Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA NNE
Hawakuwa na namna zaidi ya kumfuata wote watatu kwani hata zile tambo zao zilikuwa zimeisha kabisa, aliyekuwa mbele alikutanishwa na ule upanga ambao ulizama kwenye paja lake ukatokezea nyuma, alidondoka hapo hapo akiwa analia na kujisaidia mwenyewe kuuchomoa upanga huo ambao ulikuwa ukimletea maumivu yasiyo ya kawaida hivyo safari ya kukutana na mtu huyo ilibakia kwa wanaume wawili ambao walikuwa wamemkaribia.

Tommy baada ya kukaribiana nao, alidunda chini kwa sarakasi akajigeuza mithili ya samani ambapo alipishana na ngumi tatu kwenye sikio lake akatua nyuma ya watu hao karibu na yule ambaye alikuwa anahangaika kuuchomoa ule upanga wake. Baada ya upanga huo kuchomolewa aliuzamisha kwenye moyo wa yule mwanaume kisha akamkutanisha na buti zito la shingo ambalo lilipelekea shingo ya mtu huyo kupinda, akadondoka hapo hapo na kupoteza maisha huku mwanaume kwenye mkono wake akiwa amebakia na upanga huo wao wakiwa wamebaki wawili tu pekee.

Ni kama hofu ilianza kutanda miongoni mwao kwani walikuwa wakiangaliana kiasi kwamba kila mtu ni kama alikuwa anampa mwenzake ishara ya kwenda kwanza japo ililazimu aende kwanza mwanaume mwingine huku kiongozi wake akiwa wa mwisho. Alisogea huku akiwa na hofu ndani yake, hicho ndicho ambacho kilimpotezeshea umakini kwani hata urushaji wake wa ngumi ulikuwa wa wasiwasi sana, sarakasi ambayo alijizungusha nayo ilikuwa ya kasi ndogo sana kiasi kwamba alichotwa mtama wakati anatua, akiwa anaelekea chini mwanaume ambaye alikuwa karibu yake alimpiga mithili ya mpira wa kutengwa na kumfanya aburuzike mpaka ukutani ambapo alijibamiza vibaya sana kichwa chake ila wakati anatua hapo ukutani upanga ulikuwa sambamba na kichwa chake, ulitoboa jicho lake moja vibaya sana ukawa umezama mpaka ndani, aliishia kutoa damu na mate tu mdomoni mithili ya mtu ambaye alikuwa na jambo la kuteta lakini aliikosa nafasi ya kuweza kulisema jambo hilo.

Yule kiongozi wao ambaye alikuwa amebakia aliikunja mikono yake akiwa anakuja kwa hasira upande wa Tommy ila kilicho mkuta ni bora angetafuta sehemu mapema ya kukimbilia, makosa ambayo aliyafanya ni kuamini kwamba ile bastola ambayo Tommy aliitupa wakati ule ndiyo pekee ambayo alikuwa nayo ndiyo maana alijua kwamba mtu huyo hana silaha nyingine ikawa amani kwao kutumia mikono kama nao walivyokuwa wamejiaminisha tangu mwanzo kwa kuiamini mikono yao kuliko silaha za moto. Lakini wakati anamsogelea mwanaume huyo Tommy aliichomoa bastola nyingine kwenye kiuno chake na kumpiga risasi nyingi sana mwanaume huyo magotini na mapajani kitu ambacho kilipelekea kudondoka chini kama ndege ambaye alikuwa kwenye mwendo mkali halafu ghafla sana akapigwa na manati.

Tommy alifanya hivyo kwa sababu aliona kama anapoteza muda na wakati huo kulikuwa kunaanza kukaribia kukucha akiwa bado hajampata dada yake kitu ambacho kingekuwa hatari sana kwa upande wa usalama wa dada yake hata yeye pia kama watu wangefanikiwa kumuona. Alikuwa anazipiga hatua zake taratibu kumsogelea yule mwanaume ili aweze kumhoji ndiyo maana hakumpiga risasi sehemu mbaya ambayo ingeyahatarisha maisha yake. Akiwa amekaribia kufika pale, ghafla sana alimuona mtu huyo akiwa anatoa povu kwenye mdomo wake, baada ya kumsogelea kwa ukaribu aligundua kwamba mtu huyo alikuwa amemeza kidonge cha kuweza kuutoa uhai wake maana yake ni kwamba ilikuwa ni bora afe kuliko kuusema ukweli.

“Shiiit!” Tommy alitamka akiwa anaondoka hapo kwa mbio kali kuelekea ndani kwani alifanya uzembe ambao ulimpa nafasi ya kujiua mtu huyo, hakutakiwa kabisa kumpa hiyo nafasi kwa sababu ndiye ambaye angeweza kumpa taarifa zote kuhusu uwepo wa dada yake. Alikagua kila sehemu lakini humo ndani palikuwa kimya na peupe kabisa kusiwe na dalili ya uwepo wa mtu yeyote yule.

“Noelia” aliita kwa hasira akiwa anapiga ukuta kwa ngumi kali ambayo ilipelekea mkono wake kuanza kuvuja damu, alijua huyo mwanamke ndiye alikuwa ametoa taarifa kwa watu hao kwamba kuna mtu anaweza kwenda hilo eneo hivyo wamtoe mtu wao na ndiyo maana alichelewa kuweza kumsaidia dada yake. Alitoka nje akiwa na ghadhabu sana, alifungua geti na kuliacha wazi akahitaji kutoweka hilo eneo lakini baada ya kufika nje alihisi kuna kivuli cha mtu kimejibanza sehemu japo kulikuwa na kiza ila taa za ndani ya geti hilo ambalo aliliacha wazi zilikuwa zinasaidia kuakisi vyema hata mwili wake ulikuwa umesisimka sana.

Alisogea kwa kasi hilo eneo lakini hakumpata mtu bali alikuta kuna picha ndogo sana ikiwa imedondoshwa bila shaka hata aliye idondosha hakujua kama aliacha ushahidi ndani ya hilo eneo hivyo hakuwa na shaka, aliamini kwamba angempata mtu huyo muda wowote ule. Aliitoa simu yake mfukoni na kupiga mahali ambapo iliita kwa muda mfupi tu ikapokelewa.

“Nakuja kwako saivi” ilikuwa ni kauli moja tu kisha akaikata simu hiyo na kuingia kwenye gari yake ambayo aliitoa kwa kasi isiyo ya kawaida kuelekea hilo eneo ambalo yeye alihitaji kwenda huku akiamini kwamba muda wowote ule polisi wangeweza kufika hilo eneo.

Safari yake Tommy ilienda kuishia Msasani ambako ndiko alikuwa anaishi mtu ambaye aliwasiliana naye kwenye simu, alikuwa ametumia dakika kumi na tano tu kufika hiyo sehemu ambayo alikuwa anaishi mtu huyo ambaye aliwasiliana naye. Geti la jumba hilo lilifunguliwa kwa rimoti bila mhusika kutoka nje gari yake ikaingizwa ndani kisha naye akapita moja kwa moja mpaka ndani kana kwamba hakukuwa na mtu wa kumuuliza kuhusu uwepo wake kwani alikuwa anawaona walinzi wakiwa wamejificha mbali na geti kiasi kwamba hata mtu angeingia ndani hakuna ambaye angeweza kujua kwamba eneo hilo lilikuwa na walinzi.

Baada ya kufika mlangoni, mlango wa ndani kabisa kwenye jengo hilo la kifahari ulifunguliwa na mwanamke mrembo sana ambaye alionekana kuwa na uraia pacha wa nchi mbili, Afrika na Uingereza. Mwanamke huyo alihitaji kumkumbatia Tommy lakini mwanaume alimsukumia mpaka kwenye sofa ambapo alitoa bastola yake na kuikoki akiwa amemuelekezea mwanamke huyo na kukitoa kitambaa chake usoni kiasi kwamba mwanamke huyo akabaki anamshangaa tu.

“T1 what’s wrong?” aliuliza mwanamke huyo kwa upole huku akionyesha wazi kabisa kwamba alimjua mtu huyo vyema.

“You promised to protect my family and see what’s happening now. You guys betrayed me” aliongea kwa hasira mno huku akiwa anamsogelea mwanamke huyo karibu zaidi kumaanisha kwamba waliahidi kuilinda familia yake lakini walikuwa wamemsaliti maana kilichokuwa kinatokea kilikuwa ni tofauti na matarajio.

“No Tommy”

“Mdogo wangu wa damu amekufa, baba yangu anaipambania hali yake hospitali ambapo hajui ataamka lini, dada yangu ametekwa na mama yangu amelazwa halafu wewe unaniambia hapana, unahisi naweza kukuacha hai?” hakutaka ngonjera nyingi kutoka kwa mwanamke huyo ambaye aliishia kusikitika tu baada ya kumuona huyo mwanaume ambaye yeye alikuwa anamwita T1 akiwa kwenye hali kama hiyo.

“Unakumbuka makubaliano ambayo tuliingia na wewe?”

“It doesn’t matter”

“It’s what matters now. Tulikuguarantee kwamba miaka yote ambayo ungekuwa unaifanya kazi yetu familia yako ingekuwa salama na tumehakikisha hilo lakini kwenye makubaliano yetu ilikuwa ni kwamba mwezi mmoja kabla ya wewe kurudi mkataba wetu wa kuilinda familia yako unaisha na utakuja kuilinda mwenyewe na wewe mwenyewe ndiye ambaye ulitoa hilo pendekezo, sasa kwanini unakuja kunilaumu na kuanza kunitishia kuniua mimi?” mwanamke huyo naye alijibu kwa ukali sana kwa lugha ya Kiswahili ambayo hakuwa akiitamka vizuri sana lakini ilikuwa inaeleweka vyema. Mwanaume alichoka na kukaa chini baada ya kuambiwa maneno hayo ambayo yalionekana kumuingia vyema sana kwenye kichwa chake.


HARPER CAMPBELL
Ndiye mwanamke ambaye Tommy alikuwa amekutana naye wakati huo ambao alikuwa anafanya naye mazungumzo. Harper alikuwa ni mtendaji mkuu (CEO) na mkurugenzi mkuu (MD) wa kampuni kubwa ya bima ambayo ilikuwa ya Uingereza lakini ikifanya kazi ndani ya taifa la Tanzania, ambayo iliitwa British Insurance Company (BIC). Mwanamke huyo alikuwa ana miaka mitatu tangu ateuliwe na kuwa bosi wa kampuni hiyo kubwa ambayo ilikuwa imejioteshea mizizi yake mikoa mingi sana Tanzania na ndani ya hiyo miaka mitatu ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kuweza kufika ndani ya taifa la Tanzania.

Harper Campbell, alikuwa ni agent wa shirika la kijasusi kutoka ndani ya nchi ya Uingereza lifahamikalo kama MI6 (MILLITARY INTELIGENCE SECTION 6). Haikueleweka sababu kubwa ya jasusi wa nchi ya Uingereza kuingia ndani ya taifa la nchi hii na kuwa moja kati ya mabosi wa kampuni hiyo kubwa ya Uingereza lakini jambo la kushangaza zaidi ni yeye kuweza kujuana na Tommy ambaye miaka yake mingi sana alikuwa ameitumia huko Uingereza kusoma, lakini pia swali gumu zaidi ilikuwa ni sababu ipi hasa ya yeye kumuita T1?

Mwanamke huyo alimsogezea mwanaume maji akiwa anamuonea huruma sana

“I’m sorry Tommy yote haya ni makosa yangu mthomasibabuya@gmail.comimi, kama ningependekeza jina la mtu mwingine au ningedanganya kuhusu uwezo wako kwa mkurugenzi huenda haya yote yasingekutokea, ungekuwa unaishi kwa amani na familia yako” mwanaume aliishia kuyanywa maji yote ya baridi kwa hasira sana ili kidogo aweze kupoa maana alihisi kama kichwa kinawaka moto isivyo kawaida.

“Wewe haupaswi kuniomba mimi msamaha H2, kwa sababu kilicho fanyika hakihusiani na sisi kukutana maana hawa watu hawajui chochote kuhusu maisha yangu ya huko nje ya nchi, hata hivyo mimi nikushukuru sana wewe kwa sababu umenifanya nimekuwa mwanadamu mwenye uwezo mkubwa sana ambao utanisaidia kuwalinda ndugu zangu walio bakia maana kama ningekuwa kama nilivyo ondoka nchini hata nisingeweza kufuatilia lolote kwa sasa kwani huo uwezo nisingekuwa nao kabisa” Tommy aliongea akiwa kama mtu ambaye amekata tamaa ya maisha kabisa kwani aliona uwezo wake haukuweza kumsaidia jambo lolote lile la kuweza kuwalinda ndugu zake kiasi kwamba akawa anatanguliza lawama kwa mwanamke huyo ambaye baada ya kumkumbusha vyema alikuja kuigundua kwamba kosa lilikuwa ni la kwake na siyo huyo mwanamke wala nchi ya Uingereza kwa ujumla.

“I’m sure kila kitu kitakuwa sawa, pole sana. Kama ukihitaji msaada wowote kwangu, nipo kwa ajili yako siku zote” Harper alitamka huku akiwa anamkumbatia mwanaume huyo mbele yake.

“Naomba uweze kunipa taarifa za huyu mtu hapa” mwanaume aliitoa ile picha ambayo aliiokota kule Mikocheni ambayo alikuwa na uhakika kwamba ilikuwa ni ya mtu ambaye alikuwa akimfuatilia.

“Anahusika nini na wewe?”

“Nipe taarifa zake kwanza ndipo uniulize maswali yako, nataka kumfahamu sana nahisi ni mtu wa mhimu kwenye kazi ambayo naifanya” mwanamke huyo alimpa ishara ya kumfuata ambapo alienda kufungua ukutani kisha pakajifunga tena, wakashuka mpaka ngazi za chini kabisa ambako kulikuwa na kuta nyingine Harper aliifungua kisha wakakutana na chumba kikubwa ambacho kilikuwa na komputa nyingi sana.

Aliziwasha komputa zote na kuketi ambapo aliingiza picha hiyo kwenye mifumo yake lakini hawakupata chochote zaidi ya kivuli tu, Harper akamgeukia Tommy

“Looks like sio mtu wa kawaida, nadhani hapa mpaka nitumie mifumo ya moja kwa moja ya MI6 ndiyo ambayo inaweza kumtambua huyu mtu”

“Fanya vyovyote vile nazihitaji sana taarifa zake”
“Ila inaweza kuwa hatari sana kwani taarifa zake zitawafikia makao makuu na wanaweza wakaanza kumchunguza ili wamujue ni nani haswa”

Ukurasa wa ishirini na nne unafika mwisho.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA NNE
Hawakuwa na namna zaidi ya kumfuata wote watatu kwani hata zile tambo zao zilikuwa zimeisha kabisa, aliyekuwa mbele alikutanishwa na ule upanga ambao ulizama kwenye paja lake ukatokezea nyuma, alidondoka hapo hapo akiwa analia na kujisaidia mwenyewe kuuchomoa upanga huo ambao ulikuwa ukimletea maumivu yasiyo ya kawaida hivyo safari ya kukutana na mtu huyo ilibakia kwa wanaume wawili ambao walikuwa wamemkaribia.

Tommy baada ya kukaribiana nao, alidunda chini kwa sarakasi akajigeuza mithili ya samani ambapo alipishana na ngumi tatu kwenye sikio lake akatua nyuma ya watu hao karibu na yule ambaye alikuwa anahangaika kuuchomoa ule upanga wake. Baada ya upanga huo kuchomolewa aliuzamisha kwenye moyo wa yule mwanaume kisha akamkutanisha na buti zito la shingo ambalo lilipelekea shingo ya mtu huyo kupinda, akadondoka hapo hapo na kupoteza maisha huku mwanaume kwenye mkono wake akiwa amebakia na upanga huo wao wakiwa wamebaki wawili tu pekee.

Ni kama hofu ilianza kutanda miongoni mwao kwani walikuwa wakiangaliana kiasi kwamba kila mtu ni kama alikuwa anampa mwenzake ishara ya kwenda kwanza japo ililazimu aende kwanza mwanaume mwingine huku kiongozi wake akiwa wa mwisho. Alisogea huku akiwa na hofu ndani yake, hicho ndicho ambacho kilimpotezeshea umakini kwani hata urushaji wake wa ngumi ulikuwa wa wasiwasi sana, sarakasi ambayo alijizungusha nayo ilikuwa ya kasi ndogo sana kiasi kwamba alichotwa mtama wakati anatua, akiwa anaelekea chini mwanaume ambaye alikuwa karibu yake alimpiga mithili ya mpira wa kutengwa na kumfanya aburuzike mpaka ukutani ambapo alijibamiza vibaya sana kichwa chake ila wakati anatua hapo ukutani upanga ulikuwa sambamba na kichwa chake, ulitoboa jicho lake moja vibaya sana ukawa umezama mpaka ndani, aliishia kutoa damu na mate tu mdomoni mithili ya mtu ambaye alikuwa na jambo la kuteta lakini aliikosa nafasi ya kuweza kulisema jambo hilo.

Yule kiongozi wao ambaye alikuwa amebakia aliikunja mikono yake akiwa anakuja kwa hasira upande wa Tommy ila kilicho mkuta ni bora angetafuta sehemu mapema ya kukimbilia, makosa ambayo aliyafanya ni kuamini kwamba ile bastola ambayo Tommy aliitupa wakati ule ndiyo pekee ambayo alikuwa nayo ndiyo maana alijua kwamba mtu huyo hana silaha nyingine ikawa amani kwao kutumia mikono kama nao walivyokuwa wamejiaminisha tangu mwanzo kwa kuiamini mikono yao kuliko silaha za moto. Lakini wakati anamsogelea mwanaume huyo Tommy aliichomoa bastola nyingine kwenye kiuno chake na kumpiga risasi nyingi sana mwanaume huyo magotini na mapajani kitu ambacho kilipelekea kudondoka chini kama ndege ambaye alikuwa kwenye mwendo mkali halafu ghafla sana akapigwa na manati.

