Sakata la Warere Beach hotel kwa mtalii mgeni, Serikali ichunguze, wahusika wachukuliwe hatua, wametia doa sekta ya utalii nchini

Sakata la Warere Beach hotel kwa mtalii mgeni, Serikali ichunguze, wahusika wachukuliwe hatua, wametia doa sekta ya utalii nchini

Kipindi hiki tunataka zindua royal tour!!?
Hichi kipindi cha uzinduzi wa Royal tour ndio kipindi sahihi zaidi kwa huyo mnaigeria kulisemea, maana dunia itasikia na kulivalia njuga na huenda serikali ya Tz ikaamua kutoka usingizini ili kuchukua hatua dhidi ya wahusika.

Watanzania wote kwa pamoja tumuunge mkono huyo mnaigeria kulipigia kelele hili suala, uzalendo sio kufunika uovu. Wacha ukweli utuume lakini mwisho wa siku sote tupone.
 
Sijawahi kuwaamini wanaigeria, ni watu hatari sana linapokuja suala la pesa au kutafuta huruma kupata umaarufu.
Kama huwaamini wanaigeria basi njoo umuamini mmiliki wa Weru weru Lodge wa kule Machame ambaye alilalamika na kutoa video clip zikimhusu mkuu wa wilaya ya Hai (Ole Sabaya) aliyetinga hotelini kwake akilazimisha akalale na Nandy.
 
Katika pitapita zangu za leo nimekutana na tweet hii ya binti kutoka Nigeria,aliyekuja Tanzania kwenye matembezi na kusherekea sikukuu yake ya kuzaliwa .

Ameeleza namna ambavyo alikuwa amelala Warere beach hotel na usiku wa manane akashangaa kuna mwanaume kitandani anampapasa papasa na kutaka kumbaka.
Kwa namna alivyoandika habari hii naona kuna shida kubwa sana katika hiyo hotel..kuna shida namna polisi aliporipoti walivyolichukulia na kushughulikia jambo lake.

Lakini pia to me namuona kama binti ambaye ni very strong,kama asingekuwa na hizo evidence huenda angeambiwa kapika hili jambo.Pamoja na kwamba kalitoa wakati huu ambao tuna issue ya uzinduzi wa royal tour ni vyema serikali yetu ilifuatilia kwa karibu na kutoa majibu ya sakata hili.

Nimeangalia hiyo tweeter namna inakuwa retweeted na baadhi ya comments za watu kucancel Plans zao za kuja Tanzania baada ya hiyo habari...ni aibu kwa kweli..wahusika wawajibishwe na binti huyo arudishiwe fedha zake. Kama kuna hotel zingine wenye tabia kama hii zikomeshwe pia mara moja ili kuendelea kulinda na kukuza sekta yetu ya utalii.Raisi wetu anajitahidi sana lakini unakuta tuna watu wenye akili mgando kama hao wa hiyo hotel.Kama room ilifungwa,namna ya mtu mwingine kuingia ni kwa master key ambayo hotel inayo..ili jambo linakasirisha sanaa.

Hiyo Warere Beach hoteli ni ile ya Itigi?
 
Hivi mtanzania gani wewe unaona nchi yako unachafuliwa unashadadia hata kama kweli imetokea kulikuwa na maanaga gani yeye kwenda kwenye social media kupost sawa alienda kituo cha polisi lipiga sm ubalozini kwake he umeona kunasehemu alienda wizara ya mambo ya ndani zaidi ya kulaumu polisi ambao hata siye wazawa tunajua kweli jeshi la polisi la hovyo kwanini amue kupublish hivyo

Uyo mnaija katukosea sana tena sana ngoja niende kwanga uk
Sio kudhadadia Mtanzania mwenzetu,tunataka hawa watu waliosababisha haya wachukuliwe hatua mara moja ili mambo haya yasitokee tena.
Huyo traveller kaona yeye atumie approach hii,tatizo huwa tunadharau sana watu ndo shida..laiti wangejua huyo binti anaweza leta impact kiasi hiki naamini wangelishughulikia kwa umakini kipindi limetokea
 
Isolated event

Hatuwezi kuchafuka kwa hadithi ya mtu mmoja kutoka Kiherehere hotel
Warere Mkuu
Kweli huyo Shauna yupo, tulishaenda hapo ni pazuri, shida ya zenj ni porous, mtu awezaingilia popote siyo salama hata Kwa watoto wa kiume alone!
Kulishwa drugs na kuliwa jicho na popo bawa ni rahisi!

