamaa tayari, hakuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri kuambiwa ambacho kingefuatia.

Asubuhi na mapema kulikucha kama ilivyo kawaida, na muda huo alikuwa amefika tayari huko ambako aliitwa lakini mkewe hakukubali ilibidi waende wote huku bosi huyo akiwa amemuahidi mkewe kwamba mwanae wangempata akiwa hai. Wakiwa hilo eneo alipokea ujumbe na kuelekezwa kusogea mpaka lilipo moja ya jalala kubwa sana ndani ya Mbagala. Hawakuwa mbali sana hivyo ikawabidi wasogee eneo hilo huku watu wakiwa wanashangaa kumuona kiongozi ambaye walikuwa wanampenda sana akiwa mtaani, lakini licha ya hayo yote yeye hakuwa na muda nao bali alikuwa anakimbilia kwenye hilo jalala ambalo alikuwa ameagizwa.

Walichokutana nacho ni kilio kwa baadhi ya wamama ambao hawakuwa na roho ngumu ya uvumilivu, hata yeye alijikuta anasimama ghafla sana, alitoa ishara ya mkono kwa mlinzi wake, alielewa hivyo alimbeba mke wa bosi wake haraka sana na kwenda kumfungia kwenye gari kwani hakutakiwa kukiona hicho ambacho alikuwa amekiona tajiri huyo. Kwenye hilo jalala watu walikuwa wamezunguka baada ya mtoto mmoja wa mtaani kukutana na mfuko wenye damu wakati akiwa anatafuta mabaki ya vyakula asubuhi hiyo. Hiyo hali ilimfanya apige mekelele sana ya kuomba msaada na ndipo watu walipo anza kujazana ndani ya hilo eneo.

Walicho kiona hapo kilikuwa kinatisha sana, ulikutwa mwili wa mtoto huku ukiwa hauna kichwa, yaani ni kwamba mtoto huyo hakuwa hai. Na huyo alikuwa ni binti wa damu kabisa wa Apson Limo, aliyekuwa akijulikana kwa jila la Latifa. Baada ya kuona nguo za shule za yule mtoto na viatu vyake mguuni ndio muda ambao alimzuia mkewe asisogelee hilo eneo kwani alijua asingeweza kuhimili. Mwanae wa mwisho wa damu alikuwa ameuawa huku kichwa kikiwa kimekatwa na hakikujulikana kwamba kilikuwa wapi. Alijikuta anaishiwa nguvu na kukaa chini, sehemu hiyo ilikuwa ni chafu sana ila hata hakujali, bado hakuwa akiamini kwamba kipenzi chake alikuwa ameuliwa kikatili sana namna hiyo na wanadamu tena wakiwa wamefanya udhalilishaji wa kuondoka na kichwa chake. Machozi yalianza kushuka taratibu kwenye mashavu ya kipenzi cha watanzania Apson Limo.

Kama lilivyokuwa kusudio la muuaji wa huyo mtoto kama ni kumdhoofisha mr Apson Limo basi alifanikiwa kwa asilimia zote miamoja kwani alilegea sana mzee huyo, hakuwa na hamu ya ulimwengu wala kufanya jambo lolote lile kwenye huu ulimwengu nafsi yake ikawa inamsuta na kuhisi yeye ndiye ambaye alikuwa chanzo kikuuu cha hayo mambo yote ambayo yalikuwa yametokea. Akiwa hapo chini ni mambo mengi sana yalikuwa yanazunguka kwenye kichwa chake huku chozi likiwa linamshuka taratibu.

Alihisi huenda jambo hilo halikuwa limetokea kweli bali zilikuwa ni fikra zake tu za ndotoni na kama angeamka angemuona mwanae ila hakukuwa na ndoto yoyote ilikuwa ni asubuhi ya mapema sana hivyo kilichokuwa kinaendelea hapo ulikuwa ni uhalisia wenyewe bila chenga. Alikuwa anawaza ataanzia wapi kumwambia mkewe, ataanzia wapi kuyajibu maswali ya mkewe na atamuelewaje ikiwa alimuahidi kwamba angemrudisha mtoto akiwa hai nyumbani, alijiona dunia nzima ameibeba yeye kwenye kichwa chake, alipiga makelele makubwa sana kwa uchungu kiasi kwamba hata udenda ulianza kumtoka mdomoni.

Watu wengi sana ambao walikuwa hilo eneo walikuwa wanamuonea huruma sana mheshimiwa, alikuwa ni baba bora sana lakini alishindwa kuilinda familia yake kwa sababu ya kitu kinacho itwa siasa. Hata polisi wakati wanafika hilo eneo hakuwaona kwa sababu ya mawazo ambayo alikuwa nayo, waandishi wa habari nao hawakuwa mbali japo walizuiliwa kuchukua matukio ambayo hayakuwa salama na polisi ambao kwa kiwango kikubwa ndio ambao walishughulika na ule mwili kiasi kwamba wakawa wameondoka nao kwa ajili ya uchunguzi.