Tommy alifanya hivyo kwa sababu aliona kama anapoteza muda na wakati huo kulikuwa kunaanza kukaribia kukucha akiwa bado hajampata dada yake kitu ambacho kingekuwa hatari sana kwa upande wa usalama wa dada yake hata yeye pia kama watu wangefanikiwa kumuona. Alikuwa anazipiga hatua zake taratibu kumsogelea yule mwanaume ili aweze kumhoji ndiyo maana hakumpiga risasi sehemu mbaya ambayo ingeyahatarisha maisha yake. Akiwa amekaribia kufika pale, ghafla sana alimuona mtu huyo akiwa anatoa povu kwenye mdomo wake, baada ya kumsogelea kwa ukaribu aligundua kwamba mtu huyo alikuwa amemeza kidonge cha kuweza kuutoa uhai wake maana yake ni kwamba ilikuwa ni bora afe kuliko kuusema ukweli.

“Shiiit!” Tommy alitamka akiwa anaondoka hapo kwa mbio kali kuelekea ndani kwani alifanya uzembe ambao ulimpa nafasi ya kujiua mtu huyo, hakutakiwa kabisa kumpa hiyo nafasi kwa sababu ndiye ambaye angeweza kumpa taarifa zote kuhusu uwepo wa dada yake. Alikagua kila sehemu lakini humo ndani palikuwa kimya na peupe kabisa kusiwe na dalili ya uwepo wa mtu yeyote yule.

“Noelia” aliita kwa hasira akiwa anapiga ukuta kwa ngumi kali ambayo ilipelekea mkono wake kuanza kuvuja damu, alijua huyo mwanamke ndiye alikuwa ametoa taarifa kwa watu hao kwamba kuna mtu anaweza kwenda hilo eneo hivyo wamtoe mtu wao na ndiyo maana alichelewa kuweza kumsaidia dada yake. Alitoka nje akiwa na ghadhabu sana, alifungua geti na kuliacha wazi akahitaji kutoweka hilo eneo lakini baada ya kufika nje alihisi kuna kivuli cha mtu kimejibanza sehemu japo kulikuwa na kiza ila taa za ndani ya geti hilo ambalo aliliacha wazi zilikuwa zinasaidia kuakisi vyema hata mwili wake ulikuwa umesisimka sana.

Alisogea kwa kasi hilo eneo lakini hakumpata mtu bali alikuta kuna picha ndogo sana ikiwa imedondoshwa bila shaka hata aliye idondosha hakujua kama aliacha ushahidi ndani ya hilo eneo hivyo hakuwa na shaka, aliamini kwamba angempata mtu huyo muda wowote ule. Aliitoa simu yake mfukoni na kupiga mahali ambapo iliita kwa muda mfupi tu ikapokelewa.

“Nakuja kwako saivi” ilikuwa ni kauli moja tu kisha akaikata simu hiyo na kuingia kwenye gari yake ambayo aliitoa kwa kasi isiyo ya kawaida kuelekea hilo eneo ambalo yeye alihitaji kwenda huku akiamini kwamba muda wowote ule polisi wangeweza kufika hilo eneo.

Safari yake Tommy ilienda kuishia Msasani ambako ndiko alikuwa anaishi mtu ambaye aliwasiliana naye kwenye simu, alikuwa ametumia dakika kumi na tano tu kufika hiyo sehemu ambayo alikuwa anaishi mtu huyo ambaye aliwasiliana naye. Geti la jumba hilo lilifunguliwa kwa rimoti bila mhusika kutoka nje gari yake ikaingizwa ndani kisha naye akapita moja kwa moja mpaka ndani kana kwamba hakukuwa na mtu wa kumuuliza kuhusu uwepo wake kwani alikuwa anawaona walinzi wakiwa wamejificha mbali na geti kiasi kwamba hata mtu angeingia ndani hakuna ambaye angeweza kujua kwamba eneo hilo lilikuwa na walinzi.

Baada ya kufika mlangoni, mlango wa ndani kabisa kwenye jengo hilo la kifahari ulifunguliwa na mwanamke mrembo sana ambaye alionekana kuwa na uraia pacha wa nchi mbili, Afrika na Uingereza. Mwanamke huyo alihitaji kumkumbatia Tommy lakini mwanaume alimsukumia mpaka kwenye sofa ambapo alitoa bastola yake na kuikoki akiwa amemuelekezea mwanamke huyo na kukitoa kitambaa chake usoni kiasi kwamba mwanamke huyo akabaki anamshangaa tu.

“T1 what’s wrong?” aliuliza mwanamke huyo kwa upole huku akionyesha wazi kabisa kwamba alimjua mtu huyo vyema.

“You promised to protect my family and see what’s happening now. You guys betrayed me” aliongea kwa hasira mno huku akiwa anamsogelea mwanamke huyo karibu zaidi kumaanisha kwamba waliahidi kuilinda familia yake lakini walikuwa wamemsaliti maana kilichokuwa kinatokea kilikuwa ni tofauti na matarajio.

“No Tommy”

“Mdogo wangu wa damu amekufa, baba yangu anaipambania hali yake hospitali ambapo hajui ataamka lini, dada yangu ametekwa na mama yangu amelazwa halafu wewe unaniambia hapana, unahisi naweza kukuacha hai?” hakutaka ngonjera nyingi kutoka kwa mwanamke huyo ambaye aliishia kusikitika tu baada ya kumuona huyo mwanaume ambaye yeye alikuwa anamwita T1 akiwa kwenye hali kama hiyo.

“Unakumbuka makubaliano ambayo tuliingia na wewe?”

“It doesn’t matter”

“It’s what matters now. Tulikuguarantee kwamba miaka yote ambayo ungekuwa unaifanya kazi yetu familia yako ingekuwa salama na tumehakikisha hilo lakini kwenye makubaliano yetu ilikuwa ni kwamba mwezi mmoja kabla ya wewe kurudi mkataba wetu wa kuilinda familia yako unaisha na utakuja kuilinda mwenyewe na wewe mwenyewe ndiye ambaye ulitoa hilo pendekezo, sasa kwanini unakuja kunilaumu na kuanza kunitishia kuniua mimi?” mwanamke huyo naye alijibu kwa ukali sana kwa lugha ya Kiswahili ambayo hakuwa akiitamka vizuri sana lakini ilikuwa inaeleweka vyema. Mwanaume alichoka na kukaa chini baada ya kuambiwa maneno hayo ambayo yalionekana kumuingia vyema sana kwenye kichwa chake.


HARPER CAMPBELL
Ndiye mwanamke ambaye Tommy alikuwa amekutana naye wakati huo ambao alikuwa anafanya naye mazungumzo. Harper alikuwa ni mtendaji mkuu (CEO) na mkurugenzi mkuu (MD) wa kampuni kubwa ya bima ambayo ilikuwa ya Uingereza lakini ikifanya kazi ndani ya taifa la Tanzania, ambayo iliitwa British Insurance Company (BIC). Mwanamke huyo alikuwa ana miaka mitatu tangu ateuliwe na kuwa bosi wa kampuni hiyo kubwa ambayo ilikuwa imejioteshea mizizi yake mikoa mingi sana Tanzania na ndani ya hiyo miaka mitatu ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kuweza kufika ndani ya taifa la Tanzania.

Harper Campbell, alikuwa ni agent wa shirika la kijasusi kutoka ndani ya nchi ya Uingereza lifahamikalo kama MI6 (MILLITARY INTELIGENCE SECTION 6). Haikueleweka sababu kubwa ya jasusi wa nchi ya Uingereza kuingia ndani ya taifa la nchi hii na kuwa moja kati ya mabosi wa kampuni hiyo kubwa ya Uingereza lakini jambo la kushangaza zaidi ni yeye kuweza kujuana na Tommy ambaye miaka yake mingi sana alikuwa ameitumia huko Uingereza kusoma, lakini pia swali gumu zaidi ilikuwa ni sababu ipi hasa ya yeye kumuita T1?

Mwanamke huyo alimsogezea mwanaume maji akiwa anamuonea huruma sana

“I’m sorry Tommy yote haya ni makosa yangu mthomasibabuya@gmail.comimi, kama ningependekeza jina la mtu mwingine au ningedanganya kuhusu uwezo wako kwa mkurugenzi huenda haya yote yasingekutokea, ungekuwa unaishi kwa amani na familia yako” mwanaume aliishia kuyanywa maji yote ya baridi kwa hasira sana ili kidogo aweze kupoa maana alihisi kama kichwa kinawaka moto isivyo kawaida.

“Wewe haupaswi kuniomba mimi msamaha H2, kwa sababu kilicho fanyika hakihusiani na sisi kukutana maana hawa watu hawajui chochote kuhusu maisha yangu ya huko nje ya nchi, hata hivyo mimi nikushukuru sana wewe kwa sababu umenifanya nimekuwa mwanadamu mwenye uwezo mkubwa sana ambao utanisaidia kuwalinda ndugu zangu walio bakia maana kama ningekuwa kama nilivyo ondoka nchini hata nisingeweza kufuatilia lolote kwa sasa kwani huo uwezo nisingekuwa nao kabisa” Tommy aliongea akiwa kama mtu ambaye amekata tamaa ya maisha kabisa kwani aliona uwezo wake haukuweza kumsaidia jambo lolote lile la kuweza kuwalinda ndugu zake kiasi kwamba akawa anatanguliza lawama kwa mwanamke huyo ambaye baada ya kumkumbusha vyema alikuja kuigundua kwamba kosa lilikuwa ni la kwake na siyo huyo mwanamke wala nchi ya Uingereza kwa ujumla.

“I’m sure kila kitu kitakuwa sawa, pole sana. Kama ukihitaji msaada wowote kwangu, nipo kwa ajili yako siku zote” Harper alitamka huku akiwa anamkumbatia mwanaume huyo mbele yake.

“Naomba uweze kunipa taarifa za huyu mtu hapa” mwanaume aliitoa ile picha ambayo aliiokota kule Mikocheni ambayo alikuwa na uhakika kwamba ilikuwa ni ya mtu ambaye alikuwa akimfuatilia.

“Anahusika nini na wewe?”

“Nipe taarifa zake kwanza ndipo uniulize maswali yako, nataka kumfahamu sana nahisi ni mtu wa mhimu kwenye kazi ambayo naifanya” mwanamke huyo alimpa ishara ya kumfuata ambapo alienda kufungua ukutani kisha pakajifunga tena, wakashuka mpaka ngazi za chini kabisa ambako kulikuwa na kuta nyingine Harper aliifungua kisha wakakutana na chumba kikubwa ambacho kilikuwa na komputa nyingi sana.

Aliziwasha komputa zote na kuketi ambapo aliingiza picha hiyo kwenye mifumo yake lakini hawakupata chochote zaidi ya kivuli tu, Harper akamgeukia Tommy

“Looks like sio mtu wa kawaida, nadhani hapa mpaka nitumie mifumo ya moja kwa moja ya MI6 ndiyo ambayo inaweza kumtambua huyu mtu”

“Fanya vyovyote vile nazihitaji sana taarifa zake”
“Ila inaweza kuwa hatari sana kwani taarifa zake zitawafikia makao makuu na wanaweza wakaanza kumchunguza ili wamujue ni nani haswa”

Ukurasa wa ishirini na nne unafika mwisho.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Usisahau kutuwekea leo mkuu[mention]FEBIANI BABUYA [/mention]
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA TANO
“Nitakuwa wa kwanza kumpata, so do it” hakuwa na namna Harper zaidi ya kufanya kama alivyokuwa ameombwa na mtu huyo, aliamua kuingia kwenye mifumo ya ulinzi ya MI6 moja kwa moja ambapo ilichukua dakika moja tu pekee ilikuja picha halisi ya mwanaume huyo ambaye alikuwa kwenye hiyo picha pamoja na taarifa zake.

“Oooooh shiiiit! No way, he is an agent” kauli ya mshangao wa Harper kwamba mwanaume huyo alikuwa ni jasusi ndiyo ambayo hata Tommy ilimshangaza pia

“Whaaaaat?”

“Matiasi Ndugu, ana miaka thelathini na tano, ni jasusi kutoka ndani ya idara ya usalama ya nchi ya Tanzania. Amezaliwa ndani ya mkoa wa Kigoma Ujiji huko ambako alisoma na kujiunga na jeshi akiwa na umri mdgo kabisa na safari yake ilianzia hapo. Uwezo wake jeshini ndio ambao ulimfanya aweze kuonwa na viongozi wakuu wa idara hii nyeti na kuona anafaa ambapo waliamua kumchukua na kuendeleza uwezo wake akawa rasmi ameingia kwenye idara hiyo kwa mara ya kwanza. Amefanya kazi nyingi sana ndani ya idara ikiwemo ya kwenda Kongo kuwaokoa mateka ambao walikuwa huko na nchi zingine kama Nigeria na kwa sasa yupo ndani ya nchi” zilikuwa ni taarifa ambazo alikuwa anazitamka Harper ambazo zilimfanya Tommy abaki anashangaa sana, mwanaume ambaye alikuwa anamfuatilia alikuwa ni shushushu ndani ya nchi ya Tanzania lakini pia alikuwa amefanya kazi nyingi sana za kijasusi nje ya nchi.

“Ohhhhh shiiiit! Maana yake amesha nijua tayari”

“Kakujuaje? Kwani umekutana naye wapi?”

“Ameniona nikiwa naua watu”

“Whaaat? Wewe si umefika leo nchini usiku au”

“Yeap” Tommy alijibu huku akimpa stori nzima Harper namna mambo yalivyokuwa.

“Ohhhh my God! Hii ni hatari sana kama umejulikana kwa hawa watu mapema hivi, hauna chaguo lingine unatakiwa umtafute huyu mtu umuue vinginevyo kila kitu chako kitaharibika kwa sababu unaweza ukaishia kukamatwa ikawa hatari sana hata kwetu pia”

“Yes, nitakuwa mtu wa kwanza kukutana naye baada ya yeye kujua haya”

“Kuna jambo ambalo sijakwambia kwenye hizi taarifa zake”
“Lipi”

“Amewahi kuwa na kesi ya kumuua agent mwenzake lakini alisamehewa”
“Kivipi?”

“Kuna maelezo ambayo yameendelea huku chini yameandikwa kwa lugha ya kiebrania nadhani ni kwa sababu ya unyeti wa tukio hili ila kwa sababu mimi sio mgeni na hii lugha haijawa tatizo kwangu. Inaonekana kwamba wakati anakaribia kuoa walimteua agent mwenzake ambaye alikuwa anafanya kazi ya kuweza kumchunguza mkewe mtarajiwa ili waone kama anafaa kuwa mkewe kwa kufanya kitu ambacho huwa kinaitwa Vetting. Sasa kwa bahati mbaya yule agent ambaye alitumwa hiyo kazi alikuja kujisahau na kuingia kwenye mapenzi na mchumba wa mwenzake ambaye alikuwa anatarajia kumuoa mwisho wa siku Matiasi ambaye anatumia jina la kazi kama Nickson au Nick alikuja kujua na ndoa ikaharibika hivyo akaamua kumuua huyo agent mwenzake na huyo mwanamke ambaye yeye alitakiwa kumuoa” hayo ndiyo maelezo ambayo yalikuwa yameandikwa kwa hiyo lugha ya kiebrania

“Fu******k, mwanaume anaendeshwa na mihemko ya mapenzi namna hiyo kiasi kwamba anaharibu kazi kwa kumuua mwenzake? Sasa imewezekana vipi akawa ameachwa mpaka leo wakati kosa hilo alistahili adhabu kali sana”

“Mpaka hapo ujue kwamba kiongozi wake anajua kwamba ana umuhimu mkubwa sana”

“Asante” Tommy alianza kujongea ili atoke humo ndani baada ya kuona amekamilisha alichokuwa anakihitaji ila ni kama kuna kitu alikikumbuka hivyo ikamlazimu kuweza kurudi tena ili kuteta na mwanamke huyo.

“Harper kuna maswali ambayo nahitaji uweze kunijibu. Hivi kile kitu ambacho mlitaka niwatengenezee na nikakitengeneza ni nini hasa kiasi kwamba mkaamua kunichagua mimi wakati mna watu wengi sana wenye uwezo mkubwa zaidi yangu, na ni sababu ipi ambayo iliwafanya muone mimi ndiye mtu ninaye stahili kuwepo kwenye hiyo nafasi?” vilionekana kuwa vitu vya siri sana ambavyo alikuwa anauliza Tommy ambavyo vilimfanya Harper kushtuka sana.

“Mimi sijui lolote Tommy” alijibu huku akiwa anazuga na kuangalia pembeni upande ambao zilikuwepo komputa zake hizo.

“Sikulazimishi ila nakuuliza kama rafiki, familia yangu ipo matatani kwa sasa halafu kuna mambo kuhusu maisha yangu pia nakuwa siyajui, sidhani hata kama ungekuwa wewe ungekuwa na amani juu ya hili jambo, nakuomba sana unieleze japo kwa ufupi tu”

“Ooooooh Tommy, hili jambo kama likijulikana kwamba nimekwambia wewe basi huenda naweza hata kufa” mwanamke huyo alitamka huku akizima kila kitu humo ndani na kukagua kama hakukuwa na kifaa chochote cha mawasiliano.