Huyu alipewa drugs ila kiwango nafikiri kilikuwa kidogo hakuwa totally out!

Nimeshangaa hakuna receptionist overnight! Hatukuhitaji huduma Ila kawaida hotel zikiwa na wageni, huwa receptionist wanalala hata mapokezi chini! Shida tupo kimazoea!

Pole zake!
 
Uchunguzi
20220417_075439.jpg
 
Sio kudhadadia Mtanzania mwenzetu,tunataka hawa watu waliosababisha haya wachukuliwe hatua mara moja ili mambo haya yasitokee tena.
Huyo traveller kaona yeye atumie approach hii,tatizo huwa tunadharau sana watu ndo shida..laiti wangejua huyo binti anaweza leta impact kiasi hiki naamini wangelishughulikia kwa umakini kipindi limetokea
Sawa,
Atendewe haki, wamruudishie pesa, wazuge Tu, maneno, tunalifanyia kazi. Walinzi WA siku hiyo tumewasimamisha kupisha uchunguzi!
Blah blah blah, we take these allegations seriously! Mbona easy, hatuhitaji maguvu! Beberu anatushinda hapo! Kwenye being diplomatic & politically correct!
 
Hivi mtanzania gani wewe unaona nchi yako unachafuliwa unashadadia hata kama kweli imetokea kulikuwa na maanaga gani yeye kwenda kwenye social media kupost sawa alienda kituo cha polisi lipiga sm ubalozini kwake he umeona kunasehemu alienda wizara ya mambo ya ndani zaidi ya kulaumu polisi ambao hata siye wazawa tunajua kweli jeshi la polisi la hovyo kwanini amue kupublish hivyo

Uyo mnaija katukosea sana tena sana ngoja niende kwanga uk
Kituo cha Polisi nao wamesemwa.
Mamlaka husika wajiridhishe kama huyu mtu kipindi hicho aliingia Tanzania alafu masuala mengine yafuate

Screenshot_20220417-080515_Twitter.jpg
 
Mpaka sasa dada katupiga maana kwa ushaidi wa awali vyombo vyetu vimefail sana sio muwekezaji wala polie walionesha kutaka kumsaidia dada too sad to hear that
Hilo ndilo kero kubwa!
Manager kumwambia muongo, wakati. Angemwambia tunalichukia serious, twende police, hapa ni mahali salama. Tunaangalia CCTV, vitu kama hivyo! Tunakupa baunsa WA kuzunguka naye Kwa hizi siku 4 ulizo hapa. Baunsa unamlipa 30,000 Kwa siku! Mambo mengine siasa Tu!

Siyo kila mgeni wa like anayeenda Zanzibar, kaenda kujiuza! Hiyo mentality ndiyo iliyopelekea hayo, manager kuona mgeni ni danga na police kumuona ni danga vile vile!

Customer care! Kuna comic book ya Tommy & Jenny, huwa siachi kucheka kila nikilipitia, linatusema haswa!
 
Wa maelezo yake anaonekana ni tapeli tu yule. Wanigeria kibao wanaichafua Zanzibar. Nimesoma hizo tweets yani anajichanganya tu na anaongea vitu visivyo realistic. Haya, kasema mbakaji alikuwa hajui kingereza na alielewa neno HIV pekee, ila alipoaga kuendea condom na akasema atarudi walielewana hahah.. Mbakaji anakuita baby?
 
ujinga mtupu alikuwa wapi kusema au sababu ameona mama anazindua royal tour anataka kuharibu tatizo wa Tz tunakosa uzalendo tunafuta upepo tu kila kitu
 
Hichi kipindi cha uzinduzi wa Royal tour ndio kipindi sahihi zaidi kwa huyo mnaigeria kulisemea, maana dunia itasikia na kulivalia njuga na huenda serikali ya Tz ikaamua kutoka usingizini ili kuchukua hatua dhidi ya wahusika.

Watanzania wote kwa pamoja tumuunge mkono huyo mnaigeria kulipigia kelele hili suala, uzalendo sio kufunika uovu. Wacha ukweli utuume lakini mwisho wa siku sote tupone.
ww nawe unashindwa kutumia akili yako vizuri kwa hiyo Tanzania ikichafuka ww utafurahi
 
Back
Top Bottom