Apson Limo alikaa pale chini kwa saa zima huku asisikie hata zile pole za mapolisi ambao walikuwa wanamheshimu sana kwa sababu walihisi mtu huyo anaweza kuingia Ikulu sasa kama ukicheza naye vibaya ungejikuta nje ya mfumo hata hivyo alikuwa amewahi kuwa waziri bila kusahau kwamba alikuwa ni tajiri mkubwa sana ilikuwa ni lazima wamheshimu sana. Ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa kwani salamu hizo ziliishia kuwa kama kelele tu kwa upande wake maana hakumsikia mtu yeyote yule zaidi ya mlinzi wake ambaye alikuwa yupo pembeni yake na walinzi wengine akimwangalia boisi wake kwa uchungu sana. Baada ya saa zima kupita mzee huyo alinyanyuka na kumpa ishara mlinzi wake mkuu huyo amfuate waweze kuondoka hilo eneo.

“Bosi na kuhusu mama inakuwaje? Maana tumemfungia kwenye ile gari ambayo hawezi kuona chochote nje hivyo hakuna anacho kijua ambacho kinaendelea” mlinzi wake aliuliza kwa misingi ya kwamba ilikuwa ni vyema mkewe aweze kupewa taarifa maana ilikuwa ni haki yake kuweza kujua, mzee huyo alimpiga piga mgongoni mlinzi wake huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana kwa sababu jambo la kumwambia mkewe lilikuwa juu yake na hakujua angeanzia wapi na wangeishia wapi ila hakuwa na namna ikamlazimu kwenye kwenye ile gari na kuifungua kisha akaingia ndani ambako mkewe alimfululiza na maswali mengi na kauli za kuhitaji kumuona mwanae.

Mkewe baada ya kupokea zile taarifa ambazo hakuwa tayari kuzipokea na hata kama alijua kwamba jambo hilo lingetokea siku moja basi hakujua kama ingekuwa ni mapema hivyo kwa mwanae. Alizimia pale pale huku mwili wake ukiwa umelowa kwa jasho kiasi cha kuifanya hali yake iwe mbaya sana, zile taarifa kwake zilikuwa mbaya sana na hakuweza kuzihimili basi ikabidi mpango ubadilike badala ya kwenda nyumbani ikawalazimu kwenda hospitali na msafara huo haraka sana ili kujua hatima ya hali ya mkewe kwani alikuwa anazidi kuchanganyikiwa Apson Limo huku watanzania wengi sana wakiwa sambamba naye kwenye kipindi hicho kigumu maana taarifa zilianza kusambaa kwenye mitandao kwa kasi sana.

Baada ya kufika hospitali mkewe aliingizwa kwnye vyumba vya watu mahututi sana kwani hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya kiasi kwamba mzee huyo alizidi kuchanganyikiwa mpaka akawa hana hata uwezo wa kutembea vyema akawa anatembea kwa nguvu za mlinzi wake ambaye alikuwa amemshika mkono. Mzee huyo alikaa kwenye benchi la hapo hospitali huku nje kukiwa na mamia ya watu ambao walikuwa wamekuja kumpa pole kiongozi wao lakini hata nguvu za kusimama hapo hakuwa nazo ikamlazimu kukaa chini na kuegamia ukuta akiwa amepoteza matumaini kwenye uso wake.

Aliitoa simu yake na kuipiga kwenda kwenye namba ya mwanae wa kiume Tommy, simu hiyo iliita kwa muda mfupi sana na kupokelewa mithili ya kwamba hata mtu wa pili alikuwa anaisubiri kwa hamu sana hiyo simu.
“I need you back home son, urudi muda huu, nenda uwanja wa ndege upande ndege. Nakuhitaji haraka sana, sipo tayari kumpoteza mwanangu mwingine, hakikisha unarudi leo kwa gharama yoyote ile” mzee huyo aliongea akiwa anashusha machozi tena yale machozi ya uchungu kisha akaibamiza simu hiyo chini ambayo ilipasuka. Aliogopa sana kwamba huenda hata huyo mwanae pekee wa kiume alikuwa kwenye hatari kubwa na ukizingatia maadui zake wengi walijua hapo ndipo jicho lake lilipo hivyo alimtaka aweze kurejea nyumbani ili aweze kuwalinda wote kwa pamoja.

“Nawahitaji wanangu wote wanne wawe nyumbani, saivi nyumbani yupo mmoja tu ambaye ndiye alimtangulia ziwa Latifa, dada yao mwingine anaishi shuleni hivyo afuatwe haraka sana Tommy atakuwa hapa jioni au usiku na Linda namhitaji haraka sana naye awepo nyumbani”

“Sawa bosi tutafanya hivyo lakini princes Linda mpaka sasa hakuna taarifa ya mawasiliano yake ambayo inapatikana maana tumemfuatilia hata ofisini kwake hayupo tukahisi labda kuna sehemu yupo hata simu yake imezimwa hivyo tumehisi labda yupo kwenye faragha zake akiisikia tu hii habari anaweza kuja nyumbani”
“Whaaaaaaat?”
“Ndiyo mzee hapatikani maana hata simu yake tumeitrack sana lakini haipo hewani”
“Kwanini haujaniambia hili jambo?” mzee huyo aliuliza kwa ghadhabu sana akionyesha wazi alikuwa anazidi kuchanganyikiwa
“Nisingekwambia ukiwa kwenye hali kama hiyo mzee, nakuahidi tutampata tu na kama ikifika mchana hajapatikana basi tunaanza kumtafuta kila kona ya nchi hii mpaka tumpate”
“Hakikisha unamleta mwanangu nyumbani kwa gharama yoyote ile maana sitakusamehe juu ya hilo kama ukishindwa” alikuwa anaongea huku akiwa amemkunja kola la shati mlinzi wake huyo kwa uchungu ungehisi kwamba mlinzi huyo ndiye ambaye alikuwa amefanya hayo mambo yote.

