Sakata Mkataba wa Bandari: Wakili Mwabukusi asema asiyetaka kukosolewa aondoke kwenye ofisi za Umma

Sakata Mkataba wa Bandari: Wakili Mwabukusi asema asiyetaka kukosolewa aondoke kwenye ofisi za Umma

Inaonyesha kazi ulioipita inatokana na kamlete. Huna uzalendo kwa nchi ila kwa waliokuajiri
Mzalendo ni nani? watu wakupingapinga ndio uzalendo au?ukiunga mkono unakuwa sio mzalendo.
 
Asiye taka kukusolewa akaongoze familia yake,nchi hii sio Mali ya viongozi ni mali ya umma wote hivyo kila mtu ana wajibu wa kutetea maslahi ya taifa
 
Nyinyi mshukuru sana Mungu alimchukua JPM mapema angewarudisha kwenye mapango mlikotoka. Mama katukosea sana na huruma zake. Ingepita operation moja kabambe ndio mngeshika adabu mbwa nyie.
Exactly,Hawa mbwa dawa yao kuwashoot tu
 
Mpewe nyinyi Chadema wenye mwenyekiti wa maisha? nyinyi hata u mayor tu hampewi na mkipata tuna pendua meza sababu nyinyi hamstahili hata kuongoza kijiji. watu gani hamna sera mnadandia habari zenye ku trend. Juzi mmeanza ohh Ali Karume hawezi kufukuzwa tu hivi hivi yanawahusu nini? wale wanawake 19 wamewashinda. Na wale sio wao nguvu za CCM nyuma. Ndio ujue power tuliyonayo. Sasa subiri 2024 ndio mtatafuatana wajinga wakubwa nyinyi.
Kama hayo unayajua kilio cha ninisasa?
 
Nyinyi mshukuru sana Mungu alimchukua JPM mapema angewarudisha kwenye mapango mlikotoka. Mama katukosea sana na huruma zake. Ingepita operation moja kabambe ndio mngeshika adabu mbwa nyie.
Na Magufuli asingekubali kuja na mikataba mibovu kama hiyo.
 
Amani ya nchi bila uhuru ni kazi bure. Hatuwezi kuuzwa kirahisi kwa bei ya bazoka.

# Asiyetaka kukosolewa atoke kwenye ofisi aende akalee wajukuu#

Uzumbukuku wa mtu mmoja hauwezi kugharimu hadi vizazi ambavyo bado vipo kwenye viuno vyetu.
Kkenge nyie tutaawanyoosha
 
Kwani wewe hulijui hilo? nakushangaa sana kama unaamini iko siku utaiondoa CCM kwa kupiga kura yako. CCM haitoki CCM ni zaidi ya chama ila manweza kuja kuomba uwakilishi tu tukawapa baadhi ya viti kuonesha na nyinyi mumo mpate kula ruzuku kidogo.
Narudia tena, hizo lugha za kujigamba zitafika mwisho. Tutahakikisha njia ya Hadaa ya box la kura kwanza wananchi wanaipuuza kama wanavyozidi kuipuuza. Kisha baada ya hapo tutatafuta njia nyingine ya kuwatoa madarakani. Kama huamini hili, tunza hii post kisha utapata mrejesho wake.
 
Na nani alikuwa anawatetea wale watu wa migodi? sio Lissuna nyinyi Chadema au mnajitoa ufahamu. Risasi alipata sababu nini? si aliitwa na JPM wasaliti wa nchi sababu alikuwa kutwa akiwapigania wakati JPM alikuwa anasema hapana.
hapo nimeizungumzia Chadema au unajua Mimi ni mfuasi wa Chama gani? usiwe unakurupuka soma kitu uelewe.
 
Mimi sina shida na wewe lakini tukitaka twende vizuri na kujenga hoja ni vizuri. Nchi hii hatuwezi kukubaliana hata siku moja 100% lazima tutakuwa na maoni tofauti. Sawa na mpira tunatizama game moja pamoja lakini tukitoka tukianza kuongea ni kama tulikuwa tunatizama game tofauti lakini mshindi anakuwa na hoja zaidi. Kwenye siasa ya vyama vingi lazima tutakuwa na maono tofauti ndio maana ya democracy. CCM wana mandate ya kuamua kwa niaba yetu sababu walishinda uchaguzi na ili kushinda uchaguzi walikuwa na sera zao watu wakawachagua. Ni haki yao ku deliver walichoahidi. Wakishindwa uchaguzi ujao wapigeni chini simple.
Ccm walishinda uchaguzi kwani kulikuwa na uchaguzi? Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Na hakuna sera yoyote iliyowapa ccm kura, bali wachache waliipa kura ccm kwa mazoea.

Na ile inayoitwa ilani sio chochote wala nini, bali ni orodha ya mahitaji yote ya binadamu hata walio nje ya Tanzania. Machafuko tu ndio yatairudisha nchi hii kwenye mstari.
 
Hilo ndio jibu la wezi wa CCM ofisi ni za umma vumilia maneno yote mazuri na mabaya
 
Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi ameachiwa huru majira ya saa 12 jioni (Julai 14, 2023) baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa saba katika Ofisi ya makao kikuu ya Polisi mkoa wa Mbeya.

Akizungumza na Jambo Tv baada ya kumaliza mahojiano yake na Polisi, Mwabukusi amesema aliitwa na Jeshi hilo akituhumiwa kwa makosa ya kutoa lugha ya chuki dhidi ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa akidaiwa kwamba alihamasisha jamii kuwa Waziri Mkuu asiaminike kwa wananchi juu Suala la uwekezaji wa bandari kuwa una faida, hoja anazosema amezitolea maelezo polisi.

Aidha Mwabukusi amesema kuitwa na kuhojiwa kwake kwa muda mrefu wa zaidi ya saa saba kunampa nguvu pamoja na mawakili wenzake kuendelea kuwatetea walalamikaji ambao wananchi waliofungua kesi ya kupinga mkataba wa Bandari kwa madai kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

"Niwaambie tu kwamba kwa hili la kuitwa na kuhojiwa inanipa moyo sana na sikati tamaa pamoja na wenzangu, msimamo wangu uko palepale, inanipa moyo kwani naelewa kwamba kumbe Meseji Sent and Derivery (Ujumbe umeenda na umewafikia)", Wakili Mwabukusi.

"Mimi ninachotaka kuwaambia wa-Tanzania 'Hatujakosea', tuko sahihi, msimamo wetu ni uleule na tupo tayari kufika kwenye vyombo vya kisheria kwa namna yoyote kwasababu ninaamini tutapita tena na tena kwenye uvuli wa mauti lakini tutafika kwenye ukombozi kamili", Wakili Mwabukusi.

"Tuna haki za kikanuni na kikatiba, na mtu yeyote asiyetaka kukosolewa aondoke kwenye Ofisi za umma akakae nyumbani kwake hatutamfuata lakini mtu anayevunja Katiba tutamsema, kwahiyo siogopi, hata mtu akiwa Mbunge, Waziri mkuu au Rais hiyo ni dhamana hii nchi ninyetu sote sio ya watu wachache lazima nisimamie msimamo wangu lakini na kulinda raslimali za Taifa kwa mujibu wa Katiba", Wakili Boniface Mwabukusi.

Naye Wakili wa Mwabukusi kwenye shauri hilo Wakili Phillip Mwakilima amewashukuru wanasheria mbalimbali walioshirikiana katika sakata la kuhojiwa kwa mteja wake (Boniface Mwabukusi) akiwemo Rais wa TLS na Balozi Dkt. Wilbroad Slaa.

Amesema Mwabukusi ameamriwa kuripoti tena polisi mwanzoni mwa juma lijalo.

Hata hivyo Wakili Mwakilima amesema wamejiandaa kumfungulia mashtaka Juma Homera ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa madai kuwa amewadhihaki wateja wao (Waliofungua kesi ya bandari) kuwa wanawatetea wezi pia anadaiwa kushindwa kusimamia nafasi yake ya Mwneyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama badala yake amesikika akisema waliofungua kesi ya kupinga mkataba wa Bandari anawakabidhi kwa machifu wa kimila ili wawashughulikie.

"Kwahiyo niiombe mamlaka yake (Mkuu wa mkoa Mbeya Juma Homera), Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ampeleke kwingine kama si kumuondoa kabisa maana kwa hili tu (kuwakabidhi waliofungua kesi kwa machifu) hafai kuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama", Wakili Phillip Mwakilima.


Mtuhumiwa Wakili Boniface Mwabukusi aliingia polisi saa 3:58 asubuhi na mahojiano yalimalizika majira ya saa kumi na dakika kadhaa lakini Wakili Mwakilima alieleza kuwa bado Mwabukusi anaendelea kuwa mikononi mwa Polisi licha ya kumaliza mahojiano hadi baadaye majira ya saa moja kasoro baada ya taratibu nyingine kukamilika hasa za kujidhamini hadi atakaporipoti Jumatatu ijayo Julai 17, 2023.

Chanzo: Jambo Tv
kurusha maneno hayo kwa waziri mkuu ni issue ya mtu binafsi, sio ya kijinai, waziri mkuu kama anaona amechafuliwa akafungue kesi ya madai ya kuchafuliwa mahakamani, hapo jinai itasimamaje sasa? wakati mtu ana maushahidi kwanza, yale yote ameongea mwabukusi ushahidi upo.
 
Na nani alikuwa anawatetea wale watu wa migodi? sio Lissuna nyinyi Chadema au mnajitoa ufahamu. Risasi alipata sababu nini? si aliitwa na JPM wasaliti wa nchi sababu alikuwa kutwa akiwapigania wakati JPM alikuwa anasema hapana.
Lisu alianza kuwatetea wananchi wa migodini wakati Magufuli yuko kimya huko CCM akilinda cheo. Ni mzungu gani anasubiri kutetewa na Lisu kuhusu kumiliki migodi. Ni migodi gani hawakuwa wamepewa na CCM hadi wamsubiri Lisu?

Magufuli alichokuwa anafanya kwenye suala la migodi ni kutafuta sifa za kisiasa, akaona Lisu ndio mwenye sifa hiyo, hivyo kwa ulevi wake wa madaraka ikibidi atangeneze story za kubumba ili kumchafua Lisu, na yeye aonekane wa maana. Lisu hakusubiri kuwa rais ndio atetee wananchi wa migodini, bali Magufuli ndio alisubiri hadi awe rais ndio atetee migodi.
 
Narudia tena, hizo lugha za kujigamba zitafika mwisho. Tutahakikisha njia ya Hadaa ya box la kura kwanza wananchi wanaipuuza kama wanavyozidi kuipuuza. Kisha baada ya hapo tutatafuta njia nyingine ya kuwatoa madarakani. Kama huamini hili, tunza hii post kisha utapata mrejesho wake.
Wewe acha kujitekenya.
 
Nimeshasema kosa kubwa nyinyi Rais Samia kuwaachia na kuwa mpole alitakiwa mtu kama JPM mliuvyata mikia wote hakuna hata mbwa mmoja aliyetoka hadharani kuandamana. Yule mguu mbovu akakimbia kabisa nchi, yule muuza Bangi Arusha alikimbia kama mwizi mpakani, mwenyekiti wenu ndani kumetmbelea tu jela mlikuwa manogopa kama JPM atawashughulikia. Mlikuwa mna nini? Sugu alisema rais wa Mbeya wekwa ndani hakuna hata mtu mmoja aliyetoka barabarani. Mama Samia kaja kawaonea huruma tokeni lakini sasa mnaanza kukosa adabu lakini mnaijuwa CCM wakilitaka jambo...
Kaka utakuwa na shida si kidogo mbona unafurahia mateso ya wenzako. Mfano Lisu kupigwa risasi zote zile bado huwezi kumhurumia. Kinyume chake unamkebehi. Ila kumbuka hujafa hujaumbika.
 
hapo nimeizungumzia Chadema au unajua Mimi ni mfuasi wa Chama gani? usiwe unakurupuka soma kitu uelewe.
Nchi chama kimoja tu CCM. Unajuwa kama wachezaji mpira wa kibongo ndoto yao kuchezea Simba au Yanga, ukikosa huko ndio utawakuta Coastal, Namungo sijui Mtibwa lakini lengo lao moja tu Simba/Yanga. Ndio vyama vya siasa na wanasiasa bongo. wakikosa CCM wanakimbilia huko kwingine kuongeza kiwango wakicheza vizuri wanasajiliwa tena CCM. Kwa maana hii wapinzani wote huko wanadamu ya CCM nje ni mbwembwe waonekane. Kupenya CCM sio mchezo uwe na kiwango.
 
Back
Top Bottom