bezos2019
Member
- Apr 23, 2019
- 47
- 35
Asilimia kubwa ya wanaopinga mkataba (IGA) Hawapingi mkataba (IGA) wa bandari, kwakua ili kupinga mkataba, ni lazima uanze na sheria zitakazo ongoza mkataba kwanza, kabla ya yaliyomo, kwakua yaliyomo ni lazima yafuate sheria. Hii ni kama tu unataka kupinga kwa nia njema ya taifa. Usipofanya hivyo nisawa na kuchukua maneno, na mistari miwili kwenye vitabu vitakatifu ili iendane na haja zako. Waingereza wanaita hali kama hiyo “ulterior motives”Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi ameachiwa huru majira ya saa 12 jioni (Julai 14, 2023) baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa saba katika Ofisi ya makao kikuu ya Polisi mkoa wa Mbeya.
Akizungumza na Jambo Tv baada ya kumaliza mahojiano yake na Polisi, Mwabukusi amesema aliitwa na Jeshi hilo akituhumiwa kwa makosa ya kutoa lugha ya chuki dhidi ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa akidaiwa kwamba alihamasisha jamii kuwa Waziri Mkuu asiaminike kwa wananchi juu Suala la uwekezaji wa bandari kuwa una faida, hoja anazosema amezitolea maelezo polisi.
Aidha Mwabukusi amesema kuitwa na kuhojiwa kwake kwa muda mrefu wa zaidi ya saa saba kunampa nguvu pamoja na mawakili wenzake kuendelea kuwatetea walalamikaji ambao wananchi waliofungua kesi ya kupinga mkataba wa Bandari kwa madai kuwa hauna maslahi kwa Taifa.
"Niwaambie tu kwamba kwa hili la kuitwa na kuhojiwa inanipa moyo sana na sikati tamaa pamoja na wenzangu, msimamo wangu uko palepale, inanipa moyo kwani naelewa kwamba kumbe Meseji Sent and Derivery (Ujumbe umeenda na umewafikia)", Wakili Mwabukusi.
"Mimi ninachotaka kuwaambia wa-Tanzania 'Hatujakosea', tuko sahihi, msimamo wetu ni uleule na tupo tayari kufika kwenye vyombo vya kisheria kwa namna yoyote kwasababu ninaamini tutapita tena na tena kwenye uvuli wa mauti lakini tutafika kwenye ukombozi kamili", Wakili Mwabukusi.
"Tuna haki za kikanuni na kikatiba, na mtu yeyote asiyetaka kukosolewa aondoke kwenye Ofisi za umma akakae nyumbani kwake hatutamfuata lakini mtu anayevunja Katiba tutamsema, kwahiyo siogopi, hata mtu akiwa Mbunge, Waziri mkuu au Rais hiyo ni dhamana hii nchi ninyetu sote sio ya watu wachache lazima nisimamie msimamo wangu lakini na kulinda raslimali za Taifa kwa mujibu wa Katiba", Wakili Boniface Mwabukusi.
Naye Wakili wa Mwabukusi kwenye shauri hilo Wakili Phillip Mwakilima amewashukuru wanasheria mbalimbali walioshirikiana katika sakata la kuhojiwa kwa mteja wake (Boniface Mwabukusi) akiwemo Rais wa TLS na Balozi Dkt. Wilbroad Slaa.
Amesema Mwabukusi ameamriwa kuripoti tena polisi mwanzoni mwa juma lijalo.
Hata hivyo Wakili Mwakilima amesema wamejiandaa kumfungulia mashtaka Juma Homera ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa madai kuwa amewadhihaki wateja wao (Waliofungua kesi ya bandari) kuwa wanawatetea wezi pia anadaiwa kushindwa kusimamia nafasi yake ya Mwneyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama badala yake amesikika akisema waliofungua kesi ya kupinga mkataba wa Bandari anawakabidhi kwa machifu wa kimila ili wawashughulikie.
"Kwahiyo niiombe mamlaka yake (Mkuu wa mkoa Mbeya Juma Homera), Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ampeleke kwingine kama si kumuondoa kabisa maana kwa hili tu (kuwakabidhi waliofungua kesi kwa machifu) hafai kuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama", Wakili Phillip Mwakilima.
Mtuhumiwa Wakili Boniface Mwabukusi aliingia polisi saa 3:58 asubuhi na mahojiano yalimalizika majira ya saa kumi na dakika kadhaa lakini Wakili Mwakilima alieleza kuwa bado Mwabukusi anaendelea kuwa mikononi mwa Polisi licha ya kumaliza mahojiano hadi baadaye majira ya saa moja kasoro baada ya taratibu nyingine kukamilika hasa za kujidhamini hadi atakaporipoti Jumatatu ijayo Julai 17, 2023.
Chanzo: Jambo Tv
Kuna msukumo mkubwa kwa wanaopinga lengo Lao kuu ni wanapinga Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 🇹🇿 kuwa HURU kimapato kwa mara ya kwanza. Usione ajabu, Kaskazini wanakua na mtazamo tofauti wa mambo na sio dhambi. Hata Mangi Mkuu Mangi Marialle alipingana na Mwl kuhusu Tz kupata uhuru 09 Dec 1961, aliona muda haijafika kwanza, hatuna uwezo wa kujiongoza Bado.
Lakini Uhuru uliletwa na TANU, ambayo leo inaitwa CCM, baada ya kuugana na Afro Shirazi (ambacho likua na wapini Znz) 1977, na Kila mtu amefaidika kutokana na hilo.
unaweza kuiangalia South Africa 🇿🇦 Kijuju ukadhania bora tungechelewa kidogo kupata uhuru kama ulivyokua mtazamo wa Mangi Mkuu Mangi Marialle, japo alikua hapatani na mmoja wa mangi wadogo, mangi Shangali.
Laking Uhuru ni sasa, alisisitiza Mwl, na njia aliyofanikisha kutupitisha ndio tunaendelea nayo Leo.
Hili Jambo ni kubwa kiasi kwamba haliwezi kuwa na mkataba (IGA) mmoja wenye kurasa 38 tu, lazima iwepo mengine, pia ya kupenda na na makubaliano kati ya Tanzania 🇹🇿 na Dubai. Kuku, mbuzi, nguruwe, ngombe, ni nyama, kama vile IGA, HGA, na PA(s) yote ni mikataba, lakini nyama zote ziko Sawa? Mikataba yote iko Sawa?
Watu wanajua tofauti Za nyama, ila kutokana na shughuli zao Za Kila siku sio wote wanajua tofauti ya tofauti ya IGA, HGA, na PA(s).
Kutokua kwao usikutumie kwa faida yako kama wewe ni kiongozi wa kweli.
ukiiangalia kipengele cha 21, kipengele pekee pekee kinachoelezea sheria zitakazo ongoza mkataba, kwakua yaliyomo yote lazima yaendane na sheria.
Kimsingi tafsiri ya mkataba ni makubaliano yanayoweza kulazimishwa na sheria.
Sheria gani sasa zinaweza kulazimisha hayo makubaliano?
Jibu liko kipengele cha 21, kwamba IGA itafuata sheria Za uingereza ambazo tunazifuata tayari, zinafanana na Sheria zetu, kwakua tumezirithi kutoka serikali iliyokuwepo kabla ya 09 Dec 1961. Kipengele cha 21 pia kinasema HGA na makubaliano ya mradi yatafuata sheria Za Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Na sheria Za Tanzania tunaweza kuzibadilisha tunavyotaka bila na mkataba (IGA) inatambua hilo, na kukiri hilo. Hii inakua muhimu kwenye mapato. Ndio maana mapato hayamo kwenye IGA, yatakuwepo kwenye HGA ili yafuate sheria Za Tanzania, na hapo ndipo Prof Mbarawa, wanalinda maslahi, ya wa Tanzania, kwamba mapato yangekuwepo kwenye IGA, tusingekua na control nayo. Badala ya kufurahia hilo wanaliruka, hakuna anayepinga anaweza kukataa ukweli huu.