Hakukuwa na namna zaidi ya kuwakusanya walinzi wote wa mzee huyo na kuwasambaza maeneo mbalimbali ili kuhakikisha kwamba binti huyo anapatikana. Msako ulianzia ndani ya ofisi yake kubwa ya urembo ambako huko walikutana na taarifa za kushangaza kwani zilikuwa zimepita siku mbili bila binti huyo kuonekana ofisini kwake kitu ambacho kiliwashtua sana basi ikabidi waingie ndani ya ofisi yake ila hawakukutana na kitu chochote kile zaidi ya simu yake ambayo ndiyo alikuwa anaitumia tena ikiwa imezimwa, hilo likawapa sana shaka watu hao na kujiuliza mara mbili mbili juu ya jambo hilo.

Kilichofuatia iliwalazimu kwenda kuangalia cctv kamera za jengo hilo, walifanikiwa kumuona mara ya mwisho akiwa anatoka akiwa mwenye furaha lakini mwenye haraka sana. Safari yake iliishia kwenye parking ya magari ambako kulikuwa na gari moja ambayo ilikuwa ikimsubiri japo mtu ambaye alikuwa ndani ya hiyo gari alikuwa haonekani maana gari ilikuwa na rangi nyeusi na mtu huyo hakufanikiwa kutoka nje ili sura yake ionekane waziwazi.


Je ni kweli kwamba bidada amepotea hivi hivi? Ukurasa wa kumi na nne unafika mwisho, tukutane ndani ya kurasa zinazo fuata.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Huku umetukimbia mazima[mention]FEBIANI BABUYA [/mention]
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KUMI NA TANO
“Ametekwa” mwanaume ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa hao vijana ambao walikuwa wanaangalia video za marejeo hapo aliongea kwa sauti huku akiwa anagongesha mkono wake kwenye meza kubwa ambayo ilikuwa humo ndani.

“Ametekwa kivipi wakati hakuna hata mtu mmoja ambaye alionekana hapo na aliingia ndani ya hiyo gari akiwa na tabasamu la kutosha kwenye uso wake?” aliuliza kijana mmoja ambaye alikuwa ni mwanajeshi. Hakuona kama kuna alama yoyote ile ya mtu kutekwa lakini kiongozi wao huyo alimwangalia sana kisha akairudisha video hiyo nyuma kidogo ili aweze kuwaeleza yeye alifanikiwaje kulijua hilo jambo.

Aliikuza video hiyo na kuigandisha mpaka kwenye plate number ya gari ambayo ndiyo kwa mara ya mwisho alionekana akiwa anaipanda hapo, haikuwa na namba bali iliandikwa neno ZOO ikiwa na maana ya hifadhi ya wanyama.
“Ametekwa na mtu ambaye anamfahamu kabisa na wanajuana vizuri na huenda ni mtu wake wa karibu sana ndiyo maana hata yeye alienda bila kuwa na wasiwasi wowote na kuna asilimia kubwa sana mtu huyo akawa mpenzi wake. Huyu mtu alikuwa amecheza akili mbili na huenda anajua kabisa kwamba hili eneo lina kamera za ulinzi, jambo la kwanza ambalo alikukuwa amelifanya ni kuja na gari ambayo ni binafsi hivyo alijua kwa kutumia jina hilo kungemchanganya mfuatiliaji asije kujua kwamba mmiliki wa hiyo gari alikuwa ni nani lakini jambo la pili ni yeye kutoshuka kabisa nje ya gari hivyo napo alijua kama angeshuka basi sura yake ingetambulika. Kwa maana hiyo ni mtu ambaye alikuwa anajua kila kilichokuwa kinaendelea ndiyo maana aliifanya kazi yake kwa umakini na huenda ni mtu ambaye alishazoea kufanya kazi za namna hii ndiyo maana hata hajateseka kabisa kuweza kuifanya” alieleza kwa urefu sana kiasi kwamba wenzake walibaki wanaangaliana tu maana mwenzao aliwaza mbali sana.