“MI6 kuhakikisha kwamba tunafanya kazi kwa ufanisi tumesambaza watu wetu kila maeneo nyeti kama vile kwenye taasisi kubwa, kwenye vyuo vikubwa na maeneo nyeti pia serikalini. Hawa watu huwa wanakusanya kila taarifa ambayo inaweza kuwa mhimu kwa idara yetu lakini pia huwa wanatusaidia sana kuweza watu wapya ndani ya idara yetu. Ndani ya OXFORD pale tuna watu wetu wengi sana kuanzia kwenye utawala wa chuo mpaka baadhi ya wanafunzi wenyewe”

“Kuingia kwenye kile chuo inahitajika mtu uwe na ufaulu mkubwa sana lakini pia uwe na uwezo mkubwa sana kichwani kwa kupima intelligent quotient (IQ) ya kila mwanafunzi iwe kwa yeye kuambiwa au kuto ambiwa maana ndiyo sheria husika ya chuo. Baada ya wewe kufika pale tulipata taarifa kwamba ulikuwa na uwezo mkubwa sana kichwani kiasi kwamba ulikuwa upo tofauti mno na wanafunzi wengine hivyo tukaona kwamba ilikuwa ni nafasi nzuri sana ya sisi kuweza kuutumia uwezo wako wa akili kuweza kuyakamilisha mambo yetu ndani ya taifa letu”

“Ndipo hapo ambapo nilitumwa mimi kuja ndani ya chuo huku nikijifanya kuwa mwanafunzi pia na kuwa karibu na wewe ambapo kwa baadae nilikufuatilia mwenyewe na nikathibitisha hilo na kwa vile tulikuwa karibu basi ikawa rahisi sana mimi kujua ratiba zako nyingi ambapo pia nilifanikisha wewe kuweza kukamatwa kwako. Hapo ndipo tulikupa masharti ili uweze kukubali kutufanyia kazi yetu na kama usingefanya vile tukakupa onyo kwamba tutaua familia yako, tungeliwekea vikwazo vya uchumi taifa lako, kuchafua hali ya kisiasa kwenye taifa lako hivyo ukakubali na kutuomba tusifanye hicho kitu bali ungefanya kazi yetu na sisi hicho ndicho tulikuwa tunakihitaji”

“Baada ya wewe kukubali hilo jambo ndipo rasmi tukakusaini kuwa kama memba mpya wa MI6 na tukakwambia ukweli kuhusu taasisi yetu huku tukiwa na uhakika kwamba hakuna jambo baya ambalo unaweza kulifanya kwa sababu ya kuogopa familia kuguswa na nchi yako kwa ujumla na ndipo hapo ambapo ulianza rasmi mafunzo ambayo yamekufanya wewe kuwa dubwana la namna hiyo kwani ulichomwa na sindano za kukuongezea nguvu kwenye mwili wako”

“Ukiwa unaendelea na hayo mafunzo ndipo ukawa unatengeneza kirusi ambacho uliombwa utengeneze pamoja na dawa yake, kirusi ambacho kingekuwa hatari zaidi kuwahi kutokea duniani huku antidote yake ikipewa kipaumbele moja kwa moja. Miaka miwili kabla ya kukamilisha mafunzo yako ulikuwa umekamilisha kutengeneza kile kirusi ambacho hata wewe haukujua kazi yake kwamba ilikuwa ni nini hasa na matumizi yake yakengekuwa wapi” mwanamke huyo alimeza mate kwani alikuwa anatoboa siri za nchi kijinga sana.

“Ukweli ni kwamba kile kirusi hakikuwa kwa sababu ya kujilinda kama ambavyo wewe ulipewa taarifa zile bali kile kirusi kiliandaliwa kwa ajili ya nchi ya Urusi ambao kwa sasa wanatishia vita baridi dhidi ya mataifa ya nchi za ulaya. Hivyo tulipanga kwamba kama Urusi angekuja kuanzisha vita na mataifa ya Ulaya basi kwa kupitia majasusi wetu kule Urusi tulihitaji kukisambaza hiki kirusi ambacho bila shaka kingewaathiri sana na ili kuipata dawa yake walitakiwa kukubali masharti yetu yote ambayo tulikuwa tunawapa. Hiyo ingetupa pia nafasi kubwa sana ndani ya mataifa ya umoja wa ulaya na kutufanya tutengeneze pesa nyingi mno na kuwa taifa ambalo lingefungua fursa mpya kwa kizazi kijacho pamoja na kuanza kuirudisha taratibu Uingereza kuja kuwa kama taifa lenye nguvu zaidi duniani kama ilivyokuwa hapo zamani kidogo, hivyo mpango ulianza kutekelezeka baada ya ujio wako” hayo maelezo yalimchosha Tommy hata nguvu za kusimama hakuwa nazo tena akaishia kukaa kwenye kochi, alikuwa anaambiwa mambo ambayo yalikuwa yanamfanya ajutie sana kuweza kukutana na watu hao kwenye maisha yake hiyo stori ilikokuwa inaelekea hakukuwa kuzuri kabisa.

“Lakini jambo baya zaidi ni kwamba kirusi hicho kiliweza kuibiwa na kutoweka kwenye mikono yetu” Harper alihema kwa nguvu wakati akiwa anaendelea kuelezea jambo hilo, alitegemea kama mwanaume huyo ambaye alikuwa mbele yake angemuuliza swali lakini alikuwa amemkazia macho tu na macho ambayo ndani yake ulionekana moto wa hasira sana ukiwa unawaka.

“Kiliibiwa na agent wa MOSSAD” ni jambo ambalo hata Tommy hakulitarajia kusikia kwamba mtu ambaye aliiba kirusi hicho pamoja na antidote yake alikuwa ni jasusi kutoka ndani ya shirika la kijasusi la Israel.

“Richard Murphy, ndilo jina la mwanaume ambaye aliweza kupotea na vitu hivyo. Alikuwa ni mwingereza kwa kuzaliwa lakini wazazi wake walikuwa ni kutoka ndani ya taifa la Israel hivyo tangu akiwa mdogo ilisemekana kwamba watu hao waliwahi kumtafuta na kumlisha sumu kuhusu taifa lake hilo hivyo akawa anakua akiwa anajua kabisa kwamba yeye ni Muisrael. Hivyo baadae alikuja kupata nafasi ya kujiunga na shirika letu na kutokana na kazi nzito ambazo alizifanya alifanikiwa kuwa miongoni mwa viongozi wakubwa sana ndani ya MI6 na hilo ndilo kosa kubwa zaidi kuwahi kufanywa na MI6 kumpa nafasi mtu huyo tena ya juu sana huku wakiwa wana imani kwamba ni damu yao na mtu mwenye msimamo na nchi yake kwani licha ya kufanyiwa uchunguzi mkali hakuwahi kushtukiwa kwa jambo lolote lile”

“Kwa sababu alikuwa kwenye nafasi za juu sana basi alikuwa na taarifa nyingi sana kuhusu kila mipango mikubwa ambayo ilikuwa inaendelea hivyo baada ya kufanikiwa kutoroka navyo alitaka kukimbilia nyumbani kwao Israel ili akawape watu hao kirusi hicho na antidote yake pamoja na formula ya utengenezaji ambayo uliitengeneza wewe. Lakini kwa bahati mbaya wakati yupo Airport huko morocco ambako alipitia ili asijulikane alikamatwa na wanaume ambao walidaiwa kutokea ndani ya kundi la kigaidi ya ISIS na kupotea naye ambapo kwa baadae alikutwa akiwa amenyongwa”

“Kuuawa kwake ilimaanisha kwamba kirusi hicho kiliingia kwenye mikono ya ISIS ikawa hatari nyingine kwa dunia kwa sababu wao wangekitumia kuitishia dunia, na kama ingejulikana kwamba sisi ndio ambao tulikitengeneza basi dunia nzima ingetugeukia hata washirika wetu kama Marekani wasingeweza kabisa kutuelewa. Hivyo ikawa inatakiwa kufanyika jitihada ili tuweze kukipata kwa nama yoyote ile ambapo tulijaribu kuwashirikisha MOSSAD ili tuyamalize mezani lakini wakakana kabisa kukipata kirusi hicho na wao ndio ambao walikuja kutusaidia kutupatia taarifa kwamba kiliingia kwenye kundi la ISIS hivyo tukatakiwa kumtafuta gaidi mkubwa wa kundi hilo tuweze kukipata maana kama watu hao wangeanza kukitumia vibaya ingeweza kuwa hatari sana kwa dunia”

Ya dunia yanatisha sana, ukurasa wa ishirini na tano unafika mwisho.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA SITA
“Kweli tulifanikiwa kumpata gaidi mmoja ambaye tulimlipa pesa nyingi sana tukamhamisha na nchi ambapo kwa sasa anaishi Uingereza chini ya usimamizi wetu, yeye ndiye ambaye alitusaidia kutupa taarifa kwamba ni kweli kirusi hicho walikipata lakini kabla hakijafika kwa wakubwa kuna gaidi mmoja alikimbia nacho kwa kuamini kwamba kupitia kirusi hicho angeweza kutengeneza mabilioni ya fedha lakini kama angekipeleka kwa mabosi zake huenda wangemuua tu ili siri wabaki nayo wao hivyo aliamua kukimbia na kuelekea Tanzania ambako aliamini hakuna mtu anaweza kuja kuhisi kwamba yupo huko”

“Hivyo baada ya kupata hizo taarifa ndipo mimi nikatumwa kuja kuhu kufanya hiyo kazi ya kumpata gaidi huyo ili kuweza kuvipata hivyo vitu ila kwa bahati mbaya au nzuri mwanaume huyo kuna mtu ambaye alimkabidhi hivyo vitu na vimehifadhiwa sehemu salama kabisa ila namna ya kuvipata ndiyo imekuwa changamoto kubwa sana”

“Baada ya kuingia Tanzania aliamini kwamba licha ya kujificha kuna siku anaweza kuja kukamatwa kama sio na wenzake basi na mamlaka za usalama wa nchi hivyo akaamua kutafuta usalama wake kwanza na ndipo alipo mtafuta raisi wa nchi ya Tanzania ili kufanya makubaliano na……” mwanamke huyo alitaka kuendelea lakini Tommy alisimama na kumzuia

“No, no, no no way, haiwezekani, haiwezekani, haiwezekaniiiiiiii” alitamka kwa sauti kali sana kiasi kwamba mpaka mishipa ilijichora kwenye shingo yake, muda ulikuwa unaenda kasi sana kwa upande wake yeye lakini muda usingempa nafasi ya kuweza kumsubiri, ukweli ulikuwa unabaki kuwa ukweli hata kama asingehitaji hilo jambo liwe hivyo.

“Ni ngumu sana kuamini lakini ndivyo mambo yalivyo, mwanaume huyo alikutana na raisi na wakafanya makubaliano ya kuja kukiuza kwa pesa ndefu sana na mwanaume huyo ili kujiwekea ulinzi akatishia kwamba yeye anatokea kwenye kundi hilo la kigaidi hivyo kama akiletewa ujanja ujanja basi ataichoma nchi na kundi hilo lije kuvamia lakini pia raisi huyo kama angemzunguka basi dunia nzima ingejua ukweli kwamba yeye alikuwa anahitaji kuweza kuiteketeza nchi yake, kwahiyo akawa anahitaji raisi ndiye amlinde. Kwahiyo ndiyo sababu ya mimi kuwa hapa mpaka leo kwa sababu kirusi kipo nchini hapa lakini hata gaidi huyo yupo hapa hapa nchini ila kujulikana kwamba yuko wapi hilo ni swala ambalo hata mimi sijui bado” ni taarifa ambazo zilimfanya Tommy acheke kwa sauti kubwa sana mithili ya mtu mwenye furaha lakini haikuwa hivyo yeye alikuwa anacheka kama ishara ya mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa sana. Licha ya kuwa kwenye majonzi mazito bado aliongezewa mzigo wa mambo mazito sana kwenye kichwa chake. Aliinua uso wake na kumwangalia sana mwanamke huyo kisha akamuuliza.

“Ni jambo gani ambalo umesahau kuniambia?”
“Kuhusu ubongo wako”
“Umefanyaje”

“Wakati unafanyiwa vipimo, ubongo wako ulichukuliwa na unaendelea kutumika kuwatengena watu wenye uwezo mkubwa kama wewe” mwanaume aliitikia kwa kichwa na kuuliza;

“Kwahiyo ilipangwa baada ya kila kitu kukamilika mniue?”
“Ndiyo Tommy ila hilo ni jambo ambalo lilikuwa nje ya uwezo wangu na nimejitahidi kwa kila uwezo wangu kuweza kukulinda kwa sababu nakupenda sana ila kwa sasa hautaweza kuuawa tena kwani nchi inaamini kupitia kuvuja kwa kirusi hiki unaweza kuwa na msaada mwingine tena”

“Ni bora mje mniue ila sitaweza kuja kufanya kazi na nyie tena kwenye maisha yangu. Mimi ni Mtanzania na sio Mwingereza” aliongea kwa shida sana na hasira kali akiwa amekata tamaa Tommy
“Yes, upo sahihi lakini wewe ni memba hai wa MI6 usisahau hilo”

“Boniphace Wala wala ni nani?” maelezo ya mwanamke huyu yalimpa hasira sana akajikuta ameuliza swali kuhusu raisi wake ambaye alihusishwa na magaidi.

“Haupo sawa Tommy, nina uhakika haupo tayari kulipokea hili. Nenda halafu ukiwa sawa nitakwambia ukweli kuhusu raisi wako ili ujue kwamba mnaishi na nani nchini ila huyo raisi wako ni mtu ambaye ana kisasi kizito sana na nchi hii na huenda mipango yake mingi ya kulipa hicho kisasi anataka kuitimiza kipindi hiki cha sakata la uchaguzi ambapo utaona namna pesa inavyo tumika kuyachukua maisha ya watu wasio na hatia” mwanamke huyo aliongea na kumsukumia nje mwanaume ambaye alikuwa akimpenda sana kwani hakumuona kama alikuwa sawa kwa wakati huo na nje kulikuwa kumekucha tayari.

Tommy aliondoka kwa kujivuta, alikuwa anajuta taratibu kuweza kuzaliwa kama sio kuishi ndani ya dunia hii ambayo ukweli wake ulikuwa ni uongo wa sehemu nyingine, alikuwa ameambiwa mambo mazito sana ikiwa hata bado hajauona mwili wa mdogo wake Latifa lakini pia akiwa hajafanikiwa kumpata dada yake kipenzi Linda waweza kumuita Patrina.


Siku ilikuwa imeanza vibaya sana kwa watanzania, mambo yalikuwa yanaendelea kuwa mabaya na ya kutisha kila kulipokuwa kunakucha, asubuhi hiyo viliripotiwa vifo vingine vya hadharani maeneo ya posta ambapo kuna watu walikutwa wakiwa wamekufa vibaya sana hali ambayo ilikuwa inazidi kuleta utata kwa wananchi na kuwafanya wazidi kuingiwa na hofu kubwa sana dhidi ya mwenendo wa nchi yao.

Asubuhi hiyo hiyo wakiwa wanapokea hizo taarifa za kutisha lakini pia waliipokea taarifa nyingine ambayo iliwashangaza sana kwa mara nyingine, mhehimiwa raisi alikubali kuachia madaraka na kusema kwamba ule ungekuwa mhula wake wa mwisho kuongoza hivyo anaomba wananchi waweze kumchagua Mr Mafupa kwani binafsi yeye anahisi kwamba huyo mtu anafaa kabisa kuongoza nchi na yeye huo ulikuwa ni wakati wa kupumzika baada ya kukaa kwenye siasa muda wa kutosha.

Taarifa hizo zilikuwa ni za ghafla sana kwani mtu huyo mara ya kwanza alidaiwa kwamba ataongoza mbio hizo za kuweza kuipigania kwa mara nyingine tena hiyo nafasi yake lakini ghafla tu akawa amejitoa tena, ilikuwa ni habari ambayo ilileta mshtuko na maswali mengi sana kwa watu japo kwa bahati mbaya sana hakukuwa na mtu ambaye angeweza kuyajibu hayo maswali yao labda kama yeye mwenyewe angeamua kuyatolea ufafanuzi.

Hiyo taarifa haikuwafikia wananchi tu bali ilimfikia hata Mafupa ambaye wakati huo alikuwa ndani kwake akiwa anashangazwa na taarifa ya vifo vya vijana ambao kiuhalisia walikuwa ni vijana wake huko Posta. Namna vijana hao walivyoweza kuuawa ilimpa sana shaka mr Mafupa kwani waliuawa na mtu ambaye alionekana kuwa na uwezo mkubwa isivyo kawaida. Akiwa anaendelea kuzivuta picha za hao watu na kuzikuza kwenye simu yake ili azione kwa usahihi ndipo alipopata taarifa nyingine ya kushtua kuhusu Boniphace Walawala kukubali kuiachia nafasi hiyo na kuamua kumuachia yeye. Hakuifurahia sana hiyo taarifa bali ilimpa mashaka kiasi chake kwani ilikuwa ni ghafla sana jambo hilo kuweza kutokea na yeye hakutegemea kwamba linaweza kufikia hatua kama hiyo. Aliitoa simu yake mfukoni na kuipiga mahali ambapo alitamka kauli moja tu baada ya simu hiyo kupokelewa.
“Nakuja” alitoka humo ndani ya kuuchukua msafara wake wa magari kuelekea hiyo sehemu ambayo aliahidi kuwepo baada ya muda mchache ambao ulikuwa unafuata.

Safari yake iliishia nyumbani kwa mr Oscar ambako alikuta kuna ulinzi mkali sana tofauti na alivyokuwa amepazoea siku zote, alishangazwa sana na hilo jambo lakini hakuwa na namna zaidi ya kuingia ndani kwani mtu huyo alikuwa anamsubiria yeye tu aweze kufika ili amwelekeze jambo ambalo lilimfanya aweze kumsumbua asubuhi yote hiyo.

“Umeiona taarifa ya raisi?””
“Yes, nimeiona”
“Huyo mjinga unahisi anafanya mchezo gani labda? Maana mimi sijamuelewa”

“Lengo lako hasa wewe lilikuwa ni lipi?”
“Mimi sijali kikubwa nataka niingie Ikulu”
“Hiyo kazi ya kuongea naye si ulinipa mimi?”
“Ndiyo nakumbuka”

“Sasa mpaka sasa unajiuliza kwamba kwanini amekubali kutoka kwenye ile nafasi wakati mimi nilikuahidi kabisa kwamba nitamalizana naye mwenyewe?”
“Mhhhhhh hahahaha kumbe ni wewe ndiye umelifanikisha hili?”

“Ulihisi inawezekana mtu kukubali kuondoka Ikulu kijinga jinga namna hiyo bila kuwa na watu wenye akili kama mimi?”
“Sasa nimeiona nguvu yako, sitaki kujua ulitumia njia gani mpaka ukafanikiwa kumshawishi ila niseme asante sana kwa hili, sitalisahau kamwe”

“Mimi nimemaliza kazi yangu kwa sasa hivyo ni kazi kwako kuanza kutekeleza yale ambayo tulikubaliana”
“Usijali mheshimiwa hilo jambo nalifanyia kazi haraka sana kuanzia sasa lakini nina jambo lingine hapa ambalo limenitisha sana”

“Lipi hilo?” hakujibu bali alimrushia kiongozi huyo mstaafu simu ili aweze kuangalia kwa ukaribu sana taarifa hiyo.
“Nimeiona sema nikaipuuza nikijua ni makundi ya wahuni tu mtaani, kumbe hawa walikuwa ni watu wako?”

“Ndiyo”
“Imekuwaje hii?”

“Baada ya kufanikiwa kumteka yule binti mkubwa wa Apson Limo tulitarajia kwamba baba yake angeweka jitihada kubwa sana kuweza kumtafuta mwanae kama alivyofanya kweli lakini hakufika popote zaidi ya kuishia kupigwa risasi. Yule binti alikuwa na rafiki yake ambaye ni mpenzi wa kijana wangu ila ilikuwa ni kwa siri sana na hakuna ambaye alikuwa analijua hilo ila binti yule alikuwa akitusaidia kutupatia taarifa nyingi zaidi za ile familia huku tukiamini kwamba kama siku binti akipotea basi mshukiwa wa kwanza atakuwa ni yule rafiki yake ambaye sisi ndio tulikuwa tumemuweka pale”

“Hivyo tukawa tumewaweka watu wetu karibu ili kama kati ya watu ambao watakuwa wanamhoji akitokea hata mmoja akianza kuonyesha mashaka juu yake basi atoe taarifa kwani aliwekewa walinzi sita wa siri ambao kama taarifa ingetoka juu ya mtu ambaye alikuwa na mashaka na yule binti basi walitakiwa kumkamata na kumleta kwangu. Sasa jambo la kushangaza sana ni kwamba kijana ambaye alionyesha mashaka na binti yule ni huyo mtoto wa Apson Limo kwa taarifa ya binti hata picha zimemuonyesha yeye akiwa anaingia pale”

“Baada ya kijana yule kumhoji alionyesha kuwa na mashaka makubwa sana kiasi kwamba akaondoka pale ghafla hivyo vijana wakapewa taarifa kwamba waweze kumkamata na kumleta kwangu lakini vijana hao ndio ambao wamefanyiwa hivyo kama unavyo ona kwenye hizo picha hapo” mr Mafupa alimaliza maelezo yake akiwa anaketi chini kwani muda wote alikuwa aneongea akiwa amesimama tangu aingie humo ndani.

Ukurasa wa ishirini na sita sina la ziada.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA SABA
“Mhhhhhh huyu mtoto karudi lini? Si alikuwa nje ya nchi?”

“Kwa haya matatizo ambayo yametokea inasemekana kwamba ameingia jana usiku wa mapema”

“Nilikuonya lakini kwamba huenda anatakiwa kufuatiliwa kwa umakini”

“Yeah, huyo hanipi mimi wasiwasi ila kuna mambo ambayo nahisi yanaendelea chinichini bila hata uelewa wangu”

“Yapi hayo?”

“Nina uhakika huyu hawezi kufanya hivi ila kuna mtu atakuwa yupo nyuma yake bila uelewa wake au kuna mtu anamtumia bwana mdogo kutekeleza mambo yake” mr Mafupa alieleza akiwa anahema kiasi kwamba akaacha pumzi itoke kwenye mdomo wake ili apate nafasi ya kupumua vyema na kuendelea.
“Nakusikiliza”

“Huenda kuna watu wanazifuatilia hatua zake kisha wanatumia hiyo nafasi kufanya hayo mambo, huyu kijana nina uhakika hahusiki” mr Mafupa aliongeza akiwa ana uhakika na maneno yake

“Una uhakika gani mpaka unakuwa na jeuri ya kusema hayo?” mr Mafupa hakujibu hicho kitu bali alitoa simu nyingine na kuitafuta video moja akaisogeza jirani na mr Oscar kisha akawa ameiruhusu iweze kuanza. Kwenye video hiyo alikuwa anaonekana mwanaume mmoja akiwa anaruka ukuta kwa kasi sana kisha akatua ndani lakini kwa bahati mbaya sana sauti ilikuwa haisikiki kabisa kwenye video hiyo huenda ni kutokana na umbali wa kamera ambazo zilikuwa humo ndani mpaka eneo ambalo mhusika alikuwepo.

Waliwaua walinzi wawili kwa sekunde chache sana lakini hata wale wanaume wanne ambao walikuwa wamejificha gizani walipo jitokeza aliwafanyia mauaji ya kikatili mno isivyokuwa kawaida kitu ambacho kilimfanya mzee huyo kusisimka sana kwa hayo ambayo alikuwa anayaona mpaka alivua miwani yake usoni.

“Kama angekuwa ni yeye unahisi angejigawa vipi maana hayo matukio yametokea kwa kupishna muda mchache sana maana yake huenda kuna watu zaidi ya mmoja ambao walikuwa wanaifuatilia hii ishu kwa ukaribu sana ndiyo maana baada ya kuwa na taarifa za kutosha wakawa wamejigawa kwenye haya majukumu lakini hata hivyo nao pia walikuwa wanamtaka binti wa Apson Limo hivyo huenda nao wana dhamira ya kuweza kutekeleza jambo fulani kama sisi tulivyokuwa tunahitaji” hayo maelezo ndiyo ambayo yalimfanya mr Mafupa agome kabisa kwamba hakuwa Tommy ambaye alihusika na hilo jambo ambalo lilikuwa limetokea.

“Wewe una maadui wangapi kwenye maisha yako?” swali hilo lilimshtua mr Mafupa

“Sijajua bado, unajua kwenye siasa yanatokea mambo mengi sana na sisi wanasiasa kuna muda tunafanya mambo mengi sana ya kawaida na ya kutisha isivyo kawaida kwahiyo kuna muda unaweza ukawa unayafanya mambo ukawa unahisi kwamba upo sahihi kumbe kuna watu yanawaumiza na kuwakera sana hivyo unajikuta unakuwa kwenye kundi kubwa sana la watu ambao hawakupendi. Kwa mimi nahisi huyu anayefanya hivi huenda anataka kutafuta sehemu ya kuanza kuniangusha au kuna kitu anakihitaji kutoka kwenye ile familia hivyo nitatakiwa kumpata haraka sana na lazima nihakikishe kwamba anaingia kwenye mkono wangu”
“Unataka kumjua? Kwa njia ipi labda?”

“Nina kijana wangu mmoja ambaye amehifadhiwa pale Segerea baada ya kuhusika na mauaji ya watu kumi ndani ya usiku mmoja. Kesi yake iliwahi kuwa mahakani nikamsihi hakimu aweze kumpa hukumu ya kunyongwa ili kuzima kelele hivyo watu walijua kwamba amenyongwa lakini nisingeweza kuruhusu kijana wangu wa mhimu namna ile aweze kufa kizembe wakati nina kazi kubwa sana mbele yangu kwa sasa hivyo huyo namtoa ili awatafute hawa watu huku mimi nikiwa naendelea na siasa” mr Oscar alisikitika sana

“Unajua mr Mfupa mimi sitaweza kukulinda kila sehemu maana unaonekana kwamba unachukulia mambo kawaida sana kuliko nilivyokuwa nafikiria mwanzo. Unawaza sehemu ndogo sana kwa kujitungia maelezo yako ambayo unaona yanakifurahisha kichwa chako hali ambayo inanifanya niwe na wasiwasi sana na wewe hata huko Ikulu ambako unadai unaenda kama ukifanikiwa kufika basi jiangalie sana kwani unaweza ukajikuta unakuwa raisi ambaye ameongoza kwa miaka michache zaidi kwenye historia ya nchi hii” mr Mafupa alitabasamu baada ya kusikia hayo, alinyanyuka na kumgusa mzee huyo begani.

“Mheshimiwa wewe nafasi yako kubwa umeitumia vizuri sana kuweza kumalizana na mheshimiwa raisi, huku kunako bakia niachie mimi nitajua namna ya kumaliza na uwe na amani kabisa kwa sasa ni muda wako wa kwenda kuyafurahia maisha na kuishi utakavyo ndani ya nchi hii huku biashara zako zote zikirudi kwenye mikono yako kwa mara nyingine tena” aliongea akiwa anainama kutoa heshima kwa huyo waziri mkuu mstaafu kisha akatoweka humo ndani kama hakuwepo vile.

SEGEREA
Ndani ya gereza kubwa hilo linalopatikana ndani ya jiji la Dar es salaam, kulikuwa na mfungwa mmoja ambaye alikuwa anaogopeka sana ambaye jina lake alikuwa akijulikana kama Pablo Mkinga. Jina ambalo alilifurahia sana kwani lilikuwa linaendana na muasisi na muuzaji mkubwa wa madawa ya kulevya kutoka huko Colombia ambaye alijulikana kama Pablo Escobar. Mwanaume huyo alikuwa amepelekwa huko baada ya kuhusika na mauaji ya watu kumi ndani ya usiku mmoja ambapo alimuua afisa wa jeshi la polisi na familia yake nzima.

Afisa huyo wa jeshi la polisi alikuwa ni mtu mwadilifu sana kwenye kazi yake hivyo alikuwa anajitoa sana kuweza kuipigania kofia ambayo ilikuwa kichwani kwake lakini hakuishia hapo tu aliamini kwenye kuipeperusha bendera ya nchi yake kwa namna inayo faa akiamini kwake hiyo ndiyo zawadi kubwa zaidi ambayo alipaswa kuipigania ili kuhakikisha taifa lake linakuwa salama hususani kwa ajili ya kizazi ambacho kilikuwa kinakuja.

Afisa huyo akiwa kwenye hicho kitengo chenye hadhi ya kipolisi alikuwa akiogopwa sana hasa na wahalifu kwani hakuwaacha salama pale ambapo waliingia kwenye mifumo yake kwa sababu hakuwa mtu wa kupenda rushwa kabisa kwenye maisha yake. Kwenye kazi yake ambayo alikuwa akiifanya alifanikiwa kugundua michezo ambayo ilikuwa inafanywa na mwanasiasa Mr Mafupa ambayo ilikuwa ni utakatishaji wa fedha lakini pia kujihusisha na biashara zisizo za halali kitu ambacho kilimpelekea kulivalia njuga swala hilo ili aweze kulifuatilia kwa ukaribu sana kiasi kwamba akawa amedhamiria kumpoteza huyo mheshimiwa kama angepata ushahidi kamili wa kuweza kufanya hivyo.

Ufuatiliaji wake ulimpelekea sehemu mbaya sana kwani alionywa na tajiri huyo kwamba afuate yale mambo ambayo yanamhusu aachane na hayo mambo lakini hakuweza kuelewa akaweka msimamo wake kwamba kama kiongozi huyo ni fisadi na anaiingiza nchi yake kwenye hiyo hatari basi ni lazima amuumbue na watu waweze kuujua udhalimu wake. Hiyo misismamo yake ndiyo ambayo ilipelekea familia yake yote kuuawa na mwanaume mmoja ambaye alidaiwa kwamba aliwahi kuwa komando jeshini baadae akaja kutoweke jeshini kwenye mazingira ambayo haikueleweka kama alitoroka au alifukuzwa. Mwanaume huyo baada ya kukamilisha mauaji hayo alikamatwa na jeshi la polisi na kupelekewa mahakamani ambapo hakimu baada ya ushahidi kukamilika alitoa hukumu ya kunyongwa kwa mtu huyo ikiwa ni kama shinikizo kutoka kwa mr Mafupa hivyo mwanaume huyo akaenda kuhifadhiwa Segerea badala ya kunyongwa.

Huko gerezani alikuwa akiogopwa sana baada ya kuua watu watano tangu aingie wawili akiwa amewaulia ulingoni kwenye mapigano ambayo baadhi ya maaskari walikuwa wanayaandaa ka siri ili waweze kupata burudani huko na kuchezea kamali. Hali hiyo ilifanya mwanaume huyo aogopwe isivyo kawaida na kumfanya aishi kama vile yupo uraiani tu maana hata polisi walikuwa wakimuogopa isivyo kawaida kwa historia yake na mambo ambayo alikuwa ameyafanya ya kuwavunja miguu askari wawili huko nyuma.

Mida ya saa tatu asubuhi akiwa kwenye chumba chake anaangalia televisheni na baadhi ya vijana ambao aliwachagua kuwa kama wafuasi wake alikuja kuitwa na askari na kuambiwa kwamba kuna mtu ambaye alikuwa anahitaji kumuona lakini alitakiwa kusafishwa kwanza kisha avalishwe nguo nzuri ndipo aweze kwenda kukutana na mtu huyo. Alitabasamu sana kusikia hilo jambo kwani alijua moja kwa moja ni bosi wake ndiye ambaye alikuwa anafanya mipango yote hiyo kitu ambacho kilimuwezesha yeye kuweza kutoka hapo gerezani kama palikuwa ni getoni kwake.

Alioga na kunyolewa nywele zake vizuri kisha akapewa suti ya gharama na kuingia kwenye gari ambayo ilikuwa imekuja kumfuata hapo ndani, akaondoka kama ni mheshimiwa ambaye alikuja kufanya ukaguzi wa wafungwa ndani ya eneo hilo. Safari yake iliishia bahari beach pembezoni mwa bahari ambapo alimkuta bosi wake akiwa amezungukwa na walinzi kwenye meza kubwa sehemu ambayo ilikuwa na upepo wa kutosha.

“Vipi hali ya huko ndani?”

“Kule hakuna shida kiongozi, nakushukuru sana kwa kunikumbuka”

“Wewe ni kijana wangu hivyo ni lazima nikukumbuke nyakati zote. Kuna kazi ambayo unatakiwa kuifanya haraka sana na uniletee huyo mtu au hao watu ambao wanaaanza kunifuatilia” aliongea huku akiwa anamrushia simu ambayo ilikuwa na picha za vijana waliokuwa wameuawa na mwisho wake kukiwa na video ambayo ilikuwa inaonyesha namna mwanaume huyo alivyo fanikiwa kuwaua watu wake huko Mikocheni kwenye safe house yake.

“Naanzaia wapi kiongozi?”

“Utakutana na Sasha atakupa sehemu ya kuanzia kwa sasa nitakuwa busy kidogo hivyo sitataka usumbufu wa kunipa habari mbaya maana haitakuwa njema sana kwangu hivyo nategemea kuzipata taarifa nzuri sana kutoka kwako”
“Sawa kiongozi” aliinamana kutoa heshima kwa kiongozi wake huku mtu huyo akiwa ananyanyuka na kutoweka hilo eneo majukumu akiwa ameyaacha mikononi mwa kijana wake aliyekuwa akimuamini isivyo kawaida.

Tommy asubuhi ilikuwa mbaya sana kwa upande wake, baada ya kutoka kwa Harper hakuweza kwenda nyumbani bali aliendesha gari kwa kasi na kwenda kusimama nalo ufukweni. Kichwa chake kilikuwa kama kinahitaji kupasuka kwani hakuelewa kwamba angeanza na jambo lipi lakini pia angemaliza na jambo lipi bado akili haikuwa ikimpa kabisa akawa anajihisi kuchanganyikiwa. Dada yake hakuwepo, mdogo wake alikuwa amepotezeshwa maisha yake na mpaka wakati huo hakuwa ameuona hata mwili wake, baba yake alikuwa anayapambania maisha yake kitandani lakini hata mama yake alikuwa hospitalini ambapo asubuhi hiyo ndiyo alikuwa anatarajia kuweza kurudishwa nyumbani.

Ukiacha yote hayo bado alizipata taarifa za kutisha sana kuhusu mambo ambayo alikuwa ameyafanya akiwa huko Uingereza ambapo alitengeneza kirusi hatari sana ambacho kiliishia kwenye mikono ya magaidi na kitu cha kushangaza ni kwamba raisi wa nchi ya Tanzania ndiye ambaye alidaiwa kukihifadhi na kumsaidai moja ya magaidi ambao walikuwa wanaishi nchini. Hali nyingine ambayo ilizidi kumpa utata ni baada ya kujua kwamba watu hao walikuwa wamepanga kumuua baada ya yeye kumaliza kazi hiyo kwani alisajiliwa kama jasusi wa MI6 na yeye baada ya kumaliza kazi yake alidhani ndiyo ungekuwa mwisho wake wa yeye kukaa huko lakini kitu cha ajabu Harper alimwambia kwamba akumbuke kuwa siku zote yeye ni MI6 hata afanyaje.

Hata mimi nina maswali mengi sana kama wewe ila niseme naishia hapa kwenye ukurasa wa ishirini na saba.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
BADO NINAISHI.

Inamhusu mwanaume mmoja ambaye alikuwa ni kiongozi wa genge la kihalifu ambalo lilikuwa linaitwa SARAFU KUMI NA TANO.

Mwanaume huyo alikuwa anasakamwa na mamlaka za usalama ndani ya taifa la TANZANIA kwa miaka kumi bila mafanikio. Ndipo alitumika mwanamke mrembo ANELIA BATON ambaye alimwingiza mwanaume huyo kwenye HONEY TRAP kwa kupitia kikosi hatari kutoka ndani ya shirika la kijasusi kiitwacho HOLY TRINITY, walifanikiwa kumpata mwanaume huyo.


Alihukumiwa kifungo cha miaka sitini gerezani na baada ya hapo angenyongwa. Alipelekwa ndani ya gereza hatari la DOMINIC, huko alikutana na tajiri mmoja ambaye alikuwa amejificha ili kuyalinda maisha ya mwanae ambaye alitekwa.

Tajiri huyo alikutana na mwanaume huyo aliye itwa REMMY CLAUDE na kumuomba akamuokoe mwanae yeye anyemsaidia kumtorosha gerezani. Walifikia makubaliano mwanaume akatoroshwa gerezani.


Huko uraiani alienda kumtafuta mtoto wa kiongozi huyo lakini wakati anafanikisha hilo tajiri huyo alikuja kupata habari kwamba mfungwa huyo aliye Mtorosha gerezani hakufungwa kwa bahati mbaya bali ilikuwa ni mipango yake yeye ili akutane na tajiri huyo.

Alishangaa sana ilikuwaje mtu ajitoe kafara kufungwa gerezani kwa sababu yake? Ndipo akaja kugundua kwamba Remmy alikuwa anautafuta umoja wa watu ambao hawakuwa wakifahamika na tajiri huyo ndiye mtu pekee ambaye angemsaidia kuwajua wote ndani ya umoja huo.

Anakuja kushtuka akiwa amechelewa, mwanaume huyo alikuwa amempata mwanae tayari na kupotea naye hali ambayo ilileta maafa makubwa sana na kulilazimu shirika la kijasusi kuanza na moja kumtafuta.


SARAFU KUMI NA TANO halikuwa pambo bali ilikuwa idadi ya wanafamilia ambao waliuawa kikatili takribani miaka ishirini iliyokuwa imepita ila kwa bahati mbaya mtu mmoja alifanikiwa kuishi.

Sitaki nikumalizie uhondo. Unataka kujua huyo Remy ni nani? Kwanini alijitoa sadaka kwenda gerezani? Huo umoja una nini hasa ndani yake na unaongozwa na nani?

Nini hatima ya maisha ya Remy Claude?

Hili ni moja kati ya andiko ambalo litakufanya ujivunie sana kuyasoma maandishi.

Sasa RASMI IMEACHIWA NA UNAWEZA KUIPATA KWA PESA ZA KITANZANIA SHILINGI 5000 TU.

5000 yako unapewa andiko lote mpaka mwisho.

Unaweza kufanya malipo kwa namba hizi hapa [emoji116]

0621567672.... HALO-PESA

0745982347..... M-PESA

0714581046..... TIGO-PESA

Zote jina FEBIANI BABUYA.

Ni wakati sasa..... KARIBU INBOX.


ASHRAFU NDILO JINA LANGU
FB_IMG_1707902862253.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA NANE
Alijikuta akiwa na hasira sana, aliishia kuupiga usukani kwa hasira mno akiwa hata hajui mwelekeo wa maisha yake ulikuwa unaenda wapi.
“Lazima nizuie kila kinacho endelea na hawa walio nigusia familia yangu, naapa nitawafanya kitu ambacho hata hii nchi haitakuja kukisahau kwenye historia yake” aliongea kwa hasira akiwa anatoka nje ya gari hiyo na kufungua buti ambapo alitoa begi ambalo lilikuwa na nguo mpya, alivua zile ambazo alikuwa nazo kwenye kazi usiku kisha akavaa nguo hizo na kutoweka hilo eneo akiwa anaelekea hospitali kuianza siku yake ya kwanza akiwa ndani ya ardhi ya Tanzania, siku ambayo aliamini kwa namna yoyote ile kwamba itakuwa ngumu sana isivyo kawaida.

Safari yake iliishia Aghakhan ambako alilazwa mama yake, mama huyo alimhitaji mwanae ampe taarifa kama amempata dada yake lakini mwanaume aligoma kabisa na kumsihi mama aende kwanza nyumbani maana wanae wengine walikuwa wakimngoja sana kisha yeye angerudi baadae ili kumpa maelekezo yote. Hivyo akahakikisha mama yake ameingia kwenye gari akiwa na msafara wa walinzi ndipo naye akaelekea hospitali ya mhimbili ambako alilazwa baba yake mzazi lakini ndiko pia ambako ulikuwepo mwili wa mdogo wake ambao haukuwa hata na kichwa kwa sababu watu ambao walikuwa wamehusika kumteka binti huyo waliurudisha mwili mtupu usio na kichwa hivyo kazi ilikuwa kwa familia kama wangeweza kukipata kichwa.

Mwanaume baada ya kufika hospitalini hapo kwenye wodi za VIP huku wodi ya baba yake ikiwa na ulinzi wa kutosha, alinyoosha mpaka ndani ambapo alienda kukaa karibu na dirisha huku akiwa anamwangalia baba yake pale alipokuwa amelala. Alimuonea huruma sana mzee huyo kwani alikuwa mtu mwema sana na hakustahili kabisa kuweza kufanyiwa mambo kama hayo lakini hakuwa na chaguo kwani wanadamu walikuwa wameamua yeye aishie hapo.

Kumbukumbu zake zilimpelekea mbali sana tangu siku ambayo alikuwa anaondoka nchini kwenda kusoma huko Uingereza namna familia ilivyo muaga kwa furaha sana hususani huyo baba yake ambaye alikuwa kama pacha kwake. Mzee huyo alikuwa akimsisitiza mwanae kwamba hata siku ikitokea hayupo basi yeye anatakiwa kujijua kwamba ndiye msimamizi wa hiyo familia na anatakiwa kuiendesha kwenye misingi ambayo inahitajika na kuhakikisha familia ipo salama kabisa.

Ahadi hiyo ambayo aliitoa mbele ya baba yake ni kama ilikuwa imemshinda na inaendelea kumshinda kwani madhara yalikuwa yameanza kujitokeza ikiwa yeye hajafanya jambo lolote la maana kuweza kuilinda familia ambayo tayari ilikuwa ipo upande ambao ulikuwa mbaya sana. Alitumia saa zima akiwa amekaa na kumwangalia baba yake ambaye bado aliendelea kuipigania afya yake kitandani. Baada ya saa moja kupita aliamua kutoka humo ndani na kumfuata daktari huku akiwa anatokwa na jasho jingi sana usoni akionekana wazi mwili wake ulikuwa unatetemeka.

Lengo la kumuona daktari ni kwamba alipaswa kwenda kuuona mwili wa mdogo wake Latifa ambao ulikuwa upo Mochwari, mwili ambao haukuwa hata na kichwa hivyo alikuwa akiogopa sana Tommy. Baada ya daktari ambaye umri wake ulikuwa unaelekeana na baba yake kumuona, alimsikitikia sana kijana huyo ambaye alikuwa mbele yake kwa namna alivyokuwa na wasiwasi. Alipelekwa mpaka ndani ya hicho chumba cha kuhifadhia maiti, alimtaka daktari huyo aondoke baada ya kumuonyesha jokofu ambalo ulihifadhiwa mwili wa Latifa.

Aliliangalia kwa dakika kumi akiwa anatetemeka maana alikuwa analiogopa hata kulisogelea. Alisogea taratibu jasho likizidi kumtoka kwa kasi japo humo ndani kulikuwa na baridi kali sana. Alilifungua taratibu akiwa ameyafumba macho yake kwani hakuwa tayari kabisa kuweza kushuhudia kile ambacho angekiona. Baada ya kufumbua macho yake alikutana na kiwili wili cha kipenzi chake Latifa kikiwa bila kichwa na alikiona kwa macho yake tofauti na zile hadithi ambazo alikuwa anasimuliwa na watu wengine.

Mwanaume alikuwa amejikaza sana kwa muda mrefu ila chozi lilianza kumshuka mdogo mdogo kwenye mashavu yake, alihisi dunia haikuwa ikimfanyia sawa yeye hata kama mpango wa Mungu ni kwamba kila mtu angekufa lakini sio kwa namna kama hiyo ambayo mdogo wake alikuwa amekufa, hiyo ilikuwa ni njia mbaya sana. Tommy alilia kwa kupiga makelele humo ndani kiasi kwamba yule daktari ambaye alikuwa amempeleka akiwa nje alisikia kilio hicho, alijikuta mpaka chozi linamtoka huenda naye alisikia uchungu sana kwa sababu alikuwa ni mzazi hivyo kuona kitu kama hicho kwa mwenzake asingechukulia poa kwani huenda siku moja naye pia kingeweza kumpata kitu hicho.

Tommy alitumia saa zima akiwa karibu na mwili wa mdogo wake, alikuwa anahisi kama mdogo wake alikuwa akimhitaji hivyo kuondoka hapo angemuacha mpweke pekeyake akaamua kukaa naye kidogo angalau mdogo wake aendelee kumuona bila shaka. Hata hivyo hakuwa na namna ilikuwa ni lazima aondoke hilo eneo. Wakati anatoka hapo macho yake yalikuwa mekundu sana.

“Naomba ripoti ya uchunguzi wa kifo cha mdogo wangu haraka sana” aliongea akiwa amemkazia macho sana daktari huyo ambaye hakuwa na tatizo, waliongozana mpaka ofisini kwake akampatia mwanaume huyo hiyo ripoti hata hivyo Tommy hakuisoma ripoti hiyo bali alitoka humo ndani na kuelekea nyumbani kwa IGP ambaye alikuwa na familia yake.

Mzee huyo akiwa ndani kwake na familia yake alisikia makelele getini na baada ya kwenda alikuta walinzi wawili wamevunjwa mikono huku mbele yake akiwa amesimama Tommy.
“Jitahidi sana, hakikisha hisia hazikitawali kichwa chako maana unaweza ukakuta unajiongezea matatizo. Nakuvumilia kwa sababu baba yako amewahi kunisaidia sana” IGP aliongea akiwa anatembea taratibu kuelekea eneo ambalo lingefaa kwa ajili ya mazungumzo hivyo Tommy hakuwa na namna zaidi ya kumfuata mzee huyo hilo eneo.
“Unaweza ukaniambia kwamba ni kipi kimekuleta kwangu asubuhi hii na unahitaji nini labda?” swali lake lilimfanya Tommy amwangalie kwa macho yenye maswali mengi sana.

“Naona una familia yenye furaha sana na hauna wasiwasi wowote kwa sababu una uhakika wa kila kitu mpaka sasa lakini mimi hapa unaniona kama nakuwa msumbufu kwa sababu familia yangu ipo sehemu mbaya sana. Sishangai kwa sababu ni kawaida yenu nyie mkivaa mavazi yenu huwa mnajisifia kwamba mnawalinda wananchi lakini kiuhalisia ni kwamba huwa mnayalinda matumbo yenu tu labda na familia zenu”
“Una maanisha nini bwana mdogo?”
“Nikiwa na umri mdogo niliishi maisha ya furaha sana nyumbani, nilikuwa naiona ile furaha ya familia ambayo imeandikwa hata kwenye vitabu vya dini hivyo ilinifanya nijivunie sana kuzaliwa kwenye ile familia yangu. Kupata familia ni swala lingine na kupata familia yenye furaha ya kutosha ni swala jingine pia lakini mzee wangu alibahatika kupata vyote na ndiyo sababu akawa mtu mwenye mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake”

“Kitu cha kushangaza ni kama ndani ya siku moja tu watu wameamua kuizima ile furaha ya familia ghafla na kufanya mzee yule ajutie kuzaliwa hapa duniani kwa sababu ameshindwa kutoa ulinzi kwa familia ambayo anaipenda sana na yeye mwenyewe bado anaendelea kuipigania afya yake. Hilo tunaweza kusema kwamba ni jukumu lake kama mwanaume kuzivaa changamoto lakini vipi kuhusu mdogo wangu? Ana hatia gani yule maskini? Umri kama ule ambao mimi nilikuwa na furaha sana yeye umri ule ule amepoteza maisha tena kwa amri za watu fulani ambao wamekaa tu mahali wanaifurahia dunia na mambo yake ambayo yanendelea halafu unaniuliza nimekuja kutafuta nini hapa kwako asubuhi hii kamanda?”

“Najua unajiamini sana kwa sababu unajua unaweza ukatoa amri nikakamatwa, unahisi unaweza kunifunga au kunifanya lolote wakati wowote ambao utahitaji wewe na ndiyo maana unanitishia na maneno yako hayo ila nimekuja hapa kwa swali moja tu ambalo nayahitaji majibu yake” mwanaume aliongea huku akiwa anaitua bahasha kubwa kwenye meza hiyo ambayo alikuwa amekaa na IGP.

“Hii bahasha ndani yake kuna ripoti ya kifo cha mdogo wangu, kifo chake ni wazi aliuawa na watu na hilo linajulikana kila sehemu ya nchi na nyie ndio ambao mliahidi kwamba mtafanya uchunguzi na kutoa ripoti ikiwa ni kusaidia mtuhumiwa mwenyewe kuweza kukamatwa. Sasa swali langu ni kwamba ripoti yenu ya kazi iko wapi na mmefikia wapi kwenye huo uchunguzi wenu?” hilo ndilo swali pekee ambalo lilikuwa limempeleka kwa IGP asubuhi hiyo. IGP alipiga miayo kwanza akionekana bado hakuwa ameipata hata chai ya asubuhi.

“Naelewa vizuri hali uliyo nayo kwa sasa, najua haupo kwenye utimamu wako kwa sababu unaongozwa na hasira, hata mimi nimewahi kumpoteza mwanangu pia hivyo naelewa vizuri namna invyokuwa ila hakikisha hasira zako hazikuendeshi kiasi kwamba ukaanza kumbebesha lawama kila mtu. Uchunguzi mpaka sasa unaendelea kiasi kwamba ukiwa tayari nyie kama familia mtajulishwa ripoti mtapewa lakini kila ambaye amehusika na hili pia sheria lazima itachukua mkondo wake kuweza kuhakikisha analipa sawa sawa na aliyo yafanya”

“Mbona unanijibu kiwepesi sana mzee, una uhakika mnajua kazi yenu inapaswa kufanywa vipi au mnafanya fanya tu ilimradi muonekane mnaifanya?”
“Bwana mdogo nadhani unaanza kunikosea heshima sasa, angalia sana usije ukavuka mipaka”
“Nikivuka mpaka utafanya nini?”
“Usinilazimishe nikakufanyia kitu kibaya wakati upo kwenye hiyo hali”
“Kwahiyo unanitisha kwa sababu wewe ni IGP?”
“Usiongee na mimi kama unaongea na polisi ambaye yupo mafunzoni, unapaswa kuongea na mimi kwa heshima sana kwanza naomba uondoke nyumbani kwangu kabla sijafanya maamuzi magumu ya kukufanya ukalale selo”

“Mhhhh mzee hii kauli yako nitaihifadhi kwa ajili ya siku nyingine. Naona kiongozi mkuu wa jeshi la polisi anamtisha mwananchi wake ambaye amekuja kudai haki yake kwahiyo inamaanisha kwamba na wewe ni wale wale. Leo sijaja kwa ajili ya hili ambalo unataka kulianzisha hapa ila niamini mimi nitakurudia tena ili tuongee kiume tuone kama hiyo furaha itaendelea kuwepo kwenye familia yako” Tommy aliongea akiwa ananyanyuka na kuichukua bahasha yake maana mazungumzo yao yaliharibika na hayakwenda kama walivyokuwa wamepanga iwe lakini alisimama baada ya kumuona mzee huyo akiwa amemnyooshea bastola, alisikitika sana.

“We mtoto hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kunitisha mimi popote pale halafu wewe unakuja nyumbani kwangu na kuanza kunitishia kuhusu familia yangu? Ninaweza kukuua na hakuna ambaye atafanya lolote hivyo jiangalie sana” Tommy alimwangalia mzee huyo kwa umakini sana macho yake yakiwa mekundu, alimsogelea mpaka karibu na mkono wake ambao ulikuwa na silaha mkononi kisha akamwambia;

“Usije ukafanya hili kosa ambalo unataka kulifanya kwa kuingia kwenye huu mtego mzee utajutia maisha yako yote mpaka siku unakufa. Nadhani ndiyo maana hata vijana wako hawawezi kufanya kazi kwa sababu ya rushwa ambayo imetawala kuanzia kwenye kichwa chako inasambaa na kwao lakini kwa hili unataka kujiingiza sehemu mbaya sana. Kaa pembeni kwenye hili jambo la familia yangu maana najua hauna la kufanya zaidi ya kupiga dana dana ambazo unanitisha nazo hapa. Hili jambo nitalifuatilia mimi mwenyewe na sihitaji msaada wenu ila tu sitaki mje muingie kwenye njia yangu maana nitawaua” mwnaume aliongea kwa msisitizo sana kisha akaondoka. Maneno yake ni kitu ambacho kilimuacha kiongozi huyo wa jeshi la polisi kwenye mshangao ambao ulimfanya kuduwaa kwa muda kwani hakuwa akiamini kile ambacho kilikuwa kinaendelea.

Ukurasa wa ishirini na nane naachia kalamu hapa, tukutane tena wakati ujao.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA ISHIRINI NA TISA
Alishangazwa mno na kijana kama huyo kuja kwake na kuanza kumtishia tena akidai kwamba alikuwa anaifuatilia kesi kama hiyo mwenyewe bila kuingiliwa na polisi baada ya kuona polisi hakuna la maana ambalo wangelifanya zaidi ya kupiga danadana kama ambazo alikuwa anapigwa hapo.
“Huyu mtoto ana nini hasa ambacho kinampa kiburi sana namna hii kiasi kwamba anakuwa na ujasiri wa kuongea na mimi kama anaongea na vijana wenzake huko mtaani?” IGP alijiuliza swali ambalo hakuwa na majibu yake zaidi ya majibu ambayo angeyakisia tu na yasingekuwa sahihi hata kidogo.

Tommy alirudi mpaka nyumbani huku nyumba ikiwa imepoa sana, walikuwa wanaonekana tu walinzi wakiwa wanazunguka kila pande ya nyumba hiyo kuhakikisha usalama, aliwaangalia sana kwa umakini walinzi hao na alikuwa ameanza kupoteza imani nao kwa kiwango kikubwa sana. Taarifa ambayo aliipata kuhusu mlinzi mkuu wa baba yake ndiyo ambayo ilimfanya aanze kupoteza imani kwani alihisi kwamba mtu huyo atakuwa amemuuza mzee huyo japo hakuwa na uhakika wa moja kwa moja kama jambo hilo lilikuwa limefanyika kweli.

Baada ya kuangalia kila pande ya jumba hilo aliingia ndani ambapo alimkuta mama yake akiwa na wanae wawili sebuleni, mama huyo alikuwa jasiri sana hivyo alikuwa akiwasimulia hadithi wanae hao wawili kike ambao ndio walikuwa hapo sebuleni ili kuwapa faraja kwenye hicho kipindi kigumu ambacho walikuwa wanapitia. Tommy alikuwa ameegamia ukuta akiwa anasikiliza hadithi hiyo ambayo mama yao alikuwa akiwasimulia wanae hao, ilimkumbusha sana maisha ya nyuma kwani ilikuwa kila siku usiku anapotaka kulala akiwa mdogo mama yake alikuwa akimsimulia hadithi nzuri sana ambazo zilikuwa zinamsaidia kulala usingizi mzuri sana. Ni kweli licha ya kuwa asubuhi watoto wake hao walilala baada ya kulia kwa muda mrefu sana.

“Ukiwa mdogo baba yako alikuwa ni mtu mwenye furaha sana kupata mtoto wa kiume, na alipogundua kwamba ulikuwa unafanana naye sana nadhani alikuwa ndiye mwanaume mwenye furaha zaidi kuwahi kuzaliwa duniani. Wanaume wengi huwa wanakuwa na furaha sana pale ambapo anapata mtoto wa kiume kama yeye halafu huyo mtoto anakuwa anafanana naye, yaani furaha yake huwezi ukaifananisha na kitu chochote kile na ndivyo ilivyokuwa kwa baba yako mzazi. Alikuwa mwanaume ambaye kuzaliwa kwako kulimbadilishia vitu vingi sana akaendelea kupambana kwa nguvu sana mpaka tulipo fikia hii leo kwenye mafanikio haya makubwa sana” mama huyo aliongea akiwa anawalaza vyema wanae hao kwenye makochi hapo sebuleni na wakati huo hali yake ilikuwa imetengamaa.

“Mama umejuaje kwamba nipo hapa?” Tommy alishangaa sana mama yake anaongea naye wakati hakuwa hata amegeuka na aliingia ghafla humo ndani.
“Wewe ni mwanangu ambaye nimekuzaa na kukukuza kwenye mikono yangu, nakujua kuliko mtu yeyote yule hapa duniani. Hata kama ningekuwa kipofu ukipita karibu na nilipo nakujua kwamba wewe ni mwanangu. Mama anaweza kukosea kila kitu duniani ila hawezi kukosea kitu chochote kuhusu mwanae wa kumzaa. Wakati unaingia hapa harufu ya jasho tu imenifanya nijue kwamba ni wewe umefika hapa mwanangu ila moyo wako unaenda kasi sana unaweza ukanipa sababu?” mama huyo aliongea akiwa anaweka maji kwenye bilauri na kumpatia mwanae huyo ambaye aliishia kumwangalia kwa umakini sana huku akiwa anamshika kwenye mkono wake ila mama huyo alishtuka sana baada ya kuishika mikono ya mtoto wake.
“Wewe ni nani?” ni swali ambalo lilimshtua sana Tommy kiasi kwamba alibaki ameduwaa sana asielewe mama yake alikuwa anamaanisha nini kuuliza hilo swali.
“Mama!” aliita kwa mshangao akiwa haamini kama hayo maneno yalimtoka mama yake, alihisi huenda mama yake amepata tatizo la akili lakini haikuwa kweli maana alikuwa anaongea vitu vikubwa ambavyo mwenye matatizo ya akili asingeweza kuongea. Mama huyo alimshika mkono na kupandisha naye mpaka ghorofa ya juu kisha akamkazia macho mwanae
“Wewe ni nani?”
“Mama una uhakika upo sawa?”
“Mimi niko sawa, mimi ndiye niliye mzaa huyu mtoto ambaye yupo mbele yangu na mimi ndiye ninaye mjua sana tangu anazaliwa ila kwa sasa sina hata ujasiri wa kusema namjua mwanangu mwenyewe ambaye nilimbebea kwenye tumbo langu. Thomasi umezaliwa ukiwa mlaini sana mwanangu hata nyama zako na mifupa yako vilikuwa vilaini sana lakini kwa sasa mwili wako ni tofauti sana na ninavyokujua, najua wewe sio yule mwanangu ambaye nilikuwa namuaga siku ile anaondoka uwanja wa ndege. Sasa naomba uniambie wewe ni nani hasa labda kwa upande ambao mimi sikujui?” Tommy aliamini kwamba mtoto kwa mama hajawahi kukua hata siku moja, licha ya kuishi kwenye kificho ambacho aliamini kwamba ingekuwa siri yake lakini kwa kushikwa tu mama yake aliweza kugundua kwamba mwanae alikuwa tofauti sana na namna yeye alivyokuwa akimjua.

Tommy alishindwa hata cha kumjibu mama yake aliishia kupiga magoti mbele ya mama yake mzazi kwani asingeweza kumdanganya kwenye maisha yake kwa sababu hata kama angedanganya bado ma huma huyo angejua tu maana alikuwa anamjau mwanae huyo asipokuwa sawa, akiwa mwenye huzuni sana, akiwa anaumwa hata asipo ongea yeye pekee akimwangalia tu alikuwa anaweza kujua kwamba mwanae alikuwa ana shida gani sasa angeanzia wapi kumdanganya?

“Naomba unisamehe mama yangu, mimi sikupenda uweze kujua kuhusu hili ila sina namna” maneno yake yalimfanya mama huyo aanze kushusha machozi taratibu kwenye uso wake, mambo ambayo alikuwa anatarajia kuyasikia hapo ni yale ambayo hata maskio yake hayakuwa tayari kabisa kuyapokea.

“Ni nani amekuingiza huko?” mama alikuwa anauliza huku akiwa amesimama dirishani anaangalia nje mwanae akiwa bado amepiga magoti.
“Sio Tanzania mama” hiyo ndiyo kauli ambayo ilimfanya mama huyo ageuke maana hakuiamini kabisa
“Unamaanisha nini?”
“Ni nchini Uingereza” mama huyo hata nguvu zilimuishia kabisa hakuwa na cha kufanya tena kwa wakati huo. Jambo ambalo lilikuwa linamtisha ni baada ya kuona mabadiliko kwenye mwili wa mwanae hivyo alihisi kwamba huenda mwanae ni usalama wa taifa na anaishi kwa siri sana lakini jambo ambalo aliambiwa lilimtisha zaidi huenda ingekuwa ni bora angekuwa ndani ya idara ya usalama wa taifa ndani ya taifa lake lakini jibu la mwanae kumwambia kwamba alikuwa Uingereza lilimtisha sana kwani alijua kama ni hivyo watu hao wangeweza kuja siku yoyote kumchukua mwanae na kwenda naye mbali kama sio kuweza kumuua.

“Kwanini Thomas, kwanini mwanangu?” mama huyo yeye hakuwa akilifupisha jina la mwanae bali alikuwa analiita lote kama lilivyo.

“Hii ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuhakikisha nyie na nchi kwaujumla mnakuwa salama maana kama ningekataa kuwa hivi basi yangetokea matatizo makubwa sana” baada ya hiyo kauli yake mama huyo hakuongea kitu alianza kutoka humo ndani na kuelekea jikoni ambako hata Tommy alimfuata.
“Mama wewe umewezaje kuhusu hili?” mama huyo alimwangalia mwanae na kutabasamu akiwa anaendelea kuandaa andaa vitu ili kumpikia mtoto wake kwani ulikuwa umepita muda mrefu sana akiwa hajala chakula chake.

“Kuna wamama wa aina mbili, kuna wanawake ambao wanajifungua watoto lakini kwenye malezi wanakuwa mbali na watoto hali ambayo inawafanya wasiwajue watoto wao kiundani sana hivyo hata kumuelezea mwanae anapenda nini, yupoje anakuwa hawezi zaidi ya kuvitaja vichache sana ambavyo anakuwa amevisikia mahali. Lakini kuna kundi lingine la wanawake ambao wanajifungua watoto wao na kuwalea wenyewe tangu wakiwa wadogo mpaka wanakua hali ambayo inawafanya wanawajua watoto wao kiundani sana kuanzia wanavyo vipenda, tabia zao, udhaifu wao, uimara wao uko wapi! Hiyo ndiyo sababu mtoto na namna hiyo hawezi kudanganya chochote kwa mama yake”

“Sasa mimi ni mwanamke ambaye nipo kwenye hili kundi la pili mwanangu, wewe nimekuhifadhi kwenye tumbo langu miezi yote tisa kisha nikakulea mimi mwenyewe tangu ukiwa mtoto mpaka unakua hivyo nakujua kuliko mtu yeyote yule chini ya jua la hii dunia. Ulivyokuja tu hospitali kuniona niliona utofauti mkubwa sana kwako kuanzia ujasiri wa macho yako, kuongea kwako, ulikuwa umebadilika kila kitu kwani wewe ulikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa na aibu wakati wanakua. Haukuwa mtu ambaye ungeangaliana na mtu kwa muda mrefu machoni lakini hata mwili wako ulikuwa laini sana ila kwa sasa una mwili ambao upo tofauti sana na watu wengine hivyo baada ya kuishika tu mikono yako, nimejua kwamba wewe sio yule mwanangu ambaye nilikuwa namjua tangu mwanzo tena bali wewe ni mtu mpya ndani ya mwili wa mwanangu” mama huyo alielezea namna alivyokuwa anamjua sana mwanae

“Sasa wewe umejua vipi kwamba mimi nipo kwenye hizi kazi za usalama mama?”
“Asubuhi ya leo nimetembelewa na mkurugenzi wa usalama wa taifa ndipo nikajua kwamba wewe upo kwenye hizo kazi japo nilijua ni kwa hapa Tanzania”
“Mama nahisi utaniambia kwamba unanitania eeh?” mama huyo alisikitika akiwa anamkabidhi mwanae kikombe cha kawaha kwani alikuwa anaipenda sana
“Hapana huo ndio ukweli mwanangu”
“Haiwezekani, mkurugenzi ambaye hata mimi sijawahi kukutana naye wewe umemjulia wapi?”
“Mwanangu hii dunia ni ndogo sana kuliko unavyohisi wewe na ni wachache sana ambao wana uwezo wa kuifanya kuwa ndogo. Mimi yule najuana naye miaka mingi sana huko nyuma”
“Whaaaat?”
“Tulijuana jeshini miaka mingi sana iliyokuwa imepita na yule akaja kuwa rafiki yangu sana kwa baadae lakini baada ya kukutana na baba yako nilichagua kuwa mama wa familia na mkurugenzi ndiye ambaye alinisaidia sana mimi kuweza kukubaliwa ombi la kuachana na kazi yangu baada ya kusingizia kwamba nina tatizo la kifua”
“Hapana mama hicho kitu hakiwezekani”
“Ni ngumu sana kuweza kuamini kwa sababu hatukuwahi kukwambia maana sikuona haja ya kukumbushia maisha yangu ya nyuma sana ila ni hivyo mimi niliwahi kuwa mwanajeshi wa nchi hii lakini rafiki yangu ambaye ni yule mkurugenzi yeye alifanikiwa kuchaguliwa baadae kuingia kwenye idara ya usalama wa taifa ambako amehudumu kwa muda mrefu mpaka kufikia kile cheo kikubwa ambacho yupo nacho mpaka leo”
“Baba anajua kuhusu hili?”
“Ndiyo na wanajuana vizuri sana” Tommy alichoka kwa hayo maelezo ya mama yake.
“Kwanini mkaamua kunificha miaka yote hii mama?”
“Kwa sababu niliamua kuachana na maisha yale kabisa nikachagua kuwa mama bora wa familia. Kuna watu ambao waliwahi kufa kwa uzembe wangu hivyo ninapo yaongelea hayo mambo huwa najisikia vibaya sana ndiyo maana huwa sipendi kabisa kukumbushia hayo mambo ya nyuma maana huwa yananitoa machozi”
“Hilo limekufanyaje ukajua kwamba mimi nipo kule?”
“Wakati Lingson anakuja kuniona asubuhi sana pale hospitali, tumeongea mengi sana lakini pia amenipa taarifa juu ya mauaji ambayo yametokea huko Posta ambayo yemenishtua sana lakini pia akanieleza kila kitu kuhusu mume wangu na kilicho mtokea. Amesisitiza sana kwamba kwa mauaji yalivyokuwa inaonekana kwamba kuna mtu atakuwa na kisasi na watu wale ndiyo maana amewaua kikatili sana namna ile”

Ukurasa wa ishirini na tisa unafika mwisho hapa, panapo majaaliwa tukutane tena wakati ujao.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI
“Swali langu lilikuwa ni kwamba kama mkurugenzi mwenyewe amekataa kwamba wauaji wa sio watu wake sasa muuaji atakuwa nani maana hakuna namna watu wabaya wakauana wenyewe kirahisi sana namna ile tena hadharani na kama ni kisasi atakuwa anakilipa nani? Sina ndugu yeyote wa kiume, hata baba yako hana zaidi ya watoto wa kike ambao tunao na wa kiume ni wewe tu pekee yako. Kwahiyo unahisi ningejua ni nani hapo Thomas? Jibu rahisi ulikuwa ni wewe pekee”

“Sikutaka kuamini moja kwa moja kuhusu hilo hivyo nikapiga simu nyumbani nikaambiwa kwamba tangu jana haujarudi, nikapiga simu mhimbili ambako amelazwa baba yako na haukutaka kuniambia nako nikaambiwa haupo tangu usiku haujarudi. Nikajumlisha matukio na namna nilivyo kuona umebadilika basi nikajua moja kwa moja kwamba ni wewe ndiye ambaye ulikuwa nyuma ya kila kitu japo Lingson nilihisi ananificha jambo maana nilihisi huenda wewe ni kijana wake na nilipanga nisinge msamehe kwa hilo kumbe hata yeye hajui lolote kuhusu wewe” mama huyo alimwangalia mwanae kisha akaendelea.

“Umewaua wangapi?”
“Kumi na mbili mama”
“Kwa sasa naenda kukaa karibu na mume wa maisha yangu, atakuwa mpweke sana hospitali. Tukionana tena jiandae kunipa taarifa zako zote za miaka yote ambayo umeishi bila mimi kuelewa klilichokuwa kinaendelea” mama huyo aliongea akiwa anamkumbatia mwanae na kutoka ndani ya hicho chumba ili aelekee kumuuguza mwanaume ambaye alikuwa anampenda kuliko wanaume wote duniani.

Nchi ilikuwa kwenye mkanganyiko mkubwa sana huku kila mtu akiwa anaongea lake ambalo alikuwa anaona kwamba linamfaa, watu walikuwa wakiendelea na maandalizi ya kuweza kuwapata viongozi wao huku wengine wakiwa na mabango ambayo yalihitaji majibu kutolewa kuhusu mwafaka wa kiongozi wao Apson Limo maana hakukuwa na taarifa yoyote ile kutoka ndani ya jeshi la polisi ambayo ingewafanya wananchi waweze kuelewa nini ambacho kilikuwa kinaendelea.

Mambo yalikuwa ni mengi sana kwa watanzania na muda ulionekana kuwa ni mchache ambapo walikuwa wanehesabu wiki kadhaa ili waweze kuingia kupiga kura kumpata yule ambaye walihisi kwamba angeweza kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi kama yalivyokuwa matarajio ya wengi. Hali hiyo ilipelekea vyombo vya habari kuwa busy sana kuripoti matukio ambayo yalikuwa yakiendelea kila sehemu huku taarifa za uongo zikiwa zinapewa kipaumbele zaidi kikubwa waliangalia habari iwe kubwa tu na sio kuzungumzia uhalisia wa mambo kama ulivyokuwa.


Majira ya saa saba mchana maeneo ya Kariakoo mtaa wa Kongo ambako kuna soko kubwa sana la nguo, alionekana mwanaume mmoja ambaye alikuwa amevaa nguo safi na kofia kichwani. Mwanaume huyo kwa mwendo wake tu hakuonekana kuwa mnyonge sana wala kuwa na afya ambayo ilikuwa ya mgogoro. Aliingia kwenye duka moja la nguo za kike na kununua nguo za kutosha na kuzitia kwenye begi ambapo hata muuzaji alibaki anamshangaa tu maana hakuwa akiulizia hata size yake, alikuwa anabeba tu ambayo angeiona mbele yake kisha akalipa pesa nyingi sana ambapo hakuulizia hata bei akawa ametoka ndani ya hilo duka.

Baada ya kufika nje ya duka hilo, aliangaza kila sehemu akiwa kama mtu mwenye mashaka au kuona kama kuna mtu alikuwa anamfuatilia, baada ya kujiridhisha kwamba hakuna mtu ambaye alikuwa akimfuatilia, taratibu alianza kutoweka hilo eneo akiwa na begi lake kubwa ambalo lilikuwa na nguo za kutosha. Lakini macho yake hayakuwa sahihi kuona kwamba hilo eneo kulikuwa na usalama wa kutosha kwake kwani mita kadhaa kutoka kile sehemu ambayo alikuwa anapiga hatua kulikuwa na mwanaume ambaye kwenye masikio yake aliweka headphone kana kwamba ni mtu ambaye alikuwa anazipata hisia kali sana za muziki.

Huenda ni kwa sababu ya umati wa watu kuwa mkubwa ndiyo maana mwanaume huyo hakuweza kutambua kabisa kwamba ndani ya hilo eneo alikuwa akifuatiliwa kwa ukaribu sana na mtu ambaye hakuwa akimjua kwamba alikuwa ni nani. Mwanaume ambaye alikuwa anamfuatilia mwenzake baada ya kushuka kidogo kofia yake, ilionekana sura ya Nickson waweza kumuita Matiasi Ndugu ambaye alikuwa ni shushushu kutoka ndani ya idara ya usalama wa taifa.

Alikuwa makini sana kwenye kila hatua ambayo alikuwa anaipiga ndiyo maana ilikuwa ni ngumu sana kwa mwanaume huyo kuweza kumshtukia. Mwanaume ambaye alikuwa anafuatiliwa ndani ya hilo eneo alidondosha waleti yake makusudi kisha akajibanza kwa muuza sendo mmoja akijifanya kwamba anaulizia bei za sendo lakini lengo lake alikuwa anahitaji kujua kwamba ni nani ambaye angeiokota ile waleti yake na kama je mtu huyo ambaye angeiokota angekuwa na wasiwasi nae? Ilikuwa ni moja ya njia ya yeye kuweza kujilinda kama kungekuwa na kitu kisicho cha kawaida kingetokea hilo eneo.

Akiwa amesimama hapo anaangalia kwa wizi waleti ile, kuna kijana mmoja ambaye kwa mwonekano tu alikuwa na njaa kali sana ndiye ambaye aliikanyaga na kuivutia kwenye mguu wake mwingine, aliinama na kuiokota kisha akapotea hilo eneo haraka sana. Mwanaume huyo alitabasamu baada ya kugundua kwamba hakukuwa na mtu wa maana yeyote yule ambaye alikuwa anamfuatilia hivyo akaona kwamba kulikuwa na amani ya kutosha akaanza kuondoka.

Wakati anaingia barabarani karibu kabisa na yalipo mataa ambayo yanazigawanyisha barabara za mnazi mmoja, gerezani, Karume na Fire alihisi mwili wake unakuwa mzito sana, moja kwa moja akahisi kwamba huenda kuna mtu anamfuatilia kweli. Gari yake ilikuwa ng’ambo tu kiasi kwamba kama angevuka na kuelekea kwenye moja ya jengo la simu angeweza kuichukua na kuondoka lakini uzito huo ulimfanya amuite boda boda na kutoweka naye kwa kasi sana hilo eneo.

Nick hakuwa na wasiwasi kabisa na mtu huyo kwani alijua atajitahidi sana kumkwepa ila ilikuwa ni lazima amfuate. Hakumfuatilia bali alisogea mpaka lilipo gari la mwanaume huyo ambapo alikuwa na funguo yake mkononi, aliifungua gari hiyo kama ilikuwa yake vile kisha akaifunga tena na hakuna mtu yeyote ambaye alikuwa na muda naye kwani kila mtu alikuwa anafuata biashara ambazo zilikuwa zimempeleka eneo hilo.

Ndani ya dakika kumi mwanaume yule ambaye alikuwa ameondoka na pikipiki, alirudi ndani ya lile eneo kwa pikipiki nyingine ambayo ilimshushia karibu kabisa na ilipokuwa gari yake. Aliangaza kila upande kuona kama kuna mtu bado alikuwa anamfuatilia lakini hakuona mtu hivyo akaingia kwenye gari yake akiwa na begi lake la nguo na kuiondoa gari yake haraka sana akiwa anaishika njia ya Mbagala.

Baada ya kupita lilipo eneo la jeshi, mwanaume huyo alihisi kama ndani ya gari yake kuna ugeni kwani ni kama hali ilikuwa imebadilika hata hivyo akaamua kuyapuuza machale yake kwa sababu gari aliifungua mwenyewe. Kitu hicho kikampa ujasiri wa kuongeza mwendo ili aweze kuwahi eneo ambalo alikuwa anaenda yeye hapo ndipo alipogundua kwamba alichokuwa amekihisi alikuwa sahihi kabisa kwani humo ndani kulikuwa na mtu mwingine.

Aliangalia kwenye kioo na kuona mwanaume akiwa anaiweka sawa bastola yake hususani kukifunga kiwambo cha kuweza kuzuia sauti.
“Tulia hivyo hivyo, ukifanya ujinga wowote ule nakumwaga ubongo kwa sababu sina hasara yoyote ile nikikuua” Nick aliongea akiwa anaielekeza bastola kwenye kichwa cha mwanaume huyo ambaye bila shaka alikuwa na hofu kubwa sana.
“Unataka nini?”
“Endelea kuendesha unipeleke huko ambako ulikuwa unaenda”
“Wewe ni nani?”
“Mimi ndo nikuulize wewe ni nani mpaka unawakimbia watu? Unaanzaje kukimbia kama hauna hatia yoyote ile?”
“Huwezi kunifundisha namna sahihi ya kuyaishi maisha yangu mpuuzi mkubw……” hakumalizia sentensi yake kuweza kutukana kwani alipigwa na kitako cha bunduki kisogoni kiasi cha usukani kutaka kumshinda.
“Uangalie sana huo mdogo wako na mtu unaye ongea naye. Nina maswali kadhaa ambayo nataka nikuulize, kama ukinijibu vizuri nakuacha uendelee kuishi ila kama yatakuwa magumu sana kwa wewe kujibu basi haina tatizo nitakupunguza kwenye idadi ya watu walio hai”
“Utajutia sana hiki ambacho unahitaji kukifanya”
“Yes, napenda sana kujuta kwa sababu hayo ndiyo maisha yangu. Sasa nataka uniambie huyo binti ambaye mmemteka yuko wapi?”
“Hahahahaha hahahahahaha umeanza kujiingiza sehemu mbaya sana kijana”
“Simamisha gari” Nick alimhitaji mtu huyo asimamishe gari baada ya kumuona anakuwa na majivuno mengi badala ya kujibu alichokuwa ameulizwa. Sehemu ambayo aliweza kuipaki gari yake ilikuwa imetulia sana na hapo Nick aliona kwamba wangeongea lugha moja na huyo mtu.
“Swali langu umelisikia?”
“Hata sielewi unazungumzia kitu gani”
“Sawa haina shida” Nick aliongea akiwa anajipapasa kiunoni kwake ambapo alitoa kisu kikali sana, mwanaume huyo wakati anageuka ili aweze kuangalia Nick amekaaje alipigwa na kisu cha shavu ambacho kilichana chana vibaya sana shavu lake mpaka jino moja likawa linaonekana.
“Unaniua, unaniua” aliongea kwa sauti baada ya kushtukizwa na maumivu hayo lakini alitulizwa
“Shiiiiiiii! Kuna muda wanaume tunapaswa kuwa na mazungumzo mafupi sana kwenye kila jambo ambalo tunalifanya. Kwahiyo anapotokea mtu kama wewe unaanza kunipigisha taarabu hapa unanikosea sana heshima na kutukosea wanaume wote duniani, nadhani sasa tunaweza kuzungumza lugha moja. Yupo wapi binti wa Apson Limo na mmepanga kumfanya nini?” swali lilikua linaeleweka huku Nick akwa ameshika kisu hicho mkononi kikiwa kinatoa damu.

“Mimi sijui alipo kwa sababu nimepewa tu maagizo kwamba natakiwa kununua nguo za kike za mtu mzima kisha nizipeleke Mbagala ambapo kuna mahali nilitakiwa kuziacha kisha kuna mtu angekuja pale kuweza kuzichukua hivyo sijui yupo wapi japo nahisi amehifadhiwa Mbagala”
“Usinione mimi mjinga sana kuanza kunipa hizo stori za watoto wadogo, nimekufuatilia tangu unatoka kwenye ile kampuni ya bosi wako R hivyo nina imani haujatoka pale kwa bahati mbaya maana lazima unajua mambo mengi sana hivyo nahitaji uniambie ukweli vinginevyo nakuua muda huu hapa” Nick aliongea akiwa anaikoki vizuri bastola ambayo ilikuwa kwenye mkono wake na kumfanya mwanaume huyo ameze mate.

“Ukweli ni kwamba amehifadhiwa Mbagala ila sijajua ni jengo gani japo ni karibu na maeneo ilipo Dar live. Kuhusu kutoka kwenye kampuni ni kweli kwa sababu mimi ni miongoni mwa walinzi wa lile eneo na sina taarifa nyingi sana kuhusu haya mambo. Sisi huwa tunapewa amri tu ya nini cha kufanya na hatutakiwi kuuliza ila ukitaka kuzipata taarifa za ndani kabisa kuhusu sisi basi mtafute mtu mmoja anaitwa Jabeli, huyu ndiye kiongozi wa ulinzi wa ile kampuni yote na ana biashara yake ya vifaa vya pikipiki pale Riverside ila anaishai Kimara”
“Kuna taarifa gani ambayo unaificha kwangu?”

Ukurasa wa thelathini unafika mwisho hapa.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA MOJA
“Hakuna”
“Una uhakika”
“Ndiyo nimekwambia kila ambacho nilikuwa nakijua japo nahisi watu hao kila unapokuwa unatumwa mahali huwa ni lazima watume mtu wa pili kukufuatilia hivyo wakati unanifuatilia huenda pia kuna mtu mwingine alikuwa anatufuatilia wote wawili. Kama kulikuwa na mtu na ameonyesha mashaka basi lazima taarifa imetolewa atahamishwa aliko hifadhiwa”

“Ok, endeshe gari” mwanaume huyo wakati anaushika vizuri usukani, kisu kilizungushwa kwenye shingo yake na kuchinjwa vibaya sana. Nick hakutaka kuacha kabisa ushahidi kwani kama angemuacha hai huyo mtu huenda ingekuwa hatari sana kwa sababu angekuja kumtaja na kumletea matatizo naye hakutaka kujulikana kabisa. Yale maneno ya kuambiwa kwamba huenda kuna mtu mwingine ambaye alikuwa anawafuatilia yalimpa shaka kidogo na kuhisi huenda hata yeye alikuwa kwenye hatari au bibie angehamishwa huko alikokuwa.

Alifungua tenki la mafuta na kutoweka haraka sana ndani ya hilo eneo na kwenda kujibanza sehemu ambayo ilikuwa na jumba moja ambalo halikuonekana kukaliwa na watu kwa wakati huo. Alikaa hapo kwa dakika tatu akaona kimya hivyo akawa anahitaji kutoweka ila alihisi kama kuna gari inakuja kasi sana lile eneo, ni kweli kulikuwa na gari aina ya Alphard nyeusi ilifika pale wakashuka wanaume watatu na kulisogelea lile gari ambalo yeye alimuulia mtu wake.

Alisubiri mpaka walipo karibia kwenye gari akainyosha bastola yake na kulenga lilipokuwa tenki la mafuta ambalo lilikuwa linavujisha mafuta.
“Kimbiaaaa” mmoja wa wale wanaume aliongea lakini alikuwa amechelewa sana kwani wakati huo risasi ilikuwa imeachiwa na kwenda kutua kwenye tenki la mafuta. Wanaume hao walikuwa wameanza kukimbia ila hawakufika mbali gari hiyo ililipuka vibaya sana na kuwafanya wote watatu kupoteza maisha hapo hapo. Ile Alphard iliondoshwa lile eneo kwa kasi ya ajabu sana ikionekana wazi kwamba kuna wengine walikuwa wabebakia ndani yake.

Nick baada ya kusababisha maafa hayo makubwa hilo eneo mchana wa jua kali, alitoweka kabisa hilo eneo kana kwamba hakuwepo. Watu walianza kupiga kelele sana huku wengine ambao walikuwa wanafanyia kazi zao jirani kidogo na hilo eneo wakianza kukimbia hovyo hovyo kwa kuhisi kwamba huenda labda eneo hilo lilikuwa limevamiwa na magaidi na kama wangezubaa hapo wangepoteza maisha yao.

Licha ya siku kuwa ngumu sana kwa wananchi na mambo ambayo hayakutegemewa kuendelea kutokea, bado watu wasingepingana na uhalisia kwamba muda ulitakiwa kwenda kwa kasi sana na siku ingeisha. Nick akiwa kazini alikuwa anaishi maisha ya kawaida sana mtaani kitu ambacho kilikuwa kinamsaidia sana kuweza kuzikusanya taarifa nyingi na kujua mambo mengi ambayo yalikuwa yanaendelea.

Alikuwa anaishi Macho msasani kwa wakati huo kwa sababu lilikuwa ni eneo ambalo halikuwa mbali sana na Msasani ambako alikuwa akiishi Tommy na familia yake hivyo kazi ya kumfuatilia mwanaume huyo haikuwa ngumu sana kwani kuwa naye karibu kulirahisisha mambo mengi sana. Alikuwa amepanga chumba maeneo hayo ambapo alizoea kwenda kula chakula kwa mama mmoja kisha angeenda kulala ndani ya hicho chumba chake ambacho hakikuwa na kitu chochote zaidi ya kitanda tu na laptop yake ya kazi.

Usiku huo baada ya kutoka kupata chakula chake, akiwa anarudi alipokuwa anaishi, alihisi kama kuna mtu alikuwa akimfuatilia. Ilikuwa ni rahisi kwake kugundua hilo kwa sababu yeye mwenyewe hiyo ndiyo ilikuwa kazi yake kuweza kufuatilia watu lakini mtu huyo ambaye alionekana kumfuatilia usiku huo hakuonekana kuwa mtu wa kawaida kwani alifanya kila namna kuweza kufahamu kama eneo hilo kuna mtu ila hakubahatika kabisa kumuona japo mwili wake ulikuwa ukisisimka sana.

Nick baada ya kukaribia eneo ambalo alikuwa anaishi, alipita njia nyingine kabisa ambayo ilikuwa na uchochoro mfupi kisha angetokezea kwenye barabara ya vumbi kitu ambacho ndicho alikifanya. Baada ya kuivuka ile barabara ya vumbi, kulikuwa na uchochoro mwingine mrefu sana ambao aliamua kuufuata huku akiwa anagusa kama kiunoni kwake bastola iko sawa, lengo la kuzunguka kote huko alihitaji kumpoteza mtu ambaye anamfuatilia asijue kwamba ni wapi alikuwa anatokea na kuelekea.

Lakini akiwa kwenye huo mwendo mkali ambao alikuwa ametoka nao, wakati anakaribia kuifikia kona ya huo uchochoro ghafla sana alimuona mwanaume mbele yake akiwa amempa mgongo. Aligeuka nyuma yake kuona kama kulikuwa na mtu mwingine lakini palikuwa kimya sana kiasi kwamba walikuwa wao wawili tu.

“Unaweza ukanijibu maswali yangu kirahisi tu kama majibu yako yakiniridhisha basi hakutakuwa na haja ya kuumizana mr Matiasi” alishtuka sana na kuitoa bastola yake kuelekeza kwa huyo mtu baada ya kutajiwa jina lake halisi ambalo alikuwa analifahamu kiongozi wake tu, sasa alishangaa inakuwaje mtu ambaye wamekutana usiku tu huo awe analifahamu jina lake. Maana yake kama alikuwa analijua jina la mtu huyo basi alikuwa na taarifa zake nyingi sana ambazo huenda hakutakiwa kuzijua.
“Ni nani wewe ambaye unalijua jina langu ambalo lipo kwa watu wachache?”
“Mimi ndiye muuliza maswali na sio wewe kuniuliza mimi”
“Acha ujeuri wewe, nitakupiga risasi. Nambie wewe ni nani na unataka nini kwangu”
“Mbona unataka kuyafanya mambo kuwa magumu sana bwana Matiasi, nina imani wewe ni mtu muelewa sasa kwanini unakuwa na kichwa kigumu sana namna hiyo kuelewa jambo dogo sana namna hii?” mwanaume huyo alikuwa anaongea kwa sauti nzito sana akiwa bado kageuka na mikono yake kaiweka mfukoni.
“Unataka kujua nini?”
“Nahitaji kujua nani alikutuma wewe kunifuatilia na kwangu unataka nini?” sauti hiyo nzito ilifuatiwa na mwanaume huyo kuweza kugeukia ule upande ambao alikuwa amesimama Nick akiwa makini sana kuangaza nyuma yake maana mwanaume huyo alivyokuwa anajiamini hakutaka kuamini kwamba alikuwa mwenyewe ndani ya hilo eneo. Ukiachana na maswali ambayo alikuwa ameulizwa, alishangazwa sana na mtu ambaye alikuwa anamuona mbele yake kwa sababu huyo ndiye ambaye yeye alipewa kazi ya kumfuatilia na kumlinda kwa ukaribu sana na kiongozi wake.

Tommy ndiye mwanaume ambaye alikuwa amemtembelea shushushu huyo majira hayo ya usiku huo ili waweze kuelezana kwa urefu.
“Wewe ni nani hasa?” mwanaume huyo alihitaji kumjua mtu huyo ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa juu yeye kunyooshewa bastola kwenye mkono wake.
“Baada ya kuisoma historia yako nilivutiwa na ujasiri wako sana ila nikaja kukuona mwanaume mpumbavu sana baada ya kumuua mwenzako kwa sababu ya mapenzi. Mimi hautakiwi kabisa kunifahamu kwa sababu kama ukinifahamu basi nitakuua, hata nisipo kuua kuna watu watakutafuta ili wakuue hivyo kwa usalama wa maisha yako nahitaji unijibu nilicho kuuliza ila kama utahitaji kunijibu kwa nguvu sawa sitakuwa na chaguo ila ukiruhusu hilo lifanyike basi hakutakuwa na kurudi nyuma tena” mwanaume alikuwa akiongea huku sura yake ikionyesha kabisa kwamba hakwenda kirafiki ndani ya hilo eneo hivyo Nick maamuzi yalikuwa kwenye mkono wake juu ya nini anapaswa kukifanya ndani ya hilo eneo.

“Hakuna mwanadamu ambaye amezaliwa kwenye hii dunia akaweza kunitisha mimi hivyo nakuomba uende siku nikijisikia kuongea na wewe nitakutafuta mwenye….” alikuwa anaongea huku akiwa anairudishia bastola yake kiunoni akihitaji kuondoka lakini kila alichokuwa anakifanya kilikatishwa baada ya kuona chuma kinakuja usoni kwake. Ilikuwa ni ghafla sana hivyo alishtuka kitu kilicho pelekea kudondosha bastola yake na chuma hicho kikaenda kukita ukutani.

Wakati anageuka alichelewa sana kwani mwanaume huyo alikuwa amefika pale alipokuwa, alimpiga na buti zito la kiuno ambalo lilifuatiwa na ngumi mbili za kifua zilizo mzoa Nick mpaka ukutani. Alijibamiza vibaya sana lakini alinyanyuka na kujifuta kisha akazipanga ngumi zake kwani huyo aliyekuwa mbele yake hakuwa kirafiki hivyo alitakiwa kumchukulia kama alivyokuwa amekuja hapo. Nick alikuwa anamfuata Tommy kwa zigzag huku akiwa anaichanganya mikono yake vyema, Tommy alimsubiri mpaka mwanaume huyo alipo mkaribia sana akajivuta nyuma kwa nguvu sana kitu ambacho kilimshtua Nick kwani ngumi zake ziliishia kupiga hewa tu na kumpelekea kukosa balansi.

Uzito wa ngumi ambayo ilitua kwenye tumbo lake alihisi kama amekula vyuma vyenye moto maana aliguna kama mtoto mdogo huku akipiga magoti. Alikutanishwa na kifupi cha taya akadondoka chini, akiwa hapo chini alimuona mwanaume huyo akiwa anazunguka anaelekea alipo kwa buti kali ambalo lililenga shingo yake. Alijiviringisha pembeni na buti hilo likatua ardhini na kupelekea ardhi karibu na alipokuwepo kutetema kiasi kwamba kama lingemfikia shingoni basi habari yake na hiyo shingo yake ingeishia hapo.

Alisiamama kwa msaada wa ukuta akiwa anajiweka sawa kukabiliana na mtu huyo, alijirusha kama kucheza kamali kwa sarakasi safi kuelekea kwenye mwili wa Tommy ila kwa bahati mbaya ni kama mtu huyo alikuwa akimsubiria aweze kufika hilo eneo kwani alipokelewa na double kick ambayo ilimrudisha ukutani na kumfanya atoe sauti nzito ya kuhema kifuani kiasi kwamba kuna kitu kilikuwa kinamkaba. Damu ilikuwa inamtoka mdomoni, alitamani sana kunyanyuka aendelee kupambana lakini mwili wake uliweza kumsaliti kabisa akabaki analaani kuwa kwenye hiyo hali ambayo ilimfanya asiwe na uwezo hata wa kuyatetea maisha yake akabaki anaangalia kinacho tokea tu.

Tommy taratibu aliisogelea bastola ambayo Nick aliidondosha na kumsogelea pale alipokuwa amelala akiwa ameuweka mgongo wake ukutani.
“Mwili wako ni laini sana lakini una jeuri sana kwenye mdomo wako. Umenipotezea dakika nyingi sana mbazo nilitakiwa kuwa naifanya kazi nyingine kuirudisha familia yangu, sasa nakuuliza kwa mara nyingine, kwanini unanifuatilia na nani amekupa hii kazi?” mwanaume aliongea huku akiwa anaikoki bastola hiyo vizuri na kuielekeza lilipo goti la Nickson. Nickson huenda angetamani sana wawe chungu kimoja na huyo mtu kwa sababu jukumu lake kwa muda huo lilikuwa ni kumlinda ila kwa bahati mbaya sana haukuwa muda sahihi hivyo alitakiwa kumpatia kile ambacho angekihitaji maana kama angeenda tofauti huenda angemuua.

“Nimetumwa na mkurugenzi”
“Mimi nina husiana naye nini mpaka akutume wewe kwangu?”
“Alinipa kazi ya kukulinda”
“Kunilinda?”
“Ndiyo”
“Kwahiyo mnajua kila kinacho endelea sio?”
“Ndiyo, najua kila kitu hususani kuhusu baba yako na siku ile anapigwa risasi nilikuwa karibu na lile eneo ila nilishindwa kumsaidia”
“Kwahiyo baba yangu alipigwa risasi mbele yako”
“Ndiyo”
“Na haukuwa na cha kufanya?”
“Ndiyo, ilikuwa ni ghafla sana”
“Uliwezaje kujua kuhusu hilo jambo”

Ukurasa wa thelathini na moja nanyoosha mikono yangu hapa, tukutane tane wakati ujao.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA MBILI
“Kwa sababu bosi alikuwa amenipa kazi ya kufatilia kuhusu familia yenu” Nickson alilazimika kumwambia Tommy kila kitu kuanzia siku ya kwanza ya yeye kupewa hiyo kazi na kuanza kuitekeleza.
“Kwahiyo hata wewe haujui dada yangu yuko wapi na kichwa cha mdogo wangu kilipo?”
“Ndiyo, lakini kuna mtu ambaye nilikuwa namfuatilia baada ya kutoka kwenye ile kampuni na ndiye ambaye amenipa taarifa za uwepo wa dada yako huko Mbagala. Lakini wakati nimemaliza kumhoji kuna watu walikuja ambapo nimefanikiwa kuwaua wanne hivyo kama walikuja maana yake walijua kwamba mwenzao atakuwa ametoboa siri zao lazima wamemhamisha. Lakini alikuwa amenitajia jina la mlinzi mkuu wa ile kampuni na sehemu ambayo anafanyia kazi zake pale Riverside, huyo anaweza kutupatia mwongozo kamili wa kila kitu akatusaidia kumpata dada yako” maelezo yake yalifuatiwa na kutaja sehemu ambayo alikuwa anapatikana mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Jabeli.

“Hauna uwezo wa kuwa mlinzi wa mtu kwa sababu hata wewe hauna uwezo wa kujilinda mwenyewe. Hivyo usije ukathubutu tena kuja kunifuatilia kwenye maisha yako kwa sababu nitakuua. Mwambie kiongozi wako nahitaji kuzungumza naye” mwanaume aliongea kibabe halafu akawa ameiachia business card yake na kutoweka hilo eneo kama mzimu.


Sea Cliff Casino
Jirani kabisa na lilipo kasino hilo la kifahari majira ya usiku wa manane, kuna mwanaume alikuwa kwenye mwendo wa kawaida juu ya piki piki lake kubwa sana la bei ghali akionekana kabisa kwamba hofu haikuwa sehemu ya maisha yake na alitakiwa kuwahi eneo ambalo alikuwa anaelekea. Alikuwa ameishika njia ambayo ilikuwa inampeleka moja kwa moja kwenye kasino hilo lakini kuna sehemu aliona pana kiza kisha mbele yake mwanga uliendelea kama kawaida maana hakukuwa na dalili zozote za umeme kukatika hivyo akajua moja kwa moja kwamba eneo hilo kuna watu au mtu ambaye alikuwa ameuzima umeme kwa makusudi kabisa huenda kwa ajili ya kutimiza yale ambayo aliyakusudia.

Alipunguza mwendo baada ya kufika hilo eneo kwani alianza kuona vivuli vya watu vikiwa jirani na hiyo sehemu ambayo ndiyo pekee ilikuwa na kiza wakati huo. Alishuka bila wasiwasi na kuona kuna vijana watano ambao walikuwa na mapanga kwenye mikono yao huku miili ikiwa imejaa kuonyesha kwamba hawakuwa nyuma sana kwenye upande wa mazoezi.

“Tupatie kila ulicho nacho pamoja na funguo za pikipiki kisha utoweke hili eneo bila kupiga kelele” aliongea kijana mmoja ambaye ndiye alikuwa mbele huku akiamini panga lake lingemlinda nyakati zote. Mwanaume ambaye alikuwa ametembelea hayo maeneo hakuwa mwingine bali Pablo Mkinga ambaye alitolewa gerezani na mr Mafupa na kumtaka awatafute watu ambao walikuwa wamehusika kwenye mauaji ya vijana wake na walionekana kumfuatilia.

Pablo Mkinga kabla ya kuianza kazi yake hiyo alitakiwa kwanza akutane na mwanamke ambaye alikuwa akijulikana kama Sasha huku akitumia jina feki la Noelia, huyo ndiye angempa mwanzo mzuri wa kuanzia kwani alikuwa na taarifa nyingi zaidi na kwenye kasino hilo kubwa ndiyo sehemu ambayo alikuwa anapatikana. Hivyo safari ya majira hayo ya usiku ilikuwa ni kwa ajili ya kumfuata mrembo huyo ndani ya kasino hilo ambalo ndiyo yalikuwa maeneo yake ya kujidai muda mwingi ambao angekuwa hapo.

Ile sauti na aina ya utekaji ambao walionekana kuufanya wale vijana, vilimfanya mwanaume huyo acheke kwa nguvu sana kwani alihisi labda ni watu ambao walikuwa wanamfuatilia kwenye safari yake hiyo lakini aligundua kwamba walikuwa ni vibaya wa kawaida tu ambao huenda walikuwa wakiongozwa na njaa hivyo kwao ilikuwa ni mwiko kuweza kufanya kazi kwa bidii bali walikuwa wakitegemea kuwapora watu ili waweze kuishi.

Kicheko chake kiliwafanya vijana hao waone kama anawadharau ingali wapo kazini hivyo wakahitaji kumuonyesha mtu ambaye hawakuwa na taarifa zake kwamba aliwahi kuwa komando wa jeshi la nchi ya Tanzania. Upanga ulimkosa kidogo kwenye bega lake kiasi kwamba kama ungempata huenda ungetenganisha bega hilo, sasa aliona kwamba kitu ambacho kilikuwa kinaendelea hapo alitakiwa kukichukulia kwa uzito sana maana vijana hao kama angewachekea wangempotezea muda wake bure.

Mwanaume alimkwepa kwa mara nyinyinge kijana huyo kisha akamtwisha ngumi nzito sana ambayo ilimfanya kijana huyo atoe sauti ya maumivu kwani mkono ulivunjwa vibaya mno kisha upanga ambao ulikuwa kwenye mkono wake ukawa umetua mikononi mwa wanaume huyo ambaye hawakuelewa namna alivyo ugeuza na kuuchomeka kwenye shingo ya kijana huyo alivyokuja kuutoa kijana huyo alikuwa amekufa. Wenzake waligundua kwamba hiyo ni vita tayari hivyo walimshambulia wote na mapanga hayo. Aliwafanyia kitu kibaya sana, alikata kata shingo zao na kuzitenganisha na vichwa vyao ambapo alimuacha mmoja tu ambaye alimkata mkono wake kisha akamtamkia.

“Bwana mdogo hii dunia usije ukacheza nayo linapokuja suala la maisha yako, hayo mazoezi ambayo mnafundishwa kwenye judo huko yanawafanya mnahisi kwamba mnaijua dunia, nakuacha hai ili ukawe shahidi kwa wenzako na uwaeleze wasipende kuingia kila eneo ambalo hata hawalijui, siku nyingine ukiiona hii sura hata kwa bahati mbaya kimbia sana maana nikikuona nitakuua hapo hapo” alitamka kwa msisitizo huku akiichana sehemu ya paji la uso la kijana huyo kwa nguvu kama kumbukumbu ili asije akamsahau maishani mwake. Kijana huyo alipiga makelela ya maumivu lakini hakukuwa na msaada wowote kwani ni mambo ambayo aliyataka mwenyewe na yeye ndiye alikuwa mtu wa kujilaumu mwenyewe kwa hayo ambayo yalimkuta. Alikimbia sana kutoweka eneo hilo akiwa anavuja damu nyingi kwenye mkono wake pamoja na kwenye paji la uso.

Ndani ya kasino hilo kulikuwa na mwanamke mrembo sana ambaye alikuwa amependeza isivyo kawaida, alikuwa ametoka kwenye chumba kimoja ambako bila shaka alikuwa anatoa huduma kwa mteja kama ilivyo kawaida kwenye maeneo kama hayo ambayo zinachezwa kamali za pesa nyingi sana basi huwezi kuyakosa maua mazuri kama hayo kwa ajili ya kuwafariji wanaoliwa lakini pamoja na kuwapiga pesa za ushindi wale wanao kula.

Huyo ndiye alikuwa Sasha, wakati anatoka ndani chumba hicho alimuona mwanaume mmoja akiwa anamwangalia kwa umakini sana, basi kwa madaha akawa anasogea ndani ya lile eneo.
“Una shingapi mwanaume wa shoka?” aliuliza akiwa anamimina pombe ya Pablo kwenye glass yake na kuinywa kwa mapozi sana akiwa anamshika Pablo sehemu zake za siri, mwanaume alishindwa kuvumilia ikambidi agune kwanza.
“Mwili wako mzuri huo ni bei gani?”
“Milioni moja tu”
“Kuna chumba kizuri hapa jirani?” hakukuwa na maneno mengi sana, mrembo huyo alimpa ishara ya kumfuata mwanaume ambaye badala ya kufanya kazi yake pepo la ngono lilimuingia kwa kasi isiyo ya kawaida hivyo akaona ni sehemu sahihi ya yeye kupunguzia uzito ambao alitoka nao ndani ya gereza. Baada ya kufika ndani ya hicho chumba mrembo Sasha alizivua nguo zake zote na kwenda kulala kitandani kwa madaha akiwa anatoa ishara ya pesa kwenye mkono wake.

Mwanaume alitabasamu kwa sababu alikuwa ameshikwa pabaja hivyo ikamlazimu kutoa dola mia mia tano na kuziweka mezani ambapo alimvamia mwanamke huyo wakaanza kuyafanya mapenzi kwa fujo sana. Walitumia saa zima kila mtu kuweza kuridhika vya kutosha ndipo wakaachiana huku Sasha akiwa anahema mithili ya mtu ambaye ametoka safari ya mbali sana.

“Mwanamke kama wewe hautakiwi kuwa eneo kama hili, unatakiwa kuwa mke wa mtu kabisa uendelee kuipendezesha nyumba yako ila kwa bahati mbaya umemezwa na hii dunia ambayo haieleweki na kutoka huku ni ngumu sana. Inanisikitisha sana juu ya hilo” mwanaume huyo aliongea kwa sauti yake nzito sana huku akiwa anasogea kwenye nguo yake na kuiwasha sigara yake kubwa aliyo itoa kwenye hiyo nguo na kuivuta kwa hisia sana.
“Unanionea huruma? Kwani mimi na wewe tunafahamiana?”
“Nasikia wewe ni mpenzi wa Remsi, nilijua huenda huwezi kuvua nguo zako kwa mwanaume mwingine lakini umezivua kiwepesi sana zaidi ya nilivyokuwa nategemea” kauli ya mwanaume ilimfanya Sasha kuusogelea mkoba wake na kutoa bastola ambayo alimnyooshea Pablo.
“Wewe ni nani kabla sijakuua?” Sasha alianza kuhisi huyo mtu hakuwa salama kwake lakini Pablo aligeuka akiwa uchi kabisa na kumfanya Sasha ameze mate kwa shida ni kama alikuwa anatamani kufanya naye mapenzi tena.

“Kama ningehitaji kukuua mpaka tunavyo zungumza ningekuwa nimekuu muda mrefu sana lakini nitakuwa mwanaume mjinga sana kulipunguza ua zuri namna hiyo ambalo limenipa penzi zuri ambalo nimelikosa kwa muda mrefu sana, weka bastola yako chini kisha unisikilize” licha ya maneo yake ambayo yaliishia kumfanya Sasha ameze mate bado hakuwa tayari kuweza kuiachia hiyo bastola yake.

Pablo alitazama pembeni kitu ambacho kilimfanya naye Sasha aangalie huko ila hakujua kama alikuwa anampotezeshea umakini, kweli baada ya kugeuka kuangalia kama labda kulikuwa na kitu, alishangazwa na kasi ya mwanaume huyo ambayo alikuja nayo na kumpokonya bastola yake kisha akatoa risasi zote na kuzitupa kwa kuzitawanya humo ndani. Lilikuwa ni tukio la ghafla sana, Sasha akiwa anaendelea kushangaa mwanaume huyo alimlaza tena kitandani na kufanya naye mapenzi kwa fujo sana mpaka walipo tosheka tena ndipo wakaachiana.
“Mzee kuna kazi amenipa na ameniambia kwamba taarifa zote za sehemu ya kuanzia nitazipata kwako hivyo unaweza ukanipa taarifa zote ninazo zihitaji”
“Ohhhh shiiiit! Kwanini haukuniambia mapema?”
“Baada ya kujua nani kanituma hapa unaanza kuogopa kwamba Remsi atajua tumefanya mapenzi au?” aliitikia kwa kichwa kuweza kukubali hilo jambo.
“Hawezi kujua hili, kwani yeye hajui kwamba wewe ni Malaya na unajiuza”
“Anajua kwa sababu tulikutana kwenye mazingira haya haya”
“Kama anakuelewa shida iko wapi sasa mpaka unakuwa na hofu sana namna hiyo?”
“Kukutana kimwili na mtu wake wa karibu ambaye ni mfanyakazi wake huoni kama itakuwa ni tatizo kama tunamdharau hivi”
“Mimi sijawahi kuwa karibu na huyo bwana mdogo ila nafanya kazi na baba yake. Nafikiri itakuwa vyema kama mimi nikiichukua nafasi yake kwako bila yeye kujua” kauli hiyo kidogo ilimfanya mwanamke huyo atabasamu kwa furaha na kumsogelea Pablo akiwa anamshika shika sehemu zake za siri.
“Umenipa penzi ambalo sijawahi kulipata kwenye maisha yangu, leo kwa mara ya kwanza nimefika kileleni hivyo kwa wewe nitakuwa nakupa bure muda wowote utakao uhitaji na pesa yako sichukui” aliongea kwa madaha akiwa anausogelea mdomo wa Pablo na kuupachika wa kwake wakawa wanabadilishana juisi asilia ila Pablo aliona kabisa asipokuwa makini anaweza akasahau hata kilicho mpeleka ndani ya hilo eneo maana penzi ni kitovu cha uzembe.

Ukurasa wa thelathini na mbili unafika mwisho hapa.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom