Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA ISHIRINI NA NNE
Hawakuwa na namna zaidi ya kumfuata wote watatu kwani hata zile tambo zao zilikuwa zimeisha kabisa, aliyekuwa mbele alikutanishwa na ule upanga ambao ulizama kwenye paja lake ukatokezea nyuma, alidondoka hapo hapo akiwa analia na kujisaidia mwenyewe kuuchomoa upanga huo ambao ulikuwa ukimletea maumivu yasiyo ya kawaida hivyo safari ya kukutana na mtu huyo ilibakia kwa wanaume wawili ambao walikuwa wamemkaribia.
Tommy baada ya kukaribiana nao, alidunda chini kwa sarakasi akajigeuza mithili ya samani ambapo alipishana na ngumi tatu kwenye sikio lake akatua nyuma ya watu hao karibu na yule ambaye alikuwa anahangaika kuuchomoa ule upanga wake. Baada ya upanga huo kuchomolewa aliuzamisha kwenye moyo wa yule mwanaume kisha akamkutanisha na buti zito la shingo ambalo lilipelekea shingo ya mtu huyo kupinda, akadondoka hapo hapo na kupoteza maisha huku mwanaume kwenye mkono wake akiwa amebakia na upanga huo wao wakiwa wamebaki wawili tu pekee.
Ni kama hofu ilianza kutanda miongoni mwao kwani walikuwa wakiangaliana kiasi kwamba kila mtu ni kama alikuwa anampa mwenzake ishara ya kwenda kwanza japo ililazimu aende kwanza mwanaume mwingine huku kiongozi wake akiwa wa mwisho. Alisogea huku akiwa na hofu ndani yake, hicho ndicho ambacho kilimpotezeshea umakini kwani hata urushaji wake wa ngumi ulikuwa wa wasiwasi sana, sarakasi ambayo alijizungusha nayo ilikuwa ya kasi ndogo sana kiasi kwamba alichotwa mtama wakati anatua, akiwa anaelekea chini mwanaume ambaye alikuwa karibu yake alimpiga mithili ya mpira wa kutengwa na kumfanya aburuzike mpaka ukutani ambapo alijibamiza vibaya sana kichwa chake ila wakati anatua hapo ukutani upanga ulikuwa sambamba na kichwa chake, ulitoboa jicho lake moja vibaya sana ukawa umezama mpaka ndani, aliishia kutoa damu na mate tu mdomoni mithili ya mtu ambaye alikuwa na jambo la kuteta lakini aliikosa nafasi ya kuweza kulisema jambo hilo.
Yule kiongozi wao ambaye alikuwa amebakia aliikunja mikono yake akiwa anakuja kwa hasira upande wa Tommy ila kilicho mkuta ni bora angetafuta sehemu mapema ya kukimbilia, makosa ambayo aliyafanya ni kuamini kwamba ile bastola ambayo Tommy aliitupa wakati ule ndiyo pekee ambayo alikuwa nayo ndiyo maana alijua kwamba mtu huyo hana silaha nyingine ikawa amani kwao kutumia mikono kama nao walivyokuwa wamejiaminisha tangu mwanzo kwa kuiamini mikono yao kuliko silaha za moto. Lakini wakati anamsogelea mwanaume huyo Tommy aliichomoa bastola nyingine kwenye kiuno chake na kumpiga risasi nyingi sana mwanaume huyo magotini na mapajani kitu ambacho kilipelekea kudondoka chini kama ndege ambaye alikuwa kwenye mwendo mkali halafu ghafla sana akapigwa na manati.
Tommy alifanya hivyo kwa sababu aliona kama anapoteza muda na wakati huo kulikuwa kunaanza kukaribia kukucha akiwa bado hajampata dada yake kitu ambacho kingekuwa hatari sana kwa upande wa usalama wa dada yake hata yeye pia kama watu wangefanikiwa kumuona. Alikuwa anazipiga hatua zake taratibu kumsogelea yule mwanaume ili aweze kumhoji ndiyo maana hakumpiga risasi sehemu mbaya ambayo ingeyahatarisha maisha yake. Akiwa amekaribia kufika pale, ghafla sana alimuona mtu huyo akiwa anatoa povu kwenye mdomo wake, baada ya kumsogelea kwa ukaribu aligundua kwamba mtu huyo alikuwa amemeza kidonge cha kuweza kuutoa uhai wake maana yake ni kwamba ilikuwa ni bora afe kuliko kuusema ukweli.
“Shiiit!” Tommy alitamka akiwa anaondoka hapo kwa mbio kali kuelekea ndani kwani alifanya uzembe ambao ulimpa nafasi ya kujiua mtu huyo, hakutakiwa kabisa kumpa hiyo nafasi kwa sababu ndiye ambaye angeweza kumpa taarifa zote kuhusu uwepo wa dada yake. Alikagua kila sehemu lakini humo ndani palikuwa kimya na peupe kabisa kusiwe na dalili ya uwepo wa mtu yeyote yule.
“Noelia” aliita kwa hasira akiwa anapiga ukuta kwa ngumi kali ambayo ilipelekea mkono wake kuanza kuvuja damu, alijua huyo mwanamke ndiye alikuwa ametoa taarifa kwa watu hao kwamba kuna mtu anaweza kwenda hilo eneo hivyo wamtoe mtu wao na ndiyo maana alichelewa kuweza kumsaidia dada yake. Alitoka nje akiwa na ghadhabu sana, alifungua geti na kuliacha wazi akahitaji kutoweka hilo eneo lakini baada ya kufika nje alihisi kuna kivuli cha mtu kimejibanza sehemu japo kulikuwa na kiza ila taa za ndani ya geti hilo ambalo aliliacha wazi zilikuwa zinasaidia kuakisi vyema hata mwili wake ulikuwa umesisimka sana.
Alisogea kwa kasi hilo eneo lakini hakumpata mtu bali alikuta kuna picha ndogo sana ikiwa imedondoshwa bila shaka hata aliye idondosha hakujua kama aliacha ushahidi ndani ya hilo eneo hivyo hakuwa na shaka, aliamini kwamba angempata mtu huyo muda wowote ule. Aliitoa simu yake mfukoni na kupiga mahali ambapo iliita kwa muda mfupi tu ikapokelewa.
“Nakuja kwako saivi” ilikuwa ni kauli moja tu kisha akaikata simu hiyo na kuingia kwenye gari yake ambayo aliitoa kwa kasi isiyo ya kawaida kuelekea hilo eneo ambalo yeye alihitaji kwenda huku akiamini kwamba muda wowote ule polisi wangeweza kufika hilo eneo.
Safari yake Tommy ilienda kuishia Msasani ambako ndiko alikuwa anaishi mtu ambaye aliwasiliana naye kwenye simu, alikuwa ametumia dakika kumi na tano tu kufika hiyo sehemu ambayo alikuwa anaishi mtu huyo ambaye aliwasiliana naye. Geti la jumba hilo lilifunguliwa kwa rimoti bila mhusika kutoka nje gari yake ikaingizwa ndani kisha naye akapita moja kwa moja mpaka ndani kana kwamba hakukuwa na mtu wa kumuuliza kuhusu uwepo wake kwani alikuwa anawaona walinzi wakiwa wamejificha mbali na geti kiasi kwamba hata mtu angeingia ndani hakuna ambaye angeweza kujua kwamba eneo hilo lilikuwa na walinzi.
Baada ya kufika mlangoni, mlango wa ndani kabisa kwenye jengo hilo la kifahari ulifunguliwa na mwanamke mrembo sana ambaye alionekana kuwa na uraia pacha wa nchi mbili, Afrika na Uingereza. Mwanamke huyo alihitaji kumkumbatia Tommy lakini mwanaume alimsukumia mpaka kwenye sofa ambapo alitoa bastola yake na kuikoki akiwa amemuelekezea mwanamke huyo na kukitoa kitambaa chake usoni kiasi kwamba mwanamke huyo akabaki anamshangaa tu.
“T1 what’s wrong?” aliuliza mwanamke huyo kwa upole huku akionyesha wazi kabisa kwamba alimjua mtu huyo vyema.
“You promised to protect my family and see what’s happening now. You guys betrayed me” aliongea kwa hasira mno huku akiwa anamsogelea mwanamke huyo karibu zaidi kumaanisha kwamba waliahidi kuilinda familia yake lakini walikuwa wamemsaliti maana kilichokuwa kinatokea kilikuwa ni tofauti na matarajio.
“No Tommy”
“Mdogo wangu wa damu amekufa, baba yangu anaipambania hali yake hospitali ambapo hajui ataamka lini, dada yangu ametekwa na mama yangu amelazwa halafu wewe unaniambia hapana, unahisi naweza kukuacha hai?” hakutaka ngonjera nyingi kutoka kwa mwanamke huyo ambaye aliishia kusikitika tu baada ya kumuona huyo mwanaume ambaye yeye alikuwa anamwita T1 akiwa kwenye hali kama hiyo.
“Unakumbuka makubaliano ambayo tuliingia na wewe?”
“It doesn’t matter”
“It’s what matters now. Tulikuguarantee kwamba miaka yote ambayo ungekuwa unaifanya kazi yetu familia yako ingekuwa salama na tumehakikisha hilo lakini kwenye makubaliano yetu ilikuwa ni kwamba mwezi mmoja kabla ya wewe kurudi mkataba wetu wa kuilinda familia yako unaisha na utakuja kuilinda mwenyewe na wewe mwenyewe ndiye ambaye ulitoa hilo pendekezo, sasa kwanini unakuja kunilaumu na kuanza kunitishia kuniua mimi?” mwanamke huyo naye alijibu kwa ukali sana kwa lugha ya Kiswahili ambayo hakuwa akiitamka vizuri sana lakini ilikuwa inaeleweka vyema. Mwanaume alichoka na kukaa chini baada ya kuambiwa maneno hayo ambayo yalionekana kumuingia vyema sana kwenye kichwa chake.
HARPER CAMPBELL
Ndiye mwanamke ambaye Tommy alikuwa amekutana naye wakati huo ambao alikuwa anafanya naye mazungumzo. Harper alikuwa ni mtendaji mkuu (CEO) na mkurugenzi mkuu (MD) wa kampuni kubwa ya bima ambayo ilikuwa ya Uingereza lakini ikifanya kazi ndani ya taifa la Tanzania, ambayo iliitwa British Insurance Company (BIC). Mwanamke huyo alikuwa ana miaka mitatu tangu ateuliwe na kuwa bosi wa kampuni hiyo kubwa ambayo ilikuwa imejioteshea mizizi yake mikoa mingi sana Tanzania na ndani ya hiyo miaka mitatu ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kuweza kufika ndani ya taifa la Tanzania.
Harper Campbell, alikuwa ni agent wa shirika la kijasusi kutoka ndani ya nchi ya Uingereza lifahamikalo kama MI6 (MILLITARY INTELIGENCE SECTION 6). Haikueleweka sababu kubwa ya jasusi wa nchi ya Uingereza kuingia ndani ya taifa la nchi hii na kuwa moja kati ya mabosi wa kampuni hiyo kubwa ya Uingereza lakini jambo la kushangaza zaidi ni yeye kuweza kujuana na Tommy ambaye miaka yake mingi sana alikuwa ameitumia huko Uingereza kusoma, lakini pia swali gumu zaidi ilikuwa ni sababu ipi hasa ya yeye kumuita T1?
Mwanamke huyo alimsogezea mwanaume maji akiwa anamuonea huruma sana
“I’m sorry Tommy yote haya ni makosa yangu mthomasibabuya@gmail.comimi, kama ningependekeza jina la mtu mwingine au ningedanganya kuhusu uwezo wako kwa mkurugenzi huenda haya yote yasingekutokea, ungekuwa unaishi kwa amani na familia yako” mwanaume aliishia kuyanywa maji yote ya baridi kwa hasira sana ili kidogo aweze kupoa maana alihisi kama kichwa kinawaka moto isivyo kawaida.
“Wewe haupaswi kuniomba mimi msamaha H2, kwa sababu kilicho fanyika hakihusiani na sisi kukutana maana hawa watu hawajui chochote kuhusu maisha yangu ya huko nje ya nchi, hata hivyo mimi nikushukuru sana wewe kwa sababu umenifanya nimekuwa mwanadamu mwenye uwezo mkubwa sana ambao utanisaidia kuwalinda ndugu zangu walio bakia maana kama ningekuwa kama nilivyo ondoka nchini hata nisingeweza kufuatilia lolote kwa sasa kwani huo uwezo nisingekuwa nao kabisa” Tommy aliongea akiwa kama mtu ambaye amekata tamaa ya maisha kabisa kwani aliona uwezo wake haukuweza kumsaidia jambo lolote lile la kuweza kuwalinda ndugu zake kiasi kwamba akawa anatanguliza lawama kwa mwanamke huyo ambaye baada ya kumkumbusha vyema alikuja kuigundua kwamba kosa lilikuwa ni la kwake na siyo huyo mwanamke wala nchi ya Uingereza kwa ujumla.
“I’m sure kila kitu kitakuwa sawa, pole sana. Kama ukihitaji msaada wowote kwangu, nipo kwa ajili yako siku zote” Harper alitamka huku akiwa anamkumbatia mwanaume huyo mbele yake.
“Naomba uweze kunipa taarifa za huyu mtu hapa” mwanaume aliitoa ile picha ambayo aliiokota kule Mikocheni ambayo alikuwa na uhakika kwamba ilikuwa ni ya mtu ambaye alikuwa akimfuatilia.
“Anahusika nini na wewe?”
“Nipe taarifa zake kwanza ndipo uniulize maswali yako, nataka kumfahamu sana nahisi ni mtu wa mhimu kwenye kazi ambayo naifanya” mwanamke huyo alimpa ishara ya kumfuata ambapo alienda kufungua ukutani kisha pakajifunga tena, wakashuka mpaka ngazi za chini kabisa ambako kulikuwa na kuta nyingine Harper aliifungua kisha wakakutana na chumba kikubwa ambacho kilikuwa na komputa nyingi sana.
Aliziwasha komputa zote na kuketi ambapo aliingiza picha hiyo kwenye mifumo yake lakini hawakupata chochote zaidi ya kivuli tu, Harper akamgeukia Tommy
“Looks like sio mtu wa kawaida, nadhani hapa mpaka nitumie mifumo ya moja kwa moja ya MI6 ndiyo ambayo inaweza kumtambua huyu mtu”
“Fanya vyovyote vile nazihitaji sana taarifa zake”
“Ila inaweza kuwa hatari sana kwani taarifa zake zitawafikia makao makuu na wanaweza wakaanza kumchunguza ili wamujue ni nani haswa”
Ukurasa wa ishirini na nne unafika mwisho.
Wasalaam,
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Leo tunasoma kuwa na amani mkuuLeta cha Valentine's day kaka FEBIANI BABUYA