“Hii ni mbaya sana kama bosi kwa sasa yupo kwenye hali mbaya namna ile na bado akijua na hili itakuwa hatari mno nadhani hatakiwi kuzipata hizi taarifa kabisa kwa sasa. Inatakiwa sisi tufanye mambo mawili kwanza kabla ya kuwa na uhakika kwamba huenda ni mtu wake wa karibu amemteka kama sio mpezi wake, jambo la kwanza tunatakiwa kuzitafuta sehemu zote ambazo yeye huwa anapendelea kwenda tukaangalie huko lakini jambo la pili ndilo hilo tutaanza kuangalia watu wake wa karibu wote kisha watu hao ndio ambao watatuongoza kuweza kujua yuko wapi” kijana mwingine naye aliongeza kisha akatoa maelezo ya nini kinachotakiwa kufanyika na mawazo yake yalionekana kuwa na mashiko hivyo wakakubaliana wote kuyafanyia kazi haraka sana kabla; ya kutoa mrejesho kwa bosi wao.

Msako ulianza kwa wafanyakazi walitakiwa kutaja maeneo ambayo alikuwa anayapenda sana na watu wake wa karibu ambao muda mwingi aliutumia nao, kuhusu maeneo yote ambayo alikuwa anapendelea kwenda hawakukuta hata alama yake hivyo mpango wa pili ndio ambao pekee ulikuwa umebakia kufanyiwa kazi.

Kwa maelezo ya wafanyakazi wake ni kwamba ukiacha familia yake kulikuwa na watu wawili tu ambao ndio walikuwa nae karibu sana, mtu wa kwanza alikuwa ni rafiki yake wa kike lakini mtu wa pili alikuwa ni mpenzi wake ambaye siku za karibuni ndiye alionekana kuwa karibu naye sana isivyo kawaida. Msafara wa gari za watu hao haraka sana uliunguza mafuta mpaka maeneo ya Upanga ambako ndiko alikuwa anaishi huyo rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Noelia.

“Samahani sana kwa kuweza kukuingilia hapa kwako bibi lakini tuna shida na mjukuu wako kwa sababu kuna maswali kadhaa ambayo tunaomba atusaidie majibu yake” kiongozi wa hao wanaume aliongea kwa bibi mmoja ambaye walimkuta kwenye hiyo nyumba ambayo ndiyo ilisemekana kwamba Noelia alikuwa akiishi.

“Kuna usalama kweli wajukuu zangu maana hata siwajui nyie ni akina nani na mjukuu wangu mnamhitaji wa nini?” bibi huyo ambaye bado uzee haukuwa umemuingia sana huenda kwa sababu ya maisha safi ambayo alikuwa nayo alijibu akionyesha kuwa na mashaka ndani yake.
;
“Kuwa na amani bibi sisi ni walinzi wa mheshimiwa Apson Limo, baada ya tukio la mtoto wake mdogo kuuawa amekuwa na wasiwasi sana maana hajapokea taarifa zozote za uwepo wa mwanae wa kwanza hivyo akawa ametuagiza tumtafute kwa gharama yoyote ila lakini kwenmye kutafuta kila sehemu tukawa tumekosa hivyo ikabidi tuanze kuangalia taratibu watu wake wa karibu ndipo tukaelekezwa hapa kwamba mjukuu wako ndiye rafiki yake mkubwa zaidi kwahiyo tulikuwa tunaomba atusaidie kama anajua alipo au hata kama ana mawasiliano naye maana familia ipo kwenye hali mbaya sana” mwanaume huyo alinyoosha maelezo ambayo yalimsikitisha sana hata bibi huyo.

“Ni mtu wa watu sana yule baba Mungu amfanyie wepesi sana. Nisubiri kwa dakika mbili nikamuite maana atakuwa amelala” bibi huyo alinyanyuka na kupandisha ngazi kwenye ghorofa ya juu kumuita huyo mjukuu wake kama alivyokuwa ameahidi na baada ya dakika moja alirudi na Noelia ambaye alionekana kuwa na wasiwasi sana.

Binti huyo baada ya kuulizwa maswali kuhusu hilo jambo alikataa kabisa na kudai kwamba ilikuwa ni muda sana tangu awasiliane na rafiki yake huyo kwani alikuwa na ratiba ya safari ndiyo maana kwa siku kadhaa hawakuwa wakiwasiliana. Alikuwa anaongea huku yeye mwenyewe akiwa kama vile hana uhakika na yale maelezo yake ambayo alikuwa anayatoa, msaada wa pekee ambao yeye aliwaelekeza ni sehemu ambayo wangempata mpenzi wa Patrina au waweza kumuita Linda kama baba yake alivyokuwa akipenda kumuita ambalo lilikuwa ni jina la bibi yake mzaa baba.

“Anatudanganya huyu binti kuna siku nina imani tutamrudia tu kama mambo hayataenda kama tunavyo hitaji” aliongea tena kiongozi wa wale wanaume akiwa ana mashaka sana na yule mwanamke
“Umejuaje tena kama anadanganya?”
“Macho yake tu yanaongea, mtu kama anakudanganya mwangalie kwenye macho yake utagundua uongo ambao unakuwa unachangizwa na uoga ambao anakuwa nao”
“Vipi kama alikuwa anaogopa labda juu ya uwepo wetu pale?”
“Mhhhhh yule ni rafiki yake mkubwa, kwanza hata hajashtuka baada ya mimi kumuuliza ina maana huenda alikuwa anajua juu ya hili jambo, haiwezekanai rafiki yako kipenzi apotee kwenye mazingira ya kutatanisha halafu wewe uwe kawaida vile lazima kuna jambo hapa ambalo limejificha ila sio muda sana nina Imani tutaenda kujua kama kuna kitu nyuma ya pazia” mwanaume huyo aliingia ndani ya gari na kumuacha mwenzake kwenye mshangao maana alikuwa ni mtu wa mahesabu makali sana na kutumia akili mno kwenye kila jambo ambalo alikuwa analifanya, huo uwezo wa kufikiria hayo mambo walikwua nao watu wachache sana duniani.


R LOGISTICS, CLEARING AND FORWADING
Hilo ndilo eneo ambalo wao walienda kuishia na msafara wao ambapo ndipo walielekezwa na Noelia, hawakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kuomba kukutana na mmiliki wa kampuni hiyo ambaye ndiye alikuwa bosi mwenyewe. Aliyeruhusiwa kuingia ni yule kiongozi wa wale wanaume ili kukutana na kiongozi wa hilo eneo baada ya kutoa utambulisho wake na dhumuni kuu ambalo lilikuwa limempeleka pale.

“Habari yako mheshimiwa” alimsalimia kijana ambaye alikuwa mbele yake, alionekana kuwa bado ni kijana wa kawaida tu kwa umri lakini ndiye alikuwa tajiri mwenyewe. Huyo ndiye ambaye alikuwa mpenzi wa Linda na ndiye ambaye walielekezwa kukutana naye jina lake akiwa anaitwa Remsi ndiyo maana hata kampuni yake aliipa jina la R kikiwa ni kifupisho cha jina lake.

“Nina mambo mengi sana ya kufanya hivyo naomba uende moja kwa moja kwenye shida ambayo imekuleta hapa” Remsi hakupokea hata salamu bali aliongea kwa sauti kavu ambayo ilionyesha haikuhitaji mazoea na mtu yeyote yule.
“Nadhani unamfahamu Patrina ambaye ni mpenzi wako bila shaka”
“Haujajitambulisha wewe ni nani?” Remsi alionekana kuwa ni aina ya wale wanaume wenye dharau na majivuno sana.
“Ok naitwa Antony, natokea ndani ya jeshi la ulinzi na usalama wa nchi ila kwa sasa nafanya kazi ya kuilinda familia ya mheshimiwa Apson Limo”
“Ok, hapo sasa ndipo naweza kukusikiliza, unavamiaje ofisi za watu bila utambulisho? Hiyo sio heshima na usije ukarudia tena hususani unapokuwa mbele yangu. Kukujibu swali lako ni kweli huyo binti nilikuwa namfahamu labda itakuwa vizuri kama ukiniambia moja kwa moja kwamba unahitaji nini kwangu ambacho kitahusiana na yeye?”

“Una maanisha nini kusema ulikuwa inamfahamu? Unatumiaje wakati uliopita wakati nakuuliza wakati uliopo?”

“Nilikuwa namfahamu kwa sababu alikuwa ni moja kati ya michepuko yangu ila kwa baadae nikaja kumuacha maana sikuona kama ana vitu ambavyo nilikuwa navihitaji kwa mwanamke hivyo nikahama kwenda kwa warembo wengine ambao ni wazuri zaidi yake” aliongea kwa dharau sana kitu ambacho kilimuuma sana kamanda huyo ila hakuwa na cha kufanya kwa wakati huo alitakiwa kuwa mpole ili asije akaharibu kazi.

“Mama yako mzazi yupo hai?” ndilo swali ambalo alimuuliza Remsi lakini mwanaume huyo aliishia kumuangalia kwa macho ya hasira tu bila kumjibu.

“Ok, huenda nimeuliza siko, nahitaji kujua kwamba mara ya mwisho wewe kuonana naye ilikuwa ni lini?” baada ya kuona hajibiwi alijitia ushamba tena wa kuweza kuuliza ili azipate taarifa ambazo alikuwa anazitaka.

“Sikumbuki maana nina wanawake wengi sana. Nina mambo mengi sana ya kufanya hivyo unaweza ukaenda kama unahisi labda mimi naweza kumuoa huyo binti basi umechemka sana. Sijajua kama umekuja kumuombea ili nimuoe au analia huko aliko kwa sababu yangu ila mimi sipo tayari hivyo kuwa na heshima sana kuzungumzia habari za mapenzi ndani ya ofisi yangu utakuwa unatia mikosi tu, nakuomba kistaarabu uondoke” hili jibu la mwisho la Remsi ndilo ambalo lilimmaliza nguvu kabisa kamanda huyo akaona moja kwa moja mtu huyo licha ya kuwa na majivuno sana lakini hakuwa akihusika au hakujua lolote maana yeye alihitaji kumpeleleza kuhusu upooteaji wa mwanamke huyo lakini yeye alijua kwamba mtu huyo amekuja ni kumuombea mwanamke huyo ili aweze kuolewa na jamaa.

Alitoka nje kinyonge sana na wakati huo ilikuwa imeshafika jioni na usiku ulikuwa umeanza kuingia, baada ya kufika nje kwenye magari ambapo wenzake walikuwepo, alitikisa tu kichwa na kutamka;
“Hajui lolote” basi msafara huo ukaanza safari ya kurudi nyumbani kwa mr Limo. Lakini wakati mambo yote hayo yanaendelea Remsi alikuwa dirishani kwenye ofisi yake akiwa anachungulia ule upande wa chini walipokuwepo wale watu mpaka alipo hakikisha wanaondoka, akaishia kutabasamu tu.
Ni kweli Remsi hajui kuhusu hizo habari? Sina mengi ya kuongeza ila niseme kwamba sehemu ya kumi na tano sina la ziada inafika mwisho, panapo majaaliwa tukutane ndani ya sehemu zinazo fuata.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KUMI NA SITA
Taarifa ambazo zilimfikia mheshimiwa Apson Limo baada ya kupewa majibu na mlinzi wake mkuu kupitia vijana wake ambao alikuwa amewatuma zilimchosha na kumkosesha nguvu, sasa aliona kama akikaa kijinga hiyo familia yake yote huenda angeipoteza akiwa anaona kwa macho yake, ilikuwa ni lazima afanye jambo ambalo lingemfanya aweze kuiokoa familia yake.

“Nitawaua wote washenzi nyie” alitamka kwa hasira sana akiwa anaitoa simu yake na kupiga mahali, simu hiyo iliita mpaka ikakata yenyewe akaishia kusonya, aliitafuta namba ya pili nayo aliipiga iliita kwa dakika nzima bila kupokelewa. Aliibamiza simu hiyo chini huku akipandisha juu ghorofani na kuingia chumbani kwake ambako alikaa kwa dakika kumi na kutoka ndani ya suti yake nzito akiwa na bastola mbili mikononi akaishia kuzitia kwenye kiuno chake.

Alitoka mpaka nje ambapo mlinzi wake mkuu alikuwa sambamba naye maana hakuelewa kiongozi wake anahitaji kufanya nini. Aliwazuia walinzi wote kutoka ndani ya geti la nyuumba yake akiwasisitiza kwamba wahakikishe watu waliopo hapo wanakuwa salama huku yeye akitoka na mlinzi wake mkuu ambaye ndiye alishika jukumu la kuweza kumuendesha kwenye gari ambayo walitoka nayo hapo. Kwa hasira ambazo alikuwa nazo mzee huyo ni wazi kwamba alikuwa anaenda kulipa kisasi kwa watu ambao alihisi kwamba ndio ambao walihusika kumletea hayo matatizo kwenye familia yake.

JNIA
Masaa nane na dakika hamsini zilikuwa zimetosha kwa ndege kutoka England na kufanikiwa kutua ndani ya uwanja wa ndege huo wa kimataifa nchini Tanzania. Yalikuwa majira ya usiku ambao ndio muda aliokuwa anaingia kwenye uwanja huo wa ndege mwanaume ambaye mwili wake ulikuwa mrefu wa kuvutia huku akiwa na rangi ile ya maji ya kunde ambayo imekolea sana ungehisi mtu huyo aliishi maeneo yenye joto sana kwa muda wa maisha yake yote.

Alikuwa ndani ya suti ya gharama sana huku sura yake ikiwa inaongozwa na upole usio na hatia yoyote ile, mwendo wake wa taratibu wakati anaelekea eneo la mapokezi ndio ulio ashiria kwamba alikuwa amefika mwisho wa safari yake ambayo kwa muda mrefu aliitumia kuwa angani. Huyo ndiye ambaye alikuwa mtoto wa pekee kabisa wa kiume wa Apson Limo ambaye alikuwa anajulikana kama Tommy kilichokuwa kifupisho cha jina lake la kuzaliwa la Thomas.

Mwanaume huyo alifika eneo la mapokezi na suti yake ambayo ilikuwa imemkaa vyema sana kwenye mwili ambao ulikuwa unajieleza kwamba haukuwa wa afya ya mgogoro kabisa bali mwanaume ambaye alikuwa ameutunza vyema sana. Fikra zake alijua kwamba baba yake ndiye mtu ambaye angekuja hapo kutokana na yale ambayo alikuwa ameyaskia lakini kitu cha ajabu alikutana na walinzi tu wa nyumbani kwao ambao ndio walikuja na gari mbili kuweza kumpokea.
“Baba yuko wapi?” hilo ndilo lilikuwa swali lake la kwanza kwa hao wanaume ambao walikuja kumpokea baada ya wao kuinama na kumpa heshima yake kwani walikuwa wanamheshimu kama ambavyo walikuwa wanamheshimu baba yake mzazi.

“Mzee ametoka sio muda na Luck, wakati tunajiandaa kuja kukupokea huku alionekana akiwa kama hayupo sawa akaingia ndani na kutoka ambapo wameondoka yeye na Luck tu kwenye gari hivyo hatujajua ni wapi wameelekea kwani amegoma kabisa walizi wengine kuweza kuwafuata” hiyo kauli ya mlinzi ilimshangaza na kumchanganya sana hakuona kama baba yake alikuwa kwenye usalama wa kutosha kwani huenda kwa yale ambayo yalikuwa yametokea ndiyo ambayo yalikuwa yanamfanya mzee huyo kufanya maamuzi ambayo angehisi ni sahihi sana kwa wakati huo lakini kiuhalisia ni kwamba yangemhatarishia sana maisha yake.

Tommy aliitoa simu yake mfukoni na kuipiga namba ya baba yake mzazi, simu hiyo iliita kwa muda mfupi ikajikata yenyewe, alipopiga kwa mara nyingine tena hiyo namba haikuwa ikipatikana kabisa. Alihisi kuna tatizo hivyo akwahitaji watu hao wampeleke nyumbani haraka sana.

Ilichukua dakika ambazo hazikuzidi arobaini wao kuweza kufika kwenye mjengo wa kifahari ambao ndio ulikuwa wa kwao. Mwanaume alishuka kwenye gari haraka sana na kuingia ndani ambapo kila mlinzi alikuwa akimsalimia kwa heshima sana lakini hakuweza kabisa kujali juu ya jambo hilo. Baada ya kuingia ndani aliwakuta wadogo zake tu wawili wakiwa wamejikunyata mmoja akiwa amechukuliwa shuleni na kurudishwa nyumbani kutokana na yale matatizo ambayo yalikuwa yametokea. Wadogo zake walimkimbilia na kumkumbatia kaka yao huku wakiwa wanayatoa machozi kwa uchungu sana.

Ilibidi kuwatuliza mpaka wakanyamaza ndipo akaanza kuulizia wengine walipo lakini majibu ambayo aliyapata yalimshangaza sana. Taarifa za ghafla ambazo alizipata ni juu ya kufariki kwa mdogo wake wa mwisho kabisa lakini baada ya kufika nyumbani alishangaa baada ya kuambiwa hata mama yake mzazi pia alikuwa hospitali mpaka muda huo lakini hata dada yake ambaye yeye ndiye alikuwa amemfuata Patrina alikuwa amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha mno kiasi kwamba wakawa wameeleza kwamba alikuwa ametekwa.

Mwanaume mbele ya wadogo zake alijitahidi sana kuonyesha kwamba yupo kawaida hivyo akawachukua na kutoka nao ndani ili aende hospitali kwanza hata suala la baba yake aliliweka kando kwa muda maana hata kwenye simu hakuwa anampata. Safari yake ilienda kuishia kwenye hospitali kubwa ya Aghakhan ambako ndiko alikuwa amelazwa mama yake kipenzi tangu apokee taarifa ya mwanae wa mwisho kufariki alikuwa kwenye hali mbaya sana ndiyo maana aliendelea kubaki kwenye usimamizi wa madaktari.

Iliwachukua nusu saa kuweza kufika hapo ndani, licha ya muda wa kuwaona wagonjwa kuwa umeisha ila mwanaume huyo baada ya kujitambulisha kwamba yeye alikuwa ni nani, alipewa nafasi ya kwenda kumuona mama yake. Alibaki amesimama mlangoni kwa muda baada ya kumuona mama huyo akiwa amezungushiwa mipira ya maji kwenye mikono yake huku maji ambayo yalikuwa yanaongezwa kwenye mwili wake yakiwa yanashuka taratibu.

Alikuwa na hisia kali sana, ni kama alikuwa usingizini ila alishtuka ghafla sana na kuyafumbua macho yake, wakati anayafumbua macho hayo sura ya kwanza kuiona mbele yake ilikuwa ni ya mwanae wa peke wa kiume ambaye siku kadhaa nyuma alikuwa akimtaka arudi nyumbani ili aweze kumpikia chakula yeye mwenyewe. Alishindwa kuyazuia machozi yake pale kitandania mbayo yalikuwa yanashuka kwa maana mbili, ya kwanza alifurahi kumuona mwanae akiwa bado yu hai na mzima wa afya kwa mara nyingine maana ulipita muda mrefu sana akiwa hajamuona lakini maana ya pili hakuwa na furaha kwa sababu mwanae huyo alirejea wakati mbaya zaidi kuliko wakati wote kwenye familia yao.

Alisogea kitandani na kumfuta machozi mama yake kisha akamkumbatia kwa uchungu sana huku akiwa anayauma meno yake kiasi kwamba alikuwa na ghadhabu na mtu fulani ambaye alikuwa amemkera sana.

“Furaha yangu ilikuwa ni kuwaona nyie wote mbele ya macho yangu ila kwa bahati mbaya mmoja wamemchukua. Latifa alikuwa amekumis sana, alikuwa anauliza kila wakati “Mama kaka anarudi lini? Mimi nataka zawadi yangu halafu akija anipeleke kuangalia wanyama” hayo ni maneno ambayo alikuwa akiyarudia kila asubuhi na kila usiku kabla ya kulala. Nashukuru sana umerudi salama mwanangu, nakupenda sana” maneno ya mama yalimfanya macho yake kuwa mekundu sana ila alijikaza kiume na kumezea kana kwamba hakuna ambacho kilitokea kibaya, hakutaka kuwa dhaifu kuendelea kumtia zaidi uchungu mama yake mzazi ndiyo maana alimezea moyoni ila ni maneno ambayo yalimchoma sana.

“Nimerudi mama, mwanao nimerudi. Nimemisi sana kula chakula ambacho umepika, huko nilikokuwa wanapika vibaya sana, sijawahi kuona mwanamke ambaye anajua kupika kama wewe” maneno yake kidogo yalimfanya mama huyo atabasamu kwa mara ya kwanza, kama alivyokuwa ameongea mwanzo kwamba alitaka kumpikia mwanae huyo chakula kwa mikono yake na ndicho ambacho alikuwa anakitamani sana. Waliishia kugongesha mikono na kukumbatiana tena huku pamoja wote na wadogo zake.

“Dada yenu yuko wapi?” lilikuwa swali la mama baada ya kutulia maana alitegemea kwamba angewaona wote hapo lakini wote waliishia kutazamana tu pasipo kuwa na majibu ya kueleweka. Mama huyo alibaki anawatazama kwa umakini akitegemea kwamba wangemjibu haraka sana kwa wakati huo lakini Tommy alitikisa kichwa chake kama alama ya kukataa.
“Inasemekana bado hajajulikana alipo mpaka sasa hivyo nataka nimtafute mwenyewe kuanzia muda huu nadhani mpaka asubuhi nitamleta nyumbani kama atakuwa hajafika mwenyewe” ndiyo ilikuwa kauli ya Tommy kwa mama yake huyo ambaye wasiwasi ulizidi kupiga kwenye uso wake
“Chukua walinzi wa kutosha, naomba sana mwanangu awepo nyumbani asubuhi wakati mimi narudi. Sitaweza kuyavumilia maumivu ya kuweza kumpoteza mtoto wangu mwingine, namhitaji Patrina nyumbani” mama huyo aliongea kwa uchungu sana huku akijilaza hatimaye daktari akamchoma sindano ambayo ingemfanya apumzike kwa amani ili mawazo yasikitawale kichwa chake akaanza kuteseka usiku.

Tommy alitoka mle ndani na wadogo zake baada ya kuhakikisha ameongea na mama yake ili aweze kuwarudisha nyumbani kwani aliamini wakati huo baba yake angekuwa amerudi licha ya kutopatikana kwenye simu. Lakini baada ya kutoka nje ya hicho chumba alishangaa sana kuwaona walinzi wote wameinama kwa simanzi sana, ikamlazimu mlinzi mmoja amuite pembeni kidogo ili kuteta naye jambo ambalo kwa mwonekano wa sura tu halikuonekana kuwa zuri. Baada ya kukaa naye pembeni alimpatia simu yake ambayo ilikuwa na video iliyokuwa inatakiwa kumpa majibu ya nini ilikuwa shida mpaka watu hao wawe kwenye hiyo hali ghafla sana namna hiyo.

Ni video ambayo ilikuwa inaonyesha mwanaume mmoja akiwa anapigwa risasi za kutosha kwenye mwili wake huku mpigaji akiwa haonekani alikuwa ni nani maana aliyekuwa anaonekana alikuwa ni mpigwaji tu. Lengo la yeye kuonyeshwa video hiyo ni kwa sababu huyo ambaye alikuwa anapigwa risasi alikuwa ndiye baba yake mzazi Apson Limo. Alishtuka sana kuona hiyo hali, hakuelewa ni kwa sababu zipi mpaka mambo hayo yajitokeze ghafla sana namna hiyo kwenye familia yake, alipo iangalia kwa umakini video hiyo hakumuona Luck ambaye ndiye alikuwa mlinzi mkuu wa baba yake.

“Ni wapi hapa?” aliuliza akiwa na uso mkavu utadhani yule ambaye alikuwa anaonekana kwenye video hiyo hakuwa baba yake mzazi.

“Ni maeneo ya posta” ndilo lilikuwa jibu la mlinzi huyo
“Hakikisha Lucy na Lily wanafika nyumbani salama na walinzi wote muwe makini sana pale nyumbani na msifungue geti kwa mtu yeyote yule mpaka nirudi” alitamka maneno yake kwa msisitizo sana huku akiwa ameanza kutoka hiyo sehemu ambayo walikuwa wamesimama wawili tu.

“Bosi na kuhusu wewe vipi? Maana mzee alitupa maagizo kwamba inatakiwa tuwe na wewe sehemu yoyote ile ambayo unakuwepo”

“Sihitaji kuongozana na mtu yeyote yule, hakikisha wadogo zangu wanakuwa salama kwa gharama yoyote ile” mwanaume huyo aliongea akiwa anatoweka hilo eneo ambapo alitokea mlango wa nyuma kwani hakutaka kukutana na wadogo zake tena ambao alijua wasingekubali kumuacha aende wakati huo.

Maeneo ya posta karibu kabisa na KFC ndipo ambapo lilitokea tukio la kutisha sana, tukio ambalo lilisababisha kipenzi cha watanzania kuweza kupigwa risasi nyingi sana kwenye mwili wake na watu ambao hawakuwa wakijulikana. Ilimchukua muda mfupi sana Tommy kufika hilo eneo kwani hapakuwa mbali sana na alipokuwepo.

Mimi nakaa pembeni, nakuachia wewe hapo wakati huo sehemu ya kumi na sita inafika tamati.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom